Mkurugenzi aliyesimamia uchaguzi wa marudio Buyungu ahamishiwa Dar es salaam manispaa ya Temeke

Zawadi B Lupelo

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
2,549
3,722
Waungwana salaam!

Aliyekuwa mkurugenzi wa wilaya ya Kakonko na kada wa muda mrefu wa chama cha mapinduzi Lusubilo Mwakabibi amehamishiwa katika manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam.

Mwakabibi ambaye alijizolea umaarufu baada ya kugombea ubunge jimbo la busokelo mkoani Mbeya ambapo alishindwa katika kura za maoni za CCM.

Baada uchaguzi aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa wilaya ya kakonko na kujizolea umaarufu tena kwa mara nyingine mapema mwaka huu baada ya kusababisha kifo cha mwalimu wa shule moja aliyejinyonga na kuacha ujumbe kuwa mkurugenzi huyu asipodhibitiwa ataua wengi.
Rejea kwenye uzi husika hapa chini
KIGOMA: Mkuu wa Shule ya Sekondari Kakonko ajinyonga, asema Mkurugenzi wa Kakonko asipodhibitiwa ataua wengi - JamiiForums
Baadaye tena ameendelea kujizolea umaarufu baada ya kusimamia uchaguzi wa moja ya majimbo yaliyopo wilaya ya kakonko yaani jimbo la Buyungu. Katika uchaguzi huo kulijaa kila aina ya figisu na malalamiko makubwa mno kutoka upinzani.

Hatimaye baada ya kumaliza kazi Buyungu Mheshimiwa sana Rais Magufuli amemhamisha Lusubilo Mwakabibi kutoka kakonko mpaka Temeke jijini Dar es Salaam.

Mytake.

Mimi Nina swali hivi jimbo la Ukonga halipo Temeke?
Liwe halipo ama lipo hiyo siyo kesi je unabii uliosemwa na marehemu aliyejinyonga kwamba Mwakabibi asipodhibitiwa ataua wengi vipi? Je tutegemee kuwa "atauwa wengi" wengi huko Dar es salaam?
Screenshot_2018-08-13-17-52-16.jpg
FB_IMG_1534171885444.jpg
 
Hiyo ndio kazi ambayo magufuli kuifanya kwake ni rahisi na anaweza.

uchumi na maisha ya watanzania hivyo haviwezi kamwe yeye ni bingwa wa kuteua na kutengua kisha piga upinzani.
 
for strange reasons the international community has given the blind eye
 
Nimesikia jana akimtangaza Mtolea kuwa amepita bila kupingwa. Alikuwa na mbwembwe nyingi na kwa kweli alitumia jina la Mungu vibaya sana. Hii ni aibu kabisa kuwa na watu wa namna yake katika ofisi za umma.
 
kkkkk !!
Hiyo ndio team anayokuja nayo jiwe 2020
mpinzani ukishinda kaishukuru mizimu..
Tanzania sweetheart keshatangaza kwamba 2020 hakutokuwa na hata diwani wa upinzani Dar
 
Back
Top Bottom