Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Mafia ni jipu

Kimarondo

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
259
218
DED wa Mafia bwana Eric Mapunda ni jipu tena tatizo kweli! Mkurugenzi huyu ambaye ametokana na kushindwa ubunge huko kwao haishi vituko

1) Amekuwa na kawaida ya kuingilia taratibu za manunuzi kwa lengo la kujinufaisha binafsi, mfano ameenda mwenyewe kununua cement akijifanya alinunua kiwandani kumbe kanunua kwa mtu huko Dar.

2) Ameagiza na kununua mbao kutoka iIringa bila kufuata taratibu za manunuzi kisingizio anabana matumizi ya serikali wakati anayaongeza maradufu.

3) Amemlipa kwa impress Afisa Aridhi ambaye pia ni mwandani wake tsh 4.5 milion kwa ajili ya kutengeneza/kuchimba bwawa la maonesho ya nanenane! hakuna bwawa wala samaki walopelekwa.

4) Anawasimamisha na kuwashusha watumishi wote ambao wanajaribu kuhoji maamuzi yake mf. Mwanasheria na Dt. Mwanasheria amesimamishwa ili kumpisha mwandani wake ambaye ni mwalimu huyu ndo kaimu mwanasheria kwa sasa.

5) Ameagiza na kushonesha nguo za wauguzi na madaktari hospital ya wilaya bila kufuata sheria za manunuzi kilichotokea anakijua mwenyewe. Nguo hazikuwatosha kampuni ni yake toka kaongea.

6) Mwezi wa saba juzi lilitoka tangazo la kuwataka wanaotaka kuhama halmashauri nyingine wahame huyu bwana amekataa. Amemkatalia RAS eti Mafia haihusiki.

Mambo ni mengi lakini ikumbukwe tu kuwa huyu ni kati ya wale wakurugenzi waliotafutwa na mtukufu mpaka usiku wa mamake.

Mafia kuna vyombo kama mkuu anavyojitapa nacho, vimchunguze huyu mkurugenzi kabla hajafanya mabaya zaidi.

Natoa wito kwa PCCB ichunguze mienendo yote ya mkurugenzi huyu kuanzia ya watumishi mpaka kununua na kujua ili kujua kama bado ana credibility ya kuitwa mkurugenzi maana baadhi ya tabia hazivumiliki.
 
atakua kabana mianya ya kula ndo maana unalalamika wewe. taratibu zikiwa nyingi zinaleta mianya ya rushwa na ucheleweshaji wa maendeleo.Acha mkurugenzi apige kazi watu wanataka maendeleo siyo taratibu za manunuzi.
 
We ni wale mnao amini kuwa kila kitu kilikosewa huko nyuma? maendeleleo gani anaweza kuleta bila kufuata taratibu? kama mafia kuna wazabuni wake wa miaka yote ambao wamepatikana kisheria yeye ndugu mapunda anapata wapi mamlaka ya kwenda mwenyewe kununua cement tena kutumia mzabuni wake wa mfukoni huku akijidai kununua kiwandani? kama kuna wazabuni yy anapata wapi mamlaka ya kwenda kununua mbao iringa? anapata wapi mamlaka ya kuleta mzabuni toka songea kuja kushona nguo za watumishi? anapata wapi mamlaka ya kutengeneza magar kwa imprest/ masurufu? kama kweli mnawaminisha wa Tanzania kuwa mnajenga tz mpya huyu ni kati ya wasiofaa!
 
bei ya mzabuni ipo juu tofauti na ofisi kununua direct. hapo mkurugenzi ameamua kubana matumizi. fedha nyingi za umma hupotea kwenye manunuzi.vumilieni tu
 
3) Amemlipa kwa impress Afisa Aridhi ambaye pia ni mwandani wake tsh 4.5 milion kwa ajili ya kutengeneza/kuchimba bwawa la maonesho ya nanenane! hakuna bwawa wala samaki walopelekwa.

Hapa pangenoga kama kingekuwepo kielelezo
 
DT amekutuma ??

namshauri DED akaze kamba ili mtie adabu nyie mafisadi dagaa. mnajifanya hapo wilayani ni viumbe wateule kumbe njaa tu.

ndg ded pangua safu yote, jenga urafiki na DC na ocd ili wanaozingua zaidi walowekwe ndani.

ova
 
atakua kabana mianya ya kula ndo maana unalalamika wewe. taratibu zikiwa nyingi zinaleta mianya ya rushwa na ucheleweshaji wa maendeleo.Acha mkurugenzi apige kazi watu wanataka maendeleo siyo taratibu za manunuzi.
Unasema taratibu zikiwa nyingi wakati huo huo unaona hizo taratibu ni njia ya rushwa...!!!
Hivyo tufanye shaghalabaghala ili tuzuie rushwa???
 
Manunuzi kwa wazabuni ni kero kwa halmashauri zote sababu ya 10% pia ni chanzo kikuu cha rushwa.
 
Back
Top Bottom