Mkurugenzi Mkuu Dr Sufian Masasi na Waziri Prof.Mbarawa mulikeni hili genge la mafisadi DAWASA kabla halijawaangusha

butron

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
5,283
7,306
Wakuu salaam,ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo.
Kuna genge la watumishi wasio waadilifu ndani ya DAWASA ambao kazi yao ni kudhurumu fidia za waathirika wa miradi ya maji.Mimi binafsi Mama yangu mjane amedhurumiwa fidia ya mumewe.

Mwaka 2011 DAWASA walikuja kwenye mji wa marehemu Enock Polepole Mwakambinda uliopo SALASALA "A" kanda ya IPTL kata ya wazo zamani kunduchi wakitaka eneo kwa ajili ya kulaza bombsma jipya la Ruvu chini,walichukuwa mita tatu wakamlipa milioni kumi na moja laki tano wakati fidia halisi ilikuwa milioni 25 na hivyo kumuibia milioni kumi na tatu;walimuibia benki maana kiutaratibu wanatakiwa wapewe cheki ila walilipiwa dirishani benki ya NMB;sasa mpaka hapo utajiuliza kwanini uwalipe watu fedha bila kufuata utaratibu wa serikali!

Tathimini Hui ya kwanza ilifanywa na kampuni inaitwa SMEC Engineering.

Tathimini ya pili ilifanyika mwaka 2014 ambapo walikuja kuongeza eneo tena,awamu hii walivunja fremu mbili za duka la marehemu ambapo alikuwa anauza saruji na vifaa vya ujenzi mbalimbali.Walichukua details zote za Mali ya mzee,wakampiga picha mbele ya Mali yake na kumsainisha fomu namba 1 na wakatokomea na fomu namba 69 ambayo ni kuonesha madai kwa baadaye kama kuna lolote litatokea.Waliofanya tathimini hii ya pili ni iliongozwa na Senior Municipal Property Valuer wa kinondoni na timu yake akiwemo Mama Komba kitoka kitengo cha uthamini wizara ya ardhi.Serikali ya mtaa iliwakilishwa na mwenyekiti aitwaye Monika Timba.Baada ya tathimini wakatangaza kuwa malipo awamu ya pili yatafanyika Aprili na baadaye kuhairisha mpaka oktoba 2014.Bahati mbaya mzee ENOCK Polepole akawa amefariki April 2014 hivyo kama familia ikashindikana kuchukua malipo yake mpaka tufungue mirathi.Sasa tumeisha fungua mirathi na barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa lakini DAWASA hawataki kulipa fedha zetu kwa madai kuwa eti eneo la mzee lipo kwenye hifadhi ya bomba lao,maajabu ya Marne!!

Sasa baada ya kuona huyu mama mjane anazungushwa fidia ya mumewe,nakamuandikia barua katibu MKUU wizara ya maji Prof.Kitila tarehe 11/08/2017 ilichelewa kujibiwa nikafuatilia nikaambiwa imekwenda DAWASA kwa ajili ya kutolewa maelezo,mpaka Leo sijapewa majibu.Baada ya kuona kimya wizarani nikamwandikia Rais Magufuli tarehe 30/10/2017 ikiwa pamoja na ripoti ya mradi iliyoandaliwa na DAWASA kwenda benki ya Dunia,ukiingia tovuti ya benki ya Dunia itaiona ni namba RP464 V3.Barua ilipokekelewa na ofisi ya katibu MKUU kiongozi,wakanijibu kuwa wamepeleka wizarani kupata maelezo,mpaka leo sijapewa majibu.

Likaja zoezi la RC MAKONDA kwa watu waliodhurumiwa ardhi na Mali zao,nikampeleka huyu mama mjane lakini katika kufuatilia nikagundua faili lilifichwa.RC MAKONDA akatangaza tena wenye kero za maji wake ofisini kwake,nikaangaika kuonana naye nikashindwa,sikukata tamaa nikamwandikia barua RC MAKONDA tarehe 21/03/2018,nikaifuatilia majibu nikaambiwa barua yako inashughulikiwa na mwanasheria msomi MERCY KYAMBA,nikamfuata huyu mwanasheria wa RC akaniambia suala lako litashughulikiwa mwezi May 2018 yeye yupo busy kumbe ni muongo Katibu tawala alishatoa maelekezo na barua alikuwa ameokalia huyu mwanasheria msomi!barua ya RC MAKONDA kutaka maelezo ya DAWASA ilitolewa 04/04/2018 yeye kanipa mwezi May 2018.Aliificha kwanini Mimi sijui!!.

Baada ya kuchukua baraua hii ya RC MAKONDA niliipeleka DAWASA kwa Mkurugenzi Mkuu ikiwa na kumbukumbu namba FA.49/407/01S/64.Baada ya kufuatilia sana pale DAWASA ikajibiwa bila Mimi kupewa nakala kama nilivyopewa nakala na ofisi ya RC MAKONDA,barua ya majibu ya DAWASA ikamfikia mwanasheria msomi MERCY KYAMBA akahukumu kwamba eti familia ya marehenu ENOCK POLEPOLE MWAKAMBINDA haina haki kulipwa kwasababu yupo kwenye hifadhi ya bomba wakati majirani zake wamelipwa!Hii ndiyo DAWASA inayokwamisha haki za watu.

Mheshimiwa waziri Prof.Mbarawa kama unataka kuepukana na migogoro ya wananchi na miradi ya maji jijini Dar es salaam na Pwani ndani ya DAWASA, anza na hawa;
DAWASA
1.Bwana Chibelenje
2.Bwana Simon
3.Bwana Kakwezi
4.Bibi Rose
5.Bwana Kilecha
6.Bwana Abel
Hawa wote ni timu ya Bwana Romanus Mwang'ingo katika ufisadi wa fidia za miradi na hawa pia ndiyo ambao wanazuia mjane wa marehemu ENOCK POLEPOLE asipewe fidia ya mumewe.Hawa watu wana mtandao mpana mpaka wizarani kwako Mheshimiwa Prof.Mbarawa na nakuomba umsaidie huyu mama mjane apate stahiki zake.
Kwa maelezo zaidi:0784151762
Barua pepe:emmano841@gmail.com


Isaya10:1-34

10 Ole wao wanaotunga masharti yenye kudhuru+ na wale ambao, wakiandika sikuzote, wameandika taabu tupu, 2 ili kuwasukuma mbali watu wa hali ya chini kutoka kwenye kesi na kuwanyang’anya haki wale wanaoteseka kati ya watu wangu,+ ili wajane wawe nyara yao, na ili hata wapore wavulana wasio na baba!+3 Nanyi mtafanya nini katika ile siku ya kukaziwa uangalifu+ na wakati wa uharibifu, utakapokuja kutoka mbali?+ Je, mtamkimbilia nani kupata msaada,+ nanyi mtauacha wapi utukufu wenu,+4 isipokuwa iwe kwamba mtu atainama chini ya wafungwa na kwamba watu wataendelea kuanguka chini ya wale ambao wameuawa?+ Kwa sababu ya hayo yote hasira yake haijarudi nyuma, bali mkono wake bado umenyooshwa.+
 
Dr Masasi nilikueleza na sasa ni zamu ya Luhemeja.
MTENDAJI MKUU Ndugu Luhemeja deal with this gang immediately, hili ni genge hatari kwa mustakabari wa DAWASA.
 
Back
Top Bottom