Mkurugenzi Makumbusho ya Taifa, asimamishwa kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi Makumbusho ya Taifa, asimamishwa kazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 27, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Na Florence Majani | 26 July 2012

  MKURUGENZI wa Makumbusho ya Taifa, Jackson Kihiyo amesimamishwa kazi kwa muda usiojulikana ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili.

  Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Mkurugenzi huyo alisema aliitwa na mkubwa wake wa kazi, ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na kufahamishwa kuwa amesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi kwani kuna tuhuma kuhusu utendaji wake katika ofisi hiyo.

  "Baada ya kupewa taarifa hizo, juzi(jumanne) nilikabidhi ofisi na hivi sasa nipo nyumbani. Cha muhimu ni kuwa sijafukuzwa ila nimesimamishwa na ninaendelea kupata mshahara wangu kama kawaida haid pale watakapomaliza huo uchunguzi wao," alisema Kihiyo.

  Kihiyo alisema, hakutaka kumhoji mkuu wake wa kazi kuhusu tuhuma zinazomkabili kwa sababu alitaka wawe huru na wafuatilie kwa kina bila kuingiliwa, hivyo hadi sasa hafahamu kilichomsimamisha kazi.

  "Najua wakimaliza watanijulisha, sina mashaka yeyote kwa sababu najua hakuna kibaya nilichofanya, nikiwauliza uliza watadhani ninataka kuwaingilia katika uchunguzi wao. Waache wafanye uchunguzi kwa utaratibu na kwa uhuru wakimaliza watanieleza kilichopatikana," alisema Mkurugenzi huyo.

  Chanzo cha habari kutoka katika ofisi hiyo kilichozungumza kwa masharti ya kutotajwa jina lake kilibainisha kuwa mkurugenzi huyo amefukuzwa baada ya wafanyakazi kupeleka malalamiko kwa katibu mkuu, Maimuna Tarishi, ikiwemo utata katika ukusanyaji wa mapato na maslahi ya wafanyakazi.

  "Mkurugenzi alitoa amri ya kukusanya mapato katika vituo vyote na kisha mapato hayo katika akaunti ya makao makuu. Hili jambo lilizua maswali kwa sababu tutapelekaje mapato yote makao makuu, vituo vitajiendesha na nini? Lakini lingine ni maslahi duni ya wafanyakazi, hatujaboreshewa mishahara kwa muda mrefu," kilisema chanzo hicho.

  Chanzo hicho kiliongeza kuwa malalamiko mengine kuhusu utendaji wa mkurugenzi huyo ni kitendo cha Ofisi kutumia Menejimeti ya Umma kumuadhibu mfanyakazi badala ya kutumia Kamati ya Nidhamu jambo alilodai linasababisha uonevu mkubwa kwa wafanyakazi.

  Shutuma nyingine dhidi ya Kihiyo ni upandishwaji wa vyeo kwa wafanyakazi usiozingatia sifa stahiki na kutokuwepo mipango endelevu ya mafunzo kwa wafanyakazi.

  Kabla ya Kihiyo kushika nafasi hiyo, Mkurugenzi wa Makumbusho alikuwa ni Nobert Kayombo, ambaye alifariki Novemba 30, 2010.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Hii Ndio Style Mpya? ya kuambiwa sasa kazi basi wewe ??
   
 3. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Twende kazi.
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,336
  Likes Received: 1,801
  Trophy Points: 280
  Serikali imeanza kuamka kutoka kwa usingizi mnene
   
 5. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Kusimamishwa kazi hakutoshi, this is the same old story kuzuga wadanganyika!
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,336
  Likes Received: 1,801
  Trophy Points: 280
  Mambo yanavyoenda kuna watu watalala ndani kweli kweli
   
 7. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Waalala ndani kwa miezi 8 kisha kuruhusiwa kumiliki simu za mikononi na pindi wanapotoka jela wanapokewa kishujaa
   
 8. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Napita
   
 9. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Endeleeni kushabikia watu kufutwa kazi mkadhani ndo suluhu. Ukweli ni kwamba kuna baadhi wanapigwa majungu kirahisi rahisi na watu wana act kisiasa. Mambo ya sasa ni vululuvululu, watu wanakuangushia jumba bovu at any time.
   
 10. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Zuga toto tu mbona wale walijiudhuru kwa kashfa nzito wanadunda tu mjengoni.tena wategemewa wakiokoe chama cha majambuzi.
   
 11. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Mimi mpaka atakaposimamishwa Jakaya ndio ntaamini wako serious.
   
 12. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #12
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Ndio kawaida ya Serikali Dhaifu ya CCM kusimamisha kazi na kupangia kazi nyingine
   
 13. maria pia

  maria pia JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 516
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hakuna jipya,hata akikutwa na hatia...danadana
   
 14. k

  kimeloki JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 1,931
  Likes Received: 955
  Trophy Points: 280
  kumbe ni kihiyo? ok
   
 15. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  But hawa wakurugenzi ni vidagaa tu mbona hao wenye madaraka makubwa zaidi wanaharibu na hatujasikia wanajiwajibisha wenyewe au kuwajibishwa na aliye wateua? Tuanze taratibu!!! But all in all ni hatua nzuri hii.
   
 16. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #16
  Jul 27, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Kwa sababu walizotoa, hapo labda hilo la kupndish vyeo, mengine yote ni kawaida sana. HIlo la kuingiza hel akaunti ya makao makuu kwani zote si zimeingia kwa akaunti ya serikali? Hao workers watafute sababu nyingine nzito sio hizo nyepesi kabisa!
   
 17. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #17
  Jul 27, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Kuna assistant mwingine wa kikwete anaitwa Kihiyo, na ni yule aliyemwagwa na Lamwai ktk kesi iliyoleta matumizi ya neno Kihiyo kwa watu wasio na shule!
   
 18. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #18
  Jul 27, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,736
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mhando si wangemweka ndani kwanza wakati uchunguzi wa kina unaendela.... kumsimamisha tu bado hatoshi...
   
 19. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #19
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Hao ni watendaji. Lini wanasiasa nao watasimamishwa?
   
Loading...