SAIZI YANGU
JF-Expert Member
- Nov 8, 2013
- 381
- 83
Manispaa ya Iringa imekuwa inaongoza kieleimu kwa kipindi kirefu sasa. Hatua hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na kujitolea na ufanyaji kazi wa kujituma wa Walimu kwa ngazi mbalimbali. Lakini hivi karibuni amehamishiwa Afisa Elimu mmoja aitwae Haji Mnasi ambaye kiukweli amekuwa mbabe, dikteta na hasikii ushauri. Amekuwa akifanya kazi kwa majungu na hivyo kumfanya awe si kipenzi kwa walimu. Hali hii inatuvunja sana nguvu sisi walimu wa Manispaa hii. Kwa mtindo huu nahisi elimu inaweza kuporormoka kwani walimu wataacha tena kujituma. Naomba Mkurugenzi wa Manispaa muangalie sana Afisa Elimu huyu.