Mkurugenzi Malinyi ajitolea kumsomesha mwanafunzi aliyeolewa kabla ya matokeo ya darasa la saba

kisatu

Senior Member
Jan 16, 2015
150
95
*MKURUGENZI MALINYI AJITOLEA KUMSOMESHA MWANAFUNZI ALIYEOLEWA KABLA YA MATOKEO YA DARASA LA SABA*

Dotto Charles Heka mwenye miaka 13 aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya msingi Lupungu wilayani Malinyi hatimaye amefufua ndoto zake za kuendelea na elimu ya sekondari.
Awali baada ya kuhitimu elimu ya msingi tu wazazi wake walimshinikiza na kumlazimisha aolewe pasipo yeye mwenyewe kuridhia kuishi na mbakaji Masenga kama mme na mke, akielezea kwa uchungu mbele ya mkurugenzi wa wilaya ya Malinyi ndugu _Marcelin Ndimbwa_,

afisa elimu wa wilaya Kalagila Silivesta na mwanasheria Sospeter Kalekwa, mwanafunzi Doto Charles Heka anasema,kwakuwa hakupata kuungwa mkono na hata mmoja wa wazazi na ndugu zake alikubali kuoelewa hivyo hivyo. Baada ya matokeo kutoka baadhi ya wasamaria wema waligundua kwamba amefaulu na amechaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya kutwa ya Ngoheranga na kuamua kutoa taarifa wilayani iliyopelekea mkurugenzi kulivalia nguja jambo hilo na baada ya kujiridhisha aliweka mtego na jeshi la polisi lilifanikiwa kumkamata baba wa mtoto na kumchukua mtoto huyo ambaye mpaka sasa bado yupo chini ya uangalizi wake mkurugenzi na mtoto anaishi kwa mwalimu, akisubilia kufungua kwa shule .

Mbali na hayo yote pia mkurugenzi ameamua kujitolea kumsomesha mwanafunzi huyo kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita na amemwomba afisa elimu mkoa amtafutie nafasi ya shule ya bweni huku mbakaji Masenga akiwa aliyetoroka akiendelea kutafutwa na jeshi la polisi na kuhakikisha anatiwa nguvuni na sheria kuchukua mkondo wake na kuwa onyo na somo kwa wengine wote wenye mawazo na tabia za namna hizo ndani ya halmashauri yake. Aidha mkurugenzi amewapongeza maafisa elimu, watumishi wa halmashauri hiyo pamoja na wasamaria wema waliotoa ushirikiano na kumnusuru binti huyo. Mungu atawalipa kwa haya mliyomtendea malaika wake Dotto.
1483863580047.jpg
1483863604692.jpg
 
Naona Kasesera kapata mwanachama. Endelea kujipigia promo Mkurugenzi. Utawala wa awamu ya 5 ni utawala wa Media. Huenda wakakuona kwa nafasi za juu zaidi.
 
Ni vYema kasaidiwa ila kama alishakuwa exposed kwenYe ile starehe Ya ubaba na umama ....shule huwa Ngumu sana
 
Issue ni nini hapo? Elimu bure. Yako mambo mengi ya msingi ya kujadili sio jambo dogo kama hili. Kuna watu wanawasomesha watoto zaidi ya kumi lakini hawawezi hata picha humu.
 
Sasa hili nalo mpaka liletwe kujadili humu! kuna watu wanasomesha watoto zaidi ya kumi wametulia tu sembuse mmoja!
Au ndio yale yale ya kasesela!
 
Sasa hili nalo mpaka liletwe kujadili humu! kuna watu wanasomesha watoto zaidi ya kumi wametulia tu sembuse mmoja!
Au ndio yale yale ya kasesela!
Wewe unadhani hili ni jambo dogo?
 
Kwa hatua aliyofikia kuna ugumu kurudi shule na kuweza kumudu masomo japo ni hatua nzuri na hakuna lisilowezekana.
 
Hivi huyu si under 18? kama ndio kwa nini wachapishe picha na majina yake? au ndio watu kutaka Promo??????
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom