Mkungu wa ndizi wa Q-Chillah na T.I.D umerudisha heshima ya mziki wetu wa nyumbani

Nifah

JF-Expert Member
Feb 12, 2014
33,210
74,831
Hebu tuachane na haya mambo ya Kiba vs Diamond kwanza tuangalie wanamuziki/wasanii wetu wengine wanafanya nini.

Binafsi nimependezwa sana na kibao cha Q-Chillah akishirikiana na mwenzie T.I.D ambao awali walikuwa wanaunda kundi la Top Band kabla ya kuachana na kila mtu kufanya mziki kivyake (Solo).
Sasa wamerejea na kutoa kibao hiki matata ambacho kimenitia wazimu kabisa maana hapa tu ninapoandika hii post kiuno kinauma kwa kuserebuka....lol

Kibao hiki hakika kimerejesha hadhi ya mziki wetu wa nyumbani (mduara) na kiukweli Q- Chillah nimekuvulia kofia kuwa wewe ndio MKALI WA HIZI KAZI.
Sio kwa kulalamika kule.....umesema wanakuita Sheitwani nami nakuita Ibilisi kabisa.

Kama kuna mtu ambaye hajasikiliza hiki kibao kakosa mengi,hakika UTAKIPENDA TU!

Mie hiki kibao ndio my favourite song sasa......
"Mtoto mdogo mdogo,kabeba mkungu wa ndizi....omamaa omaaa eeeeeh"
Acha kabisa.
 
Ni Video au ni Audio tu wametoa??

Kwahiyo upo Spa sasa unafanya massage ya kiuno??
 
Hebu tuachane na haya mambo ya Kiba vs Diamond kwanza tuangalie wanamuziki/wasanii wetu wengine wanafanya nini.

Binafsi nimependezwa sana na kibao cha Q-Chillah akishirikiana na mwenzie T.I.D ambao awali walikuwa wanaunda kundi la Top Band kabla ya kuachana na kila mtu kufanya mziki kivyake (Solo).
Sasa wamerejea na kutoa kibao hiki matata ambacho kimenitia wazimu kabisa maana hapa tu ninapoandika hii post kiuno kinauma kwa kuserebuka....lol

....
mi nataka kujua video 'kwini' wa huo wimbo ni nani...basi hicho tu!
 
Ngoja niutafute niuangalie maana ukiona paka nifah kasifia ujueee....
Mkuu mimi nina audio tu,ni shida tupu.
Q-Chillah anajua bwana,utafute uusikilize kisha unipe mrejesho.
 
Watu kweli uelewa ni kazi ndo maana mnasoma wote darasani wanafauru wachache yeye anasema wimbo wa chilla na tid umerudisha heshima wewe unaulizia video mara tuwekee link ya video wewe ili ujue wimbo ni mkali mpaka uone video yake wimbo mkali anaamaanisha utunzi wa mashairi aina ya midundo iliyotumika na dogfather kashawaharibu baada ya kusema dah wimbo wako mzuri saivi mnasema video yako nzuri vp kuhusu audio c nzuri c kila ngoma iwe na video hapa anazungumzia single mpya ya Q Chilla ft Tid inaitwa mkungu wa ndizi kama bado ujaisikiliza link hii hapa http://djkidemnyama.blogspot.com/2015/11/new-music-audio-q-chilla-ft-tid-mkungu.html?m=1
 
...akina Q-Chillah wangeniomba ningewafanyia mabalaa tena free of charge.
wacha weee...naomba waione hii post yako huenda ikaleta radha mpya kwenye mziki wetu siyo kila siku hao hao tu!!
 
Ni kibao kipya,sina uhakika kama video tayari.
Hata kuattach audio sijui,ningeweza ningewawekea.
[URLhttp://djkidemnyama.blogspot.com/2015/11/new-music-audio-q-chilla-ft-tid-mkungu.html?m=1][/URL]
 
Watu kweli uelewa ni kazi ndo maana mnasoma wote darasani wanafauru wachache yeye anasema wimbo wa chilla na tid umerudisha heshima wewe unaulizia video mara tuwekee link ya video wewe ili ujue wimbo ni mkali mpaka uone video yake wimbo mkali anaamaanisha utunzi wa mashairi aina ya midundo iliyotumika na dogfather kashawaharibu baada ya kusema dah wimbo wako mzuri saivi mnasema video yako nzuri vp kuhusu audio c nzuri c kila ngoma iwe na video hapa anazungumzia single mpya ya Q Chilla ft Tid inaitwa mkungu wa ndizi kama bado ujaisikiliza link hii hapa http://djkidemnyama.blogspot.com/2015/11/new-music-audio-q-chilla-ft-tid-mkungu.html?m=1
Asante sana mkuu,shukrani.
 
Back
Top Bottom