KERO Mkurugenzi Garda World jitafakari, wafanyakazi tumekuchoka

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Udart

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
383
554
Salute.

Naomba niende kwenye maada mimi kama askari (mlinzi) wa kampuni binafsi wa Garda world nimeamua kutumia platform hii kuleta kero ya kiongozi wetu mkuu wa kampuni ya ulinzi Garda world.

Kiukweli kiongozi wetu LuQmay tangu umepata kazi kwenye kampuni yetu sisi kama walinzi upande wa ultimate zamani kiukweli umekuwa tatizo kubwa na ni kero katika ufanyaji kazi.

Kwanza tangu umepata nafasi ya kuendesha kampuni ukitokea tigo hujawahi kuitisha kikao ujue wafanyakazi wako wanapitia shida gani na Nini malengo yako katika kampuni badala yake umekuwa (MUNGU MTU).

Naomba nieleze hapa kampuni ya ultimate kabla yakuwa Gardaworld imepitia mikononi mwa wamiliki wengi na Kila walipokuwa wanaamua kuuza kampuni Kwa mmiliki mwingine tulikuwa tuitwa kinafanyika kikao tunaeleweshwa na karibu hao maboss wote watu Ziballa & shivva nk.

Walikuwa wanafanya press tunajulishwa Kila kitu na walitoa pesa ya Asante nakumbuka nilipokea 1.2m maana nilifanya kazi Kwa miaka kumi na kipindi hicho chote tukiwa ultimate Kila baadae ya miezi sita.

Mkurugenzi aliitisha kikao tukasema kero zetu na zikafanyiwa kazi sasa tangu kampuni ya ultimate iuzwe na kuchukuliwa na Garda world.

Kiufupi tunaona tunaendeshwa kihuni hivi inakuwaje tunaenda kumuona mkuu wa mkoa mh chalmila hatupati ugumu wa kumuona iweje kwako Mkurugenzi ndugu luQmay utuwekee uzibe tusikuone kuleta kero zetu.

Pli kampuni imeuzwa mmiliki ambao ni wazungu wamekupa fedha wafanyakazi walipwe kama fidia ya kubadili mikataba Yao kutoka ultimate kwenda Garda world lakini kutokana na roho yako mbaya unataka kutuzima kinguvu Ili fungu uchukue na ni pesa nyingi ukiweza kutuzima tunaamini utatajirika sana tatu week mbili nyuma umenitisha kikao tumekuja kwenye kikao umetuwekea spika ndani ya ukumbi Yani wewe na team yako ya upigaji munaongea bila kuonekana sisi tunasikia tu kwenye spika mtu hatumuoni it's ok hata kama mmeamua kutufanya wajinga lakini sio Kwa level hiyo kikao.

Kilivyoshindikana ukapanga kikao tarehe Saba ulivyosikia na sisi tunakuja na wanasheria wetu mkaahirisha kikao Kwanini kiongozi LuQmay usijifunze

Kwa wenzio akina Eliuta mwanjawike walikuwa wanakula na kipofu alikuwa hakimbiii wafanyakazi mwisho usifikiri utatuendesha kirahisi kama unavyodhani..

Pia sisi tulidhani wewe mtu mweusi uwe mkombozi wetu Kwa hao wazungu lkn wewe ndio umekuwa mwiba kwetu hata kama ukifanikiwa kutudhurumu it's tutakuombea hata Dua mbaya tu maana mahakamini tukipekeleka kesi tukishinda unakuja kuappeal then uinaweka kapuni na kutishia kufukuza kazi wafanyakazi.

Ila Kwa hili la malipo ya mikataba tutaenda hata ubalozi wa Canada kushinikiza waiitwe wamiliki wa kampuni mwisho jifunzeni G4s na SGA uone kampuni zinavyoendeshwa.
 
Say No to GARDAWADA.
Jeshi la Polisi ambao mnasajili kampuni za Ulinzi take this note kama redflag ya uhalifu ujao.
Wadau/wateja epukeni hii kampuni soon Walinzi/wafanyakazi wataanza kufanya hujuma kulipa kisasi.
Tia kwenye dustbin hii kampuni wakose wateja
 
Back
Top Bottom