Mkurugenzi Mkuu Tanesco Ajiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi Mkuu Tanesco Ajiuzulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MegaPyne, Nov 21, 2007.

 1. Kwa habari zilizonifikia sasa hivyi zinasema Mkurugenzi wa Tanesco Bw. Idrissa amejizulu kama mkurugenzi mkuu wa tanesco.

  Barua yake imetumwa leo jioni
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Nov 21, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  One down.. !
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Nov 21, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Huwezi kupandisha gharama ya umeme kwa asilimia 40 na huduma nyingine zaidi ya asilimia 100 bila kuwaonesha watu kwanini... ni kama yule jamaa aliyeamua kuwa wanafunzi wachangie elimu ya juu asilimia 40 bila kutueleza kwanini... !
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2007
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kuna maswali mengi ya kujiuliza,
  Idris Rashid (PhD) alikuwa Bosi NBC alijitahidi, then Gavana BoT alijitahidi, then akaimarisha sana Akiba Comm. Bank then Akaenda NMB, na hatimaye TANESCO. (Pia alifanyia VOdacom briefly!)
  Alifanya U turn karibu kote alikofanyia kazi! Ana uzoefu kote- kama Mtanzania!

  Huenda watu wameingiza siasa TANESCO- yeye sii mwanasiasa! Kama Mtanzania alijitahidi- he is innovative and hardworking!
   
 5. A

  August JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2007
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,509
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  kama kajiuzulu kweli, nampongeza kwa kulinda heshima yake mwenyewe na elimu yake.
  Aache kuendekeza Uswahiba.
  Lakini kama ni kwa sababu nyinginezo nampa Pole.
   
 6. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #6
  Nov 21, 2007
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  sio bure lazima kuna siasa; ni maamuzi mazito sana hayo. Siku zote wanaCCM wamekataa TANESCO iendeshwe professionally. Kuna kitu, ngoja tusubiri.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Nov 21, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ukweli ni kuwa kajiuzulu on a principle na hilo ni lazima apewe pongezi na heko nyingi kwani amefanya kile ambacho watawala wetu wengi hawathubutu kufanya nacho ni kujipima wao wenyewe na kujua kuwa kuna wakati maji yamezidi unga. Jinsi uendeshaji wa Tanesco ulivyoingiliwa na wanasiasa for a technocrat like Idris (jamani siyo idrisa.. jina la kike) siyo mahali pake. Kama alikuwa na sababu ya kuongeza bei ya umeme, na wanasiasa wakaona hilo siyo jambo muafaka wakati huu wakajaribu kumshawishi I rescind on principle lazima ajitoe otherwise hatoweza kufanya kazi!
   
 8. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2007
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Sikumbuki nani kabla yake alijiuzuru wadhifawowote, hata katibu tarafa, nikumbusheni jamani wakuu...Ni uamuzi wa kupongezwa, kwa sababu yoyote ile. Nadhani kuna kitu kizito kimemzonga. Leo Tanga Cement wamelalamika kuwa wamekatiwa umeme na Tanesco eti kwa kuwa wamechelewa kulipa sh 49 million! wakati huo wanalipa sh 450 hadi 500 million kwa mwezi. Ni hesabu gani hizi? Hata hivyo wamerudisha jioni hii, na ni wakati huo Dr katangaza kujiuzuru. Pia kuna issue ya EWURA kugoma kuruhusu Tanesco kuongeza bei ya umeme...
   
 9. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #9
  Nov 21, 2007
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  No matter what are the reasons behind Dr Rashid's resignation,amefanya kile ambacho viongozi wetu wengi wameshindwa kukifanya.I salute his bravery!!!!
   
 10. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #10
  Nov 21, 2007
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Lakini kubwa kuliko yote, TANESCO imefikishwa hapo (katika hali ngumu) na nini? hiyo ndio hoja:

  1-Kwanza TANESCO haikua ikikusanya madeni yake serikalini na katika mashirika ya umma na kwa makampuni binafsi, watumishi walikua wakiachia umeme huku wao wakikusanya fedha. Tunakumbuka hadi leo Zanzibar inadaiwa na Tanesco.

  2-Shirika halikua na maamuzi ya mkiradi isiyo na faida, walilazimishwa kupeleka umeme hata mahali ambako hakuna wateja, mara nyingi kwa sababu za kisiasa bila ya kuwapo fidia yoyote toka serikalini

  3-Tanesco haikupewa mamlaka ya kuamua ni mikataba ipi iingie na kwa maslahi yapi, mikataba yote imesukumwa na serikali na baadaye Tanesco ndio imekua na dhamana ya kulipia gharama hizo, mfano ni IPTL, RICHMOND, KIWIRA, SONGAS, na kadhalika.

  4.Kuletwa kwa menejimenti ya Net Group Solution ambayo ilikua na ubia na kampuni ya Wace Technology inayomilikiwa na familia ya mama Anna Mkapa, ikiwa na wakurugenzi Joe Maro na Mr Maganga (wa BoT) wakiwa na watoto wao.

  Hayo ni mambo ambayo Tanesco hata wafanye nini hawawezi kujikwamua kiuchumi. Dr Rashid ni muadilifu na ameonyesha uadilifu wake kwa kuamua kuachia ngazi. Huwezi kumfananisha na wengine kama Dr Balali. Dr Rashid alithubutu kumnyang'anya Mwenyekiti bodi Kazaura gari la Tanesco na ofisi kwa kuwa hakuwa Mwenyekiti Mtendaji.. Jamaa alichukia sana
   
 11. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #11
  Nov 21, 2007
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Mbalamwezi,
  Kama Tanga Cement amekata umeme leo- kama anavyosema Mwanakijiji- he is a Technocrat! Hajui kubembeleza- ukiangalia tangu akiwa NBC, BOT, ACB, NMB na sasa TANESCO he made U turn in many issues in these institutions!
  Well ni heshima kubwa sana kama amekataa siasa kutawala uendeshaji!
   
 12. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #12
  Nov 21, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Idris tulimjadili hapa JF kabla hajapata hiki cheo leo yako wapi? Kazi imemshinda haya walete mazingaombwe tena. Hii kazi itangazwe na isiwe political appointment. Je, anaondoka mwenyewe kwa hiari yake au amefukuzwa?
   
 13. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #13
  Nov 21, 2007
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Bravo, kwa Idrisa, ingawa tungependa kujua exactly kilichomfanya ajiuzulu maana behind it kunaweza kuwa na ujumbe mzito kwa viongozi wengine, sasa kujiuzulu kwake kusifanywe siasa, yaani haiwezi kusemwa wazi, ooh ni siri za serikali,

  Isemwe wazi WHY? maana najua kuwa tuna viongozi wengine wengi wanaotakiwa kujiuzulu, sasa watajaribu kuigeuza hii ishu kuwa nyeti ya serikali, au siasa za majukwaaani we do not need that,

  Na pia tungemuomba huyu mkuu ayaweke mezani wazi yaliyojiri, lakini otherwise heshima mbele kwa Mkuu Idrisa.
   
 14. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #14
  Nov 21, 2007
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Dr Rashid alikuta Net Group Hawaja invest katika net work, kwa sababu wao walikua wakihitaji faida tu. fedha ikiwa nyingi walikua wakipata kamisheni kubwa zaidi kutokana na mkataba wao,,,

  Alipokuja Dr Rashid alikuta hakuna fedha za kuwekeza katika miundombinu ya umeme... Amekua jasiri
   
 15. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #15
  Nov 21, 2007
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  nampongeza dr idrissa kwa kujiuzulu...ukweli ni kuwa serikali inaleta siasa kwenye umeme na hii inasikitisha sana kwani wakati TANESCO inaendeshwa na wageni..serikali waliipa kila uungwaji mkono ikiwemo kuwaruhusu kukata umeme majeshi,usalama,ikulu,muhimbili ets...sasa kaingia mzawa wanataka aewndeshe mambo kiswahili..haiwezekani..hata mkurugenzi akiwa kikwete gharama za umeme kupanda hazikwepeki kutokana na mzigo mkubwa ambao serikali hiyohiyo imebebesha tanesco kutokana na mikataba mibovu..hiyo siyo siri!!!!
  INGEKUWA NI AIBU KUBWA KWA MSOMI kama dr rasshid anayeweza kusoma perfomance indicators za kamapuni vizuri..kuendelea kuwa mkurugenzi wakati anajua kuwa gharama za uendeshaji haziendani kwamwe na kipato...
  MIKATABA YA TANESCO NDIO ITAKAYOIUWA..UKIWEMO WA richmond ,agreco...ets hapa karibuni niliwambia hapa kuwa mikataba ya kununua gas yetu ya songo songo kwa ajili ya uzalishaji unafanya TANESCO WANUNUE UNIT KWA BEI KUBWA ZAIDI KWA KUWA KUNA WAKUBWA WAMEWEKA COMMITION ZAO...STILL HAWA RICHMOND[DOWANS] WAO WANAUZIWA GAS KWA UNIT BEI NAFUU ZAIDI KWA KUWA HAO WAKUBWA WANA INTEREST..NA STILL TANESCO INALAZIMIKA KUWALIPA CAPACITY CHARGES or someting like that...hapo hapo dowans hawajailipa tanesco fine yakuchelewesha mradi...some millions dollars...

  kama mikataba hii haitarudiwa kupitiwa upya tanesco itabakia chaka la viongozi mafisadi kupitisha deals zao..na nini kikwete hata tukipewa malaika hataweza kuliendesha....

  ila tujue umeme ni engine ya uchumi...gharama kubwa za umeme zinakimbiza wawekezaji...na kupandisha gharama za maisha..na zinasababishwa na maamuzi ya viongozi wetu hawahawa..
   
 16. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #16
  Nov 21, 2007
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Kuna Makubwa kuliko haya tunayoyazungumza hapa,TANESCO ni Idara wazi ya CCM,inaendeshwa kisiasa mno,Mzee Idris kwa kipindi kifupi tu amekwaruzana sana na Wakuu Serikalini pamoja na kwenye CCM,Na wengi wao walikuwa wanataka awape Heshima kwa sababu ya kupewa kazi hiyo!,Binafsi alikuwa anataka kuonyesha kuwa kapewa kazi kutokana na Uwezo wake na sio Asante.Ngojeni akabidhi kazi(ofisi) ni wazi atakuwa willing kuzungumza na vyombo vya HABARI,na mengi yatajulikana hapo!!!
   
 17. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #17
  Nov 21, 2007
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Mkuu Halisi, umesahau lingine, fedha ilizokuwa inakopeshwa Tanesco na serikali zilikuwa na riba ya juu sana, wakati serikali inakopa fedha hizo IDA kwa riba ya 2%, inawapa Tanesco kwa 8%...nani analipa hii riba kama siyo watumiaji wa majumbani? Walipokuja wazungu wa Netgroup taasisi nyingi ndo zikaanza kulipa madeni yao...nini hii?
   
 18. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #18
  Nov 21, 2007
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Mawado,
  Hope this becomes the 1st step kwa technocrats wetu wasomi kusema hapana kwa ajili ya uadilifu na manufaa ya Taifa letu! However many educated elites are nor ready though- I dont know why! Idris is bold enough to say no! Huu ni moyo wa uzalendo!
   
 19. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #19
  Nov 21, 2007
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  mawado thats right kuna habari kuwa viongozi wa ccm wameshazoea kuyatumia mashirika ya umma vibaya kugharamia hata mikutano yao..au pia kutaka kufaidika binafsi..taarifa za ndani za tanesco na mashirika mengine maandamizi zinasema..
  wapo pia wanaofikia kuazama magari ya mashirika haya na hawarudishi[hili hata mkaguzi wa kimataifa aliyeletwa ule mwaka 2003 aliliona aliripoti kuwa tanesco hawakuwa hata na record za asssets zao]..sio utani wameshawahi kununua vx kama kumi wakati mmoja naz zikatoweka ..
  tatizo akiingia pale mkuruigenzi ambaye hawalindi vigogo ...ataandamwa na kila baya hadi angoke...
   
 20. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #20
  Nov 22, 2007
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Kuna Makubwa kuliko haya tunayoyazungumza hapa,TANESCO ni Idara wazi ya CCM,inaendeshwa kisiasa mno,Mzee Idris kwa kipindi kifupi tu amekwaruzana sana na Wakuu Serikalini pamoja na kwenye CCM,Na wengi wao walikuwa wanataka awape Heshima kwa sababu ya kupewa kazi hiyo!,Binafsi alikuwa anataka kuonyesha kuwa kapewa kazi kutokana na Uwezo wake na sio Asante.Ngojeni akabidhi kazi(ofisi) ni wazi atakuwa willing kuzungumza na vyombo vya HABARI,na mengi yatajulikana hapo!!!

  Mkuu Mwawado,

  Heshima mbele mkuu, ninayachukulia maneno yako kwenye uzito wa juu sana kwa kukuaminia na nafasi yako katika taifa letu, maneno yako ni mazito sana na ninategmea more dataz najua you have this under control, lete dataz mwanangu tumkome nyani hapa giladi!

  Hawa kina Butiku, wanahitaji kusoma vitu kama hivi, sasa huyu Idrisa akiandika kitabu cha siasa na yaliyojiri, I promise nitahakikisha kununua vitabu vya kutosha kwa kila mwananchi hapa forum, maana kama anayosema Mwawado ambaye ninamuamini ni kweli, basi na huyu anaingia kwenye kitabu cha kina Zitto, na Dr. slaaa, yaani Tanzania so far tunakuwa na mashujaaa tunaowafahamu wanne,

  Yes, I said it wanne tu:-

  1. Mwalimu Nyerere - Kwa kuwatoa wakoloni na kutupatia uhuru.

  2. Zitto - Kwa kutufumbua macho wananchi kuhusu uhuni unaofanyika kwenye madini yetu.

  3. Dr. Slaaa - kwa kuweka wazi tuhuma dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi.

  4. Idrisa - "kwa kukataa siasa kwenye uchumi"

  Ohhh yah, nimesema asiyetaka tough and I do not care too!, hapa tunaongelea taifa sio mpira wa Yanga na Simba, to me hawa ndio the chosen ones katika taifa letu kwa sababu wameweka maisha yao on line kwa ajili ya taifa letu, FULL STOP!
   
Loading...