Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Kahawa Adolph Kumburu ndiye tatizo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Kahawa Adolph Kumburu ndiye tatizo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by matengo, Oct 25, 2012.

 1. m

  matengo Member

  #1
  Oct 25, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna taarifa ya kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya kahawa kwa mara nyingine tena inavunjwa.
  Serikali itavunja kila Bodi itayounda kama haitashughurikia kiini cha tatizo ambacho ni Mkurugenzi Mkuu wa Bodi. Tume zote zilizoundwa zilimkuta Kumburu ndiye mwenye makosa. Ila kila wakijiandaa kuchukua hatua wale wanaotaka kuchukua hatua ndio wanao ondolewa badala ya kumchukulia hatua mhusika Kumburu.

  Hapa inaonekana kuna mchezo mchafu unachezwa na Kumburu. Kama si mchezo mchafu ebu tujiulize:
  1. Kumburu alijuaje mpango wa serikali wa kuvunjwa Bodi akaamua kukataa kuandaa kikao cha Bodi kilichotakiwa kufanyika tarehe 25/10/2012.
  2. Kumburu alipata wapi kiburi cha kukataa kutekeleza maazimio ya Bodi kabla hata ya Bodi yenyewe kuvunjwa
  3. Kumburu kwa nini sasa ameanza kukusanya vielelzo ili pindi tu itakapowekwa Bodi nyingine aweze kuvitumia kama visingizio vya kufukuza wafanyakazi.

  Lazima kama alivyokuwa amemweka mfukoni Mwenyekiti wa Bodi uiliyopita Mzee Ngeze atakuwa amempata mkubwa /wakubwa wengine waliojuu yake nao amewaweka mfukoni ambao ame/wame-mwakikishia kumlinda na ndio wanaompa siri za mpango mzima wa yatakayotokea na kumpa kiburi.

  Sasa hata mimi naanza kuamini matatizo ya Bodi sasa yanahitaji kuingiliwa na Ikulu ndipo yataweza kuisha. Na kuisha kwenyewe ni kumuweka Kumburu pembeni. Kama wanamlinda basi wamwombe ajiuzulu kunusuru shirika la umma.
   
 2. H

  HakiMoja Member

  #2
  Oct 25, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haya mambo yamezungumzwa na wafanyakazi wa bodi ya kahawa kwa zaidi ya miaka mitatu sasa na kusababisha kuvunjwa kwa bodi ya Ngeze na Mh Waziri Maghembe kuhamishiwa wizara ya maji. Inashangaza kuona kwamba Waziri Chiza anamkumbatia Kumburu ambaye kila wakati yeye anasababisha migongano baina ya wafanyakazi na menejimenti na sasa baina ya wafanyakazi wa bodi ya kahawa wenyewe. Ameunda makundi ambao hawafanyi kazi na badala yake wanasengenyana na kugombana bila sababu.

  Je kama Kumburu anaweza kuihujumu bodi na kukataa kutekeleza maagizo anayopewa, je wafanyakazi si ndiyo wananyongwa kabisa na kufa kifo cha ngamia? Mh Waziri Chiza, tatizo hapa ni Kumburu na hata kama ukivunja bodi iliyopo na kuteua ingine Kumburu akiwepo utakuwa umefanya kazi bure kwani matatizo bodi ya kahawa yataendelea na pengine hata wewe atakugeuka. Jaribu kupitia taarifa za kamati zilizoundwa. Katibu mkuu wa wizara ya Kilimo Bw Mohamed Muya anafahamu vizuri matatizo ya bodi ya kahawa kwa sababu yeye mwenyewe alishawahi kuja kufuatilia matatizo ya wafanyakazi na ufujaji wa fedha za umma na ingefaa amshirikishe amwambie ukweli juu ya bodi hii ikiwa inaongozwa na Kumburu.

  The fasfer you go, the shorter you are
  Albert Einstein
   
 3. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  This is very sad.
  Kama tume nyingi zimefanya kazi na matokeao ni hayo hayo, kuna mambo mengi ya kujiuliza.
  Bwana Kumburu ni mteule wa Rais, na sina hakika kama haya anayajua.
  All in all, kuna mengi yanayosemwa, mojawapo ni Increasing American influence in Tanzania.
  Probably, Mr Kumburu is one of the products
   
 4. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mimi napita naona kama mambo yenu ya ndani ya ofisi zaidi manake nimeona giza tu hapo.
   
 5. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  utashangaa mhe.zambi anaingia kuwa mjumbe wa bodi ya kahawa maana alipambana vilivyo bungeni kuhusu wajumbe wengi wa bodi ya sasa kwamba wanatoka eneo moja la mkoa wa Kilimanjaro,hilo ni kweli kwani maghembe alivyounda bodi hiyo hakuwa anafahamu?,na kama alifahamu alikuwa analipa fadhila kwa nani kati ya hao?,hii pangua pangua ya bodi ya kahawa haina tija kwa wakulima wa zao la kahawa nchini ambao wengi wao wanaendelea kunyonywa na makampuni binafsi ya kununmua kahawa ambayo baadhi yamefikia hata kununua kahawa ikiwa shambani tena ikiwa mbichi na kina chizza na maghembe na hata rais wapo wanaangalia tu.
   
 6. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  04/02/2012 MHESHIMIWA KATIBU MKUU (CHIEF SECRETARY) IKULU – DAR ES SALAAM S.L.P 9120 DAR ES SALAAM.
  YAH: AGENDA YA SIRI YA KUUA ZAO LA KAHAWA NA MAENDELEO YA WAKULIMA MKOA WA MBEYA NA UCHUMI WA TAIFA.
  Somo tajwa hapo juu la husika sana. Mh. Rais. Sisi ni wakulima maelfu kutika Wilaya ya Mbozi, Mbeya vijijini, Rungwe na Ileje Mkoni Mbeya, tumekuandikia barua hii ili kukuonyesha kero zinazotengenezwa na watendaji serikalini ili kugandamiza wakulima, kuua zao la kahawa na kwa kutumia madaraka yao vibaya hali inayochochea migogoro vijijini. Mhe Rais mwaka 2011 ilifanyika agenda na mbinu chafu mno kati ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya wakati huo kwa kushirikishiana na Wakuu wa Wilaya za Mbeya, Mbozi, Rungwe na Ileje wakiwemo wakurugenzi watendaji wa Mbozi, Mbeya na Rungwe zilizolenga kumuondoa mwekezaji LIMA kwenye ununuzi wa kahawa mbivu (red cherry). Kutokana na LIMA kufanya vizuri sana katika kuboresha zao la kahawa na maisha ya mkulima kuliko vikundi na kampuni yote. Mhe Rais kampuni ya uwekezaji LIMA ambayo hapa Tanzania inaendeshwa na watanzania wenyewe wenye taaluma ya kahawa tangu 2004 imeleta mabadiliko makubwa kwetu wakulima kwa kujenga viwanda vya kumenya kahawa mbivu mabwawa ya maji na ugavi na madawati mashuleni na uchangiaji wa huduma za afya kwenye hospitali. Kampuni LIMA ndiyo inayoongoza kwa kutoa ajira kwa wananchi na vijana wengi Mkoani Mbeya pamoja na huduma ya ugani kwa mkulima wa kahawa na mashamba darasa. LIMA ndiyo kampuni pekee ambayo imefanikiwa kuboresha kahawa yetu kimataifa na kwa sasa tumepata masoko Marekani na Japan siyo hivyo tu LIMA imehamasisha vijana kupenda kilimo hususani kahawa kwa asilimia 80 na kuondoa uhalifu hasa hasa Wilayani Mbozi ambako jeshi la polisi Mkoani Mbeya lina kata ya mfano wa usalama, kata ya Isansa ambayo ilikuwa inaongoza kwa uhalifu Mkoani Mbeya, lakini leo vijana wapo kwenye kilimo cha kahawa kwa msaada wa LIMA. Sisi wakulima tumeona faida kubwa kwenye mauzo ya kahawa mbivu au cherry kwani inatuondolea usumbufu kwenye maandalizi kutokana na uhaba wa maji na vitendea kazi vingine ili kufikia ubora, ukiuzwa kahawa mbivu kwa LIMA unalipwa na mabaki kila mara bei zinapopanda kwenye soko. Kama uliza kilo moja kwa Tshs 2000 na bei zikapanda mara mbili kwenye soko mkulima analipwa Tshs 5000 kwa kilo ya kahawa mbivu. (kupita hata bei elekeziza serikali). Mhe, mbinu hiyo chafu ilitokana na mwekezaji LIMA kufanya kazi vizuri ya kumfufua mkulima wa zao la kahawa ambaye nyuma yake tulikuwa wafu. Kutokana na kudolola kwa bei za kahawa, ujio wa mwekezaji LIMA ambaye alipoingia Mkoani Mbeya mwaka 2004 amekuwa mkombozi kwetu wakulima wadogowadogo na wakati ni asilimia 100 ya wakulima wote Mkoani Mbeya, kwa kuongeza ubora wa kahawa, bei na kutupatia mbolea bila riba. Hivyo kitendo cha kumpiga vita LIMA ni kuwapiga vita maelfu wakulima wadogo na wakati ambao tunakombolewa na mwekezaji LIMA kwani tumegundua kuwa umaskini tuliokuwa nao wa kukosa mbolea na bei duni za kahawa, ulikuwa mtaji kwa mafisadi wakiwemo wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi watendaji tuliowataja kwenye Wilaya hizi kwani wao wanauza pembe jeo kwa bei ya juu mno ambapo mbolea aina ya DAP wanatuuzia kwa Tshs 240,000/= walanguzi hao pamoja walioko na watendaji wako wanauza pia mbolea aina ya UREA kwa Tshs 180,000/= CAN 120,000/= wakati mwekezaji LIMA mbolea hizo hizo atuuzia kwa Tshs 75, 000/= , UREA 65,000/= na CAN 50,000/= unaweza kuona tofauti hii. Mhe Rais hii ni orodha chache tu ya viongozi wanaojishughulisha na ununuzi wa kahawa kwa kutengeneza vikundi hewa, vya kitapeli na vikundi vya kifamilia ili kutengeneza migogoro kwa lengo la kuendelea kufaidi jasho letu huku wakisimama majukwaani na hawakubali bei za kionyonyaji kwa mkulima wa kahawa kumbe wao ndiyo wanyonyaji na mafisadi na wanafiki wabaya. Na ndio maana mpango wa vocha za mbole umeshindwa kumsaidia mkulima, kutokana na vocha hizo kuishia mikononi mwa majambazi hawa, yaani Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Madiwani na Wafanyabiashara majambazi. Tumekutumia barua za siri za utekelezaji wa maagizo ya kumjumu LIMA kutoka kwa Wakurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya kulingana na agizo la siri lilllosambazwa na mafisadi hao kwa kupitia Mkuu wa Mkoa wakati huo na jambo ambalo ni kinyume kabisa na sheri Na. 23/1001 ya kahawa. Mkuuu wa Wilaya Mhe. Gabriel Kimalo anajihusisha na kufanya biashara chini ya mwamvuli wa kikundi cha Peoples Coffee Group na Mpito Coffee Group. Vikundi hivi hujihusisha na ununuzi wa kahawa mbivu ambayo Mhe. Gabriel anaikataza kampuni ya LIMA isinunue licha ya kampuni hiyo kuwekeza kwenye ujenzi wa mitambo ya kumenyea kahawa mbivu 23 ya thamani ya mabilioni ya fedha kwenye Wilaya zote za kahawa. Aidha Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya Mbozi Ndigu Aloyce Mdalavuma ni mnunuzi wa kahawa mbivu na anamiliki kikundi cha Guzyo Farmers Group. Yeye ni Mwenyekiti wa kikundi hicho na hadi leo hajawalipa wakulima. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya anaitwa Eric Ambakisye Minga. Yeye ni mwanahisa kwenye kikundi kinachoitwa Peoples Coffee Group. Kikundi hiki kinanunua na kusindika kahawa mbivu. Afisa Ntumishi wa Wilaya Ndugu Ngaikwela ana mahasiano ya kibiashara na Ndug Adam Kalonge mmiliki wa Mpito Coffee Group ambaye ni mnunuzi wa kahawa mbivu. Ndugu Burton Sinienga Diwani ya kata ya Ipunga ni mmiliki wa kikundi kinachoitwa Ifungo Coffee Group,. Kikundi chake bado kinadaiwa na wakulima. Ndugu Sende Shula Diwani ya kata ya Myovizi ni mmikliki wa kikundi cha Ichesa Coffee Group., na katibu wa kikundi hicho. Mpaka hivi tunavyozungumza anadaiwa na wakulima. Mbunge Godfrey Zambi anafanya biashara kwa ushilikiano wa siri na Musa Zambi na Burton Sinienga Diwani wa kata ya Ipunga kupitia kikundi kiitwacho Ifungo Coffee Group. Mhe. Rais zichukuliwe hatua za haraka kuzuia agenda hiyo chafu ambayo imepangwa na mafisadi kupitia watendaji wa Halmashauri ili kuhujumu wanunuzi wanaojali maslai ya wakulima kama LIMA kwa lengo la kupata nafasi kuhodhi soko na wakulima tusiwe na uchaguzi wa mahali bora pa kuuza kahawa yetu. Iundwe tume kuchunguza mwenendo wa viongozi wa Mkoa na hasa Wakuu wa Wilaya wa Mbeya, Mbozi na Rungwe ambapo kwa mfano Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe amepora kilo 483 za kahawa mbivu na kilo 1090 za kahawa kavu kutoka kwa wanunuzi wa kampuni ya LIMA vijijini na kwenda kuiuza kusikojulikana je? Haya ni maadili ya utumishi wa um,ma? Mhe. Rais tunaomba usifumbie macho siri iliyojificha kwenye mkanganyiko uliojitokeza wakati wa ziara ya Waziri wa kilimo na chakula Mhe. Jumanne Magembe ambapo watendaji hao bila aibu waliamua kumtukana na kumdhalilisha Waziri na kumnyima kabisa fursa ya kuongea na wakulima ambao ndio tulikuwa tunamsubili kwa hamu sana. Mhe. Rais mfumo wa bodi ya kahawa TCB ubadilishwe ili bodi iwe na jukumu la kutafuta masoko, kusimamia, ubora na bei badala ya sasa ambapo bodi inafanya biashara kwani viongozi wakuu wa bodi (TCB) wako nyuma ya mbinu hii chafu. Mwenyekiti mhe. Pius Genze na Mkurugenzi (Adolph Kumbulu) wa bodi ya kahawa walifanya vikao katika kila Wilaya wakishauri Makampuni wanyimwe vibali vya kufanya biashara ya kahawa mbivu (cherry). Tunaamini japo ili lina siri nzito nyuma yake kwani Mkurugenzi (Adolph Kumbulu) pamoja na Mwenyekiti (Mhe. Ngeze ) wa bodi ya kahawa kwa pamoja wana maslahi kwa biashara iendeshwayo na Kilcafe chini ya ushauri wa kitaalamu unaotolewa na Technoserve. Ili kulinda maslahi ya Kilcafe Mkurugenzi ameamua kwa makusudi kushawishi Halmashauri zipige marufuku biashara ya kahawa mbivu. Msukumo huu ulitokana na Kilcafe kushindwa kabisa kuhimili ushindani wa ununuzi wa kahawa mbivu, hivyo namna pekee ya kuinusuru ambayo ilibuniwa na Mkurugenzi wa bodi ya kahawa ni kusitisha utoaji wa leseni ya ununuzi wa kahawa mbivu. Usitishaji huu ulianza mara tu Adolph Kumbulu alipoteuliwa kuwa Mkurugenzi wa bodi ya kahawa 2008/2009. Mhe. Rais migogoro hii ni chanzo chake kikubwa ni Mkurugenzi wa bodi ya kahawa (TCB) ambaye ameigeuza bodi hiyo kama zizi lake la mbuzi anachinja apendavyo, ndiye anayetumika na mafisadi maneno yake ni tofauti na matendo yake chonde chonde sisi wakulima tunaiona TBC mzogo mkubwa kwetu. Mhe. Rais tunaungana na Waziri wa kilimo Ushirika na chakula kusisitiza ushindani wenye lengo la kuboresha kahawa na bei, ndio uwe msisitizo na si vinginevyo vita hii ya kimaslai tunaiona kwamba itatudhuru wakulima kwani uuzaji wa kahawa mbivu umetuondoa kwenye umaskini kwa sasa tunalipa karo za watoto wetu kwa wakati, kununua pembe jeo kwa wakati na pia imetoa ajira kwa vijana wetu na kupunguza matukio ya kihalifu. Mhe. Rais MUHIMU LESENI na vibali vya ununuzi wa zao la kahawa vitoke wizarani na sio kwenye Halmashauri wala bodi ya kahawa. Bodi na Halmashauri wabaki na jukumu la kusimamia sheria zao la kahawa Na. 23 ya 2001 tu ili kuondoa ukiritiba na mianya ya rushwa kwa Wakurugenzi na Watendaji wa Halmashauri. Mbinu za kuzuia ununuzi wa kahawa mbivu (red cherry) zina lengo la kuua ubora wa kahawa na kurudisha umaskini kwa wakulima kwani ni asilimia 20 tu ya kahawa mbivu zonazopita kwenye viwanda vya kumenyea kahawa hiyo katika Mikoa ya nyanda za juu wakati wenzetu wa Kigoma zaidi ya asilimia 70 ya kahawa mbivu zinapita kwenye viwanda (CPU). Mhe. Rais sisi wakulima wa zao la kahawa hususani Wilaya ya Mbozi, Mbeya, Ireje na Rungwe tunayo imani na wewe na serikali yako kwamba kilio chetu kitafanyiwa kazi, ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha mara moja Wakuu wa Wilaya za Mbozi, Rungwe na Mbeye na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi ambaye dhahili hana maadili ya uongozi kwani kitendo cha kumtukana Waziri wa kilimo na Rais aliye mteua hadharani kimewaacha wananchi na taswira tofauti tangu tarehe 16/01/2012. Mhe. Rais baada ya kukupatia picha sahihi, ya kero, hujuma na matumizi mabaya madaraka ya baadhi ya watendaji Mkoani hapa tunavyotendewa, CHONDE CHONDE Mhe. Rais na Mhe. Waziri wa Wizara ya kilimo na Ushirika na chakula tunaomba serikali itoe haraka Leseni na Kibali kwa mwekezaji LIMA ili ianze kutugawia mbolea kwani mpaka sasa anasubili Leseni na vibali na sisi wakulima tungali tumepanga foleni kwake kusubili mbolea. Ili tuanze kumwaga mashambani kwani mwaka huu kahawa zimeanza vizuri na kama hatutapata mbolea mapema punje zitaharibika. Na mwisho wakulima tumeapa kamwe hatupo tayari kuruhusu kampuni nyingine za mafisadi kuchukua kahawa zetu zaidi ya LIMA mkombozi wa mkulima wa kahawa nyanda za juu kusini ambaye tumeamua kuingia mikataba ya kumuuzia kahawa mbivu (red cherry). Kikao cha muungano kw Wakulima wa kahawa 1240 kilichofanyika tarehe 04/02/2012 mji mdogo wa Mlowo. Chini ya Mwenyekiti Japhet Kibona…………………………………………………………… Dickison Nzowa ……………………………………… Joel Mwakangale ………………………………….. na Abeli Mwashamba……………………………………………………….. Tunawakilisha kwako Mheshimiwa Rais. Kutika kata za:- 1. Bugoba – Tukuyu 2. Luswiswi – Ileje 3. Iluya – Mbozi 4. Kagwina – Tukuyu 5. Ikuti – Tukuyu 6. Kijiji cha bara – Mbozi 7. Kijiji cha Mlangali – Mbozi 8. Igamba – Mbozi 9. Kijiji acha Msia – Ireje 10. Kijiji cha Luwati – Mbozi 11. Kijiji cha Magamba – Mbozi 12. Kijiji cha Ruanda – Mbozi 13. Kijiji cha Uhowa – Mbozi 14. Kata ya Isansa 15. Kata ya Ihanda 16. Kata ya Igamba 17. Kata ya Ipunga 18. Kata ya Nyimbili 19. Kata ya Iyula 20. Kata ya Halungu 21. Kata ya Itaka 22. Kata ya Msiya 23. Kata ya Itengule – Mbeya vijijini 24. Kata ya Mlangali 25. Kata ya Myovizi 26. Kata ya Ruanda 27. Kata ya Nambinzo NAKALA:- MHE: WAZIRI MKUU, MIZENGI PINDA – (MB), S.L.P 1923 DAR ES SALAAM/DODOMA. WAZIRI KILIMO NA USHIRIKA MHE. PROF J. MAGHEMBE, S.L.P 9192, DAR ES SALAAM. [FONT=&quot]Re: Mbunge Zambi ashitakiwa mahakamani [/FONT]
  Kwanijuavyo mimi kuhusu hii biashara ya kahawa kwa kweli ni kamari na wengi wetuhapa hatujui kinachoendelea kwenye biashara hii. Biashara hii ni biasharaambayo haitakiwi kabisa kuingizwa Siasa ndani yake klakini wengi wetu hatujui,badalayake inageuzwa ni Siasa.[FONT=&quot]
  [/FONT]Biashara ya kahawa inaongozwa na soko kuu la kahawa duniani (stock exchange)lilipo New York kwa kahawa laini yaani Mild Arabica na London kwakahawa ngumu yaani Robusta. Kahawakwa ujumla naweza kusema ni kama kamari bei ya leo sio bei ya kesho aukeshokutwa au hata jana na juzi.
  Swali la msingi hapa ni tujiulize jetunamsaidiaje mkulima wa kahawa ambaye hana uwezo mkubwa ? Jetunamsaidiaje mkulima wa kahawa kwenye kuendeleza zao la kahawa na kuongeza kgalizo nazo na kipato chake kwa sasa ?Ununuziwa madawa na mbolea ? Jetunamsaidiaje mkulima pale anapotaka kumpeleka mtoto shule wakati anasubirikahawa yake ikauke ndipo aiuze ? je hizo shule zinasubiria ?Jetunamsaidiaje ili aweze kujikimu na maisha mpaka hapo atakapo kausha kahawa yake? au hatakuwa na njaa kwa wakati huo?Tufikiriekwa mapana na marefu bila kukurupuka na kuanza kutupiana maneno bila kutumiaakili kwa manufaa ya wachache wanaofikiria kwa ufupi.Mtakuwawatu wa maana kama atatokea mtu mmoja au mwana siasa ambaye ataonyesha kumteteamkulima katika misingi sahihi badala ya huu utaratibu unaotumiwa wa sasa ilituweze kuongeza zao la kahawa nchini kutoka tani 50,000 mpaka kufikia ton 100,000ifikapo 2015Wotekwa sasa tunafahamu kuwa ulaji wa kahawa soko la ndani lenyewe ni 3% tu wakatiwenzetu kama Ethiopia na wengine soko la ndani peke yake ni 40%Nitawaelewawanasiasa na wadau wengine wa kahawa kama watakuwa wa kwanza kumsaidia mkulimakuongeza uzalishaji badala ya staili iliyoko sasa hivi ya kujitokeza nakumpangia mkulima sheria nyingi baada ya mkulima kuvuna kahawa yake nakumlazimisha kuuza tunavyotaka sisi badala ya yeye mkulima kujipangia aonavyomwenyewe.Mwakawa 2000 kahawa ilishuka sana bei na hata mkulima kuuza kahawa yake kwa bei yash 400/kg mbona wakati huo hakuna aliyejitokeza hata mmoja kumsaidia mkulima kamakweli mlifanyalo ni sawa? Nchi zilizoendelea waliweza kumfidia mkulima kutokana hasara ili wasikate tamaa je sisi tunaweza kufanya hivyo Iwapo sokolikaporomoka sasa hivi ? Nijuavyomimi hakuna mahali popote duniani penye wanywaji wa kahawa ambao hawatakikahawa nzuri na yenye ubora wa juu ukasikia imekosa soko.Kama nikumbukavyo kipindihicho zilijitokeza kampuni ambazo ziliamua kumsaidia mkulima kwa kujenga vinuvya kumenya na kusafisha kahawa ziitwazo Soochack na Tropex ambazo zilifungavinu vya kusafisha kahawa mbichi kusini mwa Tanzania, Mbinga na mkulimaaliponea hapo baada ya kupatikana kahawa safi na wakati huo kahawa ya kusiniilikuwa ikijulikana kwa jina la AMEX TYPE yaani kahawa iliyo chini ya ubora.Hatabaadae ndipo ilipoingia kampuni ya Lima Kusini Mbeya na kufanya hivyohivyohakuna mkulima aliye lalamika kuwa anapunjwa kutokana na kuuza kahawa mbichi.Nahii ilisaidia kahawa ya kusini kuuzwa bei sawa na kahawa ya kasikazini na hatabaadae kuipita ya kasikazini.Neno AB au AA au Amex likafa na kahawa zote zikawazinauzwa kama FAQ south au FAQ North.Nakumbuka Nchi ya kwanza kuanza kununuakahawa ya kusini ilikuwa Japani ambayo ndio walikuwa wakiongoza kwa kununuakahawa ya Kasikazini wakati huo.Hivyobasi kwa kuanzia, Mgogoro huu wa cherry ulianzia mwaka 2008 wakati uongozi wa juuwa Bodi ya kahawa ulipobadilika na kuingia uongozi mpya.Katika kikaoalichokiongoza Mkurugenzi mkuu wa bodi ya kahawa Bw A.Kumburu huko Mbeya, Mbozina Mbinga mwezi December 2008 kwakutangaza kupiga marufuku ununuzi wa cherry lakini bila kueleza atamsaidiajemkulima anaetegemea kahawa hiyo ili apeleke watoto wake shule kwa wakatimuafaka na pia kujikimu na maisha,pia bila kujali wenye viwanda hivyowatalipaje madeni yao benki kwa fedha walizokopa.Hakuna asiye fahamu kuwa maandaliziya kahawa kutoka kuvuna mpaka kuuza inachukua muda gani takribani sio chini yamiezi 3- 4 ,sasa jiulize kwa mkulimamasikini anafanyaje wakati huo wote? Je anakula nini wakati anaangalia jua kamalitatoka ili aanike kahawa yake ikauke aweze kuiuza?.Tufikewakati sasa tuwe na mawazo tofauti tusiwe watu wa kutumiwa na wazungu tu maranyingine wanatumaliza bila sisi kujua. Suala la kupinga ununuzi wa cherywilayani Mbozi ni janja ya kuitumia wilaya hiyo pamoja na Mb wao Mh Zambi pamojana uongozi wa juu wa wilaya na mkoa hii ni kianzio tu cha upotoshwaji iliikifanikiwa sumu hiyo isambae mikoa mingine yote inayolima kahawa. Hii nikatika harakati za kuwasaidia wazungu ambao hawataki kuwekeza kwenye mashinehizo ili waweze kupata kahawa aliyoitayarisha mkulima mwenyewe kwa jasho kubwana kuinunua kwa bei ambayo itakakuwepo wakati huo.Tusidanganyane hapa kwamba kunamfanya biashara anaefanya biashara hii bila kufuata soko la dunia lilivyo labdaukute wale wachache ambao waliuza kahawa hewa hivyo atanunua hata kwa hasaraili amridhishe mnunuzi wake na hapa akikuta bei zimedondoka basi na aliuza beiya juu basi na inabidi apate hasara, mfano rahisi ni mwaka jana wakati soko ladunia likiwa juu yaani NY $250lb huku Tanzaniamkulima aliuza kahawa yake kwa bei ya sh 5000, leo soko la dunia liko$151lb na kg ya kahawa kwa sasa ni sh2500-3000 hapa mnunuzi hajajumlisha overheads zake tutumie akili na upotoshwajiuondoke.Kwanzanapenda kusema kuwa kuuza kahawa ikiwa cherry inampunguzia mkulima kuondokanana Gharama za kuimenya,kuivundika,kuiosha na kama hana maji safi basi ndiohivyo tena mkulima wa ulimwengu wa tatu na mwisho kuianika hii yote ni gharamakwa mkulima. Mfanoili upate kg 1 ya parchment unatakiwa upate kg 5 za cherryuzimenye,uvundike,uoshe, uanike n.k ndio upate kg 1 ya parchment na kwa sasa bei yakahawa aliyoikausha mkulima mwenyewe ni Sh 2500 – 3000.Sasa hapa anaeuza cherryKg 1 ni sh 600 huyu gharama yake ni kuitoa shambani tu hanagharama nyingine zaidi je hapa nani anaefaidi zaidi? Hilo ni swali dogo sana walahuitaji kufikiria kwa mtu mwenye akili timamu kama sio kichaa ambae anafikirimaisha anayoishi ya kupewa mshahara ni sawa na ya mkulima masikini kulekijijini ambae hajui hata chai na sambusa ya saa nne ni kitu gani yeye anaishikwa mlo mmoja tu tena kwa tabu sana kuupata.HivyoMkurugenzi mkuu wa bodi Bw A.Kumburu ni bora uachane kabisa na tabia hiyo, wotetunaelewa fika mission/mipango yako uliyoingia nayo bodi ya kuwalinda wazunguna kupiga vita wazawa ambao wanajitolea kumlinda mkulima mdogo.Swalidogo sana kama Bw Kumburu utaweza kujibu itafurahisha sana.UlipokuwaTechnoserve/Sustainable Harvest ambazo zilikuja kwa mgongo wa kumsaidia mkulima kama ushirika ili wasilipe kodije mlikuwa mnamsaidia kwa bei ya hapa yaani mlikuwa mna share faida na mkulimalocaly au ni pamoja na faida ya kahawamlizokuwa mnauza nje ya nchi yaani international.Basikama sio internationally hivyo tunakuomba uache tabia yako ya kupotoshawakulima na wananchi wa Tanzania kwa ujumla pamoja na wanasiasa unaowatumia kamaMh Zambi ambae hajui unachokifanya, wote tunajua unayoyafanya kama kwa sasaulivyofanikiwa kuhamisha funds zilizokuwa zikitoka kwa Bill Gates and BelindaFoundation kwenda kwa Technoserve na kwa kutumia cheo chako umeweza kudhaminifunds hizo kwenda ECOM ambayo ni kampuni ya wazungu na ndio kampuni mama yamakumpuni ya MAWENZI LTD NA TUTUNZE LTD ambao hawana nia ya kuwekeza mashine zacherry ila wanahitaji zaidi kahawa iliyo tayari yaani parchment iliyotayarishwana mkulima mvuja jasho.wao wabebe na kujiondokea muonee huruma huyu mkulima waTanzania. Nafikirihuu ni wakati mzuri sana wa kurekebisha haya yote kama alivyosema Mwenyekiti wabodi Dr Eve Sinare na bodi yake,ukiwa kama kiongozi unaeongoza kumpiga vitakupitia kwa wanasiasa kama Mh Zambi kwa kuwa ameingia na sera ya kumlindamkulima myonge na kwa kuwa huwezi kumsokota kutokana na kuwa hana njaa kama alizokuwa nazo Mwenyekitialiyepita ambaye uliweza kumsokota unavyotaka kiasi cha kukuona kama Mungu sasahayo yamekwisha,kawaombe wazungu radhi kuwa imeshindikana watakusamehe tu,hawa wakulimawatakuachia laana mbaya sana na utakuja kufa kifo cha mateso cha kuozeakitandani kabla ya kufa. Jaribu kangalia soko linavyoporomoka kwa kasi hukokwenye soko la dunia.TunamuombaWaziri wa kilimo chakula na ushirika aokoe hili jaazi kabla halijatumbukiakubaya akuondoe mapema ili mkulima asiumie zaidi.Mhwaziri tunashindwa kuelewa ni kwa nini Bw Kumburu anabishana na mwenyekiti wakekwa maamuzi aliyoyatoa ya kuwa MKULIMAAACHWE AAMUE MWENYEWE KUUZA ANAKOTAKA YAANI AKITAKA KUUZA KAHAWA MBICHI SAWAAKITAKA KUUZA ILIYOKAUKA PIA NI SAWA maamuzi aachiwe mkulima aliyelimakahawa yake mwenyewe kinachokuuma wewe naMh Zambi pamoja na uongozi wote wa Mbozi na Mkoa ni nini hasa ? Je kunaulichomsaidia mkulima huyo kama fedha au mbolea au madawa ? je wewe na Mh Zambimnapata hasara gani huko basi kama mnawajali sana wafungieni vinu vya kumenyeakahawa ndio tujue mna uchungu nao kama walivyofanya wenzenu msitumie vyeo namadaraka yenu mliyo nayo kujiingiza kwenye kumuumiza mkulima na kumfaidishamzungu,wao hawana wakulima wala ndugu zao huku Tanzania lijueni hilo kwa makiniacheni kuwa kama malimbukeni mnao taka kummaliza mkulima na kuvunja ajira zawale walioajiriwa kwenye viwanda hivyo. Mh Zambi jaribu kuangalia kwenye jimbolako ni vijana wangapi ambao watakosa kazi kwa wewe kusimamia zoezi zima lakufunga viwanda hivyo na 2015 utawarudia hao hao kuwaomba kura?PiaBw Adolph Kumburu tunakuomba ujue kikao mlichokaa pamoja na Mh Zambi pamoja nauongozi wa wilaya ya Mbozi ofisi kwako Moshi kwenye jengo la kahawa tarehe28/5/2012 na ukawa ndio mwandishi wa barua aliyomwandikia Waziri waKilimo,Chakula na Ushirika Eng Chiza kupitia kwa Mh Zambi barua ambayo piaameitoa kwenye gazeti la Mwanahalisi kuwa tunajua ni wewe Kumburu wewe ndio uliyekuwamwandishi mkuu wa barua hiyo.Tunaombakukuambia kuwa hufai kuwa kiongozi wa kumlinda mkulima na hii inathibitishaulivyoingia bodi ukapiga marufuku kuheshimu reserve za wakulima wavuja jashoili wazungu wajibebee kahawa kwa bei poa acha kabisa kumuua mkulima na hakunaheshima kubwa utakayoipata toka kwa wakulima kama ukiachia ngazi mwenyewe mapemazaidi ili upishe mtawala mwingine ambae hatakuwa kibaraka wa wazungu nchini.Nendakaendeleze kikundi chako na Padre aliyeko Ujerumani kule Mbinga kiitwachoSongea Net work Data zote tunazo. Mtu hatari sana wewe mwenye wivu mkali,mfitini, mchonganishi na muongo.Sasakesi kafunguliwa Zambi Moshi wewe ndio utakuwa unamlipia kuja kwenye kesi hiyoau ni wazungu wako wanaokutumia nae anaenda kichwa kichwa tu Kwamara nyingine tena Waziri tunakuomba chondechonde omba ruhusa kwa Mh Raisiumuondoe huyu Bwana kabla hajakuingiza mkenge wewe uwajibishwe kwa kosa ambaloungeweza kuliepuka mapema. Alipotosha bodi iliyopita na mwisho wake bodi yoteilifukuzwa na akabaki yeye. Hana urafiki na mtu mweusi huyu Bw Adolph waswahiliwanasema "ukicheza na mbwa atakufuata mpaka msikitini".Bodiiliyopo sasa hivi ni bodi imara na uteuzi wa Bw Eric ni wa halali akiwa kamamwakilishi wa wanunuzi binafsi wa kahawa PCB kama alivyokuwa Amir Hamza kwenyebodi iliyopita akiwakilisha exporters TCA,Uteuzi Bw James Teri ni wa halalikama alivyokuwa bw Kirenga akiwakilisha wizara, uteuzi wa Msuya ni wa halalikwani hata Ndossi alikuwa ni mtaalam wa misitu kwenye bodi iliyopita na sualala kusema bodi haina mwakilishi kutoka Mbeya sio sahihi kwani hata kwenye bodiiliyopita kulikuwa hakuna mwakilishi kutoka Mbinga na mwisho suala la kusemabodi imejazwa watu wa kasikazini sio sahihi kwani hata bodi iliyopita ilikuwana wawakilishi watatu kutoka Kagera na mmoja wao ni aliyekuwa Mwenyekiti-Bw Pius Ngeze. Mwenyekuchangia na achangie ila tuache kuwa wabishi tusiotumia akili Tanzania ni mojana tuelewe kuwa nchi yetu haina ukabila hata kidogo tuachane dhana potovutunayotaka kujengewa na wachache walionunuliwa na wazungu.Nawatakienikila la kheri na Mkulima mnyonge wa Tanzania,
  [FONT=&quot] [/FONT]
   
 7. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  04/02/2012 MHESHIMIWA KATIBU MKUU (CHIEF SECRETARY) IKULU – DAR ES SALAAM S.L.P 9120 DAR ES SALAAM.
  YAH: AGENDA YA SIRI YA KUUA ZAO LA KAHAWA NA MAENDELEO YA WAKULIMA MKOA WA MBEYA NA UCHUMI WA TAIFA.
  Somo tajwa hapo juu la husika sana. Mh. Rais. Sisi ni wakulima maelfu kutika Wilaya ya Mbozi, Mbeya vijijini, Rungwe na Ileje Mkoni Mbeya, tumekuandikia barua hii ili kukuonyesha kero zinazotengenezwa na watendaji serikalini ili kugandamiza wakulima, kuua zao la kahawa na kwa kutumia madaraka yao vibaya hali inayochochea migogoro vijijini. Mhe Rais mwaka 2011 ilifanyika agenda na mbinu chafu mno kati ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya wakati huo kwa kushirikishiana na Wakuu wa Wilaya za Mbeya, Mbozi, Rungwe na Ileje wakiwemo wakurugenzi watendaji wa Mbozi, Mbeya na Rungwe zilizolenga kumuondoa mwekezaji LIMA kwenye ununuzi wa kahawa mbivu (red cherry). Kutokana na LIMA kufanya vizuri sana katika kuboresha zao la kahawa na maisha ya mkulima kuliko vikundi na kampuni yote. Mhe Rais kampuni ya uwekezaji LIMA ambayo hapa Tanzania inaendeshwa na watanzania wenyewe wenye taaluma ya kahawa tangu 2004 imeleta mabadiliko makubwa kwetu wakulima kwa kujenga viwanda vya kumenya kahawa mbivu mabwawa ya maji na ugavi na madawati mashuleni na uchangiaji wa huduma za afya kwenye hospitali. Kampuni LIMA ndiyo inayoongoza kwa kutoa ajira kwa wananchi na vijana wengi Mkoani Mbeya pamoja na huduma ya ugani kwa mkulima wa kahawa na mashamba darasa. LIMA ndiyo kampuni pekee ambayo imefanikiwa kuboresha kahawa yetu kimataifa na kwa sasa tumepata masoko Marekani na Japan siyo hivyo tu LIMA imehamasisha vijana kupenda kilimo hususani kahawa kwa asilimia 80 na kuondoa uhalifu hasa hasa Wilayani Mbozi ambako jeshi la polisi Mkoani Mbeya lina kata ya mfano wa usalama, kata ya Isansa ambayo ilikuwa inaongoza kwa uhalifu Mkoani Mbeya, lakini leo vijana wapo kwenye kilimo cha kahawa kwa msaada wa LIMA. Sisi wakulima tumeona faida kubwa kwenye mauzo ya kahawa mbivu au cherry kwani inatuondolea usumbufu kwenye maandalizi kutokana na uhaba wa maji na vitendea kazi vingine ili kufikia ubora, ukiuzwa kahawa mbivu kwa LIMA unalipwa na mabaki kila mara bei zinapopanda kwenye soko. Kama uliza kilo moja kwa Tshs 2000 na bei zikapanda mara mbili kwenye soko mkulima analipwa Tshs 5000 kwa kilo ya kahawa mbivu. (kupita hata bei elekeziza serikali). Mhe, mbinu hiyo chafu ilitokana na mwekezaji LIMA kufanya kazi vizuri ya kumfufua mkulima wa zao la kahawa ambaye nyuma yake tulikuwa wafu. Kutokana na kudolola kwa bei za kahawa, ujio wa mwekezaji LIMA ambaye alipoingia Mkoani Mbeya mwaka 2004 amekuwa mkombozi kwetu wakulima wadogowadogo na wakati ni asilimia 100 ya wakulima wote Mkoani Mbeya, kwa kuongeza ubora wa kahawa, bei na kutupatia mbolea bila riba. Hivyo kitendo cha kumpiga vita LIMA ni kuwapiga vita maelfu wakulima wadogo na wakati ambao tunakombolewa na mwekezaji LIMA kwani tumegundua kuwa umaskini tuliokuwa nao wa kukosa mbolea na bei duni za kahawa, ulikuwa mtaji kwa mafisadi wakiwemo wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi watendaji tuliowataja kwenye Wilaya hizi kwani wao wanauza pembe jeo kwa bei ya juu mno ambapo mbolea aina ya DAP wanatuuzia kwa Tshs 240,000/= walanguzi hao pamoja walioko na watendaji wako wanauza pia mbolea aina ya UREA kwa Tshs 180,000/= CAN 120,000/= wakati mwekezaji LIMA mbolea hizo hizo atuuzia kwa Tshs 75, 000/= , UREA 65,000/= na CAN 50,000/= unaweza kuona tofauti hii. Mhe Rais hii ni orodha chache tu ya viongozi wanaojishughulisha na ununuzi wa kahawa kwa kutengeneza vikundi hewa, vya kitapeli na vikundi vya kifamilia ili kutengeneza migogoro kwa lengo la kuendelea kufaidi jasho letu huku wakisimama majukwaani na hawakubali bei za kionyonyaji kwa mkulima wa kahawa kumbe wao ndiyo wanyonyaji na mafisadi na wanafiki wabaya. Na ndio maana mpango wa vocha za mbole umeshindwa kumsaidia mkulima, kutokana na vocha hizo kuishia mikononi mwa majambazi hawa, yaani Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Madiwani na Wafanyabiashara majambazi. Tumekutumia barua za siri za utekelezaji wa maagizo ya kumjumu LIMA kutoka kwa Wakurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya kulingana na agizo la siri lilllosambazwa na mafisadi hao kwa kupitia Mkuu wa Mkoa wakati huo na jambo ambalo ni kinyume kabisa na sheri Na. 23/1001 ya kahawa. Mkuuu wa Wilaya Mhe. Gabriel Kimalo anajihusisha na kufanya biashara chini ya mwamvuli wa kikundi cha Peoples Coffee Group na Mpito Coffee Group. Vikundi hivi hujihusisha na ununuzi wa kahawa mbivu ambayo Mhe. Gabriel anaikataza kampuni ya LIMA isinunue licha ya kampuni hiyo kuwekeza kwenye ujenzi wa mitambo ya kumenyea kahawa mbivu 23 ya thamani ya mabilioni ya fedha kwenye Wilaya zote za kahawa. Aidha Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya Mbozi Ndigu Aloyce Mdalavuma ni mnunuzi wa kahawa mbivu na anamiliki kikundi cha Guzyo Farmers Group. Yeye ni Mwenyekiti wa kikundi hicho na hadi leo hajawalipa wakulima. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya anaitwa Eric Ambakisye Minga. Yeye ni mwanahisa kwenye kikundi kinachoitwa Peoples Coffee Group. Kikundi hiki kinanunua na kusindika kahawa mbivu. Afisa Ntumishi wa Wilaya Ndugu Ngaikwela ana mahasiano ya kibiashara na Ndug Adam Kalonge mmiliki wa Mpito Coffee Group ambaye ni mnunuzi wa kahawa mbivu. Ndugu Burton Sinienga Diwani ya kata ya Ipunga ni mmiliki wa kikundi kinachoitwa Ifungo Coffee Group,. Kikundi chake bado kinadaiwa na wakulima. Ndugu Sende Shula Diwani ya kata ya Myovizi ni mmikliki wa kikundi cha Ichesa Coffee Group., na katibu wa kikundi hicho. Mpaka hivi tunavyozungumza anadaiwa na wakulima. Mbunge Godfrey Zambi anafanya biashara kwa ushilikiano wa siri na Musa Zambi na Burton Sinienga Diwani wa kata ya Ipunga kupitia kikundi kiitwacho Ifungo Coffee Group. Mhe. Rais zichukuliwe hatua za haraka kuzuia agenda hiyo chafu ambayo imepangwa na mafisadi kupitia watendaji wa Halmashauri ili kuhujumu wanunuzi wanaojali maslai ya wakulima kama LIMA kwa lengo la kupata nafasi kuhodhi soko na wakulima tusiwe na uchaguzi wa mahali bora pa kuuza kahawa yetu. Iundwe tume kuchunguza mwenendo wa viongozi wa Mkoa na hasa Wakuu wa Wilaya wa Mbeya, Mbozi na Rungwe ambapo kwa mfano Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe amepora kilo 483 za kahawa mbivu na kilo 1090 za kahawa kavu kutoka kwa wanunuzi wa kampuni ya LIMA vijijini na kwenda kuiuza kusikojulikana je? Haya ni maadili ya utumishi wa um,ma? Mhe. Rais tunaomba usifumbie macho siri iliyojificha kwenye mkanganyiko uliojitokeza wakati wa ziara ya Waziri wa kilimo na chakula Mhe. Jumanne Magembe ambapo watendaji hao bila aibu waliamua kumtukana na kumdhalilisha Waziri na kumnyima kabisa fursa ya kuongea na wakulima ambao ndio tulikuwa tunamsubili kwa hamu sana. Mhe. Rais mfumo wa bodi ya kahawa TCB ubadilishwe ili bodi iwe na jukumu la kutafuta masoko, kusimamia, ubora na bei badala ya sasa ambapo bodi inafanya biashara kwani viongozi wakuu wa bodi (TCB) wako nyuma ya mbinu hii chafu. Mwenyekiti mhe. Pius Genze na Mkurugenzi (Adolph Kumbulu) wa bodi ya kahawa walifanya vikao katika kila Wilaya wakishauri Makampuni wanyimwe vibali vya kufanya biashara ya kahawa mbivu (cherry). Tunaamini japo ili lina siri nzito nyuma yake kwani Mkurugenzi (Adolph Kumbulu) pamoja na Mwenyekiti (Mhe. Ngeze ) wa bodi ya kahawa kwa pamoja wana maslahi kwa biashara iendeshwayo na Kilcafe chini ya ushauri wa kitaalamu unaotolewa na Technoserve. Ili kulinda maslahi ya Kilcafe Mkurugenzi ameamua kwa makusudi kushawishi Halmashauri zipige marufuku biashara ya kahawa mbivu. Msukumo huu ulitokana na Kilcafe kushindwa kabisa kuhimili ushindani wa ununuzi wa kahawa mbivu, hivyo namna pekee ya kuinusuru ambayo ilibuniwa na Mkurugenzi wa bodi ya kahawa ni kusitisha utoaji wa leseni ya ununuzi wa kahawa mbivu. Usitishaji huu ulianza mara tu Adolph Kumbulu alipoteuliwa kuwa Mkurugenzi wa bodi ya kahawa 2008/2009. Mhe. Rais migogoro hii ni chanzo chake kikubwa ni Mkurugenzi wa bodi ya kahawa (TCB) ambaye ameigeuza bodi hiyo kama zizi lake la mbuzi anachinja apendavyo, ndiye anayetumika na mafisadi maneno yake ni tofauti na matendo yake chonde chonde sisi wakulima tunaiona TBC mzogo mkubwa kwetu. Mhe. Rais tunaungana na Waziri wa kilimo Ushirika na chakula kusisitiza ushindani wenye lengo la kuboresha kahawa na bei, ndio uwe msisitizo na si vinginevyo vita hii ya kimaslai tunaiona kwamba itatudhuru wakulima kwani uuzaji wa kahawa mbivu umetuondoa kwenye umaskini kwa sasa tunalipa karo za watoto wetu kwa wakati, kununua pembe jeo kwa wakati na pia imetoa ajira kwa vijana wetu na kupunguza matukio ya kihalifu. Mhe. Rais MUHIMU LESENI na vibali vya ununuzi wa zao la kahawa vitoke wizarani na sio kwenye Halmashauri wala bodi ya kahawa. Bodi na Halmashauri wabaki na jukumu la kusimamia sheria zao la kahawa Na. 23 ya 2001 tu ili kuondoa ukiritiba na mianya ya rushwa kwa Wakurugenzi na Watendaji wa Halmashauri. Mbinu za kuzuia ununuzi wa kahawa mbivu (red cherry) zina lengo la kuua ubora wa kahawa na kurudisha umaskini kwa wakulima kwani ni asilimia 20 tu ya kahawa mbivu zonazopita kwenye viwanda vya kumenyea kahawa hiyo katika Mikoa ya nyanda za juu wakati wenzetu wa Kigoma zaidi ya asilimia 70 ya kahawa mbivu zinapita kwenye viwanda (CPU). Mhe. Rais sisi wakulima wa zao la kahawa hususani Wilaya ya Mbozi, Mbeya, Ireje na Rungwe tunayo imani na wewe na serikali yako kwamba kilio chetu kitafanyiwa kazi, ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha mara moja Wakuu wa Wilaya za Mbozi, Rungwe na Mbeye na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi ambaye dhahili hana maadili ya uongozi kwani kitendo cha kumtukana Waziri wa kilimo na Rais aliye mteua hadharani kimewaacha wananchi na taswira tofauti tangu tarehe 16/01/2012. Mhe. Rais baada ya kukupatia picha sahihi, ya kero, hujuma na matumizi mabaya madaraka ya baadhi ya watendaji Mkoani hapa tunavyotendewa, CHONDE CHONDE Mhe. Rais na Mhe. Waziri wa Wizara ya kilimo na Ushirika na chakula tunaomba serikali itoe haraka Leseni na Kibali kwa mwekezaji LIMA ili ianze kutugawia mbolea kwani mpaka sasa anasubili Leseni na vibali na sisi wakulima tungali tumepanga foleni kwake kusubili mbolea. Ili tuanze kumwaga mashambani kwani mwaka huu kahawa zimeanza vizuri na kama hatutapata mbolea mapema punje zitaharibika. Na mwisho wakulima tumeapa kamwe hatupo tayari kuruhusu kampuni nyingine za mafisadi kuchukua kahawa zetu zaidi ya LIMA mkombozi wa mkulima wa kahawa nyanda za juu kusini ambaye tumeamua kuingia mikataba ya kumuuzia kahawa mbivu (red cherry). Kikao cha muungano kw Wakulima wa kahawa 1240 kilichofanyika tarehe 04/02/2012 mji mdogo wa Mlowo. Chini ya Mwenyekiti Japhet Kibona…………………………………………………………… Dickison Nzowa ……………………………………… Joel Mwakangale ………………………………….. na Abeli Mwashamba……………………………………………………….. Tunawakilisha kwako Mheshimiwa Rais. Kutika kata za:- 1. Bugoba – Tukuyu 2. Luswiswi – Ileje 3. Iluya – Mbozi 4. Kagwina – Tukuyu 5. Ikuti – Tukuyu 6. Kijiji cha bara – Mbozi 7. Kijiji cha Mlangali – Mbozi 8. Igamba – Mbozi 9. Kijiji acha Msia – Ireje 10. Kijiji cha Luwati – Mbozi 11. Kijiji cha Magamba – Mbozi 12. Kijiji cha Ruanda – Mbozi 13. Kijiji cha Uhowa – Mbozi 14. Kata ya Isansa 15. Kata ya Ihanda 16. Kata ya Igamba 17. Kata ya Ipunga 18. Kata ya Nyimbili 19. Kata ya Iyula 20. Kata ya Halungu 21. Kata ya Itaka 22. Kata ya Msiya 23. Kata ya Itengule – Mbeya vijijini 24. Kata ya Mlangali 25. Kata ya Myovizi 26. Kata ya Ruanda 27. Kata ya Nambinzo NAKALA:- MHE: WAZIRI MKUU, MIZENGI PINDA – (MB), S.L.P 1923 DAR ES SALAAM/DODOMA. WAZIRI KILIMO NA USHIRIKA MHE. PROF J. MAGHEMBE, S.L.P 9192, DAR ES SALAAM. [FONT=&quot]Re: Mbunge Zambi ashitakiwa mahakamani [/FONT]
  Kwanijuavyo mimi kuhusu hii biashara ya kahawa kwa kweli ni kamari na wengi wetuhapa hatujui kinachoendelea kwenye biashara hii. Biashara hii ni biasharaambayo haitakiwi kabisa kuingizwa Siasa ndani yake klakini wengi wetu hatujui,badalayake inageuzwa ni Siasa.[FONT=&quot]
  [/FONT]Biashara ya kahawa inaongozwa na soko kuu la kahawa duniani (stock exchange)lilipo New York kwa kahawa laini yaani Mild Arabica na London kwakahawa ngumu yaani Robusta. Kahawakwa ujumla naweza kusema ni kama kamari bei ya leo sio bei ya kesho aukeshokutwa au hata jana na juzi.
  Swali la msingi hapa ni tujiulize jetunamsaidiaje mkulima wa kahawa ambaye hana uwezo mkubwa ? Jetunamsaidiaje mkulima wa kahawa kwenye kuendeleza zao la kahawa na kuongeza kgalizo nazo na kipato chake kwa sasa ?Ununuziwa madawa na mbolea ? Jetunamsaidiaje mkulima pale anapotaka kumpeleka mtoto shule wakati anasubirikahawa yake ikauke ndipo aiuze ? je hizo shule zinasubiria ?Jetunamsaidiaje ili aweze kujikimu na maisha mpaka hapo atakapo kausha kahawa yake? au hatakuwa na njaa kwa wakati huo?Tufikiriekwa mapana na marefu bila kukurupuka na kuanza kutupiana maneno bila kutumiaakili kwa manufaa ya wachache wanaofikiria kwa ufupi.Mtakuwawatu wa maana kama atatokea mtu mmoja au mwana siasa ambaye ataonyesha kumteteamkulima katika misingi sahihi badala ya huu utaratibu unaotumiwa wa sasa ilituweze kuongeza zao la kahawa nchini kutoka tani 50,000 mpaka kufikia ton 100,000ifikapo 2015Wotekwa sasa tunafahamu kuwa ulaji wa kahawa soko la ndani lenyewe ni 3% tu wakatiwenzetu kama Ethiopia na wengine soko la ndani peke yake ni 40%Nitawaelewawanasiasa na wadau wengine wa kahawa kama watakuwa wa kwanza kumsaidia mkulimakuongeza uzalishaji badala ya staili iliyoko sasa hivi ya kujitokeza nakumpangia mkulima sheria nyingi baada ya mkulima kuvuna kahawa yake nakumlazimisha kuuza tunavyotaka sisi badala ya yeye mkulima kujipangia aonavyomwenyewe.Mwakawa 2000 kahawa ilishuka sana bei na hata mkulima kuuza kahawa yake kwa bei yash 400/kg mbona wakati huo hakuna aliyejitokeza hata mmoja kumsaidia mkulima kamakweli mlifanyalo ni sawa? Nchi zilizoendelea waliweza kumfidia mkulima kutokana hasara ili wasikate tamaa je sisi tunaweza kufanya hivyo Iwapo sokolikaporomoka sasa hivi ? Nijuavyomimi hakuna mahali popote duniani penye wanywaji wa kahawa ambao hawatakikahawa nzuri na yenye ubora wa juu ukasikia imekosa soko.Kama nikumbukavyo kipindihicho zilijitokeza kampuni ambazo ziliamua kumsaidia mkulima kwa kujenga vinuvya kumenya na kusafisha kahawa ziitwazo Soochack na Tropex ambazo zilifungavinu vya kusafisha kahawa mbichi kusini mwa Tanzania, Mbinga na mkulimaaliponea hapo baada ya kupatikana kahawa safi na wakati huo kahawa ya kusiniilikuwa ikijulikana kwa jina la AMEX TYPE yaani kahawa iliyo chini ya ubora.Hatabaadae ndipo ilipoingia kampuni ya Lima Kusini Mbeya na kufanya hivyohivyohakuna mkulima aliye lalamika kuwa anapunjwa kutokana na kuuza kahawa mbichi.Nahii ilisaidia kahawa ya kusini kuuzwa bei sawa na kahawa ya kasikazini na hatabaadae kuipita ya kasikazini.Neno AB au AA au Amex likafa na kahawa zote zikawazinauzwa kama FAQ south au FAQ North.Nakumbuka Nchi ya kwanza kuanza kununuakahawa ya kusini ilikuwa Japani ambayo ndio walikuwa wakiongoza kwa kununuakahawa ya Kasikazini wakati huo.Hivyobasi kwa kuanzia, Mgogoro huu wa cherry ulianzia mwaka 2008 wakati uongozi wa juuwa Bodi ya kahawa ulipobadilika na kuingia uongozi mpya.Katika kikaoalichokiongoza Mkurugenzi mkuu wa bodi ya kahawa Bw A.Kumburu huko Mbeya, Mbozina Mbinga mwezi December 2008 kwakutangaza kupiga marufuku ununuzi wa cherry lakini bila kueleza atamsaidiajemkulima anaetegemea kahawa hiyo ili apeleke watoto wake shule kwa wakatimuafaka na pia kujikimu na maisha,pia bila kujali wenye viwanda hivyowatalipaje madeni yao benki kwa fedha walizokopa.Hakuna asiye fahamu kuwa maandaliziya kahawa kutoka kuvuna mpaka kuuza inachukua muda gani takribani sio chini yamiezi 3- 4 ,sasa jiulize kwa mkulimamasikini anafanyaje wakati huo wote? Je anakula nini wakati anaangalia jua kamalitatoka ili aanike kahawa yake ikauke aweze kuiuza?.Tufikewakati sasa tuwe na mawazo tofauti tusiwe watu wa kutumiwa na wazungu tu maranyingine wanatumaliza bila sisi kujua. Suala la kupinga ununuzi wa cherywilayani Mbozi ni janja ya kuitumia wilaya hiyo pamoja na Mb wao Mh Zambi pamojana uongozi wa juu wa wilaya na mkoa hii ni kianzio tu cha upotoshwaji iliikifanikiwa sumu hiyo isambae mikoa mingine yote inayolima kahawa. Hii nikatika harakati za kuwasaidia wazungu ambao hawataki kuwekeza kwenye mashinehizo ili waweze kupata kahawa aliyoitayarisha mkulima mwenyewe kwa jasho kubwana kuinunua kwa bei ambayo itakakuwepo wakati huo.Tusidanganyane hapa kwamba kunamfanya biashara anaefanya biashara hii bila kufuata soko la dunia lilivyo labdaukute wale wachache ambao waliuza kahawa hewa hivyo atanunua hata kwa hasaraili amridhishe mnunuzi wake na hapa akikuta bei zimedondoka basi na aliuza beiya juu basi na inabidi apate hasara, mfano rahisi ni mwaka jana wakati soko ladunia likiwa juu yaani NY $250lb huku Tanzaniamkulima aliuza kahawa yake kwa bei ya sh 5000, leo soko la dunia liko$151lb na kg ya kahawa kwa sasa ni sh2500-3000 hapa mnunuzi hajajumlisha overheads zake tutumie akili na upotoshwajiuondoke.Kwanzanapenda kusema kuwa kuuza kahawa ikiwa cherry inampunguzia mkulima kuondokanana Gharama za kuimenya,kuivundika,kuiosha na kama hana maji safi basi ndiohivyo tena mkulima wa ulimwengu wa tatu na mwisho kuianika hii yote ni gharamakwa mkulima. Mfanoili upate kg 1 ya parchment unatakiwa upate kg 5 za cherryuzimenye,uvundike,uoshe, uanike n.k ndio upate kg 1 ya parchment na kwa sasa bei yakahawa aliyoikausha mkulima mwenyewe ni Sh 2500 – 3000.Sasa hapa anaeuza cherryKg 1 ni sh 600 huyu gharama yake ni kuitoa shambani tu hanagharama nyingine zaidi je hapa nani anaefaidi zaidi? Hilo ni swali dogo sana walahuitaji kufikiria kwa mtu mwenye akili timamu kama sio kichaa ambae anafikirimaisha anayoishi ya kupewa mshahara ni sawa na ya mkulima masikini kulekijijini ambae hajui hata chai na sambusa ya saa nne ni kitu gani yeye anaishikwa mlo mmoja tu tena kwa tabu sana kuupata.HivyoMkurugenzi mkuu wa bodi Bw A.Kumburu ni bora uachane kabisa na tabia hiyo, wotetunaelewa fika mission/mipango yako uliyoingia nayo bodi ya kuwalinda wazunguna kupiga vita wazawa ambao wanajitolea kumlinda mkulima mdogo.Swalidogo sana kama Bw Kumburu utaweza kujibu itafurahisha sana.UlipokuwaTechnoserve/Sustainable Harvest ambazo zilikuja kwa mgongo wa kumsaidia mkulima kama ushirika ili wasilipe kodije mlikuwa mnamsaidia kwa bei ya hapa yaani mlikuwa mna share faida na mkulimalocaly au ni pamoja na faida ya kahawamlizokuwa mnauza nje ya nchi yaani international.Basikama sio internationally hivyo tunakuomba uache tabia yako ya kupotoshawakulima na wananchi wa Tanzania kwa ujumla pamoja na wanasiasa unaowatumia kamaMh Zambi ambae hajui unachokifanya, wote tunajua unayoyafanya kama kwa sasaulivyofanikiwa kuhamisha funds zilizokuwa zikitoka kwa Bill Gates and BelindaFoundation kwenda kwa Technoserve na kwa kutumia cheo chako umeweza kudhaminifunds hizo kwenda ECOM ambayo ni kampuni ya wazungu na ndio kampuni mama yamakumpuni ya MAWENZI LTD NA TUTUNZE LTD ambao hawana nia ya kuwekeza mashine zacherry ila wanahitaji zaidi kahawa iliyo tayari yaani parchment iliyotayarishwana mkulima mvuja jasho.wao wabebe na kujiondokea muonee huruma huyu mkulima waTanzania. Nafikirihuu ni wakati mzuri sana wa kurekebisha haya yote kama alivyosema Mwenyekiti wabodi Dr Eve Sinare na bodi yake,ukiwa kama kiongozi unaeongoza kumpiga vitakupitia kwa wanasiasa kama Mh Zambi kwa kuwa ameingia na sera ya kumlindamkulima myonge na kwa kuwa huwezi kumsokota kutokana na kuwa hana njaa kama alizokuwa nazo Mwenyekitialiyepita ambaye uliweza kumsokota unavyotaka kiasi cha kukuona kama Mungu sasahayo yamekwisha,kawaombe wazungu radhi kuwa imeshindikana watakusamehe tu,hawa wakulimawatakuachia laana mbaya sana na utakuja kufa kifo cha mateso cha kuozeakitandani kabla ya kufa. Jaribu kangalia soko linavyoporomoka kwa kasi hukokwenye soko la dunia.TunamuombaWaziri wa kilimo chakula na ushirika aokoe hili jaazi kabla halijatumbukiakubaya akuondoe mapema ili mkulima asiumie zaidi.Mhwaziri tunashindwa kuelewa ni kwa nini Bw Kumburu anabishana na mwenyekiti wakekwa maamuzi aliyoyatoa ya kuwa MKULIMAAACHWE AAMUE MWENYEWE KUUZA ANAKOTAKA YAANI AKITAKA KUUZA KAHAWA MBICHI SAWAAKITAKA KUUZA ILIYOKAUKA PIA NI SAWA maamuzi aachiwe mkulima aliyelimakahawa yake mwenyewe kinachokuuma wewe naMh Zambi pamoja na uongozi wote wa Mbozi na Mkoa ni nini hasa ? Je kunaulichomsaidia mkulima huyo kama fedha au mbolea au madawa ? je wewe na Mh Zambimnapata hasara gani huko basi kama mnawajali sana wafungieni vinu vya kumenyeakahawa ndio tujue mna uchungu nao kama walivyofanya wenzenu msitumie vyeo namadaraka yenu mliyo nayo kujiingiza kwenye kumuumiza mkulima na kumfaidishamzungu,wao hawana wakulima wala ndugu zao huku Tanzania lijueni hilo kwa makiniacheni kuwa kama malimbukeni mnao taka kummaliza mkulima na kuvunja ajira zawale walioajiriwa kwenye viwanda hivyo. Mh Zambi jaribu kuangalia kwenye jimbolako ni vijana wangapi ambao watakosa kazi kwa wewe kusimamia zoezi zima lakufunga viwanda hivyo na 2015 utawarudia hao hao kuwaomba kura?PiaBw Adolph Kumburu tunakuomba ujue kikao mlichokaa pamoja na Mh Zambi pamoja nauongozi wa wilaya ya Mbozi ofisi kwako Moshi kwenye jengo la kahawa tarehe28/5/2012 na ukawa ndio mwandishi wa barua aliyomwandikia Waziri waKilimo,Chakula na Ushirika Eng Chiza kupitia kwa Mh Zambi barua ambayo piaameitoa kwenye gazeti la Mwanahalisi kuwa tunajua ni wewe Kumburu wewe ndio uliyekuwamwandishi mkuu wa barua hiyo.Tunaombakukuambia kuwa hufai kuwa kiongozi wa kumlinda mkulima na hii inathibitishaulivyoingia bodi ukapiga marufuku kuheshimu reserve za wakulima wavuja jashoili wazungu wajibebee kahawa kwa bei poa acha kabisa kumuua mkulima na hakunaheshima kubwa utakayoipata toka kwa wakulima kama ukiachia ngazi mwenyewe mapemazaidi ili upishe mtawala mwingine ambae hatakuwa kibaraka wa wazungu nchini.Nendakaendeleze kikundi chako na Padre aliyeko Ujerumani kule Mbinga kiitwachoSongea Net work Data zote tunazo. Mtu hatari sana wewe mwenye wivu mkali,mfitini, mchonganishi na muongo.Sasakesi kafunguliwa Zambi Moshi wewe ndio utakuwa unamlipia kuja kwenye kesi hiyoau ni wazungu wako wanaokutumia nae anaenda kichwa kichwa tu Kwamara nyingine tena Waziri tunakuomba chondechonde omba ruhusa kwa Mh Raisiumuondoe huyu Bwana kabla hajakuingiza mkenge wewe uwajibishwe kwa kosa ambaloungeweza kuliepuka mapema. Alipotosha bodi iliyopita na mwisho wake bodi yoteilifukuzwa na akabaki yeye. Hana urafiki na mtu mweusi huyu Bw Adolph waswahiliwanasema “ukicheza na mbwa atakufuata mpaka msikitini”.Bodiiliyopo sasa hivi ni bodi imara na uteuzi wa Bw Eric ni wa halali akiwa kamamwakilishi wa wanunuzi binafsi wa kahawa PCB kama alivyokuwa Amir Hamza kwenyebodi iliyopita akiwakilisha exporters TCA,Uteuzi Bw James Teri ni wa halalikama alivyokuwa bw Kirenga akiwakilisha wizara, uteuzi wa Msuya ni wa halalikwani hata Ndossi alikuwa ni mtaalam wa misitu kwenye bodi iliyopita na sualala kusema bodi haina mwakilishi kutoka Mbeya sio sahihi kwani hata kwenye bodiiliyopita kulikuwa hakuna mwakilishi kutoka Mbinga na mwisho suala la kusemabodi imejazwa watu wa kasikazini sio sahihi kwani hata bodi iliyopita ilikuwana wawakilishi watatu kutoka Kagera na mmoja wao ni aliyekuwa Mwenyekiti-Bw Pius Ngeze. Mwenyekuchangia na achangie ila tuache kuwa wabishi tusiotumia akili Tanzania ni mojana tuelewe kuwa nchi yetu haina ukabila hata kidogo tuachane dhana potovutunayotaka kujengewa na wachache walionunuliwa na wazungu.Nawatakienikila la kheri na Mkulima mnyonge wa Tanzania,
  [FONT=&quot] [/FONT]
   
 8. M

  M4C ARUSHA Member

  #8
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi sio rais ila nimeiona njia pekee ya kukomboa zao la kahawa ni pamoja na kuwaondo baadhi ya wajumbe wa bodi ambao ni wabadhirifu kama mernad swai mwenyekiti wa kncu na vilwe vile mwenyekiti wa tccco ambayo imekufa lkakini dawa hasa ni kuchagua chama makini 2015 katika kuongoza hii nchi ambayo viongozi wake kwa sasa ni dhaifu
   
 9. m

  matengo Member

  #9
  Oct 26, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sawa kabisa through e-com,Tutunze Kahawa, Solidaridad, Cafe Africa, Sustainable Harvest syndicate.
   
 10. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Watu wa nanna hiyo nchale tu, bwana wewe kunchekea nyani matokeo yake ndo hayo, Bhaaa!
   
Loading...