Katika kuonesha kukaidi maagizo ya waziri wa elimu Bi Joyce Ndalichako, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Masasi Bi Getrude Gimbana ameamua kuwahamisha walimu 55 kutoka shuile za sekondari kwenda shule za msingi
Ikumbukwe kuwa waziri Ndalichako amekuwa akipinga wazo hile kwa kile kinachoelezwa halitaleta ufanisi, huku mheshimiwa Rais JPM akisisitizwa kulipwa kwa stahiki zote za mtumishi kabla ya kuhama
Katika kikao alichofanya na walimu hao juzi Ijumaa, mkurugenzi huyo alieleza uamuzi wake huo, huku walimu hao wakipinga maamuzi hayo na kuelezea tatizo la rushwa, upendeleo na urafiki kutumiwa na wakuu wa shule kupendekeza majina yao. pia walimu hao wameonyesha wasiwasi kama haki nzao zitazingatiwa, ikiwemo malipo ya uhamisho hivyo kuiomba TAKUKURU ifanye uchunguzi
wakati huohuo, wanafunzi katika shule mbalimbali wamepinga uamuzi huo uliojaaa utata, huku wale wa Shule ya Masasi Girls wakiendesha mgomo hapo siku ya jumamosi kupinga kuondolewa kwa mwalimu wao tegemeo wa somo la Historia kwa kile kinachoelezwa chuki binafsi za mkuu washule
Haya sasa, hao ndio wakurugenzi wanaomuangusha mheshimiwa rais hivyo kumfanya aonekane mbaya kwa kukaidi maagizo yake na wateule wake
More to follow.....