Mkurugenzi, Diwani (CCM) wazichapa wakigombea Posho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi, Diwani (CCM) wazichapa wakigombea Posho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mku, Dec 29, 2011.

 1. mku

  mku Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hizi posho zitawatoa macho.......ivi kumbe ukiwa kiongozi wa CCM wewe na posho ni pete na kidole?

  MKURUGENZI wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Lewis Kalinjuna amepigana hadharani na Diwani wa Kata ya Machinjioni (CCM), Salum Akilimali kutokana na kile kilichodaiwa ni kutofautiana kuhusu malipo ya posho ya vikao vya Baraza la Madiwani.

  Ugomvi huo umetokea muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao maalumu cha Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo kilichokuwa kikijadili mgogoro wa kugawa maeneo ya ujenzi wa viwanja katika Kata za Rusimbi, Kibirizi na Buhanda kutokana na ugawaji wa awali kukiuka sheria, kanuni na taratibu.

  Mashuhuda wa ugomvi huo walisema kwamba diwani huyo akiwa na baadhi ya wenzake walimwuliza mkurugenzi huyo kuhusu hatima ya kulipwa posho yao ya kikao kilichofanyika Desemba 23, mwaka huu kilichokuwa kimeitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya.

  Kwa mujibu wa mashuhuda hao, kitendo hicho kilimuudhi mkurugenzi huyo na katika majibizano, alipiga kichwa kumlenga diwani huyo ambaye hata hivyo, alikizuia kwa mikono yake. Baada ya kuona hali hiyo, viongozi mbalimbali waliokuwepo katika eneo hilo waliingilia kati na kuamua.

  "'Mimi nimeshangaa kuwaona wakisukumana na ndipo Mkurugenzi (Kalinjuna) akampiga yule diwani kichwa, hata hivyo, jamaa alikizuia kwa mikono. Kwa kweli ni aibu kubwa hawa jamaa kupigana hadharani, kama wana matatizo yao ni bora wangeyamalizia hukohuko ndani na siyo kuja kutuonyesha ubabe wao hapa,"' alisema mmoja wa mashuhuda hao, Shaaban Juma mkazi wa Ujiji.

  Diwani wa Kata ya Businde, Saidi Maulid alisema kwamba uamuzi wa kumwuliza mkurugenzi kuhusu hatima ya posho zao kwa kuwa hawakulipwa lakini akasema walishindwa kuelewana lugha na ndipo ilipotokea hali ya vurugu.

  "Licha ya kikao chetu cha leo (Jumatano) kwenda vibaya na dhahiri mkurugenzi akiwa katibu wa baraza kuonekana akishindwa kueleza ukweli ndani ya kikao kuhusu mgogoro na ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za kugawa viwanja, bado anaonekana kuwa na chuki binafsi dhidi yetu sisi madiwani wa CCM," alisema Maulid.

  Kauli za wahusika

  Kwa upande wake, Mkurugenzi huyo alisema amekuwa akionewa na madiwani wa CCM ambao wamekuwa wakimshutumu kwa kuwasaidia Chadema katika hoja nyingi zinazoibuka ndani ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, jambo ambalo alisema siyo la kweli.

  Alisema amepigwa bila sababu za msingi kwa vile kama hoja ni suala la kuwalipa madiwani posho zao za vikao, aliwajibu kwamba kwa sasa halmashauri haina fedha na pindi zitakapopatikana, ni wazi kila mmoja atalipwa kiasi anachodai.

  Kwa upande wake, Akilimali alisema licha ya mkurugenzi huyo kumtwanga kichwa kilichoishia mikononi, bado hana kinyongo naye kwa vile hakutaka ugomvi na kupigana hadharani tena mbele ya wananchi na watumishi wa manispaa hiyo baada ya kumaliza kikao cha baraza.

  "Mimi nikimpiga mtu ngumu ni lazima aumie sana, sasa kama ningesema baada ya kupigwa kichwa na mkurugenzi nami nijibu bila shaka yangetokea mambo mengine kwa vile ninajijua nilivyo na nina hakika madhara yangekuwa makubwa sana," alitamba Akilimali.

  Kwa muda mrefu sasa, vikao vingi vya Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kigoma Ujiji vimekuwa vikigubikwa na malumbano ya kiitikadi kati ya CCM na Chadema na kusababisha mgawanyiko ambao umeelezwa kuathiri maendeleo yake.


  Source mwananchi 29.12.2011
   
 2. k

  kicha JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 509
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 180
  dah fedha ni nouma
   
 3. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Mi najitolea kudhamini pambano litavutia saana, na wanaweza kupata pesa Nyingi tu michezo furaha kuliko kupigana hobelahobela kitaa bora wapande ulingoni wapate hela na wamalize hasira
   
 4. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi alipata zawadi ya "Mchapakazi bora" kutokana na uwezo wake wa kupambana na madiwani wa Chadema kuhusu posho.

  Ila hii ya "Kalimazila" imanifurahisha kweli:
  “Mimi nikimpiga mtu ngumu ni lazima aumie sana, sasa kama ningesema baada ya kupigwa kichwa na mkurugenzi nami nijibu bila shaka yangetokea mambo mengine kwa vile ninajijua nilivyo na nina hakika madhara yangekuwa makubwa sana,” alitamba Akilimali.
   
 5. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ndiyo maana tunasema kila siku posho zifutwe! Mtu anaenda kwenye kikao kutekeleza sehemu ya Majukumu yake badala ya kuumiza akili kung'amua hoja zilizo mezani anawaza baada ya kikao atasaini Shilingi ngapi!
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hizi posho zinatupeleka pabaya!
   
 7. Amani Nyekele

  Amani Nyekele Senior Member

  #7
  Dec 29, 2011
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  posho hatari..!
   
 8. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Ngoja siku watakaposhindwa kuwalipa kina FF and company tuone kama wataendelea kutetea magamba hapa ukumbini.
   
 9. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Posho ndio mtaji wa ccm, nawe ni mmoja wa viongozi ccm, ingekuwa hatari mngezifuta kama chadema wanavyopendekeza, cha kushangaza ndiyo mnaziongeza!!!!!!
   
 10. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  kule KIGOMA kuna kitu/vitu huitwa KINGUVU. Ukitumia dawa hizo, ngumi moja ni sawa na kupigwa na kito kizito sana labda tusema nondo ya kilo kumi kupigwa nayo usoni. Hivyo diwani alijua, kama kweli angerudisha mapigo kwa mkurugenzi, kuna uwezekano mzito angelezwa hosptali pale maweni. Kupona kwake ni yeye kuwa sehemu ya utamaduni wa kigoma, kutumia dawa hizo

   
 11. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #11
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Posho zitatugawa!

  Aibu kuuu hii yaani viongozi tunaowaamini washughulikie matatizo yetu wao wanaenda kugombea posho!!
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Aibu yao wenyewe
   
 13. samilakadunda

  samilakadunda JF-Expert Member

  #13
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 1,701
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mafisaaaadiiii! Chapaneni weee,kisha nabungeni wachapaneee! Hadikitaeleweka.walafi wakubwa nyiee msie tambua hata kwamba nchi imefilisika,ni mwaka mmoja tu toka mingie madarakani madeni kibao.achieni nchi wengine muone kamamtapigana.nimempenda diwani kwa maneno yake.
   
 14. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #14
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Haki haiombwi bali inadaiwa...
   
 15. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #15
  Dec 29, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Bora wote wa magamba wanagombea posho hii hatari
   
 16. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #16
  Dec 29, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii habari nimeisoma katika Mwananchi la leo, kwa kweli wana JF nimecheka sana; hasa hapa Diwani Akilimali anaposema
  Nanukuu
  [FONT=Times New Roman, serif]Miminikimpiga mtu ngumu ni lazima aumie sana, sasa kama ningesema baadaya kupigwa kichwa na mkurugenzi nami nijibu bila shaka yangetokeamambo mengine kwa vile ninajijua nilivyo na nina hakika madharayangekuwa makubwa sana,”
  [/FONT]
   
 17. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #17
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  CCM ni laana tupu
   
 18. h

  hans79 JF-Expert Member

  #18
  Dec 29, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  wapi msugu,ffox etc leo hii imekula kwao vidomo domo kimya
   
 19. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #19
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu aibu yao aibu yetu!!

  MAdiwani tumewachagua watuwakilishe kumbe wanaenda kupigania posho. Nadhani wabunge nao muda si mrefu watatwangana juu ya posho!! Hivi huoni kwamba bundi la posho liko Bungeni?
   
 20. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #20
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mabondia wetu wanashindwa kutuletea medali za kimataifa kumbe wenye uwezo huo tunawaacha Kigoma!
   
Loading...