Mkulo atupe majina ya kampuni hizo na kiasi cha pesa toka kila kampuni

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,820
287,889
Pia atufahamishe kampuni hizo zilikuwa zinafanya biashara gani ya kuweza kuwa na mapesa mengi kiasi hicho. Hivi ni kweli kampuni binafsi zinaweza kuacha mapesa yao mengi kiasi hicho yapotee kirahisi namna hiyo? :confused::confused::confused:


Mkulo asisitiza fedha za EPA si za serikali
Mwandishi Wetu, Dodoma
Daily News; Wednesday,June 25, 2008 @08:41

WAZIRI wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo amesema aliyoyasema bungeni kuhusu wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu Tanzania (BoT), ndiyo ukweli na kwamba waliohusika watachukuliwa hatua.

Mkulo alisema jana kuwa fedha hizo zilikuwa ni za kampuni binafsi na zilihamishiwa (BoT) kutoka Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ya zamani.

“Kwa maneno haya, mimi sikutamka kwamba waliohusika na fedha za EPA hawatachukuliwa hatua, bali hatua zitachukuliwa baada ya Mheshimiwa Rais kupokea taarifa ya Kamati Maalumu na kuagiza utekelezaji wake,” alisema Mkulo, akitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa yaliyojitokeza wakati wabunge wakijadili Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2008/2009, likiwamo suala la EPA na takwimu.

Kwa mujibu wa Mkulo, BoT ilikuwa wakala tu wa kulipa fedha hizo hivyo hakuna mantiki ya kuhoji kwa nini fedha za EPA hazikujumuishwa kwenye Bajeti ya Serikali.

Alisema waliopata fedha hizo kwa njia zisizo halali hawana uhusiano na waliokuwa wanaidai NBC.

“Nilisema kwamba akaunti ya EPA ilitokana na akaunti za wafanyabiashara wa Tanzania zilizokuwa katika iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambao katika miaka ya 1980, walikopa kutoka nje ya nchi, malighafi za viwanda, vipuri, na zana nyingine za uzalishaji kwa njia ya suppliers credits,” alisema Mkulo.

Mwishoni mwa wiki baada ya Mkulo kuhitimisha mjadala wa Bajeti na kupitishwa na wabunge, baadhi ya wabunge wa upinzani walidai kuwa Waziri huyo amelidanganya Bunge kwa kueleza kuwa fedha za EPA zilizochotwa BoT, hazikuwa za serikali wala BoT; hivyo wakapania kuibana serikali wiki hii hasa katika hotuba ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Kuhusu takwimu, Mkulo alisema takwimu zote za Bajeti ya Serikali zilikuwa sahihi na ni jambo la kawaida kuzibadili wakati wabunge wakiendelea kuijadili.

“Serikali inarudia tena kusema kwamba hakuna takwimu za bajeti ambazo hazikuwa sahihi, na bajeti iliyoidhinishwa ndiyo iliyowasilishwa kwa kusomwa bungeni na Waziri wa Fedha,” alisema.

Kwa mujibu wa Mkulo, tofauti ya takwimu zilisababishwa na mabadiliko ya taarifa za fedha na kwamba mabadiliko hayo yalifanywa baada ya vitabu kupelekwa kwa Mpigachapa.

“Kwa kuwa taarifa ya mwisho imekuja baada ya vitabu vya bajeti kupelekwa kwa Mpigachapa, na baada ya Hotuba Bajeti kuandikwa na kuchapishwa, kiasi hiki cha shilingi bilioni 60.0 hakikuonyeshwa, bali kimeingizwa katika masahihisho,” alisema Mkulo.
 
Huyu,mkulo hana jipya,ni mwana mtandao,anajua mambo yameshawachwea,ndo anaanza kutapatap!atuambie tu ukweli vinginevyo patachimbika!
 
Afu nahisi hana mshauri mzuri, wakati mwingine mambo yakichachia busara ni kukaa kimya kwanza ukajipanga vyema, ikibidi una jishusha na kukiri kughathirika!

Kwani vyovyote vile 'iwe EPA ni ya ser.. ama si ya, hilo hali halalishi mafisadi wazichote pesa hizo period! na kamwe haliwa epushi na hukumu ya ukwapuaji huo.
 
Mkulo katumwa aseme hivyo kuonyesha njia ya ripoti ya EPA inayokuja.Hiyo ni kauli nzito ambayo ina support kubwa ya mafisadi nyuma yake.

Mwezi ujao ndipo IGP,Mwasheria mkuu na timu yake wanatoa ripoti walivyoshughulikia swala la EPA,jinsi walivyoshindwa kuwachukulia hatua wafanyabiashara walioghushi kwa kuwa pesa zilikuwa zao na waliamua kuzitunza tu ktk hiyo akaunti ya madeni ya nje.

Pinda alishasema mafisadi ni watu hatari sana na wana pesa nyingi na hiyo ripoti usishangae kusikia kama hayo Mkulo aliyosema bungeni,Usishangae kusikia hizo zilikuwa pesa za ra au manji n.k.

The movie is too political
 
Wameshatengenea mlango wa kutokea. Ujasiri huo wa kusema wameupata wapi?
Ni kwa nini hawakusema tangu mwanzo?
 
Aende wapi? Yupo!! Anakula mafao waliojilimbikiziaa....wapiga deal hao!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom