Mkurugenzi Mkuu wa Posta Ivory Coast atembelea Posta Tanzania

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
664
829
MKURUGENZI MKUU WA POSTA IVORY COAST ATEMBELEA POSTA TANZANIA.

Na Mwandishi Wetu, Dar e's Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Posta Ivory Coast na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) na Umoja wa Posta Duniani (UPU), Ndugu Isaac Gnamba Yao ametembelea Makao Makuu ya Shirika la Posta Jijini Dar e's Salaam na kujionea namna Shirika hilo linavyofanya kazi zake hasa katika kipindi hiki cha ukuaji wa Teknolojia.

Ziara hiyo iliyofanyika leo tarehe 13 Septemba, ililenga kukuza ushirikiano baina ya Posta za Nchi hizi mbili pamoja na kuangalia fursa za kibiashara zitakazowezesha kukuza pato la Mashirika haya.

Katika ziara yake Ndugu Isaac, alipokelewa na Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara za Shirika la Posta Tanzania, Ndugu Constantine Kasese ambae alieleza hatua mbalimbali zilizofikiwa na Shirika la Posta Tanzania katika utoaji huduma kiteknolojia.

Aidha Ndugu Isaac alipata nafasi ya kuongea na Menejimenti ya Shirika la Posta Tanzania huku akiwataka kuongeza bidii na kuwa wanyumbufu katika kutoa huduma kwa niaba ya Serikali Ili kuwafikia wananchi.

Alisisitiza kuwa, Posta ni Taasisi pekee iliyo karibu na wananchi, na Serikali Inahitaji kuwafikia Wananchi wake , hivyo basi kupitia Posta, Serikali itaweza kuwafikia wananchi wengi kwa urahisi.

Katika kukamilish Ziara yake , kiongozi huyo alitembelea Posta Kuu ya Dar e's Salaam (GPO) na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa katika ofisi hiyo ikiwemo kituo cha "Huduma pamoja".

Imetolewa na:
Ofisi ya Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania.

IMG-20210913-WA0200.jpg

IMG-20210913-WA0202.jpg

IMG-20210913-WA0204.jpg
 
Moja ya vitu ninavyojivunia toka nijiunge JF ni wazo hili nililolitoa miaka michache iliyopita ndani humu, naona wamelifanyia kazi. Nitafuatilia kujua ni kwa kiasi jani maono yangu haya yametekelezwa.
 
Kama amekuja kujifunza pota tz nje ya kuwa amekuja kiutawala basi posta Afrika ina Safari ndefu😂😂
 
Back
Top Bottom