MKUMBUKENI BALISIDYA PATRIC Vs MAFISADI

Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,550
6,060
WanaJF,
Nimeingia leo KLH kwa MwanaKIJIJI na badala ya kupata ya makala niliyokuwa natafuta, nikaishia kusikiliza miziki ya zilipenda. Humo ndani nikafika na kukuta wimbo wa Patric Balisidya. Katika nyimbo zake nyingi, huu wa "NI MASHAKA" leo umenifanya niwe mnyonge sana. Naufahamu kwa miaka mingi ila miaka yote nilikuwa nashindwa kujua anaimba nini (ninamatatizo ya kuelewa mtu anaimba nini). Leo nimeusikiliza na kutafakari maneno yake. Inasikitisha sana kuwa tangu miaka ile hadi leo uonevu uko pale pale. Si ajabu wengine wanaoonea (mafisadi), wakati huo na wao walikuwa wanaonewa. Cha kusikitisha zaidi ni hili neno "WEMA HAWANA MAISHA". Ukiusikilza haraka haraka unaweza kusema watu kama Mwakyembe, Zitto, Mama Malecela, Dr. Slaa na wale wote wanaopigania HAKI YA MTANZANIA kila siku wanaweza KUKAA TAMAA. Lakini kabla hawajafanya hivyo nawaomba wakaangalie ile film ya Antonio BANDERAS iitwayo "The 13th Warrior (1999)." Humo kuna VIKING mmoja pamoja na kuwa alikuwa kachanjwa chale yenye SUMU na yule Kibibi Gura Malikia, na akawa mgonjwa hoi, walipomletea VITA mlangoni, alisimama na kuchukua Silaha yake na kwenda pigana (samahani kama nimechanganya) na walimuomba na kumwambia kuwa anaweza kufa alisema " ... binadamu POA ni yule anayeishi na akifa, vizazi vitamkumbuka na kumuwekea ukumbusho kama wa SANAMU, Mnara, Nyimbo nk. na si kuishi maisha marefu...." Mafisadi mnaotumia VITISHO, Mauwaji na taka nyingine kama za Mugabe mjue HISTORIA itawasau au itawakumbuka kwa upande wa HITLER, Savimbi, Stalin Joe, nk na si Upande wa Mashujaa kama Sokoine, Nyerere, Sankara, Ngwabi na Mashujaa wote wanaopingana na NYIE kwa sasa. Naomba huu wimbo uwe changamoto kwa wanaJF popote pale walipo. They will kill your body but your soul will keep GOING STRONG. Kwa bahati Tanzania siyo Russia maana huko kweli Mungu hayupo na SOUL za watu wema hupotea kimoja.... Kweli dawa ni moja tu nayo ni kuwa BEGA KWA BEGA na WEMA wetu. Mwenye kuweza kuweka maneno ya huu wimbo ntamshukuru sana.
 
Sikonge, wewe umekufanya uwe mnyonge lakini wengine hulia! Marehemu Patrick Balisidya ataendelea kuishi, huo wimbo unaitwa "dunia ya mashaka" wema hawana maisha! Wakati huo wa Afro 70 band miaka ya 1970! Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina!

Wakati huo bendi za muziki zinapiga muziki wa kweli, kumbuka Jamhuri Jazz Band (Wanyama Wakali), Dar Jazz (wana Mundo) we acha tu, watu hupita lakini maneno/ kauri zao huishi kizazi hadi kizazi!
 
Sikonge, wewe umekufanya uwe mnyonge lakini wengine hulia! Marehemu Patrick Balisidya ataendelea kuishi, huo wimbo unaitwa "dunia ya mashaka" wema hawana maisha! Wakati huo wa Afro 70 band miaka ya 1970! Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina!

Wakati huo bendi za muziki zinapiga muziki wa kweli, kumbuka Jamhuri Jazz Band (Wanyama Wakali), Dar Jazz (wana Mundo) we acha tu, watu hupita lakini maneno/ kauri zao huishi kizazi hadi kizazi!
Think BIG,
Asante kwa usahihisho. Miaka hiyo kweli nilikuwa mdogo sana kujua hata tittle za nyimbo. Nililiishi na dada yake Patrick yaani Mei Materu au Ndanao Balisidya (wote RIP) kuanzia kule kule Roleza secondary, na baadaye Korogwe girls na baadaye akahamia UDSM. Tulipohamia Dar basi tulienda kumtembelea huyu mama na baadaye kaja kijana na vifaa mfuko wa suruali wa nyuma. Kufika hakutaka hata chai wala nini na kuuliza liko wapi? Akaonyeshwa jiko la umeme na kulitengeneza. Nilikuja kujua baadaye kuwa alikuwa FUNDI MCHUNDO wa umeme (Dar tech). Yule mama ilibidi atuambie kuwa huyo tumuonaye mbele yetu ndiye kaka yake Patrick. Hii ilikuwa mwaka 1974. Ehhh wakati huo miziki kweli hadi uende Radio Tanzani kurekodi inabidi ufanye kazi sana. Ila matokeo ni kuwa hadi leo nyimbo zao zinatesa. Kweli haitoshi kuishi sana au kuwa FISADI. Unaweza kuweka HISTORIA jina lako kwa njia nyingi sana. Kama pesa hawa mabwana wanazo za kutosha sanasana watoto wao wataishia kujifanya MAJOKA na kubugia unga.
Huu wimbo kwa kweli inabidi uwe ni wimbo wa WAPIGANIA HAKI YA WADANGANYIKA. Inatia sana uchungu usikiapo kuanzia hii sehemu ya 3:50 hadi 4:25 "Wema watauwawa, Tutabaki kuonewa, Waafrika hadi tung'onyeke, wema wangelibakia, neema tungelizipata ... wema hawana maisha.." Too sad.
 
Halafu unajua yeye marehemu Patric alivyokuja hujumiwa na Chediel Mgonja, aliyekuwa waziri enzi za awamu ya kwanza, hakuweza ku-recover na ndicho hasa kilichompelekea kufa mapema, Mkulu Wangu Patric Mungu amuweke mahali pema peponi,

Mdogo wake Freedom anajaribu sasa hivi ni kibendi kimoja uchwara, lakini hawezi kabisa fikia kipaji cha Patric.
 
Halafu unajua yeye marehemu Patric alivyokuja hujumiwa na Chediel Mgonja, aliyekuwa waziri enzi za awamu ya kwanza, hakuweza ku-recover na ndicho hasa kilichompelekea kufa mapema, Mkulu Wangu Patric Mungu amuweke mahali pema peponi,

Mdogo wake Freedom anajaribu sasa hivi ni kibendi kimoja uchwara, lakini hawezi kabisa fikia kipaji cha Patric.

Nafikiri huyu Chediel Mgonja akisoma hapo juu na kusikiliza wimbo huo ataona jinsi alivyochangia kufupisha maisha ya mtu. Mtu Waziri bado unahujumu wengine jamani? Sasa mtu wa kawaida kama Dr. POLISI, hakimu, mfanyakazi ofisini nk wao wafanyaje? Sijui ni Roho korosho au ndiyo WIVU? Sijui alifaidika vipi kwa hujuma zake hizo.
Freeman kweli anajitahidi ila kumfikia Patrick haiwezekani. Yule jamaa alikuwa na kipaji alichozaliwa nacho huko Ugogoni kwa watani wangu. Anyway ndiyo hiyo watu wanasema Utauwa mwili ila ROHO yake itaendelea kukusuta. Sijui Mgonja akienda Harusini na kusikia wimbo wa jamaa anajisikiaje. Au anasikiliza redio au popote pale sauti ya jamaa, nafikiri akiwa home huwaambia watoto "hebu zimeni hiyo redio.."
 
Patrick alikuwa kiboko, wimbo wa dunia ya mashaka, Frelimo na Mabeberu siku zote zinanilazimisha kumuweka Patrick katika list ya watanzania wachache waliotumia vipaji vyao kwa ajili ya kuielimisha na kuiongoza jamii yetu.
 
Halafu unajua yeye marehemu Patric alivyokuja hujumiwa na Chediel Mgonja, aliyekuwa waziri enzi za awamu ya kwanza, hakuweza ku-recover na ndicho hasa kilichompelekea kufa mapema, Mkulu Wangu Patric Mungu amuweke mahali pema peponi,

Mdogo wake Freedom anajaribu sasa hivi ni kibendi kimoja uchwara, lakini hawezi kabisa fikia kipaji cha Patric.

Hebu nipasheni juu ya huyu Mgonja. Sifahamu kama ndo alimuhujumu Patrick. Najua alikuwa Waziri 'kijogoo' wa Elimu. alimfanyia nini?

Bahati Nzuri Mgonja yuko hai na maisha yamempiga kweli kweli! Naona ni laana.
 
Wana JF,
Mkisoma juu ya kifo cha Mwanawasa, unaona kabisa maneno ya Patrick yalikuwa kweli. Mugabe na Mafisadi tutakuwa nayo wee hadi sisi vijana tufe tuyaache yenyewe yanadunda. Mugabe yule jana nilimuona akisukuma waandishi wa habari kuingia ndani hadi huamini kuwa ana umri ule, mhhh kasheshe.
 
Hebu nipasheni juu ya huyu Mgonja. Sifahamu kama ndo alimuhujumu Patrick. Najua alikuwa Waziri 'kijogoo' wa Elimu. alimfanyia nini?

Patric na bendi yake Afro 70, walishinda mashindano na kutuwakilisha Lagos, ambako walipewa vyombo vipya vya muziki na Serikali(Mgonja) akiwa waziri wa utamaduni, Mgonja alimuahidi Patric kuwa vile vitakuwa ni vyombo vyao yaani Afro 70 baada ya kutuwakilisha kule Lagos, kumbe Mgonja alikuwa akijpinda na mkewe Patric na vyombo ilikuwa ni kumnyamazisha akijua,

By the time wanarudi Lagos, Patric alikwua ameshashituka kuwa Mgonja sio mtu mwema kama alivyotegemea, alimpom-confront Mgonja akamwambia basi na vyombo urudishe mara moja, wakati Afro 70, ilikuwa imeamua collectivelly kuuza vile vyombo vyao vya zamani baada ya kuhakikishiwa na Mgonja kuwa hivi vipya ni zawadi yao, ukawa ndio mwisho wa Patric, alijaribu kuamka tena lakini wapi, alipiga kidogo Masantula na King Kiki, baadaye akajaribu kupiga peke yake lakini kuporwa mkewe lilikuwa ni pigo kubwa mno kwake, hakuweza tena kuamka,

Mara ya mwisho alienda Zimbabwe na kurekodi album, lakini haikulipa sana halafu wenziwe aliokuwa nao Afro 70, wote walimgeuka kuwa hawana mpango wa kupiga naye tena, haikuchukua muda akatangulia mbele ya haki, long live Patric, nilikuwa ninamfahamu kwa karibu sana na ninajua majaribu yote aliyoyapitia mwishoni wa maisha yake, ilifikia mahali kuwa kutangulia kwake kwenye haki ilikuwa no bora kuliko kuendelea kuishi, kwa kweli nina kila muziki alioutunga Patric toka alipoanza kupiga Dar Jazz (Mundo Ngoma), na mpaka alipoanzisha bendi yake ya Afro 70, kuna mdogo wake aliyekuwa akiimba nye yaani Steven, yeye sasa ni mmoja wa wakurugenzi wakubwa pale Bima na hataki kabisa tena mambo ya muziki, ingawa ameombwa sana kurudia lakini amekataa kabisaa,

Mungu Akuweke Pema Patric, bado tunakukumbuka bro!
 
Mara ya mwisho alienda Zimbabwe na kurekodi album, lakini haikulipa sana

Safi sana kuhusu maisha ya Patrick. Nafurahi kusikia hiyo ingawa inasikitisha sana.

Naamini huyo mke waliachana maana mimi binafsi nilimfahamu Patrick akiwa anaishi Tandika Nyumba za NHC pembeni ya Magorofa ya Tandika. Alikuwa akipiga mziki na dada wa-Kizuru. Bahati mbaya hatukufahamu yote hayo tukadhani hakuwahi hata kuoa!

Very very stupid with Mgonja.
Unafahamu kwamba sasa hivi Mgonja ni kama omba omba?
 
FMes, sasa nimekupata.
Hivi huyu jamaa hakuwa waziri wa Elimu miaka ya 70? Si huyu alipigwa na chapati huko Mbeya (secondary ya Iyunga) kwa kutangaza kuwa wanawake shuleni watavaa suruali na wanaume kaptura? Nilikuwa nasikia sifa zake wakati huo ndiyo naanza shule ya masingi. Nilikuwa siamini mtu waziri awe mpuuzi kiasi hiki.
Juu ya Vyombo mie nilisikia story inafanana ila kidogo tofauti. Mie nilisikia kuwa alipewa vyombo vya serikali na kwenda Nigeria. Kufika huko akauza na pesa akatia ndani na aliporudi nyumbani basi serikali ikachukua vyake. Ila naanza kuamini kuwa hii ndiyo ukweli mwenyewe. Wakati huo kila kitu kilikuwa state owned. Hakuna ambaye angeliweza kusema ukweli au kumtetea Pady na kumuumbua waziri. Mie nilipokaa nakaa Ilala, mzee mmoja wa kipare pamoja na kusema alikuwa na pesa zake na watoto wawili, alinyang'anywa mkewe na Naibu waziri. Jina silikumbuki na mama ghafla akawa anakuja kapendeza huyo? Sijui sasa yuko wapi na huyo mumewe. Mhh, mawaziri wanatesa tangu zamani na wake za watu? Sasa nasikia hata Mongela alibebewa mkewe na FISADI. Kazi kweli kweli.
 
Safi sana kuhusu maisha ya Patrick. Nafurahi kusikia hiyo ingawa inasikitisha sana. Naamini huyo mke waliachana maana mimi binafsi nilimfahamu Patrick akiwa anaishi Tandika Nyumba za NHC pembeni ya Magorofa ya Tandika. Alikuwa akipiga mziki na dada wa-Kizuru. Bahati mbaya hatukufahamu yote hayo tukadhani hakuwahi hata kuoa!

1. Patric alikuwa na mke saafi sana aliyekuwa akiitwa Lidia, na ndio maana aliwahi kutunga wimbo mmoja safi sana unaitwa "Dada Lida",

2. huyu Mwanamama wa Ki-zulu, kwa jila la "Ninie" alikuwa muimbaji wa Afro 70 wa muda mrefu sana, ambaye alikuwa ameamini sana in kipaji cha Patric cha muziki mpaka akawa hataki kurudi kwao, baada ya mambo kuanza kumuendea vibaya Patric kimuziki, alikimbiwa mpaka na ndugu zake wa karibu ambao alikuwa akipiga nao Afro 70, lakini ni huyu mama peke yake alisimama naye mpaka mwisho, ingawa mwishoni alikuwa akitumia sana ganja na huyu mama,

Maisha ni tambara bovu, ninakumbuka enzi za Patric akiongea na ku-hang out mpaka na mawaziri, hata kuonana na Mwalimu akiwepo chamwino kwake haikuwa taabu, ninakumbuka enzi zake akienda kurekodi album Nairobi na kurudi na vidudu, Patric ndiye aliyekuwa bina-adam wa kwanza kwangu kumuona amevaa Raizoni na Bugaluu au Pekosi, Patric ndiye mtu wa kwanza kunipeleka muziki nikiwa in the teenager, ninakumbuka hiyo siku yaani mara yangu ya kwanza kuona live bendi ya muziki ilikuwa bendi yake inapiga kwenye ukumbi wa kikosi cha Anga, Ukonga, mara yangu ya kwanza kuona watu wazima wanacheza mziki wa Dansi na hasa kukumbatiana, I was lost wallahi! maana pale waliletwa wasichana toka shule ya Jangwani yaani Hosteli,

He was a good man na pia alikuwa na mapungufu yake kama Bin-adam, alikuwa ni mstaarabu na pia alikuwa na heshima sana kwa wengine na hasa ndugu zake, ndio maana aliwaingiza wote kwenye bendi yake na kuwaleta mjini kutoka Dodoma, I mean ingawa maisha yalipokuja kumgeuka wote walimkana kabisaaa,

Patric alipenda sana muziki wa aina ya Osibisa, na alikubalika sana ki-muziki, maana nakumbuka hata ile siku Lwambo alipokuja bongo, alimpa nafasi sana ya kupiga naye pale uwanja wa taifa, lakini mwisho wa maisha yake ulikuwa ni fedheha kubwa sana, ukweli alichanganyikiwa kabisaa Mungu amuweke mahali pema!

Very very stupid with Mgonja.
Unafahamu kwamba sasa hivi Mgonja ni kama omba omba?

Ooh yah! siku moja niliwahi kumuona kwenye viwanja vya bunge Dodoma, yaani viongozi wetu wamemgeuza Ze -Comedy! Kweli mshahara wa Dhambi ni mauti!
 
Hivi huyu jamaa hakuwa waziri wa Elimu miaka ya 70?

Enzi hizo utamaduni ulikuwa chini ya wizara yake Mgonja, yaani elimu ambayo baadaye ilitenganishwa na kuwa wizara kamili ya michezo under Sarakikya.
 
WanaJF,
Wimbo wa Patric Balisidya wa "NI MASHAKA YA DUNIA" leo nimeukumbuka tena. Huu uko ZILIPENDWA kwenye redio ya Mwana Kijiji. Hii nilishaandika mapema ila nimeona niiweke tena hasa kipindi hiki cha Msiba tata wa Wangwe.
Inasikitisha sana kuwa tangu miaka ile hadi leo uonevu uko pale pale. Si ajabu wengine wanaoonea (mafisadi), wakati huo na wao walikuwa wanaonewa. Cha kusikitisha zaidi ni hili neno "WEMA HAWANA MAISHA". Ukiusikiliza haraka haraka unaweza kusema watu kama Mwakyembe, Zitto, Mama Malecela, Dr. Slaa na wale wote wanaopigania HAKI YA MTANZANIA kila siku wanaweza KUKAA TAMAA. Lakini kabla hawajafanya hivyo nawaomba wakaangalie ile film ya Antonio BANDERAS iitwayo "The 13th Warrior (1999)." Humo kuna VIKING mmoja pamoja na kuwa alikuwa kachanjwa chale yenye SUMU na yule Kibibi Gura Malikia, na akawa mgonjwa hoi, walipomletea VITA mlangoni, alisimama na kuchukua Silaha yake na kwenda pigana (samahani kama nimechanganya) na walimuomba na kumwambia kuwa anaweza kufa alisema " ... binadamu POA ni yule anayeishi na akifa, vizazi vitamkumbuka na kumuwekea ukumbusho kama wa SANAMU, Mnara, Nyimbo nk. na si kuishi maisha marefu...." Mafisadi mnaotumia VITISHO, Mauwaji na taka nyingine kama za Mugabe mjue HISTORIA itawasau au itawakumbuka kwa upande wa HITLER, Savimbi, Stalin Joe, nk na si Upande wa Mashujaa kama Sokoine, Nyerere, Sankara, Ngwabi na Mashujaa wote wanaopingana na NYIE kwa sasa. Naomba huu wimbo uwe changamoto kwa wanaJF popote pale walipo. They will kill your body but your soul will keep GOING STRONG. Kwa bahati Tanzania siyo Russia maana huko kweli Mungu hayupo na SOUL za watu wema hupotea kimoja.... Kweli dawa ni moja tu nayo ni kuwa BEGA KWA BEGA na WEMA wetu.
Kama kwei huyu alikuwa Mpiganaji, basi ni heri TUMUENZI. Kama si Dar basi walau huko kwao Tarime apewe Mtaa au shule ya Secondary ya jina lake.
 
Hebu nipasheni juu ya huyu Mgonja. Sifahamu kama ndo alimuhujumu Patrick. Najua alikuwa Waziri 'kijogoo' wa Elimu. alimfanyia nini?

Bahati Nzuri Mgonja yuko hai na maisha yamempiga kweli kweli! Naona ni laana.

Ilikuwa ni muda wa kampeni ya jambo fulani sikumbuki gari lililo beba vifaa vya Muziki wa bendi ya Afro 70 lilipata ajali na kuharibu vifaa vingi.
Kwa vile ile ziara ilikuwa ni ya kitaifa serikali iliahidi/ilishauriwa imfidie Patrick lakini MH Mgonja litumia wadhifa wake kuhakikisha kwamba patrick halipwi hata shilingi.
Leo hii yeye mwenyewe yuko wapi??

Si hivyo tu huyu MH alichochea kwa nguvu sana zoezi la kutaifisha shule za makanisa pamoja na ukweli kwamba zilimfaa yeye mwenyewe na familia yake.

Alitaka pia kuitafisha Radio Sauti ya Injili iliyomilikiwa na kanisa la Lutherani, zoezi hilo lilishindikana baada ya kugundua kwamba matangazo ya radio hiyo hurekodowa Arusha na kurushwa kutokea katika kituo cha radio kilichoko Addis Ababa Ethiopia. Arusha hakukuwa na kituo cha radio ilikuwa ni studio ya kurekodi tu.
Ikumbukwe kwamba yeye mwenyewe ni muumini wa kanisa la Lutherani.
 
Jamani Hakuna Mwenye Pcha Ya Balisdya Hapo Wengine Hatumjui

Pezzo,
Ngoja tusubiri FMes aje maana huyo nafikiri alikuwa akimfahamu Patrick kwa karibu sana na atakuwa na uwezo wa kupata picha au tayari anazo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom