Mkurugenzi halmashauri ya manispaa ya dodoma tusaidie wafanyakazi wako tunadhulumiwa

Aman Ng'oma

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
954
510
Ni wafanyakazi wengi unakuta wametimiza muda wa kupata promotion lakini hawapewi promotion wakati promotion ni haki ya msingi ya mfanyakazi.Hebu fikiria wafanyakazi wenzao wote ambao wameajiriwa nao pamoja na wakapangiwa halmashauri nyingine,wao wamepewa promotion hata bila kudai,dodoma manispaa hadi sasa bado kulikoni?Huu urasimu kwa kweli unashusha ari ya kufanya kazi na kujihisi mnyonge,hebu fikiria ugumu wa maisha ya dodoma,ni maumivui kiasi gani mfanyakazi anayapata!Wabunge wenyewe pamoja na mahela yote wanayopata bado wanalia kutokana na ugumu wa maisha ya Dodoma,inakuwaje kwa mfanyakazi wa kawaida?Ni maumivu makali sana. Tunaomba mkurugenzi atazame pia dhulma inayofanywa kwenye halmashauri yake hatujui ni nani anayenufaika,unakuta mfanyakazi ana miaka 4 kazini bado analipwa TGSC2 ambayo alikuwa analipwa akiwa mwaka wa pili wakati wafanyakazi wenzake alioajiriwa nao pamoja ambao wamepangiwa kwenye halmashauri nyingine walipokukuwa mwaka wa tatu walikuwa wanalipwa TGSC3 ambapo kimshahara wanakuwa mbele kwa tsh kama 9300 kwa mwezi.Mwaka wa nne huu wenzao wamepewa promotion toka mwezi wa sita na kuingia TGSD1 LAKINI Manispaa Dodoma bado wanacheza na TGSC2,huu si wizi?hela yeo inakwenda wapi,kwani kisheria kila mwaka mfanyakazi hupanda ngazi level moja na kunakuwa na ongezeko kwa ajili ya upandaji huo.Kwanini hakuna huruma kwa wafanyakazi? Afisa utumishi anaulizwa anasema yeye hajui mambo hayo na anasema pia kuhusu kupewa promotion tusitarajie kwani halmashauri haina pesa ya kukaa ili wapitishe majina ya wafanyakazi wanaostahili kupewa promotion.Ikiwa hivyo ndivyo,mnaona raha gani kuwadhulumu wafanyakazi na kuwafanya wasononeke moyoni? Hilo jasho lao mnalowadhulumu,mnaona ni haki yenu kabisa?Tunakuomba mkurugenzi ambayo tunajua mgeni ndio kwanza umeanza kuitumikia manispaa yetu tusaidie,afisa utumishi anatunyanyasa sana hataki kuwajibika kwetu,tunahisi yeye ndiye anayenufaika na hata haguswi na malalamiko yetu.Isitoshe majibu yake ni ya dharau sana kana kwamba mfanyakazi ni yeye peke yake na wengine sio.
 
Back
Top Bottom