Mkurugenzi IMF atiwa mbaroni tuhuma za jaribio la Kubaka... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi IMF atiwa mbaroni tuhuma za jaribio la Kubaka...

Discussion in 'International Forum' started by Mzee Mwanakijiji, May 15, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 15, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Mkurugenzi wa Shirika la Fedha Duniani Bw. Dominique Strauss-Kahn anahojiwa na Polisi wa Jiji la New York (NYPD) kufuatia madai ya kuhusishwa na kitendo cha shambulizi la kingono dhidi ya mtumishi wa hoteli ambayo alikuwa amefikia Jijini New York. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari Bw. Strauss-Kahn ambaye ni raia wa Ufaransa na ambaye alikuwa anatarajiwa kuwa mgombea wa Urais wa Ufaransa aliteremshwa kutoka kwenye ndege ya Air France muda mfupi kabla ndege hiyo kuruka kuelekea Ufaransa siku ya Jumamosi.

  Kwa mujibu wa vyanzo vya habari mtumishi wa kike wa usafi wa Hoteli ya Sofitel mwenye umri wa miaka 32 amedai kuwa majira ya saa saba mchana (saa za NY) aliingia chumbani kwa Bw. Strauss-Kahn kwa ajili ya kufanya usafi na kujikuta uso kwa uso na Mkurugenzi huyo ambaye alikuwa uchi wa mnyama. Kwa mujibu wa malalamiko yaliyotolewa na mfanyakazi huyo Bw. Strauss-Kahn alijaribu kumuangusha chini na kutaka kumuingia kimwili lakini aliweza kumzidi nguvu na kuponyoka.

  Mara baada ya kuponyoka mtumishi huyo (jina lake limehifadhiwa) alitoa taarifa kwa uongozi wa hoteli hiyo ya kifahari ambao uongozi huo ulitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ambapo maafisa wa Kikosi Maalum kinachochughulikia mambo hayo ya mashambulizi ya kingono (Special Victims Unit) walifika hoteli hiyo ili kufanya uchunguzI. Hata hivyo walipofika walikuta Bw. Strauss-Kahn amekwishaondoka huku akiwa ameacha baadhi ya vitu mbalimbali hotelini hapo na kufanya ihisiwe kuwa aliondoka kwa haraka haraka.

  UchunguzI wa haraka wa NYPD ulionesha kuwa Bw. Kahn alikuwa uwanja wa ndege wa John F. Kennedy na taarifa zilitolewa kwa kikosi cha Polisi cha Mamlaka za Usafiri kilimfuatilia na kumkuta akiwa ndani ya ndege hiyo ambapo waliweza kumtaka ashuke na kufuatana nao kwa ajili ya kutoa maelezo ambayo yataisaidia Polisi kuona kama kuna mashtaka yoyote yanaweza kuletwa dhidi yake.

  Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa Bw. Kahn hata kama itakutwa amejihusisha na kitendo kama hicho asikutwe na mkono mkali wa sheria kwani yawezekana analindwa na Kinga ya Kibalozi na hivyo kitu pekee ambacho kinaweza kufanyika ni yeye kuondoka Marekani. Hadi jioni ya Jumamosi Shirika la Fedha Duniani halikuwa na kauli yoyote rasmi dhidi ya Mkurugenzi wake huyo.

  Miaka minne tu iliyopita kashfa ya mahusiano ya kingono ilimkumba Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Bw. Paul Wolfowitz ambaye alidaiwa kumpandishia mshahara kinyume cha taratibu mpenzi wake Shaha Riza. Pamoja na kashfa hiyo na nyingine ambazo zilimkuta Bw. Wolfowitz alilazimika kujiuzulu nafasi yake hiyo mwezi Mei 2007. Maoni ya wadadisi wa masuala ya uwajibikaji yanaonesha kuwa uzito wa tuhuma hidi dhidi ya Bw. Strauss Kahn vitasababisha ajiuzulu nafasi yake aibu na kupoteza hata uwezekano wa kuwa Rais wa Ufaransa.

  Bw. Kahn amekuwa na uhusiano wa karibu na serikali ya Tanzania katika kuisaidia kwenye sera zake mbalimbali za Uchumi. Mwaka 2009 alikuwa ni mmoja wa wageni mashuhuri katika Mkutano wa IMF uliofanyika nchini ambao Rais Kikwete alikuwa ni mwenyeji wake.

  Bw. Strauss-Kahn ambaye ni mjamaa amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi huko Ufaransa ikiwa ni pamoja na Uwaziri wa Viwanda na Uwaziri wa Fedha. Ameoa na ana watoto wanne.

  [​IMG]


  Strauss-Kahn (kushoto), Rais Kikwete na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan. (Picha na IMF)


  Kutoka http://www.FikraPevu.Com
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Du!!!!!
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  May 15, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nyambala bolebole?
   
 4. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,972
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Eee, na JK yumo au picha imekosewa?
   
 5. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #5
  May 15, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,601
  Likes Received: 6,767
  Trophy Points: 280
  Historia inatuleza, pindi unapokwenda kinyume na Masilahi ya wakubwa, kusukiwa zengwe huwa ni silaha mojawapo ya kukumaliza!!!, hususan zengwe hili la ngono ni tego gumu kweli kulivuka kwa wanaume Wengi!!!. anyway sijui A wala B ya hiyo ishu ya huyo jamaa, lakini usije ukakuta jamaa wamemlia timing kummaliza!.
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yaani mkuu, nimebaki speechless.....
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  May 15, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tayari mmeshaanza conspiracy theories! Yale yale ya Osama is still alive.......
   
 8. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #8
  May 15, 2011
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kweli Dr. Strusss sasa amekuwa stressed out mpaka anashindwa kucontrol zipu yake. Huu kweli ni muziki maridadi kwa Presidaa Sarkozy.
   
 9. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #9
  May 15, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,601
  Likes Received: 6,767
  Trophy Points: 280
  angalia usije ukawa unafauata "official conspiracy"!. always try to look things in more than one dimension!.

  Huyu jamaa simjui, lakini ninakwambia Nyambala, ukimess na wakubwa utaiona joto ya jiwe,watajaribu kukunyonga kwa kamba hiyo hiyo ya udhaifu wako, wakishindwa wanakumaliza upotee kabisa katika anga zao!.

  baada ya kusema hivyo simaanishi najua kinachoendelea huko IMF, lakini najaribu kuangalia mambo katika angle nyingi tofauti tofauti. siku hizi nimeacha kujump kwenye bandwagon za habari kutoka kwenye TV na magazeti, najaribu "za kuambiwa nachanganya na za kwangu".
   
 10. Niko

  Niko Member

  #10
  May 15, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  This is the second time since he took the helm of the IMF in November 2007 that Strauss-Kahn has faced allegations of misconduct.

  In 2008, he had a relationship with Piroska Nagy, a female economist at the IMF, who quit in August of that year. An investigation by the IMF board, released in October 2008, concluded that while he had made a "serious error of judgment," he shouldn't be fired.

  Strauss-Kahn apologized to his staff and family, which includes four children from two previous marriages.
   
 11. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #11
  May 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  MMMMMMhh then kuna mueleko wa kuhusika............kwa nini a-rush eapoti ikiwa he was clean?
   
 12. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #12
  May 15, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,533
  Likes Received: 2,114
  Trophy Points: 280
  May 14th, 2011. New York.

  The IMF head Mr. Dominique Strauss- Kahn has been charged with the sexual assault of a hotel maid, after he was arrested and removed from a plane on the tarmac of John F. Kennedy Airport.

  [​IMG]
  File Photo (March 2009) - Strauss-Kahn in Tanzania attending a two-day conference that brought together a diverse group of participants examining the unprecedented challenge for African policymakers posed by the current global financial crisis.

  Dominique Strauss-Kahn (French pronunciation: [dɔminik stʁos kan]; born 25 April 1949), often referred to as DSK,[1] is a French economist, lawyer, and politician, member of the Socialist Party of France (PS). He was selected as the new Managing Director of the International Monetary Fund (IMF) on 28 September 2007 with the backing of Nicolas Sarkozy.
  He is full professor of economics at the Paris Institute for Political Studies ("Sciences Po").
  Strauss-Kahn was Minister of Economy and Finance from 1997 to 1999 as part of Lionel Jospin's "Plural Left" government. He belongs to the center-left wing of the PS and sought the nomination in the primaries to the Socialist presidential candidacy for the 2007 election, but he was defeated by Ségolène Royal in November 2006.
  On 14 May 2011, Strauss-Kahn was arrested in New York following an allegation of sexual assault and subsequently charged.[2][3][4]
   
 13. M

  Mutambukamalogo JF-Expert Member

  #13
  May 15, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Pesa ukiwa nazo nyingi matatizo,na ukiwa hauna matatizo zaidi!
   
 14. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #14
  May 15, 2011
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Kweli matajiri hawaishi vituko. Yaani Stess-Khan spends $ 3000 per night to sleep, kiwango cha kumuwezesha Mtanzania wa kima cha chini kuishi kwa miaka kadhaa, halafu unaenda kubaka a maid ambaye labda analipwa $ 12 kwa saa. Wacha hii Dunia ijiishie May 21st!
   
 15. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #15
  May 15, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,932
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Haya mambo sijui yapoje! Wanaume wengi waliofanikiwa katika nyanja mbalimali mara nyingi wanaanguka katika kashfa kama hizi au ndoa zao zinakuwa na mushkeli!
   
 16. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #16
  May 15, 2011
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,276
  Trophy Points: 280
  Hii inasemwa kwamba ni moja ya mbinu za mchezo mchafu unaofanywa na raisi wa France Nicolas Sarkozy ambae umaarufu wake umezidi kudorora kuelekea uchaguzi wa rais nchini humo.

  Bwana Dominique Strauss-Kahn ambae ana umri wa miaka 62 anatarajiwa kugombea uraisi nchini Ufaransa unaotarajiwa kufanyika mwakani.

  Strauss-Kahn alipata sifa mwaka 2008 kwa kuliongoza vema IMF kupita kwenye wakti mgumu kiuchumi na baade kwenye mwanguko mkuu wa kuchumi duniani "global recession".

  Pia hivi karibuni mzee huyo mtaalam wa uchumi alibuni mpango wa kuzinusuru nchi kadhaa za Ula kama Ireland na Greece kuepukana na kufilisika kiuchumi kwa kuchangisha fwedha za kuweka uwiano unaoridhisha kwenye uchumi wa Ulaya.

  Lakini huyu mzee ambae ameoa na ana watoto wanne, anapenda mabinti na pale binti yoyote anapoonesha dalili za kuvutiwa nae mzee huweweseka na ndio inasemekana mtego ukawekwa hapo.

  Raisi Sarkozy aliposhinda uraisi alimpigia debe mzee huyu ili apate kazi IMF ikiwa ni kumuondoa kwenye ulingo wa siasa nchini Ufaransa.

  Strauss-Kahn ambae aliwahi kuwa mhadhiri wa uchumi ni mjamaa na ni mwanachama wa chama cha Socialist na amewahi kuwa meya wa mji wa Sarcelles ambao umejaa wahamiaji. Pia amewahi kuwa waziri kwenye serikali ya raisi Francois Mitterrand.
   
 17. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #17
  May 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,944
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nahisi ni mtego.Kama dogo dogo ni udhaifu wake,basi inawezekana kabisa wakawa wamemtega since ana ambition ya kuwa rais.Wakati anaelekea kwenye kampeni zake za urais,wamemzulia NY police.
   
 18. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #18
  May 15, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180

  hakubisha hodi ama kumjulisha ujio wake?maana ni VIP huyu...au aliingia kama guest zetu za uswaz??
   
 19. k

  kagamba kadogo Senior Member

  #19
  May 15, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  viongozi wetu wengi wanafanya kwa dada zetu na hawasemi kitu maana wanajua kutembea na kigogo ndo kuyatoa maisha, mademu wa kizungu wanajua haki zao.... Ingekuwa amina au asha au brenda jamaa angekula kiulaini na tigo angepewa ya kumwaga
   
 20. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #20
  May 15, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  mtego wa totoz ni mbaya sana.wachache sana wanaweza kuchoropoka hapo!
   
Loading...