Mkurugenzi ATCL: Ndege ya ATCL ilitengenezwa kwa siku moja na tayari inaendelea na safari zake

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mkurugenzi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladslaus Matindi amesema ndege aina Bombardier Q400 iliyokuwa katika matengenezo imeanza kufanya safari zake kama kawaida.

Ametoa ufafanuzi huo leo Jumatano Agosti 21, 2019 katika kipindi cha Power Breakfast cha Redio Clouds akizungumzia taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zikionyesha picha ya ndege hiyo ikiwa katika matengenezo.

Katika maelezo yake Matindi amesema ndege hiyo ilikuwa na hitilafu na ilitengenezwa kwa siku moja na tayari imerejea katika ratiba zake za safari za kila siku.

“Ndege inaweza kuharibika, kupata hitilafu au kuingiliwa na kitu kutoka nje muda wowote kwakuwa ni mashine hakuna namna ya kuzuia hilo ni jambo la kawaida kwa mashine hata binadamu,” amesema Matindi.

Amesema ndege hiyo ipo Dar es Saalam tangu jana na matengenezo yake yalichukua siku moja, akibainisha kuwa yalianza Jumatatu mchana hadi jana mchana, “Usiku jana iliruka kurudi Dar es Salaam.”

“Ndege zinazoharibika sio za ATCL pekee bali popote hata KLM ndege zao huwa zinaharibika, British Airways na Emirates wakisema ndege zao hazijawahi kuharibika ndipo tujiulize kwa nini zetu ziharibike.”

zaidi, soma;

Tatizo hapa ni kusubiria CEO ndiye kutoa taarifa ambazo ni 'petty' kama hizi, ndio maana naona taasisi nyingi hata za serikari kama NMB Tanzania, TANESCO, nk wana accounts kwenye mitandao yote ya kijamii ili kujibu swala lolote kwa wakati hata kama ni la kizushi au la kijinga maana wajinga pia tupo wengi.
Pia kila taasisi inajulikana kuwa ina msemaji ambaye kimsingi inabidi kutoa briefings za kila siku regardless kuna shida au neema.
 
kuna watu wana roho mbaya sana yaani eti kuna mtu kiushabiki kabisa anaandika ndege imekwama znz siku sijui tatu anasikia rahaaaaaaaaa ni upumbavu kushangilia matatizo ya nchi yako
kwi kwi kwi kwi kwiiiiiiiii :D :D 😂😂😂😂😂
 
Ni wapumbavu na wanafiki wachache ambao hufurahia mali za umma zinapopata dosari, embu watanzania tuache kuwa wapumbavu kuwa na furaha pindi pale mali za umma zinapoapata hitilafu, Na mabya zaidi chuki hizo kwa mali za umma zinahamishiwa kwa Mh. Rais...

Niwakumbushe tu, Mh Rais ataondoka ataziacha hizi ndege zikiwatumikia watanzania, Embu watanzania tufike mahali tujaribu kuwa wazalendo na kuwa na uchungu na mali zetu bila kusahau kuzipenda pia...
 
kuna watu wana roho mbaya sana yaani eti kuna mtu kiushabiki kabisa anaandika ndege imekwama znz siku sijui tatu anasikia rahaaaaaaaaa ni upumbavu kushangilia matatizo ya nchi yako
Inareflect utashi wetu hata kwenye maisha yetu ya kawaida wako watu wana tabia ya kushadadia matatizo ya wengine!
 
Ni wapumbavu na wanafiki wachache ambao hufurahia mali za umma zinapopata dosari, embu watanzania tuache kuwa wapumbavu kuwa na furaha pindi pale mali za umma zinapoapata hitilafu, Na mabya zaidi chuki hizo kwa mali za umma zinahamishiwa kwa Mh. Rais...

Niwakumbushe tu, Mh Rais ataondoka ataziacha hizi ndege zikiwatumikia watanzania, Embu watanzania tufike mahali tujaribu kuwa wazalendo na kuwa na uchungu na mali zetu bila kusahau kuzipenda pia...
Wewe acha kutumia neno watanzania kama vile wote hatuna akili kama wewe, huo ni ujinga uliopigwa brashi
 
Ni wapumbavu na wanafiki wachache ambao hufurahia mali za umma zinapopata dosari, embu watanzania tuache kuwa wapumbavu kuwa na furaha pindi pale mali za umma zinapoapata hitilafu, Na mabya zaidi chuki hizo kwa mali za umma zinahamishiwa kwa Mh. Rais...

Niwakumbushe tu, Mh Rais ataondoka ataziacha hizi ndege zikiwatumikia watanzania, Embu watanzania tufike mahali tujaribu kuwa wazalendo na kuwa na uchungu na mali zetu bila kusahau kuzipenda pia...
asante sana mkuu umenisaidia maana kuna mipumbavu humu inafurahiaga kweli kusikia kitu kimeharibika
 
Back
Top Bottom