Mkurugenzi Mkuu ATCL: Hatuwezi kuweka wazi idadi ya abiria waliokata ticket za Dreamliner kwa sababu za kibiashara

Wanasiasa mngesoma hili nafikiri akili ya kisiasa isingewaongoza kusema hayo ya kisiasa "Ni ndege yetu na shirika hili ni la umma lakini hiyo haibadilishi sheria za mchezo, kwenye biashara sheria zinabaki vilevile." Kaisema vizuri ila kama akili yako ni ya kupinga kila jambo ni haki yako kuitafutia upinzani!

Siku tatu kabla ya kuzinduliwa kwa safari za ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladslaus Matindi amesema maandalizi yote yamekamilika.

Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba watu 262, itaanza kupasua anga ya Tanzania Jumapili Julai 29, 2018 kwa safari za Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza.

Akizungumza na MCL Digital leo Alhamisi Julai 26, 2018 Matindi amesema kwa siku ndege hiyo itafanya safari mbili, moja asubuhi na nyingine jioni.

Kuhusu idadi ya abiria waliokata tiketi hadi sasa kwa ajili ya kusafiri na ndege hiyo ya kisasa, amesema jambo hilo haliwezi kuwekwa wazi kwa sababu za kibiashara.

Soma Zaidi:

Ukarabati uwanja wa ndege Mwanza mbioni kuanza

“Hayo hayawezi kusemwa kwa sababu najua wapinzani wetu nao wanasubiri kusikia hilo. Subirini siku hiyo mtashuhudia,” amesema Matindi.

“Ni ndege yetu na shirika hili ni la umma lakini hiyo haibadilishi sheria za mchezo, kwenye biashara sheria zinabaki vilevile. Nia yetu ni kufanya vizuri kwenye soko.”
Ndege hiyo iliyopewa jina la Kilimanjaro Hapa Kazi Tu iliwasili nchini Julai 8, 2018 saa 11:29 jioni na kupokelewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais John Magufuli.

Dreamliner inafanya idadi ya ndege ambazo zimeshanunuliwa na Serikali kufikia nne kati ya saba ambazo zinatarajiwa kununuliwa kwa lengo la kuifufua ATCL iliyokuwa na ndege moja pekee yenye uwezo wa kubeba abiria 51.

Ndege zingine tatu zilizowasili nchini ni aina ya Bombardier Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja.
 
ukiona wanafichaficha ujue kwamba wanaenda mswaki .
Acheni kubeza kila kitu, tatizo akili zetu kama nyumbu mmoja akikoment upupu wooooote kama mazombi tunabeza. Ingia TOVUTI ya ATCL then jifanye unataka ticket hata ya kesho ulete majibu! Almost SOLD OUT through out a week. Halafu mazwazwa wanasema mswaki, mapimbi yatapata sana sheeedar
 
Siku tatu kabla ya kuzinduliwa kwa safari za ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladslaus Matindi amesema maandalizi yote yamekamilika.

Ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba watu 262, itaanza kupasua anga ya Tanzania Jumapili Julai 29, 2018 kwa safari za Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza.

Akizungumza na MCL Digital leo Alhamisi Julai 26, 2018 Matindi amesema kwa siku ndege hiyo itafanya safari mbili, moja asubuhi na nyingine jioni.

Kuhusu idadi ya abiria waliokata tiketi hadi sasa kwa ajili ya kusafiri na ndege hiyo ya kisasa, amesema jambo hilo haliwezi kuwekwa wazi kwa sababu za kibiashara.

Soma Zaidi:

Ukarabati uwanja wa ndege Mwanza mbioni kuanza

“Hayo hayawezi kusemwa kwa sababu najua wapinzani wetu nao wanasubiri kusikia hilo. Subirini siku hiyo mtashuhudia,” amesema Matindi.

“Ni ndege yetu na shirika hili ni la umma lakini hiyo haibadilishi sheria za mchezo, kwenye biashara sheria zinabaki vilevile. Nia yetu ni kufanya vizuri kwenye soko.”
Ndege hiyo iliyopewa jina la Kilimanjaro Hapa Kazi Tu iliwasili nchini Julai 8, 2018 saa 11:29 jioni na kupokelewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais John Magufuli.

Dreamliner inafanya idadi ya ndege ambazo zimeshanunuliwa na Serikali kufikia nne kati ya saba ambazo zinatarajiwa kununuliwa kwa lengo la kuifufua ATCL iliyokuwa na ndege moja pekee yenye uwezo wa kubeba abiria 51.

Ndege zingine tatu zilizowasili nchini ni aina ya Bombardier Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja.
Hongereni sana,pigeni kazi,msituaibishe.
 
Hivi Pascal kwa uelewa wangu mdogo jee niko sahihi hapa? Kwamba hapo asubuhi ni trip mbili na jioni ni mbili? Maana ile safari ya asubuhi kwenda Mwanza ina namba yake na kutoka Mwanza kuja Dar pia na namba yake kwa hiyo hizo ni safari mbili tofauti.
Kwa maana hiyo asubuhi na jioni ziko safari nne. Au nakosea?
Ndege inapofanya safari, ni round trip, kwenda na kurudi.

P.
 
Kuna watu watasafirishwa bure ili kujaza ndege. Kama CCM wakati wa uchaguzi wanavyobeba watu kuwapeleka kwenye mikutano ya kampeni ili waonekane wamejaza uwanja.

Nilikuwa nafikiri weeee, kwanini iwe siri kutajwa nafasi tu ambazo ni booked.....sbb za CEO wala hazikuniingia!!

Lakini all the way, naona wewe umenipa jibu na hakika hiki ndicho kitakachofanyika!!

Nakubaliana na wewe kabisa kwa kuzingatia tabia ya "Jiwe" jinsi zilivyo....

Wewe kama tu siku ile ndege inafika kutoka dukani kununuliwa Jiwe akaamurisha viongozi wakuu wa karibu serikali nzima mpaka marais wastaafu kuwa uwanjani kuipokea na kuipungia mikono Dreamliner 787 - 8 ikitua atashindwaje kuamuru wajumbe wote wa NEC - CCM kwenda kujaza viti ili kutwa nzima wawe wanazunguka nayo ili waseme "nauli iko poa, Dreamliner imejaa watanzania wanyonge " !!???
 
Last edited:
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom