Mkurugenzi Mkuu NSSF, Masha Mshomba hizo ajira 271 ni kaa la moto kwako, chukua tahadhari

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
16,365
12,823
Julian Assange The Whistle Blower,Alishawai kusema kwamba Taifa lolote ambalo halina wapaza sauti KWA maslahi ya wengi basi ni Taifa legelege,

Nimefanikiwa kuipata inside story isiyo na mashaka hata chembe kutoka ndan ya shirika la Taifa la hifadh ya jamii Nssf hakika kweli sikio la kufa haliskii dawa..!Kwan hapo Nssf kuna nini kinachowafanya msitulie na kufanya kazi ya kujenga Taifa,mashirika ya umma yako mengi Sana,why always muwe kwenye headlines za mitandao ya kijamii?

Mkurugenzi Mkuu ndugu Masha,tafadhali kaa chonjo na Director of human resources and admistration Julius Kamuganga,na Manager wa Human resources Leah Mahali,wamechomeka hoja ya kibali Cha ajira takriban 271 za watu ambao wapo hapo Nssf wakifanya temporary Jobs,Hoja hiyo bila shaka iliwepo tokea enzi za William Erio na kuondoka kwake ghafla ndan ya shirika hilo kabla ya kufanikisha KWA mpango huo umewaacha wengi wa watu wao njia panda Sana.

Mkurugenzi huyo wa utawala hivi sasa yupo hapa Dodoma akihaha kwenye corridor za Katibu Mkuu wa utumishi akijaribu kufanya kila awezalo Ili kufanikisha nia hiyo,

Kumbuka william Erio alipofika hapo NSSF alikuja na ajenda kubwa ya kuwaondoa staffs wengi waliopo Nssf na kuwapeleka kwenye halmashauri mbali mbali na taasisi zingine kinyume na utaratibu Ili aweze kupata nafasi ya kuwaweka hao temporary staffs na kuwaleta wengine wengi ambao alitoka nao PPF.

Nia hiyo Ovu ya Kamuganga na Leah Mahali ni ya kupiga vita na kulaaniwa vikali Sana.

Vijana wengi wapo mtaani hawana kazi,na wapo ambao wapo competent kwanin ajira nyingi kama hizo 271 zisitangazwe KWA uwazi na hawa vijana waliopo huku mitaani wakagombania hizo nafasi fairly?

Iweje wanapeleka hoja ya kuwajir watu wengi hivyo kinyemela huku wakijua fika makosa katika maadili ya utumishi wa umma na ajira KWA ujumla?

Nasikia wanafanya vitu vya hovyo sana hapo,wamechukuwa watu ambao wapo temporary kisha wanawapa promotions without confirmation huo ni utaratibu wa wapi wanautumia.

Leah Mahali ameshiriki kuwaondoa mameneja takriban 12 ambao walikuwa ni staffs wa NSSF kinyume na utaratibu na wengine kuwapeleka halmshaur mbali mbali ambako hadi hivi leo yasemekana wanalipwa na payroll ya hapo hapo Nssf.

Taarifa zinasema kwamba anachukua hadi Rushwa Ili aweze kuwapa promotions baadhi ya watu mfano aliekawa muhasibu mwanza amehonga pesa nyingi KWA Leah Mahali then akafanya lobbying na kupewa Kuwa Regional manager Mbeya,mwingine aliekawa senior officer rukwa amehonga pesa KWA njia hizo hizo na kupewa Regional Manager Katavi,ni taarifa zisizo na shaka na ikibid Takukuru waliangalie suala hilo.

Ndug Masha,MKURUGENZI MKUU KWA taarifa zako za utendaji unaonekana ni mtu mwenye weledi mkubwa, mchamungu,usiependa majungu,makundi,Rushwa,dhulma,unyanyasi na upendeleo.

Simama katika misngi yako kama hiyo bila shaka yoyote huwezi kuyumba,umeaminiwa na kupewa nafasi kubwa kama hiyo kutokana na weledi wako,Huyo Mkurugenzi wa utawala Kamuganga na huyo manager wake Leah Mahali wanakuingiza shimoni,tuliza akili yako tafuta team yako ambayo haitaendekeza majungu na migogoro.

Hizo Ajira ambazo wanataka kuzitoa KWA upendeleo tafadhal kama kweli basi zitangazwe KWA uwazi vijana wenye sifa waombe na ufanyike usaili wa haki bila upendeleo wa aina yoyote.

KWA hali ilivyo hao jamaa hutaweza fanya nao kazi hata kidogo,hujamaliza hata mwez nadhan tokea umeteuliwa lakin wameshaanza choko choko za kutaka kukukwamisha na kukutoa kwenye reli,kaa kwa TAHADHARI kubwa sana.

Weka misingi imara na ya haki Ili uweze kuonesha tofauto baina yako na watu failures na wenye Roho Mbaya Mbaya kama william Erio.

William Erio ni mmakuwa wa masasi,ana roho ya kukunja Sana na siku zote mtu mwenye roho mbaya mwisho wake unakuwa ni wa aibu, tafadhal usifuate legacy mbovu kama ya william Erio hapo Nssf,tenda haki Ili uongoze kwa amani.
 
Taarifa kama hizi peleka takukuru!! Ndo kazi yao!! Lakini ukweli ndo huu kwamba rushwa haitaisha Kwenye nchi hii!! Mm ninaamini hata hao 271 ni watanzania wenzetu sema ni vzr ajira zikatangazwa kwa uwazi vijana wachangamkie sio kinyemela hivyo, hapo ndo wanakosea

Ni kweli Rushwa kuisha ni ngum Sana,na siyo tuh nchi hii bali dunian KWA ujumla,

Rushwa Ina addiction kama dawa za kulevya hivii,that's why ishu kama hizi nafasi ya kusema ikiwepo it's better tuseme washindwe wenyewe wenye mamlaka kufanyia mask,but tusiache kusema
 
Mnufaika wa zama za Ramadhan Dau na Bi. Chiku Matesa ukiwa kazini kuchafua uongozi mpya

Ofcourse, Ramadhan Dau hajaninufaisha Mimi tuh,kama kiongoz alipokuwa anaongoza hilo shirika kama nchi tumenufaika,mwenye macho haambiwi tazama,hilo daraja la kigambon kila siku mnapita KWA mbwembwe na majivuno,unadhan ni chini ya utendaji wa Mkurugenz mkuu yupi kama siyo Dau??

Hajaninufaisha Mimi,kanufaisha Taifa,huyo chiku matesa ni nani??Nifafanulie
 
Alikuwa Bosi wa Human Resource, Dau alimpenda sana
Kwa sababu alikuwa akitumika vyema katika mission zao (zenu) ovu

Naamini unamjua ila una zuga

Thanks for clarification,simfaham though,but what I believe she was smart,

Kama Dau aliiweza kumuamin,basi naamin she was smart,smart people believe and trust on each other,

Tunachojua sisi,hilo shirika ni Dr Dau kaliweka kwenye Raman ya TANZANIA immediately baada ya mkapa kumteua na kuchukua nafasi ya Mustafa Mkulo,watu kama nyinyi mnaona vyaelea tuuuh na kivitaman kumbe mnasahau kuwa vimeundwa,hamjifunzi kwanza kutoa appreciations,mnachojua ni kutaka kufuja na kujaza jamaa zenu KWA upendeleo kufakamia vitu ambavyo wenzenu wameviunda
 
Hi show ya sasa hivi anaisimamia mwnyewe Waziri mwenye dhamana ya ajira, yaani Jesista Mhagama. Mkurugenzi pamoja na Meneja wa HR wanatumika tu katika kutekeleza agenda ovu ya "kufagia" watu kibaguzi. Kuna nepotism ya hali ya juu na udini uliotukuka sio tu katika ajira mpya hapo NSSF bali hata kwenye silent reshuffle iliyokua imeasisiwa na Erio
 
Hi show ya sasa hivi anaisimamia mwnyewe Waziri mwenye dhamana ya ajira, yaani Jesista Mhagama. Mkurugenzi pamoja na Meneja wa HR wanatumika tu katika kutekeleza agenda ovu ya "kufagia" watu kibaguzi. Kuna nepotism ya hali ya juu na udini uliotukuka sio tu katika ajira mpya hapo NSSF bali hata kwenye silent reshuffle iliyokua imeasisiwa na Erio

Mkuu,so to say hayo yanayoendelea ni kwamba yana baraka ya huyo Jenister Mhagama??

Maana mperahimo huyo Naye KWA chuki za chini chini yuko vizur sana
 
Kama ni temporary staffs na anatpambania waajiriwe acha afanye hivyo awasaidie hao wanaotumikishwa. Jamani WTZ tuache Roho mbaya
 
Taarifa kama hizi peleka takukuru!! Ndo kazi yao!! Lakini ukweli ndo huu kwamba rushwa haitaisha Kwenye nchi hii!! Mm ninaamini hata hao 271 ni watanzania wenzetu sema ni vzr ajira zikatangazwa kwa uwazi vijana wachangamkie sio kinyemela hivyo, hapo ndo wanakosea
Watu wamekaa ofisini miaka 2 na zaidi wanajitolea afu uite watu wapya? Gharama zinginr hizi mnazitaka wenyewe. Wanaojitolea ndio waajiriwe hao hao. Hapa ofisini kwetu kuna madogo wa Intern kutoka TAESA yaan wanajituma sana mwaka jana taasisi imeajiri watu wapya kabisa wakati hawa vijana wapo na wanajua kazi, sio haki kabisa. Binafsi ningeanza ma hao wanaojitolea kuwaajiri wote kisha nirudi mtaani, kwanza tayari wanajua kazi, hivyo kupunguza gharama za training na vitu kibao.
Tuwe positive katika mambo mengi kwann alyways tunawawazia wenzetu kuwa wala Rushwa?
 
Mkuu,so to say hayo yanayoendelea ni kwamba yana baraka ya huyo Jenister Mhagama??

Maana mperahimo huyo Naye KWA chuki za chini chini yuko vizur sana
Sio mambo ya chini chini mkuu. Chuki zake anazisema kwenye vikao rasmi kabisa na watendaji wa shirika, yaani hao ma HR akiamini ni watu wa imani moja na yeye. Anatamka wazi kabisa "hizo shungi zifagieni zote pelekeni Halmashauri mnawaacha hapa wanini?".

Bahati nzuri wengine ni watu wa imani na hawapendi uonevu japo una wa favor watu wa imani yao na ndio wanapenyeza habari kumuhusu huyo mama. Kwa ujumla udini wa mama Mhagama umepitiliza na hata kikiundwa chombo kufatilia ni rahisi mno kuthibitisha hili
 
Back
Top Bottom