Mkurugenzi mtendaji Gotham ni Mkurugenzi wa utafiti na ICT - TIC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi mtendaji Gotham ni Mkurugenzi wa utafiti na ICT - TIC

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by izihaka, Feb 24, 2009.

 1. i

  izihaka Member

  #1
  Feb 24, 2009
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tanzania sijui ni lini mtaamka ofisa wa serikali ngazi ya ukurugenzi anaanzisha kampuni akiwa ndani ya serikali then ana-apply kuishauri serikali anapewa mkataba bado watu wanasema kulikuwa hakuna mchezo mchafu?

  Pambanueni wadanganyika muone wenyewe kampuni hiyo na huyo JJ Kyaruzi ambaye anajiita Doctor huku akijua kuwa hakuupata u-Doctor na pia akiwa na record mbaya kabisa ya zile smart card za pale mlimani ambazo mpaka leo sie ambao tulichangishwa na kupewa hatujui zilikuwa na tofauti gani na id za kawaida leo hii anaishauri serikali juu ya ID?

  Waulizeni CRDB benki watawaambia alichofanya pale! JK amka Maimu na Kyaruzi watakuchafua sasa hivi.

  UDSM walimtimua Kyaruzi kwa kushindwa kazi ya just students ID tu za kuingilia library!
   
 2. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni kweli mradi wa smart card UDSM unaonekana ni failure to large extent. Wakati nipo hapo kulikuwa na case za wanafunzi kulipwa mara mbili sababu ikiwa kukosekana kwa terminal za kuweza kuread hizo card ndani ya ofisi za malipo.

  Kama kwa eneo dogo la UDSM imeshindakana kuona mafanikio ya teknolojia hii sijui tutegemee nini kwa taifa zima ambalo tunajua kuwa 10% tu ndio wana umeme (ikiimanisha kuna wilaya bado hazina umeme)
   
 3. Zalendohalisi

  Zalendohalisi Senior Member

  #3
  Feb 24, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona alishaodoka huko miaka mingi akiaga kuwa kapewa ukurugenzi wa mradi wa vitambulisho! Na bado mengi yatajitokeza. Hata huyo Jack alishatumwa kwa jamaa yangu mmoja na Membe ili amsaidie technical insights kuhusu nyanja za ID systems. Jamaa akamtolea nje Jack baada ya kuliona tangazao katika Daily News toka TISS likuwatahadharisha wananchi kuwa yeye siyo mtumishi wa TISS ingawa ana-claim hivyo.

  Hiyo project study ya National IDs walioiandika ni Computer Science Department ya Chuo Kikuu. Wizara ya Mambo ya Ndani ikaikalia na ikawapa hao kina Jack wakaidandia na kui-massage na kuigeuza kuwa yao. Ndio mwanzao wa kumleta Kyaruzai kwa vile alikuwepo kwenye lile jopo la Chuo Kikuu mwanzoni. Usahaidi upo na kama Jack au Kyruzi au Wizari inabisha basi waiweke hiyo document hadharani (Project Writeup) watalaamu wa plagiarism waipitie. Za mwizi ni arobaini tu!


  ZalendoHalisi
   
 4. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  jamaaa ni kweli alikuwa TIC ndo kamchongo inaonekana kametengenezwa ili kula hela.
  huyu kyaruzi hata uelewa wake katika IT sio wa kijivunia kwani hana rekodi nzuri.
  jamanii naomba tuendeleee kushinikiza huu ufisadi wa vitambulishoo ukomeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.
   
 5. K

  KGM Senior Member

  #5
  Feb 24, 2009
  Joined: May 21, 2007
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Binafisi nilipoona Kyaruzi yumo ndani ya Gothamu nilishangaa ndio nikajua kumbe ndio maana wamepata hiyo kazi.

  Kifupi ni kuwa, huwezi kumutenganisha Maimu na Kyaruzi. Wanafahamiana vizuri na wameshashiriki kwenye madudu mengi wakati Maimu akiwa pale Utumishi.

  Hawa jamaa ni "majambazi" wa kutupwa na binafsi sijui serikali inafanyaje kazi na watu hawa.
  Kwa kweli imenishitua sana kumbe Kyaruzi ndio Gotham.

  Kwa kweli NCHI hii imekwenda kubaya sana.

  KYARUZI=GOTHAM=MAIMU=KYARUZI
   
 6. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  - Na wote tuseme kwa SAUTI kubwa "Huu ni mojawapo wa miradi iliyoshindwa kabla ya kuanza"

  - Wakati utasema!

  - Na itaundwa tume ya kuchunguza nini kilichojiri na baadhi ya wajumbe wa tume watateuliwa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani na Chuo Kikuu Computer Science Department na Mweyekiti wa Tume atakuwa Dr Twa... Baada ya hapo Serikali itasema imegundua mapungufu katika kumpata mwendesha mradi na kwahiyo kwenye budget ya 2010/11 gharama ya mradi itafikia 400bil na wabunge wetu watapitisha (kwa kupiga makofi mazito). Of course "tendering process itaanza upya"!!!!!!!!!!!!!!!!!! And the sh*** will go on and on and on

  - Ohoo Dear God please help!!!!!!!!!!!
   
 7. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2009
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Joe john kyaruzi !!!!!! Haya kumbe marsha alisema ukweli. Kazi kwenu maana mie alikuwa boss wangu huyu
   
 8. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2009
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  HUYU ANA SIFA MOJA KUU, AKING'ANG'ANIA JAMBO ATALISIMAMIA KWA MIGUU NA MIKONO AILI MURADI FUNGU LIINGIE MFUKONI, HAPO UDSM ALIKIMBIZWA NA PROF. MATHEW LUHANGA KWA SABABU NYINGI LAKINI PIA SMART CARD PROJECT NDIO CHANZO KIKUU NA KUTOMALIZIA Phd YAKE.

  KUMBE NDIO MAANA WALIMMINYA PROF. YULE WA UCC KWENYE UTEUZI WA KACHEO FULANI KTK ICT ISSUES KWA NCHI!!!!

  KWELI WATU WANACHUNGULIA MBALI SANA ILA TUOMBE MUNGU YASITUFIKE MABAYA TU
   
 9. Mzalendo

  Mzalendo Senior Member

  #9
  Feb 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hapa patamu

  kuna wanaozania wanajua kumbe...... na kuna ambao hawajui lakini hawajui kama hawajui, yani the perfect majadiliana yakitanzania

  you gatta love JF!!!!!!

  mungu ibariki Tanzania
   
 10. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #10
  Feb 24, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mradi huu ni wizi mtupu, wanatafuta fedha kwa ajili ya kampeni 2010 na sio vinginevyo.
   
 11. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mkuu,

  - Wewe ni Mzalendo kweli? Kama nn yako invyoonyesha?

  - Au umekuja kusoma mabandiko ya wanaojua na wasiojua?

  - Wewe upo katika kundi lipi?

  - Kama unajua na unajua kuwa unajua kwanini usibandike unachokijua kwa manufaa ya jamii nzima?

  - Miafrika ndivyo tulivyo!
   
 12. w

  wajinga Senior Member

  #12
  Feb 24, 2009
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata wakingangania kuufanya wananchi wakatae hizo ID
   
 13. Mzalendo

  Mzalendo Senior Member

  #13
  Feb 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu baba enock,
  kama mdanganyika nimelifwatilia sana hili swala mpaka kufikia kwenda kujifanya mwandishi na kuzama ndani ya hiyo press confrence waliotisha hao kina gotham,kudhibitisha,yule kubenea aliingia na islam wa thisday pamoja,yule lina denny wa channel10 aliondoka mapema,nilipata hadi handout ya presentation,nilistuka kumskia sarah mossi sijui wa RAI kusema,kwamba aliwaambia wenzake kuhusu ukweli wa gotham wao wakasema tumbamize tu anajifanya mjanja!!kama kuna mwandishi humu ndani aliudhuria atakumbuka hilo,mlangoni kulikuwa na wakribishaji wawili mmoja mrefu mmoja mfupi(sijui wa hoteli au wa gotham)

  sasa,mie hapo juu niona ni kuchafuana tu,amna swali la msingi,mara wizi mtupu(hii ishakuwa komedi)mara kyarusi sio DR( halafu?) swala hapa ni vitambulisho vya utaifa hili jamvi ni juu zaidi ya mtu yeyote hapa,mie naweza kuscan page mbili za hiyo presentation ya hao kina gotham iliyosimama(inajieleza) je wewe na hizo shtuma zako unaweza kuthibitisha au habari kutoka mtu wa tatu?

  hapo nyuma nilisema tuache kupotoshana,hilo naona kwako wewe imekuwa ngumu umechukuwa hili personal(eti mie mzalendo kweli?) sasa uoni hapo unataka tuache mada tuanze kujadiliana?

  basi wewe ni mzalendo zaidi yangu maradufu,je umeweza kupata usingizi?
   
 14. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #14
  Feb 24, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu usiwe na hasira tunajadili kitu kwa ajiri ya masirahi ya taifa, kama una information tofauti mwaga watu wajue ukweli ni hupi kwani kulalamika tu hakusaidii kitu.
   
 15. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #15
  Feb 24, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hapa patamu,tupige kelele zaidi.Pamoja na kutompenda Mengi kwa kulalamika kila siku nadhani habari hii tukifikisha kwake itasambaa.
   
 16. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Kuna mwenye picha ya Dr profesa mshaija kyaruzi?
   
 17. Mzalendo

  Mzalendo Senior Member

  #17
  Feb 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Swala sio hasira wala kulalamika hila,nikuchoshwa naupotoshaji uliozidi mipaka,mfano mmoja tu hapa dsm kuanzia majuzi yani lyumba katoweka,uzushi karibia kila gazeti,mara PCCB watoa donge nono,leo chaku shangaza huyo anaingia kisutu.

  wauza magazeti faida yao pale pale ,wananchi wanaoamini magazeti wamechukua kama yalivyo,hapa tayari kuna watu wamedhurika kwa hizi habari.

  mkuu jamco_co,
  hapa ni swala moja tu, mie niko tayari kudhibitisha kuwa hii hoja ni jungu lisilo manufaa katika jamii yetu na taifa letu,nahuhakika walioleta hapa hawawezi kuilinda hoja yao(zao) na ndugu,angalia sana hii miezi inayofwata jinsi,upumbavu wawapotoshaji utavyo tuaribia tunaopenda kujisomea magazeti.

  lakini kweli ukweli unauma,na unauma zaidi ukishtukizwa

  mungu ibariki Tanzania
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Feb 24, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Gotham alianza lini kuwa mshauri (consultant) wa mradi wa Vitambulisho?
   
 19. A

  August JF-Expert Member

  #19
  Feb 24, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Mzalendo ni kweli kwenye magazeti kuna upotoshaji kwenye mambo mengi tu, kikuu unachotakiwa kukifuata ni akili yako na elimu ndogo uliyo nayo katika jambo linalo ongelewa. Maana kama upotoshaji upo pande zote zenye kutaka huu mradi na wale wanaopinga fulani kupitishwa etc etc.
  Sasa jaribu kurudi kwenye jambo tunalo jadili hapa, usifuate la Sarah sijui what and what, fuata akili yako inakuonyesha nini juu ya jambo hili au kwa elimu yako unaona nini? tofauti ya hapo itakuwa upotoshaji wa habari kwa kutumia elimu ya makanjanja au ya wale waandishi walio nunuliwa na upande fulani. naomba usiwe mtumwa wa mtu , be a man by yourself
   
 20. K

  KGM Senior Member

  #20
  Feb 24, 2009
  Joined: May 21, 2007
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mzalendo, acha ubabaishaji, twambie unachojua wewe kuhusu gotham na umnjibu mmj swali lake, gotham kaanza lini u consultance wa mambo ya vitambulisho.

  1. ukatae kuwa kyaruzi hakushindwa na mradi wa smart card pale mlimani
  2. uthibitishe kuwa kyaruzi kafanikiwa kuwa dr
  3. na ukatae kuwa kyaruzi si rafiki wa karibu wa maimu na hivyo kuufanya mradi wenyewe uwe wa maimu.
   
Loading...