Mkurugenzi asusia, madiwani wa CDM waendelea na kikao-Moshi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkurugenzi asusia, madiwani wa CDM waendelea na kikao-Moshi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Quinine, Apr 21, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,859
  Likes Received: 11,978
  Trophy Points: 280
  MGOGORO wa kugombea mali za Halmashauri ya Moshi zinazodaiwa kumilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana ulichukua sura mpya baada ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Bernadette Kinabo, kususia ajenda hiyo na kutoka nje ya kikao cha baraza la madiwani.

  Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa nne asubuhi wakati wa kikao hicho maalumu na kuwalazimu madiwani wa CHADEMA kumchagua katibu wa muda wa kuendesha kikao hicho.

  Wakati hali ikiwa hivyo ndani ya halmashauri, nje ya eneo hilo na mitaa mbalimbali ya mji wa Moshi polisi waliweka ulinzi mkali na kufunga barabara kwa kile kilichoelezwa kuwa walihofia vurugu zingetokea.

  Kikao hicho awali kilikuwa kifanyike Machi 31 mwaka huu lakini kilishindikana baada ya Mkurugenzi huyo kukiahirisha kwa kile alichoeleza kuwa kungeweza kutokea kwa vurugu.

  Mkurugenzi huyo ambaye ni katibu wa kikao hicho alitoka wakati walipokuwa wakithibitisha ajenda za kikao hicho ambapo alitaka ajenga namba 7 iliyokuwa inahusu kujadili majengo ya manispaa hiyo yanayokaliwa na CCM isijadiliwe kwani tayari alikuwa na maagizo ya mahakama (court order).

  Kinabo alisema barua hiyo ya mahakama aliipokea siku iliyopita saa tisa alasiri, hivyo akataka kikao hicho kisijadili hoja hiyo, ambapo Meya wa manispaa hiyo, Jafar Michael, aliyekuwa akiendesha kikao hicho aliamua kusikiliza maoni ya madiwani.

  Mwanasheria wa halmashauri hiyo ambaye ni mgeni aliyetambulishwa kwenye kikao hicho, Deograsius Nyoni, aliwasomea madiwani ‘oder’ hiyo iliyoweka zuio la kuhamisha au kuharibu mali kwenye viwanja namba 54 Block BBB na namba 19 Block B, ambavyo vinakaliwa na CCM.

  Alisema shauri hilo linalosikilizwa na Jaji wa Mahakama Kuu, Stella Mgasha, lilifunguliwa Aprili 13 mwaka huu na bodi ya wadhamini wa CCM kupitia mwanasheria wao, Beth Minde, ambapo mshitakiwa pekee kwenye shauri hilo ni mkurugenzi wa halmashauri.

  Alifafanua kuwa CCM iliomba malalamiko yao kusikilizwa kwa shauri hilo kwa hati ya dharura ambapo mahakama iliyasikiliza Aprili 14, mwaka huu sasa 8 mchana lakini usikilizwaji huo ulifanyika kwa upande mmoja.

  Alisema kuwa maombi hayo ya CCM yaliyowasilishwa mahakamani yalilazimika kusikilizwa kwa haraka kuhofia maamuzi ya kikao cha baraza la madiwani wa Manispaa ya Moshi kilichokaa jana Aprili 20, huku mwanasheria akitaka kutojadiliwa kwa ‘oder’ hiyo ya mahakama.

  Mwanasheria huyo alifafanua kuwa ‘oder’ hiyo inaelekeza kutofanyika kwa shughuli yoyote kwenye viwanja hivyo ambavyo kesi ipo mahakamani.

  Baada ya maelezo hayo kutoka kwa mkurugenzi, madiwani walitakiwa wajadili kwa pamoja juu ya kuondolewa kwa hoja namba 7 kwenye kikao hicho, hali ambayo ilikuwa vigumu kwa madiwani wa CHADEMA kukubali maamuzi hayo ya mkurugenzi ya kuondolewa kwa hoja hiyo huku wakitaka badala ya kujadili ajenda hiyo basi wajadili ‘order’ iliyotolewa na mahakama ili waone namna watakavyokabiliana na kesi hiyo.

  Pia madiwani walihoji juu ya kutopatiwa ‘oder’ hiyo siku iliyopita kwani walikuwa kwenye kikao cha awali cha baraza la madiwani ambacho kilidumu mpaka saa 12 jioni kama kweli mkurugenzi alipata barua hiyo saa 9 alasiri.

  Baada ya kutoa maelezo ya kuondolewa kwa hoja namba 7, mkurugenzi huyo alisema kuwa yeye ndiye mtendaji wa serikali na anachotaka ni vikao hivyo vifuate utaratibu na hatimaye kunyanyuka na kutoka nje ya kikao.

  Baada ya mkurugenzi kutoka nje na kufuatiwa na wataalamu wa halmashauri na madiwani wa CCM, madiwani wa CHADEMA waliendelea kukaa ndani ya ukumbi huo wakijadiliana ni nini kifanyike ili waweze kuendelea na kikao.

  Baada ya kujadiliana walikubaliana kuahirisha kikao kwa muda ili wamwandikie barua mkuu wa mkoa aweze kuwapatia katibu atakayeweza kuendelea na kikao. Hata hivyo, baada ya saa mbili kupita waliingia kwenye ukumbi majira ya saa saba mchana na kuendelea na kikao.

  Meya huyo alisema baada ya kupitia kanuni za kudumu za halmashauri hiyo walibaini kuwa wanaweza kuendelea na kikao kwa kuchagua katibu wa muda baada ya kubaini kuwa hakuna kifungu kinachowazuia kumchagua katibu au kutomchagua.
  Alisema kuwa madiwani ndio wenye maamuzi ya kuweka hoja na kuiondoa na katika kikao cha baraza walitaka kupitisha maazimio ya kufuta maazimio ya awali yaliyotolewa ya kuwamilikisha CCM majengo ya halmashauri.

  Hoja iliyotakiwa kuondolewa ni ile ya kujadili viwanja viwili, kiwanja chenye namba 056038/94 ilipo ofisi ya wilaya ya CCM na namba 15686 ilipo ofisi ya UVCCM mkoa.
  “Lengo la Mkurugenzi kutoka nje ya kikao ni kutaka CHADEMA waonekane kuwa wana vurugu na sisi hili tutaliepuka, na baada ya hapo endapo akifanikiwa kwa kisngizio hicho basi baraza hili la CHADEMA livunjwe ...lakini CHADEMA kwa hili hatupo tayari,” alisisitiza Jafari.

  Katika kikao hicho ambacho walimchagua Diwani wa Kata ya Longuo B, Raymond Mboya, kuwa katibu wa muda, walipitisha maazimio matatu, ikiwemo madiwani kuwa sehemu ya kesi iliyofunguliwa na CCM dhidi ya mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Moshi.

  Diwani wa Kata ya Bondeni, Abdulrahman Sharif, alisema lengo ni kumdhibiti mkurugenzi kwa kuhofia kufikishwa mahakamani na kukubali kuwa mali hizo ni za CCM pamoja na kumtafuta wakili kwa ajili ya kesi hiyo.

  Azimio jingine walilolipitisha ni la kumpeleka mkurugenzi kwenye kamati ya maadili kwa kile walichoeleza kuwa ni kudharau kikao kwa kutoka na watendaji na kumuacha mweyekiti huku kikao kikiwa bado kinaendelea, ambacho kitakuwa na wajibu wa kupeleka mapendekezo kwa mwajiri wake au waziri mwenye dhamana kwa ajili ya utekelezaji.

  Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, alisema mkurugenzi huyo alitoka nje kwa hoja kuwa ‘order’ ya mahakama haipaswi kujadiliwa lakini maelezo hayo hayana hoja, kwa sababu kilichotaka kufanywa si kujadili ‘order’ bali kujadili jinsi ya kukabiliana na kesi hiyo.

  Ndesamburo alisema kulikuwa na haja ya kujadili juu ya kuweka wakili kwenye kesi hiyo ambayo walisema hawataki kutumika kwa mwanasheria wa halmashauri hiyo, ambaye ndiye kwanza wamemuona jana pamoja na kumuweka kando mkurugenzi kwenye suala hilo baada ya kuonekana kuwa na masilahi binafsi.

  Polisi wengi wenye silaha walionekana maeneo ya kuzunguka halmashauri hiyo huku Barabara ya Florida inayotumiwa kuingia kwenye jengo la mkuu wa mkoa, manispaa na kituo cha uwekezaji nchini (TIC) zikiwa zimefungwa kuanzia saa nne asubuhi hadi saa 8:30 mchana.
  Hali hiyo ilisababisha usumbufu kwa wananchi kutokana na kuwa barabara hiyo inatumika kuelekea maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi na viunga vyake.

  Kwa upande wake, Kinabo akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake baadaye, alisema kuwa aliamua kutoka kwenye kikao hicho baada ya kuona hapewi nafasi ya kuongea pamoja na madiwani wa CHADEMA kuamua kujadili ‘oder’ ambayo kisheria hairuhusiwi kujadiliwa.
   
 2. Chilipamwao

  Chilipamwao JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  bila shaka mkurugenzi huyo ni mwana ccm na hapo amekalia kuti kavu. hapo moto ni mkali na CHADEMA ni mwendo mdundo.
   
 3. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #3
  Apr 21, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  WanaJF,
  Huu sasa ni uharamia. Sina hakika kama Jaji Stella alishinikizwa au vipi, lakini uharaka huo wa klusikiliza shauri hilo upasnde mmoja una sura ile ile ya mwaka 1993. Ninao ushahidi kuwa tarehe 1 Julai 1993, Mfumo wa vyama Vingi ulipoanza rasmi kwa mujibu wa sheria No 5 ya 1992, CCM ilituma wataalamu wake kuzunguka nchi nzima kuandikisha mali walizoziita za CCM. Kwa wale wasiokumbuka Tume ya Nyalali ambayo ndio mwanzo wa vyama vingi (awamu ya pili TZ), ilisema mali zote zilizotokana na jasho la wananchi wote, irudishwe Serikalini ili iwanufaishe watanzania wote, kwa msingi kuwa mambo yote yalifanyika na watanzania wote kwa kuwa wakati huo viongozi walikuwa na kofia mbili, ya TANU/CCM na utendaji wa Serikali. Hivyo mambo mengi yalichangiwa na wananchi wote. Kati ya Julai na September 1992, wataalamu hao walipopita kila wilaya walifika kwa viongozi wa serikali ngazi zote ambao wote walikuwa bado na kofia ya CCM na utendaji wakaorodhesha, bila kuhusisha chombo chochote, wala wananchi hawakushirikishwa kutoa maoni yao kuhusu mali hizo. Wakaandikisha nyumba, ploti, mashamba, ofisi yote yaliyojengwa na wananchi wote kama mali ya CCM. Ndiyo maana, CCM Moshi ndio inaanza kuhangaikia Hati Miliki sasa. Kama walikuwa na haki nayo ni kwanini hawakutafuta hati toka wakati huo? Ushauri wangu kwa wananchi wa Moshi wajitokeze kueleza jinsi ploti hizo na majengo hayo yalivyojengwa, kikao ganmi kiliuzia CCM na kwa Kumbukumbu ya kikao gani. Karatu tulikuwa hivyo hivyo. Maeneo mengi(vijiji) ambayo Chadema imetawala toka mwaka 2000 wananchi wameisha kurudisha mali zao mikononi mwa serikali za vijiji kama ilivyopendekezwa na Tume ya Nyalali. CCM walijaribu kwenda mahakamani kudai kuwa mali hizo k.m Zahanati ya Kijiji cha Gongali, Ofisi ya Kijiji cha Ayalabe, Ofisi ya kijiji cha Kilimamoja na mashamba mengi. Kesi zote hizo zilikufa katika hatua ya PH/PO kwa kushindwa kuonyesha uhalali wa umiliki wao kwa kuonyesha walipataje, kikao kilichowauzia au kuwagawia n.k. Madiwani wa Moshi kazeni buti, ukombozi wa mali zetu umekaribia kwa nchi nzima. Hatuwezi kamwe kuruhusu uvamizi wa mali ya watanzania kwa kuwa tiu waklati huo ccm ilikuwa chama pekee, na wote tulilazimika kufanya kazi chini ya mwavuli wa chama hicho kimoja. Alimradi mkifanikiwa kuzirudisha msiziweke chini ya Chadema bali Serikali ya Wilaya ili chama chochote kitakachokuwa kinatawala kwa wakati wowote ule waweze kutumia mali hizo, au vijana wa Watanzania bila kubagua itikadi zao watumie mali hizo.Mkurugenzi Kinabo ni kada wa ccm, na tunazo nyaraka kuonyesha hivyo, mathalan alipokuwa DED Singida vijijini aliagiza na kuchangisha fedha kupitia watendaji wa Kata na vijiji kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa CCM Dodoma. Kama anabisha atoke hadharani tumshughulikie. Yeye kama Municipal Director hapaswi kuwa mtetezi wa CCM. Kama kesi iko mahakamani na Halmashauri ndiyo inayoshitakiwa alipaswa kushikamana na Madiwani kulinda mali ya Halmashauri. Anashangaza sana kusimama upande wa CCM. Hafai kabisa kuwa mlinzi na mwenye dhamana ya mali ya wananchi wa Manispaa ya Moshi. Madiwani msirudi nyuma achukuliwe hatua anamaliza muda wake vibaya aende kustaafu vibaya.   
 4. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hawa CCM mbona kila kukicha wao ni kutapatapa tu? Hivi kwa nini hakuna hata jambo la kujivunia kwao ambalo wanalifanya kwa kufuata sheria na misingi ya haki sawa kwa watu na vyama vya siasa?
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,859
  Likes Received: 11,978
  Trophy Points: 280
  Asante Dr Slaa.

  Huu ndio ujanja unaotumiwa na CCM siku zote waliahirisha kikao cha trh 31/3 kwa kisingizio cha vurugu ili wakimbilie mahakamani kwa hati ya dharura. Lakini naona hawa wanacheza na moto ninauhakika there is one day mali zote walizozitaifisha toka kwa wananchi zitarudi mikononi mwa wenyewe it is just matter of time.
   
 6. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #6
  Apr 21, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  DR SLAA,

  Kwa nini CHADEMA na vyama vya upinzani wasiungane kuishtaki ccm mahakamani kurejesha mali zote walizohodhi wakati wa mfumo wa chama kimoja na hawakuzirejesha serikarini baada ya mfumo wa vyama vingi? au tunaweza kufungua kesi kama wananchi tuliongana kuidai ccm kurejesha mali ya umma?
   
 7. M

  Mary Chuwa Senior Member

  #7
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Dr Slaa aksante sana kwa kuendelea kutufungua macho,naamini kabisa wakati wa Ukombozi wa Watanganyika na Nchi yao ni sasa,kila la kheri kwa madiwani wa CDM-Moshi,huo ni mwanzo na mwendelezo mzuri kila mtu afaidi kilicho halali yake.
  Mkurugenzi huyu kilio cha kusaga meno kinamngoja hatutachoka kumwomba Mungu awalinde wapiganaji wetu.
  Kila la kheri
   
 8. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #8
  Apr 21, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280

  Muheshimwa ..hili suala la kudai mali za wananchi zirudishwe kwenye halmashauri husika lipewe umuhimu...vijana wengi hawajui kuwa mali hizi tumezijenga kwa kuchangishwa tena hadi kwa nguvu ,kuanzia watoto wa shule,wafanyakazi,askari,kodi kwenye bidhaa,na hadi kazi za msaragambo za kujenga Taifa....haingilii akilini kweli leo hii kundi dogo la watu watake kuzimiliki wao tu....na sehemu nyingi viwanja vimejeuka malisho ya Ngombe kwa kuwa chama kimeelemewa na hakina mpango maalum wa estate development....jibu ni moja MALI ZOTE ZIPELEKWE KWENYE HALMASHAURI ZIENDELEZWE....kama ambavyo Chimwaga ilivosaidia kuanzisha chuo kikuuu dodoma.....tuliichanga wote kujenga chimwaga.....

  Natoa Rai kwa viongozi na wananchi wote mikoani wazitambue mali zote zilizopatikana kwa nguvu na ccm ambazo zilijengwa kwa jasho la wananchi.....WANAHARAKATI WAFUNGUE KESI YA KITAIFA YA KUDAI MALI ZA WANANCHI wasiachiwe wakazi wa Moshi ,na Iringa[wanaodai uwanja wa samora]...list iendeleee..

  Tunataka viwanja vya ....MAJIMAJI,SAMORA,ILULU,VITA,ALI HASSAN MWINYI,LAKE TANGANYIKA,KAITABA,CCM - KIRUMBA,NYERERE[MARA],KAMBARAGE[SHY],SINGIDA,JAMHURI DOM,JAMHURI MORO,MKWAKWANI ,SHEIKH AMRI ABEID,NYERERE - MBULU,MEIMORIAL STADIUM [under construction MOSHI],SOKOINE [mbeya].....Tunataka na ofisi na majengo mengine yote yaliyopatikana kwa njia ya kujenga Taifa.....
  KAMA KWELI CCM WANATAKA KUJIVUA GAMBA WAKATAE NA UFISADI HUU WA KUNGANGANIA MALI ZA UMMA...WAZIKABIDHI KWENYE HALMASHAURI HUSIKA....na hawatanyangannywa chochote walichopata baada ya 1992!
   
 9. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #9
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Nawashauri madiwani wa moshi wamkatae mkurugenzi,
   
 10. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Watu wa Moshi wataonyesha nia ya jisni ya kurudisha mali ya umma iliyoporwa na ccm. Siku inakuja ambapo hata ccm yenyewe itafutwa katika vitabu vya kumbukumbu kama kile chama cha Ben Ali w Tunisia!
   
 11. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  moshi tunaomba muwe chachu ya ukombozi.
  huyo mkurugenzi awe ni mfano kwa wote.
   
 12. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #12
  Apr 21, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Nadhani sasa utetezi wa haki za Watanzania usiachwe mikononi mwa CHADEMA peke yao, kwani itachukuliwa kisiasa na kuhujumiwa. Nadhani kuna haja ya kuundwa (kama hamna) kwa makundi ya wabaharakati ya kutetea haki za wananchi, na wakaanza mara moja hatua za kisheria na mashinikizo ya kutaka mali zetu zirudishwe.
   
 13. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwa kiasi kikubwa sana Mh Mkurugenzi hakuwa na sababu ya kutoka kikaoni . Hii inajionyesha wazi Mkurugenzi huyu asivyojua sheria na kuendekeza mapenzi na ushabiki wa CCM hata kama halmashauri ile kutoongozwa na CCM.

  kazi ipo kuondoa makovu ya viongozi wa Serikali kujiona wanatekeleza kazi za kiserikali na sio vyama
   
Loading...