Mkurugenzi Mkuu wa Bandari asimamishwa kazi!

kuna tetesi kwamba Mkurungenzi Mkuu Mamlaka ya Bandari amesimamishwa kazi..kuna mtu mwenye taarifa?


UPDATES:

Waziri wa Uchukuzi Tanzania Dk. Harisson Mwakyembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA Ephrahim Mgawe pamoja na wasaidizi wake wawili.

SOURCE : East Africa TV

Kwa Maelezo zaidi:-[Hongera mwakyembe tunakuona mwalafyale ukivuja jasho kwa ajili ya watoto wa tanzania, naomba mshauri mwezio wa Elimu Dr. Kawambwa asilale, mambo sio mambo katika taasisi zilizo katika wizara yake hususani VETA]
 
Swali langu linahusu misingi ya utawala bora, je mamlka ya nidhamu ya DG taasisi ya umma yapo kwa bodi , inakuwaje mawaziri tena wanasiasa anaamka anakurupuka anamsimamisha DG kazi. Naomba tujadili suala hili chini ya misingi ya utawala bora regardless ya kuwa mgawe ana makosa AMA la. Mawaziri wengi mnawafahamu Tabia zao za hovyo, mnakumbuka ishu ya chc na mkulo.

Narudia lile jibu langu kwa Ruta juu ya thread ya kupima utendaji wa Mheshimiwa Mwakyembe:

Kufuata ngazi na taratibu zote za kiutawala inafanyika ndani ya taasisi na serikali ambapo viongozi tegemewa chini yako ni wastaarabu na wote wanawajibika kama inavyotakiwa.

Kwa hali ilivyo sasa mimi naona hata bado hajafika kiwango ninachotaka. Yaani kama mtu anachekacheka na kuminya haki za raia na kuleta ubadhilifu eti tuendelee na mfumo wa kuunda tume na kuchekeana huku wanyonge wanaendelea kuumia? Piga chini tena hadharani kisha weka mwingine ndipo ma-CO’s na viongozi wengine popote watajua kuwa wanapopewa kazi wao sio indispensable!


Tukitaka kuondoka tulipofika katika Serikali yetu, mwendo lazima uwe wa a situational management style.
Hali za Wizara nyingi nchini sasa ni kama moto unaunguza nyumba hapo hakuna cha demokrasi ya kuitana vikao na kuanza na maombi marefu na kuendelea polepole kuuliza sijui tuanze kuzima wapi moto na ni nani aende kwenye fire extinguisher na kisha tupige kura nani atoe taarifa fire brigade, kabla ya kuanza kuona ni mchakato na mkakati gani tutatumia kuhamisha vitu kutoka ndani.
Ruta, tukiendelea na staili hii nyumba itateketea!

Fikiria, ni wazi na kweli kuwa Wafanyabiashara waliuawa bila hatia kwa kusingiziwa kuwa ni wezi lakini waliohusika wakaachiwa eti mashtaka yalikosewa!! Hapo kuna uhalali wa kuiacha mahakama na polisi eti kwa vile taratibu za kimenejiment na haki ya kutoiingilia mahakama zimefuatwa? Hiyo Mngt style ni kwa faida ya nani sasa???

Sisemi kuwa huyu Mh. ni perfecet lakini tumpe support aondoe uozo na Wizara zote ziwe hivi!
 
Mwakyembe ebu gusua na wale wanaochomoa vitu vyetu kwenye magari

Huo ni mtandao uliosukwa kwa ufundi mkubwa kuanzaia recruitment na ukasukika vilivyo, kuna jamaa zangu wa pale walinisimulia huu mtandao kutoka upakuaji wa mizigo --> gate #1 mpaka la mwisho na mbaya zaidi hujui yupi si mwanamtandao na ukijifanya mzalendo soon you will RIP au utabadilishwa kitengo kama si kupoteza kabisa ajira.
Hapa mwakyembe asijidanganye kuwasimamisha hao jamaa ndio ataondoa wizi/uozo.. ingekuwa vizuri iwapo angewafukuza wafanyakazi wote wa bandari na kuajiri damu mpya.
 
  • Thanks
Reactions: KVM
Wameonewa

Sijakoma wasiwasi wenye uelekeo huu pia aliuonyesha Ruta akaandika humu hivi:

Luta:
" Mwakyembe is walking faster but is he walking further....................... ...the answer is in negativity................hizi mbio za sakafuni huishia ukingoni na zitammaliza yeye"


Nikamjibu:
Please Luta, do not be a pessimist who sees only the dark side of the clouds.

Hata M. Luther King alionekana kwenda mbio na kasi yake ikatafsiriwa kuishia jioni ya saa 1:05 Aprili 04, 1968, baada ya kupigwa risasi pale Lorraine Motel (hatuombei haya), lakini tunajua ukweli kuwa huo haukuwa mwisho na sasa leo tunaona alichokipigania Marekani. Luta, nikukumbushe kauli ya kutia moyo ya MLK pale ktk hekaluni Memphis, aliposema,


"I may not get there with you. But I want you to know tonight, that we, as a people, will get to the promised land. So I'm happy, tonight. I'm not worried about anything. I'm not fearing any man. Mine eyes have seen the glory of the coming of the Lord".



Sitashangaa kusikia genge la ma CEOs wa mishe-mishe na raia ambao walikuwa wanafaidika kutoka katika mabomba ya kifisadi yanayokatwa na baadhi ya Mawaziri wachapakazi, kujiunga pamoja na kujaribu kuwanyamazisha; hawataweza for we, as people, will get to the promised land! Tumechoka na kuchekeana chekeana na huku tunaangamia in the name of bureaucracy! Watu wajiheshimu na kuwa na maadili ya kazi zao.

Inapokuja kwenye suala la maslahi ya umma hapa huwa sina cha chama, nasema tena kuwa Waziri yeyote anayetumia mamlaka aliyopewa kusafisha uozo na kurejesha nidhamu kazini mimi namuunga mkono. Ni aibu kuwa Waziri, halafu baadaye unaanza kulialia kwenye vyombo vya habari kama vile huna uwezo. Either you take actions or you step down! Wengine wenye guts wachukue hatua! Nani asiyejua uozo uliokuwepo TPA?
 
Mwakyembe ebu gusua na wale wanaochomoa vitu vyetu kwenye magari ni aibu na fedhaha watz wote tunaonekana wadokozi kwa ajili ya washenzi wachache
I know you can


Kwa kweli tunatia aibu ya ajabu. Watu wanaofanya hivyo TPA wanawaelewa lakini wanalindana.
 
wakina Nundu na nundu zao walikuwa hawayajui haya?? au nao walikuwa na mgao? kama kuna hasara wamesababisha akiba na amana zao zitumike kufidia hiyo hasara. siyo kuwaacha kama wakina jairo
 
SAFI sanaaaaaaaaaa, ila tatizo ni kwamba replacement anakuwa ndaga fijo mwenzake

Waziri wa Uchukuzi Tanzania Dk. Harisson Mwakyembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA Ephrahim Mgawe pamoja na wasaidizi wake wawili.

SOURCE: East Africa TV

Kwa Maelezo zaidi:-
 
Mgawe mie nilisema tangu Kikwete alipomteua kwamba si mtu wa kuiweza ile kazi.

Basically tatizo limeanza na uteuzi wa Kikwete.

kama mwakembe amemtimua kwa kushindwa kazi, na unasema tatizo lilianza kwa aliyemchagua basi kwa nini na sisi tusimtoe aliyemchagua mkurugenzi huyo maana naye hafai.
 
Swali langu linahusu misingi ya utawala bora, je mamlka ya nidhamu ya DG taasisi ya umma yapo kwa bodi , inakuwaje mawaziri tena wanasiasa anaamka anakurupuka anamsimamisha DG kazi. Naomba tujadili suala hili chini ya misingi ya utawala bora regardless ya kuwa mgawe ana makosa AMA la. Mawaziri wengi mnawafahamu Tabia zao za hovyo, mnakumbuka ishu ya chc na mkulo.

DG ni mteule wa Rais. Hata kama aliomba hiyo kazi anayemteua ni Rais. Nionavyo mimi ni kuwa Rais ameamua kuwapa madaraka mawaziri kushughulikia matatizo ya mashirika yaliyo chini yao pamoja na kuwaadabisha wakuu wa hayo mashirika. Kwa utawala bora ilitakiwa kwanza kuwe na Bodi ya Wakurugenzi iliyo huru na ambayo inaajiriwa mtendaji mkuu wa shirika na kumsimamia. Wakurugenze wa Bodi waombe kazi na DG aombe kazi.
 
kama mwakembe amemtimua kwa kushindwa kazi, na unasema tatizo lilianza kwa aliyemchagua basi kwa nini na sisi tusimtoe aliyemchagua mkurugenzi huyo maana naye hafai.

Kwa system ya sasa impeachment ni ndoto. Na Kikwete hana re-election inayokuja.
 
Hilo ni moja, pili tunataka tuone matokeo ya tume alounda yafanyiwe kazi ili tuone mabadiliko ya kweli katika utendaji wake,maana ni utamaduni wa idara na wizara za serikali kuunda tume lakini matokeo yake yanaishia kuliwa na mchwa katika makabrasha.Ninaamini anaweza kuleta mabadiliko ya kweli.
 
One after the other. Soon all of them will be gone and what will remain will be a story
 
Huo ni mtandao uliosukwa kwa ufundi mkubwa kuanzaia recruitment na ukasukika vilivyo, kuna jamaa zangu wa pale walinisimulia huu mtandao kutoka upakuaji wa mizigo --> gate #1 mpaka la mwisho na mbaya zaidi hujui yupi si mwanamtandao na ukijifanya mzalendo soon you will RIP au utabadilishwa kitengo kama si kupoteza kabisa ajira.
Hapa mwakyembe asijidanganye kuwasimamisha hao jamaa ndio ataondoa wizi/uozo.. ingekuwa vizuri iwapo angewafukuza wafanyakazi wote wa bandari na kuajiri damu mpya.

Kwa kweli anatakiwa afanye hivyo lakini itahitaji serikali ndiyo ifanye hivyo. Mbona TRA waliweza?
 
Ninajisikia ufahari siku hizi kupitisha mizigo yangu mombasa. No more losses, no more harrassment, no more time losses.....

Mkuu nilikuwa nasikia tu juu ya ufanisi wa bandari ya Mombasa, lakini baada ya kupitisha gari yangu huko nimeona mwenyewe tofauti ya utendaji wa bandari yetu na huko kwingine.Compratively huku kwetu ni aibu! Urasimu,wizi,unnecessary delays, unnecessary victimization ndio sifa za bandari yetu. Mombasa Ilinichukua siku 2 kutoa gari yangu na kuanza safari ya kurudi Dar es salaam. Hopefully Mh. Mwakyembe atabadilisha hii hali.
 
Back
Top Bottom