Mkurugenzi Mkuu ATCL: Hatuwezi kuweka wazi idadi ya abiria waliokata ticket za Dreamliner kwa sababu za kibiashara

Eti sababu za kibiashara! Ujinga tu! Waseme tu wakitangaza idadi ya abiria watasababisha ' fastrasheni '. Prof. Assad hatujasahau ahadi yako, mwakani kagua hili shirika.
 
Watu weusi uwa tunamatatizo sana kila kitu usiri. Unasikia waziri anasema tukitamka nyongeza ya mshahara kutakuwa na mfumuko wa bei, wachezaji wakisajiriwa napo usiri, madini hawataki ya kaguliewe na CAG napo usiri, ndege kusema idadi ya abiria napo usiri ngozi nyeusi tunamatatiza sana
Na tutashangaa sana
Mishahara inatangazwa lakini huku inaingia siasa zaidi

20180727_110246.jpeg
 
Jee kama ni Dar-Mwanza-Kinshasa na kulala huko hiyo nayo ni round trip?
Round trip maana yake kwenda na kurudi, haijalishi inapitia wapi.

Hivyo ukiambiwa ATCL ita fly twice per day to Kinsasha inamaanisha Dar-Kinsa ni round trip.

P.
 
Bei za Dreamliner ni za promosheni tu joshua_ok baada ya hapo tunarudia bei za kawaida.. Hiyo ya kuzunguka FN ataendelea kutupiga bao, abiria kukaa masaa 2.30dk kwa safari ya saa 1.15dk.

Ila pia 262seater kuwapata kwa route ya Dar - Mza sio rahisi labda kama nauli ni Tsh50,000

Ngoja tusubiri hizo zingine labda hali itakuwa tofauti
B787 zinga la dude lazima CHAGADEMA wakae. CCM nakupenda kwa moyo wote
 
B787 zinga la dude lazima CHAGADEMA wakae. CCM nakupenda kwa moyo wote
Kumbe ccm ndio wamenunua? Wana pesa sana hawa, kama walivyojenga viwanja vya michezo na majengo ya maofisi kila mkoa.
Unayo haki kuwapenda kwa moyo wote hata ikibidi wapende kwa ...n..
 
Kumbe ccm ndio wamenunua? Wana pesa sana hawa, kama walivyojenga viwanja vya michezo na majengo ya maofisi kila mkoa.
Unayo haki kuwapenda kwa moyo wote hata ikibidi wapende kwa ...n..
Sifichi mm ni mwana CCM kindakindaki. Hongera mwenyekiti. Hongera sana kwa kufufua ATCL taifa lenye umri wa nusu karne kukosa ndege ya taifa ni aibu
 
Eti sababu za kibiashara! Ujinga tu! Waseme tu wakitangaza idadi ya abiria watasababisha ' fastrasheni '. Prof. Assad hatujasahau ahadi yako, mwakani kagua hili shirika.
.....wapi atapa hiyo Ruhusa maana kama aliwavua Nguo kupigwa 1.5t kwenye hilo limwewe atawainamisha kabisa
 
Kumbe ccm ndio wamenunua? Wana pesa sana hawa, kama walivyojenga viwanja vya michezo na majengo ya maofisi kila mkoa.
Unayo haki kuwapenda kwa moyo wote hata ikibidi wapende kwa ...n..
wamenunua halafu CHADEMA tumbo joto wafuasi wa CCM saizi yao pilau na kofia na ma dera. Sasa kama unapewa pilau ili upige kura kweli hiyo nauli ya ndege itakuwa nayo au itaishia kuwa washangiliaji?
 
Siku tatu kabla ya kuzinduliwa kwa safari za ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladslaus Matindi amesema maandalizi yote yamekamilika.

Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba watu 262, itaanza kupasua anga ya Tanzania Jumapili Julai 29, 2018 kwa safari za Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza.

Akizungumza na MCL Digital leo Alhamisi Julai 26, 2018 Matindi amesema kwa siku ndege hiyo itafanya safari mbili, moja asubuhi na nyingine jioni.

Kuhusu idadi ya abiria waliokata tiketi hadi sasa kwa ajili ya kusafiri na ndege hiyo ya kisasa, amesema jambo hilo haliwezi kuwekwa wazi kwa sababu za kibiashara.

Soma Zaidi:

Ukarabati uwanja wa ndege Mwanza mbioni kuanza

“Hayo hayawezi kusemwa kwa sababu najua wapinzani wetu nao wanasubiri kusikia hilo. Subirini siku hiyo mtashuhudia,” amesema Matindi.

“Ni ndege yetu na shirika hili ni la umma lakini hiyo haibadilishi sheria za mchezo, kwenye biashara sheria zinabaki vilevile. Nia yetu ni kufanya vizuri kwenye soko.”
Ndege hiyo iliyopewa jina la Kilimanjaro Hapa Kazi Tu iliwasili nchini Julai 8, 2018 saa 11:29 jioni na kupokelewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais John Magufuli.

Dreamliner inafanya idadi ya ndege ambazo zimeshanunuliwa na Serikali kufikia nne kati ya saba ambazo zinatarajiwa kununuliwa kwa lengo la kuifufua ATCL iliyokuwa na ndege moja pekee yenye uwezo wa kubeba abiria 51.

Ndege zingine tatu zilizowasili nchini ni aina ya Bombardier Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja.
Jana ndio nilielewa kwanini mkurugenzi alishindwa kutaja idadi ya abiria walio kuwa wasafiri na dream liner yetu.
Kumbe alikuwa haja pewa list toka Lumumba ambao wange safiri na ndege kwenda kupiga selfie Kilimanjaro na Mwanza.
Kwa mtindo huu.... Mhhhh naona ATCL ikifa mapema sana... Sidhani kama ndio yalikuwa malengo ya Mkuu kununua ndege..
 
wamenunua halafu CHADEMA tumbo joto wafuasi wa CCM saizi yao pilau na kofia na ma dera. Sasa kama unapewa pilau ili upige kura kweli hiyo nauli ya ndege itakuwa nayo au itaishia kuwa washangiliaji?
Wewe endelea kulalama sisi tunakata mawingu KIA, Mwanza-Dar.
 
ATCL inakata mawingu siyo nyinyi na hilo shirika ni mali ya wananchi siyo yenu endelea kujidanganya kuwa ni mali ya CCM
Aliyesema Shirika la CCM ni nani? Acheni kuweweseka. Awamu hii ni ya vitendo si blah blah!
 
Back
Top Bottom