Mkuranga: Serikali yakifunga Kiwanda cha Nondo kutokana na vifo vya Wafanyakazi wawili

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Mkurugenzi mkuu wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc), Dk Samuel Gwamaka amekifunga kiwanda cha nondo cha Fujian Hexingwang kwa sababu hakina mazingira mazuri ya watu kufanya kazi.

Hatua hiyo imetokana na vifo vya wafanyakazi wawili wa kiwanda hicho kilichopo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani baada ya kutokea mlipuko kwenye tanuru la kuyeyusha vyuma chakavu.

Dk Gwamaka amekitembelea kiwanda hicho leo Jumatano Mei 5, 2021 na kubaini kwamba hakijaweka mazingira mazuri kwa ajili ya usalama wa wafanyakazi, jambo ambalo limesababisha vifo vya watu wawili waliokuwa kazini.

"Kuanzia sasa ninakifunga kiwanda hiki mpaka watakapoboresha mazingira ya ufanyaji kazi na kuzingatia usalama wa wafanyakazi," amesema mkurugenzi huyo wa Nemc.

Amesema miaka mitatu iliyopita Nemc imekuwa ikigombana na kiwanda hicho hasa katika masuala ya uhifadhi wa mazingira na waliwahi kukifungia na kukipiga faini kwa nyakati tofauti.

Dk Gwamaka amesema wafanyakazi hao wamefariki kwa sababu kiwanda hicho hakijaweka utaratibu maalumu wa kuwalinda wafanyakazi wake, hakitafunguliwa mpaka wazingatie maelekezo waliyopewa.

"Tutafanya ukaguzi kwenye viwanda vyote vya nondo kuhakikisha mazingira ya wafanyakazi ni salama na rafiki kwao. Hatutaki kuona watu wengine wanapoteza maisha," amesema Dk Gwamaka.


Mwananchi
 
ni hatari sana aiseee NDUGU yangu almanusra akatwe mkono huko
 
natumai uthubutu wake utaonekana wa tija

kuna sehemu nyingi NEMC wanashindwa kufika nakufanya maamuzi magumu kisa wenye biashara ni waarabu ama wahindi!

labda hili litawashtusha wengine!

Kudos kwa NEMC
 
Kukifunga sio suluhisho,watu wamekula kutokana na mazingira magumu,sasa ukikifunga wanaenda kufa kwa njaa
 
Ujinga mtupu mnasubiri madhara yatokee ndo mtoe tamko? Mlikiruhusu vipi kufanya kazi ili hali kina mapungufu? Nini kilipaswa kuanza kati ya risk assesment na production?

Taasisi zinazokagua viwanda mko zaidi ya moja, nyote hamkuona tatizo mpaka watu wafe ndo muende na makamera?
 
Back
Top Bottom