Mkurugenzi Mtendaji Liwale Lindi Ashinda Kura Za Maoni CCM Singida Kaskazini

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
41,196
2,000
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale mkoani Lindi, Joseph Monko ameshinda kura ya maoni CCM katika jimbo la Singida Kaskazini.

Ndg Joseph Monko alifanikiwa kupata kura 22 kati ya kura 112 zilizopigwa. Uchaguzi huo uliofanyika katika kijiji cha Ilongera wilayabi Singida ulishirikisha jumla ya wagombea 22.

Uchaguzi huo ulikuwa wa marudio baada ya ule wa awali kufutwa kwa tuhuma za kugubikwa na rushwa.

Mshindi wa pili akikuwa Ndg Choyo Japhet ambaye alipata kura 20. Zoezi la kura za maoni ni sehemu tu ya mchakato wenye lengo la kupata maoni ili kujua mgombea gani anakubalika na kuuzika lakini uteuzi rasmi unafanywa na vikao vya juu vya Chama cha Mapinduzi.
 

baro

JF-Expert Member
May 12, 2014
2,511
2,000
Huyu monko aligombea 2015 na aliacha Kazi Tanga cement

Aliupenda sana ubunge mwacheni aupate
 

GIUSEPPE

JF-Expert Member
Dec 31, 2011
5,266
2,000
Huyu monko aligombea 2015 na aliacha Kazi Tanga cement

Aliupenda sana ubunge mwacheni aupate

Kwa hiyo baada ya kujaribu ubunge akashindwa ndo akapewa kifuta jasho cha ukurugenzi wa manisipaa? Sasa ndo wameamua kumpa ubunge baada ya kufanya kazi nzuri ya kutetea chama akiwa mkurugenzi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom