comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Tao Zhang amewasili nchini kwa ziara ya kikazi na kupokelewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango.
Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Fedha, imesema Zhang amewasili leo akiwa pamoja na Maofisa wengine waandamizi wa Serikali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Akiwa nchini, Tao Zhang,atafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam
Pia Zhang atawasilisha mtazamo wa IMF kwa wadau hapa nchini kwa lengo la kuifanya Tanzania kuwa na maendeleo endelevu, kuimarisha uchumi mkubwa (Macroeconomy) na kuwa na uchumi shirikishi.