February 10, 2020
Bwawa la Mtera lenye uwezo wa kufua umeme megawatts 80 linazidi kujaa maji na hivyo TANESCO huenda wakalazimika kufungulia maji, hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco. Maji yakitoka hapo pia huenda kituo cha Kidatu na kufua umeme mwingine wa Megawatts 204. Hii inatokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwa miezi miwili iliyopita nchini.
Kufuatia hatua hiyo wananchi wa mikoa ya Dodoma, Morogoro na Bonde la Ruaha /Rufiji wametakiwa kuchukua tahadhari maana mkondo wa maji ktk mito ya maji kama Mtera itazidi kujaa katika maeneo yao iwapo bwawa la Mtera litazidi kujaa maji kufikia ukomo wake na kulazimika kufungulia maji.
Maeneo yatakayopata ongezoko la mtiririko wa maji ktk mito na vijito ni wilaya za Mpwapwa, Kilolo, Kilombero, Kilosa na Bonde la Mto Rufiji.
Hivyo wananchi wanaoishi maeneo hayo waendelee kufuatilia taarifa juu ya hali ya Bwawa la Mtera zitakazokuwa zinatolewa na Tanesco kila mara. Mara ya mwisho kufungulia bwawa la Mtera ili kutiririsha maji ya ziada kulifanyika mwaka 2008 hivyo TANESCO ina uzoefu wa kufanya zoezi hili kwa usalama bila kuleta madhara kwa watu waoishi katika mkondo wa maji. Taasisi zingine zote zimetaarifiwa kuhusu tahadhari hiyo. Mwisho wa kumnukuu Mkurugezi Mtendaji wa Tanesco Dr. Tito Mwinuka.
Source: TANESCO Yetu