Mkurugenzi abanwa kwa kugoma kumlipia Makamu wa Rais malazi

Hii safi!!

Yaani malazi na chakula siku 1 shs millioni 2?

Hii pesa sii bora ikajenga madarasa??

Kumbe hawa viongozi huzunguka mikoani kila siku kwa gharama za nani??

Hizi ziara zina manufaa gani?

Kwani Karatu ndo waliomwita Shein akatembee huko?

Labda Vingunge wetu wanakula Almasi na Dhahabu ndiyo maana mlo wao wa siku moja una gharama kubwa!!!! Kwa hiyo Chakula na Malazi ya mwezi mzima ni millioni 60!!!! Ndiyo maana visafari safari vyao haviishi!!!! Kweli Tanzania itajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno!!!!
 
Jamani msianze kusifia wakati mnashusha guard zetu..kuweni makini sana na swala hili laweza kuwa zito kuliko tunavyofikiria.
Ogah kauliza swali zuri sana.. Je ni utaratibu gani hufanyika wakati wa misafara ya viongozi kama hii..Tuachane na maswala ya bajeti kwa sababu Tanzania ni nchi inayoongozwa kiholela..Tuna hakika Ofisi ya Makamu wa rais ina bajeti inayo cover misafara kama hii tena humegewa allowance juu kwa siku kinachotakiwa ni (receipt) supporting document ziwakilishwe wizarani...

Sasa nachoshindwa kuelewa ni utaratibu gani umetangulia kwani yawezekana Makamu wa rais amealikwa na wilaya na utaratibu unasema ukimwalika kiongozi unalipia gharama! who knows utaratibu ktk nchi ya Wadanganyika..
Je, ktk maswala ya mwaliko ni nani anachukua dhamana ya matumizi?.. kuna maswali mengi sana inabidi tufahamu kilichotokea na zaidi ya yote tuwe tayari kumlinda mkurugenzi huyu..
Je, akifukuzwa kazi tutafanya nini?
 
Saaafi sana Mkurugenzi,

Makamu wa rais mzima hawezi kuwa freeloader.Mkurugenzi anatekeleza maagizo yaliyowekwa na utawala wa sheria.

Tukipata watu wengi zaidi kama mkurugenzi huyu tunaweza kupandisha "fiscal responsibility" na labda tunaweza kupiga hatua.

Inakuwaje Makamu wa rais, mtu wa pili katika mamlaka ya serikali kuu, aende kuhudumiwa na halmashauri? Na ukata wote unaozikabili halmashauri hizi?

Again,

Saafi sana mkurugenzi, huyu ni kati ya watu wachache sana wanaoweza kuchukua maamuzi ya msimamo bila kuogopa.Wengi sana wangeogopa cheo cha Makamu wa rais.

Shame on the Vice Presidents office.
 
Naamini huu ujumbe wa waziri mkuu, Makamu wa rais na hata rais mwenyewe anapotoka kwenda ziarani mikoani huwa ana budget yake. Kwa nini tena wakifika kule Halmashauri zinalipia gharama hizo hizo. Hawa watu walioandamana nao wanakuwa wameshalipwa gharama za malazi then how comes tena wanalipiwe chakula na malazi na Halmashauri.

Kweli CCM mna laana nyie, na aliyewalaani alishafariki.
 
Naamini huu ujumbe wa waziri mkuu, Makamu wa rais na hata rais mwenyewe anapotoka kwenda ziarani mikoani huwa ana budget yake. Kwa nini tena wakifika kule Halmashauri zinalipia gharama hizo hizo. Hawa watu walioandamana nao wanakuwa wameshalipwa gharama za malazi then how comes tena wanalipiwe chakula na malazi na Halmashauri.

Kweli CCM mna laana nyie, na aliyewalaani alishafariki.

kwahiyo hakuna mwenye kuweza kuondoa hiyo laana!! kwi! kwi! kwi! kwi! kwi! watakufa nayo!
 
Jamani lakini Mkurugenzi kasema waliopinga kupitisha matumizi hayo ni Madiwani.. hivyo sifa hizi ziwafikie Madiwani kwa sababu huyu Mkurugenzi kulingana na utetezi wake, kama Madiwani wangeweka sahihi asingesita kulipa..
 
Jamani lakini Mkurugenzi kasema waliopinga kupitisha matumizi hayo ni Madiwani.. hivyo sifa hizi ziwafikie Madiwani kwa sababu huyu Mkurugenzi kulingana na utetezi wake, kama Madiwani wangeweka sahihi asingesita kulipa..

Mkurugenzi anasifiwa kwa ku uphold principles na rule of law, kawaida ni kuona watu walio katika position ya mkurugenzi ku trump over madiwani kwa kujipendekeza kwa makamu wa rais na mkuu wa wilaya.

Madiwani nao wanapongezwa kwa sababu bila wao mkurugenzi angekosa basis ya nguvu kukataa.

In any case kilichofanyika kinaonyesha a shifting tectonic plate in Tanzanian politics, wananchi washachoka ndiyo maana rais anapigwa mawe, makamu wake anatolewa nje kulipiwa bill, na mstaafu, well, hata kama ni kutoka kwa kichaa (not endorsing, merely reading the signs of time) anapigwa kibao wakati mwingine anazomewa kwa ufisadi.

These are unprecedented times and the CCM ruling class will do well to take note and act accordingly before the situation is completely out of hand.
 
Jamani lakini Mkurugenzi kasema waliopinga kupitisha matumizi hayo ni Madiwani.. hivyo sifa hizi ziwafikie Madiwani kwa sababu huyu Mkurugenzi kulingana na utetezi wake, kama Madiwani wangeweka sahihi asingesita kulipa..

Ni kweli ni madiwani wanastahili pongezi lakini na yeye pia kama kiongozi mwenye kusikiliza wengine na kusimamia sheria na si kukurupuka tu na maamuzi...
 
Jamani msianze kusifia wakati mnashusha guard zetu..

Kusifia hapa si kushusha guard, actually ni kupandisha guard, kupandisha guard ya fiscal responsibility, kupandisha guard ya accountability, kupandisha guard ya ethics, kupandisha guard ya fairness, kupandisha guard ya mipaka kati ya central and local governments, kupandisha guard na attention kuhusu issues zinazohitaji civil disobedience, kupandisha guard kuhusu taratibu zetu....

kuweni makini sana na swala hili laweza kuwa zito kuliko tunavyofikiria.
Ogah kauliza swali zuri sana.. Je ni utaratibu gani hufanyika wakati wa misafara ya viongozi kama hii..

Swali zuri sana, lakini regardless ya jibu, makamu wa rais (mwenye resources nyingi sana) kuji impose kwenye local governments zimlipie siyo fair, siyo fiscally responsible, siyo ethical, haionyeshi leadership.Ni kama baba tajiri anayejipeleka kwa mtoto wake asiye na uwezo na kumtaka mtoto wake amhudumie kwa malazi ya hali ya juu sana ambayo yataharibu bajeti ya mwanae ambayo ingeweza kutumika kwa vitu vingi vinavyohitaji fedha hizi.

Kwa hiyo kama kwa kawaida fedha hizi hulipwa na ofisi ya makamu wa rais, then madiwani na mkurugenzi wamefanya vizuri kutotaka kulipa.Kama kwa kawaida gharama hizi hulipwa na serikali za mitaa/ halmashauri, then this is wrong and unfair and should be changed, and this act is good as a precedent for civil disobedience.

Tuachane na maswala ya bajeti kwa sababu Tanzania ni nchi inayoongozwa kiholela..

Kwa hiyo mkuu unatetea uholela? The way forward ni kuachana na bajeti na kuendelea kiholela? hivi ndivyo tutatoka kwenye umasikini wetu? then unategemea maendeleo kweli?

Tuna hakika Ofisi ya Makamu wa rais ina bajeti inayo cover misafara kama hii tena humegewa allowance juu kwa siku kinachotakiwa ni (receipt) supporting document ziwakilishwe wizarani...

Sasa nachoshindwa kuelewa ni utaratibu gani umetangulia kwani yawezekana Makamu wa rais amealikwa na wilaya na utaratibu unasema ukimwalika kiongozi unalipia gharama!

Wilaya ingemualika kwa kufuata utaratibu na kuwashirikisha madiwani na mkurugenzi sidhani kama wangekataa kulipia.Watanzania ni wakarimu peer to peer, sembuse kwa makamu wa rais? Kama mkuu wa wilaya kamkaribisha makamu wa rais wakati hana bajeti ya kumkirimu halafu akaingiza mkono katika mifuko ya halmashauri ku cover expenses, bila kuwashirikisha madiwani na mkurugenzi then mkurugenzi na madiwani wana haki ya kukataa gharama.

who knows utaratibu ktk nchi ya Wadanganyika..

Even the more reason ku demand accountability na transparency, na ku encourage vitendo vya mkurugenzi. katika nchi isiyo na utaratibu kama Tanzania, mtu yeyote anayeelekea kuongozwa na utaratibu kama mkurugenzi huyu ni wa kusikilizwa na kuigwa, inawezekana utaratibu haupo na kesi kama hii ndiyo ikawa precedent ya kuanzisha utaratibu.

Inawezekana kuna wakurugenzi kibao wa wilaya wamefurahi sana kwa sababu ziara hizi zinawatia gharama ila hawana courage ya kuzikataa gharama hizi.Huyu mkurugenzi kamwe si mtu wa kupuzwa.

Je, ktk maswala ya mwaliko ni nani anachukua dhamana ya matumizi?..

Hili limejibiwa hapo juu, sitegemei madiwani wote na mkurugenzi wao wakakosa uungwana kiasi cha kumuadhiri makamu wa rais waliyemualika na kuelewa kuwa watapata gharama, inaonekana wamebambikiwa gharama bila kujua.

kuna maswali mengi sana inabidi tufahamu kilichotokea na zaidi ya yote tuwe tayari kumlinda mkurugenzi huyu..

Na msimamo wa mkurugenzi unasaidia kutoa mwanga kumulika hapa kuona maswali zaidi na kupata majibu.Mkurugenzi angekubali kulipa wala tusingejua makamu wa rais anajichana vipi kwa siku, all the more reason to encourage this guy

Je, akifukuzwa kazi tutafanya nini?

Huyu mkuu anaonekana ana fiscal responsibility, akifukuzwa kazi itakuwa loss ya halmashauri na watu wanaojua principles za fiscal responsibility na concept ya "profiles in courage" hawawezi kumuacha huyu.hata hapa tunaweza kumpigia kampeni kama symbol of hope in the midst of timid and corrupt leaders.

Mkuu unanipa impression kwamba uko concerned kuhusu kibarua kuota majani na kitumbua kuingia mchanga kwa mtu mmoja kuliko maslahi ya taifa na trend nzima ya fiscal responsibility bongo. This is worrying if not disappointing.
 
Mkuu unanipa impression kwamba uko concerned kuhusu kibarua kuota majani na kitumbua kuingia mchanga kwa mtu mmoja kuliko maslahi ya taifa na trend nzima ya fiscal responsibility bongo. This is worrying if not disappointing.

Hapo Watanzania wengi ndipo tunapokuwa wajinga. Ipo siku mtu atalazimiswa mambo ya kipuuzi na yeye akubali tu kwa sababu ya kuogopa kupoteza kibaru. Ndiyo maana akina mama wanafanyishwa ngono za ajabu ajabu na si ajabu pia kuna akina baba wanaingizwa kwenye mchezo mchafu!!

Suala la double payment hapa Tz limekuwa la kawaida sana. Mtu anachukua pesa wizarani then anaenda kukomalia malipo mengine huko alikotembelea. Ndo maana biashara ya kuuza receipts mjini ni deal sana. Yaani ukianzisha mradi wa kuuza receipts kuanzia za mafuta, hotel, taxi etc utapata pesa nyingi sana. Huu mfano wa Karatu unaweza kutusaidia kutoka hapa tulipo ingawa safari bado ni ndefu sana. Hii ni kwa sababu viongozi wengi ni waonga na wengine hawana sifa za kazi wanazofanya. Kwa hiyo kujipendekeza inakuwa ndiyo njia pekee ya kulinda ajira zao.
 
Ninavyojua mimi, Makamu wa Rais ana bajeti yake ya ziara kutoka ofisini kwake. Watu anaoambatana nao pia wana perdiem zao kulingana na vyeo vyao. Makamu wa Rais anapewa perdiem,lakini kutokana na wadhifa alionao,gharama zake za malazi na chakula ofisi yake inagharamia. Watumishi wengine alioambatana nao wanapewa perdiem ambazo kihalali inatakiwa walipie malazi. Lakini cha ajabu mara nyingi watu hupewa perdiem na malazi wanalipiwa. Haya si matumizi mazuri ya pesa ya umma,lakini ndiyo hivyo tena imezoeleka hivyo na hakuna anayeshtuka serikalini kwani idara zote wanafanya hivyo.
Pesa inayokwenda halmashauri ina bajeti yake, ila sidhani kama kuna bajeti ya malazi ya Makamu wa Rais. Maana yangu ni kuwa, kama siku moja ni Tshs 2m,then kwa hesabu ya haraka ziara ya siku kumi inaweza kutumia Tshs 20m. Hii ni nje ya perdiem wanazolipwa.Pesa kama hii kwa halmashauri ni kubwa sana,ukizingatia haikuwa budgeted for this activity. Maana yangu ni kuwa pesa hii ilitengwa kununua madawa na kusimamia shughuli zingine za maendeleo halmashauri kama barabara. Kwa maana nyingine ni kuwa barabara haitajengwa wala madawa kununuliwa na mambo kama hayo.
WATANZANIA TURUDIKWENYE BASICS, OTHERWISE MAENDELEO NI NDOTO.
 
Jamani msianze kusifia wakati mnashusha guard zetu..kuweni makini sana na swala hili laweza kuwa zito kuliko tunavyofikiria.
Ogah kauliza swali zuri sana.. Je ni utaratibu gani hufanyika wakati wa misafara ya viongozi kama hii..Tuachane na maswala ya bajeti kwa sababu Tanzania ni nchi inayoongozwa kiholela..Tuna hakika Ofisi ya Makamu wa rais ina bajeti inayo cover misafara kama hii tena humegewa allowance juu kwa siku kinachotakiwa ni (receipt) supporting document ziwakilishwe wizarani...

Sasa nachoshindwa kuelewa ni utaratibu gani umetangulia kwani yawezekana Makamu wa rais amealikwa na wilaya na utaratibu unasema ukimwalika kiongozi unalipia gharama! who knows utaratibu ktk nchi ya Wadanganyika..
Je, ktk maswala ya mwaliko ni nani anachukua dhamana ya matumizi?.. kuna maswali mengi sana inabidi tufahamu kilichotokea na zaidi ya yote tuwe tayari kumlinda mkurugenzi huyu..
Je, akifukuzwa kazi tutafanya nini?

Mkuu! Kwetu ni vigumu sana wilaya imwalike mheshimiwa kama huyo halafu isimgharimie! Kama wangemwalika, ingekuwa kwa shughuli maalum na si kutembelea tu. Kwa namna hiyo gharama zake wangezibeba na kuziweka kwenye bajeti yao.

Viongozi wetu wamejisahau. Wao neno bajeti wanaona ni watu wa chini. Na wanaposafiri hawaangalii uwezo wa wenyeji wao. Hivi nani anaweza kweli katika kawilaya kama hako kujastifai matumizi ya hayo mamilioni kwa siku moja?

Jamaa anastahili pongezi.

Amandla........
 
Hapo siyo suala la utaratibu bali ni bajeti na uwepo wa fedha. Kwa wakati tulionao Tanzania tunatumia mfumo wa cash budget kwa maana kwamba ilishughuli itekelezwe lazima iwe ilishatengewa na kuidhinishiwa bajeti yake; halafu wakati wa kuitekeleza lazima kuhakikisha kuwe fedha ya kuitekeleza ipo. Makamu wa Rais ana wizara yake ambayo kimsingi ndiyo yenye wajibu wa kumwandalia bajeti ya ziara zake kwani hao ndo wanafahamu atakuwa na ziara ngapi kwa mwaka.


Kwanza tunampa pole Mkurugenzi wa Karatu kwa kutaka kuwajibishwa kwenye suala ambalo kimsingi anayepaswa kuwajibika ni Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais na Katibu wa Makamu wa Rais. Kumvamia tu Mkurugenzi na kutaka atoe maelezo kuonyesha tusivyofahamu taratibu za uendeshaji wa serikali hasa namna ya kuhudumia viongozi wakuu wa serikali. Aliyepaswa kugharimia ziara hiyo ni Katibu Ofisi ya Makamu wa Rais na si Mkurugenzi wa Karatu. Tunavyofahamu na ndivyo ulivyo utaratibu wa serikali kila mtumishi anaposafiri nje ya kituo cha kazi hulipwa posho ya kujikimu kwa maana ya kulipia chakula na malazi. Inashangaza hao wasaidizi wa makamu wa Rais pesa hizo wamefanyia nini hata wakafika mahali pa kuanza kumdai Mkurugenzi awalipe malazi. Katika siku za hivi karibuni kumezuka wimbi la wasaidizi wa viongozi wakuu wa nchi kusumbua watendaji mikoani kwa madai ya kulipiwa malazi na wakati mwingine hudai hata mafuta ya magari wanayoendesha wakati wanajua fika wamepewa pesa kutoka kwenye ofisi wanazotoka. Wasaidizi hawa pamoja na kupewa fedha za kutosha hukataa hata mahali wanapopangiwa kulala kwaajili ya kutaka kubana tu fedha. Vijana hawa hawaangalii tena nafasi waliyonayo na ugumu wa kazi ya kuwa wasaidizi wa viongozi. Hali hii si nzuri ikiachwa iendelee kwani inadhalilisha viongozi wetu na taifa letu kwa ujumla.Kwa hili tunashauri yafuatayo, (a) Katibu Mkuu kiongozi amtake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais kutoa maelezo ni kwanini ameshindwa kulipia gharama hizo au kushirikiana na Mkoa wa manyara kupanga vizuri safari hiyo kiasi cha kumdhalilisha kiongozi wetu,(b) Katibu Mkuu Kiongozi auombe radhi uongozi wa Manyara na amuombe radhi yeye binafsi Mhe. Makamu wa Rais kwa haya yaliyotokea na (c) Katibu Mkuu Kiongozi akae na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu na Mkuu wa Usalama wa Taifa waone namna wanavyoweza kudhibiti nidhamu ya watumishi wanaowazunguka viongozi wakuu wa taifa letu ili kuaminiwa kwao kusiwe kero kwa jamii. Wamepewa dhamana nyeti wasiwe wasumbufu wasaidie viongozi mikoani na wilayani kufanikisha ziara za viongozi wetu.
 
endapo mkuu kama huyo anatembelea sehemu........je utaratibu wa matumizi yake ukoje?

Hili swali zuri, mimi naamini bajeti ya Ofisi ya Makamu wa ina-cover gharama zote za safari. Huu wizi wa Serikali Kuu dhidi ya Serikali za Mitaa eti walipie safari za Rais, Makamu Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri, Wajumbe wa Kamati mbalimbali za CCM. Ni wizi mkubwa dhidi ya visenti vichache vya walipa kodi masokono na wakulima. Wizi mtupu na aibu kwa Makamu Rais.

Bravo Mkurugenzi, tukipata watendaji wengi kama wewe lazima tutasonga mbele.
 
Heko Wana-Karatu. Mfano wa Karatu ni wa kuigwa kwa kuwa viongozi hawa wana Bajeti na siyo kutembeza bakuli kila wanapotembelea maeneo ya kazi.
Nampongeza Dr. Slaa (Mbunge) alipohutubia pale Karatu Mjini na kusema kuwa huyo DC atafute wilaya yake ya CCM.
 
Kwa nini mkuu wa wilaya hakulipa kutoka kwenye mfuko wa ofisi yake?

Kwa kawaida, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa hutegemea fedha za OC ya serikali toka hazina. Fedha hizi siku zote ni kiduchu ndio maana wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kifedha halali ni choka mbaya.

Wote humtegemea Mkurugenzi wa Halmashauri ndiye mwenye fungu kutokana na kumiliki vyanzo vya mapato.

Kunapotokea ziara yoyote, maofisa wote wa serikali hulipwa per diem zao, bali kila wafikapo, hula bure na kulala bure kama takrima na wakati mwingine mpakwa hulipwa malipo mengine kama marupurupu.

Kitendo cha mkurugenzi, japo kimeidhalilisha ofisi ya MR lakini imefungua macho kwa wananchi kuzijua baadhi ya neema za ukubwa, kwa jasho lao.

Baadhi ya safari za mabosi wa bongo, sio kufanya unachotakiwa bali ni kuyakumba mahela. Niliwahi kuhudhuria ka kozi morello web publishing uk. Kozi ilikuwa kwa ajili ya junior officers na web masters. Kutoka serikalini alikuja top boss na bonge la laptop lake huku hajui lolote, kazi alikuwa busy na shopping kuhalalisha ulaji.

Usikute hata hiyo ziara ya makamu was well budgeted, ila walikuwa wanataka takrima ili per diem zao wazigeuze marupurupu.
 
Kwa nini wale waliodai kulipiwa wakati wamelipwa per diem wasiulizwe kulikoni? Kama wamekiuka taratibu basi hatua za nidhamu zichukuliwe.
 
Labda Vingunge wetu wanakula Almasi na Dhahabu ndiyo maana mlo wao wa siku moja una gharama kubwa!!!! Kwa hiyo Chakula na Malazi ya mwezi mzima ni millioni 60!!!! Ndiyo maana visafari safari vyao haviishi!!!! Kweli Tanzania itajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno!!!!

Mkuu kwani M/Raisi alikuwa na ujumbe wa watu wangapi??
Manake yawezekana aliongozana na ujumbe mkubwa kiasi cha kutosha pamoja na 10% ya waandaji.
 
Na Leon Bahati

SAKATA la Halmashauri ya Karatu, kugomea kulipia malazi ya Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein na ujumbe wake limechukuwa sura mpya, baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Celina Kombani kuunga mkono uamuzi wa halmashauri ni sahihi.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili, Kombani alisema halmashauri za wilaya haziwajibiki kuchangia ziara za mawaziri, rais au makamu wake, wanapotembelea katika maeneo yao.

Kombani alibainisha kuwa kama ingekuwa utaratibu huo upo, halmashauri nyingi zingefilisika hasa ambazo mawaziri wanatoka, kwa sababu wana utaratibu maalumu wa kutembelea zaidi ya mara tano kwenye maeneo yao, kwa mwaka.

"Kwa mfano kwa mwaka mimi hufanya ziara mara sita katika wilaya yangu ya Ulanga (Morogoro). Tukisema wanigharamie basi ingefilisika pamoja na halmashauri nyingine ambazo zina mawaziri," alisema Kombani ambaye ni Mbunge wa Ulanga Mashariki.

Akielezea kuhusu taratibu za matumizi ya fedha kwenye halmashauri, alisema kwa kawaida matumizi yote hupitishwa kwenye vikao vya madiwani.

Alibainisha kuwa gharama za msafara wa rais, makamu wa rais na mawaziri hugharamiwa na serikali kuu, kulingana na taratibu zilizowekwa.

"Ndiyo maana rais anapokuwa kwenye ziara huenda na vyakula vyake," alisema Kombani lakini akafahamisha kuwa halmashauri zinaweza kutenga fungu kwa ajili ya kuuandalia ugeni kwenye maeneo yao chakula cha jioni.

Iwapo halmashauri itaamua kufanya hivyo, alisema kuwa ni lazima fungu hilo liwe limepitishwa na halmashauri kupitia vikao vyake halali na si mkurugenzi na watendaji wake.

Alipoulizwa juu ya adhabu ya kiongozi wa halmashauri atakayetoa fedha pasipokufuata taratibu; alisema kila halmashauri ina taratibu zake za kuwajadili viongozi au maofisa waliokiuka taratibu na kuwachukulia hatua.

Suala la Halmashauri ya Karatu, kugomea kulipia malazi ya Makamu wa Rais pamoja na ujumbe wake liliripotiwa na gazeti la Mwananchi Jumatano iliyopita likionyesha kuwa Mkuu wa wilaya hiyo, Mathew Sedoyeka alimjia juu na kumtaka aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Majid Myao, aandike barua ya kujieleza kwanini alikataa kutoa fedha za kulipia ziara ya makamu wa rais wilayani humo.

Sedoyeka hakufurahishwa na kitendo cha halmashauri hiyo kugoma kulipa kiasi cha Sh2 milioni ambazo ni malipo ya kulala siku moja pamoja na chakula kwa ujumbe huo wa makamu wa rais, katika hoteli ya Bougain Villea ya mjini Karatu.

Kwenye barua ya kujieleza iliyoandikwa Machi 3, 2009 yenye kumbukumbu namba kdc/ded/cv.3/1/121, Myao amejitetea kuwa uamuzi wa kutolipiwa ziara hiyo, umetokana na kamati ya fedha ya madiwani kukataa kuidhinisha fedha hizo.

Alisema kutokana na kutoidhinishwa malipo hayo, aliona angekiuka Sheria namba tisa ya mwaka 1982 ambayo inahusu masuala ya matumizi ya fedha za halmashauri na maamuzi ya kamati ya fedha.

“Kama mimi ningetoa malipo hayo ni wazi ningekiuka sheria za serikali za mitaa hasa ikizingatiwa madiwani katika kikao chao halali ndio waligomea,” alieleza Myao.

Akizungumzia sakata hilo, Mbunge wa Jimbo la Karatu, Dk Willibrod Slaa alisema alichofanya ofisa huyo wa serikali ilikuwa halali kwa sababu walikuwa hawana bajeti ya malipo hayo.

Dk Slaa alitoa wito kwa serikali kutomuadhibu mtendaji yoyote wa halmashauri hiyo kutokana na uamuzi uliochukuliwa, ambao ulizingatia maadili ya kazi na utekelezaji wa utawala bora.

Kutoka Magazeti ya Tz.
Hii sasa inadhihirisha kuwa mawaziri wetu wameanza kufahamu kuwa tunaelewa namna serikali yetu inavyoendeshwa. Hongera wana JF kwa kuonyesha upeo mkubwa wa mambo. Kinachotakiwa sasa ni Bw. Phillemon Luhanjo kuachia ngazi baada ya kuruhusu Makamu kudhalilishwa. Sheria ya Utumishi wa Umma na. 8 ya 2002 inamtaja Katibu Mkuu Kiongozi kuwa ndiye Mkuu wa Utumishi wa Umma na Katibu wa Baraza la Mawaziri. Na kama mnafahamu yeye ndiye anayewajibika moja kwa moja kwa niaba ya watendaji wote serikalini kuhakikisha chombo kinaitwa serikali hakiendi nje ya maadili. Sasa kama aliona hili ni jepesi au kwakuwa tu Makamu ni Mzanzibari basi hafai kubakia kwenye nafasi yake. Akiachwa kwa hili basi tusihukumu watumishi wengine kwa makosa mengine ya kimaadili.
 
Back
Top Bottom