Mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia DR MARA MARWICK aihakikishikia Tanzania ushirikiano mwema kwenye masuala ya Maendeleo

Corticopontine

JF-Expert Member
Sep 20, 2019
664
1,272
PROF. KABUDI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKAZI WA BENKI YA DUNIA.

Dar es Salaam, 5 Februari 2020
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia hapa nchini Tanzania, Bi. Mara Marwick ameihakikishia Serikali ya Tanzania ushirikiano katika sekta mbalimbali ili kufikia maendeleo yaliyokusudiwa.

Bi. Marwick ameyasema hayo leo tarehe 5 Februari 2020 alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi katika Ofisi Ndogo za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam.

Bi. Marwick amesema kuwa, uhusiano baina ya benki hiyo na Tanzania ni mzuri na kwamba Benki ya Dunia inathamini uhusiano huo wa tangu miaka ya 1960 hadi leo na iko tayari kuendelea kuunga mkono kwa njia ya ufadhili au mikopo miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.

"Tuna uhusiano mzuri katika miradi na uwekezaji ambapo tunaiwezesha Serikali katika maeneo mbalimbali. Pia tunafanya kazi pamoja katika masuala muhimu kama vile uchambuzi wa sera za maendeleo, hii inaashiria kuwa Benki ya Dunia itaendeleza ushirikiano huu katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na mahusiano imara pamoja na maendeleo endelevu," Amesema Bi. Marwick.

Ameongeza kuwa, katika mazungumzo hayo, wamejadili masuala muhimu kuhusu maendeleo ya Tanzania hususan elimu, miradi ya miundombinu, uchumi wa viwanda, pamoja na maendeleo ya wananchi kwa ujumla.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema kwamba, Tanzania itaendeleza mahusiano na Benki ya Dunia na kuwataka watanzania kupuuza uzushi na uvumi unaosambazwa katika mitandao ya kijamii kuhusu mahusiano baina ya Tanzania na Benki hiyo na badala yake wasubiri taarifa rasmi kutoka kwa Serikali na Benki ya Dunia.
 
Corticopontine,
Hivi kabudi na wengine hamjui nguvu ya USA katika maamuzi ya benkinya dunia? Acheni kujidanganya kwamba unaweza kushupalia US ukabaki salama
 
Back
Top Bottom