Nzelajape
Member
- Nov 7, 2019
- 12
- 9
Nawasalimu wanajukwaa.
Bila kupoteza muda, naleta hoja yangu kwa DED MAGU; itokanayo na hotuba yake aliyoitoa majuzi kwenye semina ya mtihani wa darasa la nne kwa waalimu wa shule za msingi.
Kati ya mengi uliyoongea, ulimzungumzia pia Mwl. Mary Maganga wa Magu S/Msingi, ukionyesha kuridhishwa na utendaji wake shuleni hapo na kusisitiza kwamba hutamwondoa licha ya kuandikwa kwenye mitandao ya kijamii.
DED; yaliyoandikwa awali kuhusu huyu mwalimu unayajua na jamii inayajua, ni kweli yalitokea na mengine yanaendelea kutokea.
Alihamishwa kutoka Nyanguge kwenda Nyambitilwa kwa sababu ya migogoro na jamii; akahamishwa kutoka Nyambitilwa kuja Magu kwa sababu ya migogoro na jamii mpaka watu wa Nyambitilwa kufikia hatua ya kumchomea ofisi.
Hapo Magu S/Msingi amelalamikiwa kwa mambo mengi kutokana na uongozi wake usiofaa, ikiwa ni pamoja na kushindwa kufanya kazi na Kamati ya Shule; kamati ambayo ipo kimuundo wa wizara, lakini Mwl. huyu ameipuuza hata kufikia hatua ya wanakamati kumsusia.
DED; wewe uliona ni sawa watoto hadi wadogo wa darasa la II kwenda kuteka maji bwawani kwa kuvuka barabara bila kuwa na mwalimu wa kuwasindikiza?
Unajua matokeo yake, kwamba watoto wawili waligongwa wakati wakivuka barabara kwenda kuchota maji.
Hilo likitokea, shuleni kuna bomba la maji lakini lilikuwa halitoi maji eti kwa sababu mita iliibiwa! Ufumbuzi ulikuwa ni kutuma watoto wakachote maji bwawani badala kuwekwa mita nyingine?
Mbona baada ya watoto kupata ajali wakienda bwawani kuchota maji mita iliwekwa? Mlikuwa mnasubiri watoto wetu waumie ndipo mchukue hatua?
Usiendelee kutunanga wana-Magu kwa sababu ya utendaji mbovu wa Mwl. Maganga kwa kusema eti hutamtoa! Usimtoe, tutamtoa!! Mbona Nyambitilwa walimtoa, unadhani sisi tunashindwa? Sisi hatuchomi mali za shule wala za yeyote, lakini tunafuata taratibu zingine, maana wewe huoni kwamba huyo mwalimu anaumiza jamii ambayo wewe ni mkurugenzi wake, msimamizi wa maendeleo yetu lakini umetupuuza na umeamua kumlinda mtumishi mwenzako at our expense!
Waraka wa elimu ulishatoka siku nyingi kuhusu waalimu wakuu kwamba wanatakiwa kuwa wenye stashahada (Diploma); waalimu walisisitizwa kujiendeleza na waalimu wengi wamefuzu na kupata stashahada, wengine mpaka shahada za elimu wanazo.
Badala ya waalimu hawa wenye sifa stahiki kuwapa madaraka ya ualimu mkuu, halmashauri yako imeendelea kuwakumbatia waalimu wakuu wenye vyeti (certificate), badala ya diploma na degree (kama waraka unavyoagiza)
Halmashauri nyingi zimeshawaondoa waalimu wakuu wasiokuwa na diploma au degree; Magu mnasubiri nini wakati hilo ni agizo na kisera?
Mnawavunja moyo waalimu waliojiendeleza na kufaulu; wapeni haki zao za ualimu mkuu.
Kila mtu anayejiendeleza kielimu anafanya hivyo ili kuboresha maisha yake, siyo abaki palepale. Hata wewe DED na maofisa wako wote hapo wilayani, mlijiendeleza kielimu ili mpande madaraja na mpate maslahi bora kazini. Kwa nini mnawabania wenzenu? It's not fair!
Inawezekana mnaogopa challenge kama mtawapa madaraka waalimu wenye sifa stahiki; maana hiyo idara ya elimu Magu DC vilaza ni wengi. Ndio maana mnawakumbatia waalimu wasiokuwa na sifa maana mnaweza kuwaendesha mtakavyo; mnawapoka posho zao, mnawalazimisha kugharamia mitihani, michezo na matumizi mengine ya shule kwa posho zao! Wananyenyekea, wanatii maagizo yenu batili kwa sababu wanajua wamekalia viti visivyokuwa vyao!
Naamini DED Magu DC utachukua hatua stahiki badala ya kutoa mipasho vikaoni; unawaumiza waliochukua hatua ya kujiendeleza, watendee haki.
Good day.