Mkurugenzi Mkuu wa JamiiForums anahojiwa Wasafi FM

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,801
11,961
Mkurugenzi Mkuu wa JamiiForums, Maxence Melo yupo live wa Wasafi FM kwenye kipindi Cha Mgahawa akihojiwa mambo mbalimbali lakini pia interview hii inarushwa live Youtube kwenye channel ya Wasafi media


===
Updates.

Melo: Nchi nyingi zinatamani kuwa na JamiiForums na tunaenda kufungua JamiiForums kwa nchi nane.

Maudhui ndio yanayoenda kuamua namna ambavyo watu wanafikiri na hata kuweza kuweka mawazo sahihi juu ya kiongozi ambae wananchi wanaenda kumchagua. Ni lazima kuwa makini na mtu anayedhibiti maudhui wa kuamua nini usikie.

Digitali ina fursa nyingi lakini ni lazima ipate mtu wa kuzielezea. Nafurahi kuona wananchi wanazidi kutumia digitali na kufunguka

Zamani taarifa za mtandaoni watu wanapuuza kwa kusema 'ni watu wa mtandaoni' lakini kwa sasa hali ni tofauti.

Zamani kulikuwa na wahariri na waandishi kwa sasa wanahabari ni wananchi wenyewe (Citizen Journalists).

Tusifanye mitandao kuwa sio sehemu ya maisha, yanayoongelewa mitandaoni ndio yapo kwenye maisha ya kila siku.

Sehemu yeyote unapokuwa na kumkosoa yeyote ni haki yako. JamiiForums kuna watu wanakosoa na kutoa maoni ya namna ya kurekebisha. Kwa sasa suala la kubadili mtaala wa elimu watu wengi wanatoa maoni mazuri.

Asilimia 90 ya waliomtandaoni ni wananchi wazuri na ni watumiaji wazuri wa mtandao.

Si kweli kwamba vurugu zinaanzia mtandaoni, Vurugu za Mwembechai hazikuchochewa na mtandao. Offline wana nguvu kuliko Online, ukidhibiti watu online huku offline ndio kutakuwa na shida zaidi.

Kila mwananchi ana haki ya kupata taarifa awe twitter, facebook nk, sisi tunapotoa taarifa na kupeleka kwenye mitandao mingine ni tofauti na wanavyofanya vyombo vya habari.

Matajiri wajao sio wale wenye viwanda bali ni watu wanaofanya mapinduzi kwenye ulimwengu wa digitali.
 
Nilivyoona anahojiwa nikajua anahojiwa na vyombo.
Bahati nzuri siku hizi vyombo vyetu haviko interest sana na ishu hizo.
 
Back
Top Bottom