Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba atembelea Shirika la Utangazaji Japan

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
2a5c9614756ccd5a88fb8aee96c94df7.jpg
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC, Dkt. Ayub Rioba amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirika la Utangazaji la Japan - NHK Ryoichi Ueda na kukubaliana kuendeleza ushirikiano baina ya mashirika hayo ya utangazaji

Dkt. Rioba yuko jijini Tokyo kwa mwaliko wa NHK kujifunza namna shirika hilo kubwa la Utangazaji linavyotekeleza jukumu lake kama chombo cha umma

Ushirikiano baina ya NHK na TBC umedumu kwa miongo kadhaa na Dkt. Rioba anakuwa kiongozi wa kwanza kutembelea NHK.

Katika siku yake ya kwanza ya ziara ndani ya NHK, mbali na kukutana na Ueda, Dkt. Rioba amepata fursa ya kutembelea taasisi ya teknolojia na utafiti ya NHK na kujionea teknolojia ya kisasa kabisa television ya 8K.

Chanzo: TBC habari
 
Kupata viongozi wenye uwezo ni changamoto kubwa dunia nzima. Ndio maana naamini Makonda akijirekebisha anaweza kuwa kiongozi mzuri. Ana uthubutu
 
Alipokuwa nje alikuwa muongeaji sana na mtu wa mipango mingi mizuri!,tangu aingie hapo sioni jipya na TBC inazidi kupoteza watazamaji na wasikilizaji...
Amecopy mfumo wa Wanasiasa...walivyo. Kwenye jukwaa wazuri sana, ahadi kedekede

Subiri aingie mjengoni hata kutembelea jimbo tu shida, kutwa kucha Dar
 
2a5c9614756ccd5a88fb8aee96c94df7.jpg
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC, Dkt. Ayub Rioba amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirika la Utangazaji la Japan - NHK Ryoichi Ueda na kukubaliana kuendeleza ushirikiano baina ya mashirika hayo ya utangazaji

Dkt. Rioba yuko jijini Tokyo kwa mwaliko wa NHK kujifunza namna shirika hilo kubwa la Utangazaji linavyotekeleza jukumu lake kama chombo cha umma

Ushirikiano baina ya NHK na TBC umedumu kwa miongo kadhaa na Dkt. Rioba anakuwa kiongozi wa kwanza kutembelea NHK.

Katika siku yake ya kwanza ya ziara ndani ya NHK, mbali na kukutana na Ueda, Dkt. Rioba amepata fursa ya kutembelea taasisi ya teknolojia na utafiti ya NHK na kujionea teknolojia ya kisasa kabisa television ya 8K.

Chanzo: TBC habari
amejifunza nini au kaenda shopping! Kujifunza eti wanavyotekeleza majukumu yao ya utangazaji, kuminya habari chombo cha propaganda za chama tawala!
 
Nafikiri Ayoub Rioba inabid ajitathimini kwa sababu mkuu wa kaya amegeuza Clouds TV na radio kuwa radio za Taifa
 
TBC wamekosa ubunifu kabisaaaaaaaaaa hadi inakera na kuboa...ye akalie kupiga picha tu huko ila ajue huku shirika halifai kabisa kiwango hiki cha serikali ya magu...
 
Back
Top Bottom