Mkurugenzi amtupa gerezani mwenyekiti wa mtaa - Mabibo

the mkerewe

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
232
14
Mwenyekiti wa mtaa wa mabibo jitegemee (CUF) anashikiliwa na polisi tokea jana na amepelekwa Segerea.

Ishu ilikuwa hivi:

1. Mabwana afya kutoka halmashauri walifika katika soko lililopo mtaani hapo kukagua usafi wa mtaa wa jitegemee na kutoza faini wakazi wa majumbani

2. Mwenyekiti aliwasihi wakazi wakubali kukaguliwa ila wakaazi waligoma wakishinikiza taka za soko zizolewe kwanza kwani halmashauri/bwana afya na wenyewe ni wachafu mno.
(Ikumbukwe halmashauri ndiyo inayokusanya ushuru sokoni hapo na inawajibika kuzoa taka soko halijazolewa taka kwa mwezi mzima)

Wakazi wakapandwa jazba na hivyo wakaguzi wakala kona. Ofisini kwa Mkurugenzi wakaguzi wakadai mwenyekiti wa mtaa aliwachochea wanainchi kupitia pazia la uani (kiujanja) hivyo Director amemshikilia toka jana na kanyima dhamana
 
Duh nampa pole lakini kwa chama chake anaweza kukaa mpaka mwezi ujao amuulize Magdalena Sakaya.............
 
Duh nampa pole lakini kwa chama chake anaweza kukaa mpaka mwezi ujao amuulize Magdalena Sakaya.............

Angekuwa anatoka chama cha kusaga visigino tungesikia wamefanya vurugu na hata kudhalilisha au kujaribu kubaka.
 
Angekuwa anatoka chama cha kusaga visigino tungesikia wamefanya vurugu na hata kudhalilisha au kujaribu kubaka.

nA ingetoka chama cha zamani hata angefumaniwa na mke wa mtu mmewe angepozwa huku akipanda majukwaani macho makavu........
 
kasomewa mashtaka gani hayo hadi kukosa dhamana? ni shinikizo la Mkurugenzi kutopatikana dhamana au yeye mwenyewe watu wake hawakujipanga sawasawa maana mahakamani napo longo longo mingi sana
 
Back
Top Bottom