Opera Min
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 901
- 658
Katika hali ya kushangaza na hulka za wateule wa Magufuli kujiamria mambo pasipo na weledi Mkurugenzi wa halmashauri ya Lushoto bwana Makwega Kazimbaya ameziua shule zote za msingi na sekondari zisifungwe kwa muhula huu wa kwanza unaoishia mwezi june 2 na hakuna kwenda likizo kwa walimu na wanafunzi wote wabaki shuleni.
Hali hii ni kukiuka utaratibu wa kitaaluma kwamba mihula imewekwa na wataalam ili kuwapa nafasi wanafunzi kupumzika kila wamalizapo nusu muhula na muhula.
Jana tulikua na kikao cha wakuu wa shule na Mkurugenzi, tulibaki midomo wazi kwa ubabe anao utumia huyu jamaa na inaonyesha kabisa anatumia ubabe mwingi kukandamiza watumishi wa halmashauri ya Lushoto. Waziri wa elimu ingilia kati jambo hili la sivyo litachochea vinyongo(ambavyo bado watu wanavyo) na migomo baridi itakayowaumiza watoto wa watu ambao kimsingi hawana hatia.
Chanzo: Ni mimi mwenyewe.