Mkurugenzi Mkuu wa Bandari asimamishwa kazi!

kamsimamisha pia Port Manager dar. kwa ujumla waliosimamishwa ni wanane pamoja na DG

Mzee iweke orodha yao vizuri ili tuwafahamu. Katika hao ambao tayari wametajwa nashukuru mjomba wangu hayumo. Malizia hao wengine mzee.
 
Mwakyembe ebu gusua na wale wanaochomoa vitu vyetu kwenye magari ni aibu na fedhaha watz wote tunaonekana wadokozi kwa ajili ya washenzi wachache
I know you can

Hivi hawa mamchwa hawatosheki na kuiba hivyo vya umma visivyo na wenyewe hadi wanachomoa vitu kwenye magari na makotena?
Hak ya nani! Natamani nimpige mtu
.
 
Safi sana. Natumaini wizi utapungua. Juzi juzi nilikwenda bandari kavu mojawapo yaani kila gari nililoliona lilikuwa limeibiwa kitu.

Watu wanaiba spare tyre unajiuliza inapitaje pale getini? Magari mengi yalikuwa transit kwenda Rwanda hata mimi nilisafishwa mizigo yangu!! SAD. Naambiwa vinaibiwa kwenye meli nonsense!!
 
Mimi nimefilisika from first container tu nilio order toka Europe, nimesumbuliwa mwisho wake nakuja ambiwa nilipe makumi ya maelfu ya dola na mbona hailipi.

Nikashindwa mali yangu mtaji wangu na madeni ikaishia kutaifishwa, nadhubutu kusema hatufiki popote Tanzania
.
 
Mwakyembe ebu gusua na wale wanaochomoa vitu vyetu kwenye magari ni aibu na fedhaha watz wote tunaonekana wadokozi kwa ajili ya washenzi wachache
I know you can

waliiba spare tyre yangu wakachomoa na redio mpya nina usongo nao sana!!
 
Mi nasubiri tarehe 01 October ifike tuanze kupanda train ubungo mpaka centroo
 
Swali langu linahusu misingi ya utawala bora, je mamlka ya nidhamu ya DG taasisi ya umma yapo kwa bodi , inakuwaje mawaziri tena wanasiasa anaamka anakurupuka anamsimamisha DG kazi. Naomba tujadili suala hili chini ya misingi ya utawala bora regardless ya kuwa mgawe ana makosa AMA la. Mawaziri wengi mnawafahamu Tabia zao za hovyo, mnakumbuka ishu ya chc na mkulo.
 
Hawa ndiyo mawaziri tunawataka, lakini subiri mtaona atahamishwa muda si mrefu kwenda wizara ya kazi na maendeleo ya vijana.

Ni heri akipelekwa Wizara hiyo bado atasafisha madudu.

Sema kwamba Rais akiona anaumbua watendaji wake ataamua kumpeleka Ofisi ya Rais ili kumfunga mdomo. sERIKALI YETU NI YA KULEANA KINDUGU

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Mimi nimefilisika from first container tu nilio order toka Europe, nimesumbuliwa mwisho wake nakuja ambiwa nilipe makumi ya maelfu ya dola na mbona hailipi.

Nikashindwa mali yangu mtaji wangu na madeni ikaishia kutaifishwa, nadhubutu kusema hatufiki popote Tanzania
.

duh.! Mkuu pole sana,lakini yanamwisho haya.!
 
Hivi hawa ndio wale baba Mwanaasha aliosema kuwa anawajua na atataja majina yao hadharani?
Job true true!
 
Swali langu linahusu misingi ya utawala bora, je mamlka ya nidhamu ya DG taasisi ya umma yapo kwa bodi , inakuwaje mawaziri tena wanasiasa anaamka anakurupuka anamsimamisha DG kazi. Naomba tujadili suala hili chini ya misingi ya utawala bora regardless ya kuwa mgawe ana makosa AMA la. Mawaziri wengi mnawafahamu Tabia zao za hovyo, mnakumbuka ishu ya chc na mkulo.

Mkulo na CHC tofauti na suala hili.hakuna cha kujadili.tuonane baada ya uchunguzi kwisha
 
Wakuu,

Muda si mrefu Mkurugenzi Mkuu wa Bandari Bw. Mgawe na wakurugenzi wengine watatu pamoja na Meneja wa Bandari ya Dar Es Salaam Bwana Cassian Ngamillo wamesimamishwa kazi na waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa Mwakyembe.

Inasemekana, kama kawaida yake amewasimamisha vigogo hao mbele ya kikao cha wafanyakazi kilichofanyika leo muda si mrefu..

Source: Mfanyakazi wa TPA aliyekuwa kwenye kikao.

More updates to follow, stay tuned.

Si useme tu kama ulikuwepo?

Halafu huelezi katoa sababu gani?? ukitoa taarifa toa kitu kinachoeleweka
 
  • Thanks
Reactions: ODM
Ninajisikia ufahari siku hizi kupitisha mizigo yangu mombasa. No more losses, no more harrassment, no more time losses.....
 
Back
Top Bottom