Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Tarime amsimamisha kazi Afisa Utumishi

WAIKORU

JF-Expert Member
Dec 9, 2015
1,586
2,443
Hapo jana katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Tarime, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mji-Tarime alimsimamisha kazi Afisa Utumishi kwa kosa la kula njama ya kuiibia serikali..

Kwa mujibu wa Mkurugenzi, Afisa Utumishi huyo kwa Jina la Marwa...amekuwa akishirikiana na watumishi wengine idadi yao ikiwa ni sitini (60) kuondoa makato kwenye salary slip zao ikiwa tayari wana mikopo benki..na hivyo kuwafanya watumishi hao kuwa na sifa ya kukopesheka tena...

iko hivi, mtumishi A anaenda benki NMB anakopa milion tano kwa miaka mitatu ambapo makato yake kwa mwezi ni laki mbili... analipa miezi miwili..then anaenda kwa huyo Afisa Utumishi wanakula dili...anamwondolea makato..afu anamprintia salary slip inayoonesha kuwa mtumishi A hadaiwi...

kwa hiyo Mtumishi A..anebda benki nyingine. say CRDB anakopa tena...ukikatwa miezi miwili mitatu...wanafanya yao...anaenda benki nyingine tena kukopa...

Kwa kuwa Mwajiri (mkurugenzi) ndio anaweka dhamana kwa watumishi..analazimika kulipa fidia kwa Benki zinazodai kupata hasara...

Hivo baada ya kufanya uchunguzi kwa muda ...amegungua mchezo huo kati ya Afisa Utumishi huyo na watumishi wengine 60..wengi wao wakiwa ni Walimu...

source: mimi mwenyewe nlienda kwenye hicho kikao.
 
Watu wana madili aisee...Ila awamu hii noma...wataumbuka sana...
 
Watu wana madili aisee...Ila awamu hii noma...wataumbuka sana...
Dah hii kali. Ila ingekuwa mimi,nikishakamilisha mzigo wa benki zote,ningefungua saccos ya riba kubwa na kuendelea kurejesha bila wao kugundua. Cha ajabu,utakuta wengi wao hawakuwa na mpango wowote wa maana zaidi ya masanga!
 
Dah hii kali. Ila ingekuwa mimi,nikishakamilisha mzigo wa benki zote,ningefungua saccos ya riba kubwa na kuendelea kurejesha bila wao kugundua. Cha ajabu,utakuta wengi wao hawakuwa na mpango wowote wa maana zaidi ya masanga!
Inawezekana mkuu...lakini pia kwa maelezo ya mkurugenzi, wote walioshiriki katika mchezo huo watachukuliwa hatua za kinidham na ikitibithika wana makosa watafukuzwa kazi....

sasa kama ulichukua mikopo kadhaa na hukufanya lolote..ndio kimbembe kinaanzia hapo
 
Back
Top Bottom