Mkulo ataka kumshughulikia Zitto kwa fedha za fisadi

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Baada ya Zitto kumbana Mkulo ktk sakata la CHC, taarifa zinasema kwamba kwa sasa kiasi kikubwa cha fedha kimetengwa kuwanunua wabunge ili wamrudi Zitto na kumuondoa katika kamati yake ya POAC.

Hata hivo, taarifa zinasema Zitto na wabunge wa kamati yake wakiwamo wale wa CCM wana msimamo mmoja na hivyo ajenda ya fisadi huyo na Mkulo wake huenda ikaota mbawa.

Tusubiri hii sinema mpya maana taarifa zinasema ina mambo mengi nyuma ya pazia hasa kwa maelezo kwamba hata CEO aliyesimamishwa aliingizwa mkenge na Mkulo kisha akamtosa.

Kama ikithibitika hii ni kashfa ya tatu ya wabunge kuhongwa ama kutaka kuhongwa ikiwamo ile maarufu ya David Jairo.
 
Hawa ccm wanalindana sana na hawatabiriki wameweka matumno mbele... Lolote laweza kutokea na hii ndio ccm siwezi kushangaaa
Zitto gangamala wananchi wapo na wewe
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu Halisi, hii kashfa nahisi itazimwa kimya kimya. Si unajua yule Mkuu wa kaya yupo yupo tu hataki kujihusisha na chochote kile chenye kashfa ndio sababu pamoja na kashfa chungu nzima kule Madini na Nishati, Ngeleja, Malima na Jairo bado wanapeta.

Hili labda Zitto alivalie njuga za hali ya juu ili kupambana na Mkullo, vinginevyo litaminywa kiaina aina na Mkullo kuendelea kula kuku zake.
 
Ama kweli Kikwete ameleta utamaduni mpya Tanzania...... ukiona kiwingu mbele wewe mwaga pesa. Hivi ndivyo alivyonunua urais na li-mkapa likakaa tu kaa boga.
 
Magamba kwa tiktak ni balaa,cha kushangaza jamaa Msoga yuko kimyaa,sijui kaweka pamba masikioni?au hii sio kazi yake?
 
Wabunge wote lazima waungane kwenye hili bila kujali itikadi za vyama vyao nakumbuka jinsi walivyo jadili issue ya CHC nakuwa kitu ki1 alichofanya Mkulo nikulidharau Bunge zima na lazima Bunge liiwajibishe Serikali iwapo haitamchukulia hatua Mkulo...Makinda tunakutazama kwenye hili kuona utareact vipi kulinda hadhi na heshima ya Bunge.
 
Tutapambana hadi mwisho Zitto sima kidete hakika mwisho tuko nyuma yako .
 
Zitto should not be trusted either as he sails in the same boat with Mkulo. He has never controverted allegations that Barrick once tipped him in an attempt to tighten his lips and deaden his acerbic remarks against the mining firm. So while he accuses Mkulo for crookedness scandal he should also remember to put his house in order.
 
Tayari mkakati wa kwanza wa Mkulo umeanza kwa Mwandishi wa JamboLeo ambaye hakika ametumwa na Mkulo na fisadi mmoja akianza kutekeleza na kesho gazeti hilo linaweza kuwa na taarifa isemayo kwamba Zitto anatumiwa na vigogo wa CHC kuwatetea na wamempa milioni 100 za kummaliza Wazir Mkulo na kwamba kiwanja anachokipigania Zitto kiliuzwa na aliyekuwa Waziri wa mipango wa Mkapa, Dr Abdalah Kigoda na siyo Mkulo. Kumekuvha
 
Baada ya Zitto kumbana Mkulo ktk sakata la CHC, taarifa zinasema kwamba kwa sasa kiasi kikubwa cha fedha kimetengwa kuwanunua wabunge ili wamrudi Zitto na kumuondoa katika kamati yake ya POAC.

Hata hivo, taarifa zinasema Zitto na wabunge wa kamati yake wakiwamo wale wa CCM wana msimamo mmoja na hivyo ajenda ya fisadi huyo na Mkulo wake huenda ikaota mbawa.

Tusubiri hii sinema mpya maana taarifa zinasema ina mambo mengi nyuma ya pazia hasa kwa maelezo kwamba hata CEO aliyesimamishwa aliingizwa mkenge na Mkulo kisha akamtosa.

Kama ikithibitika hii ni kashfa ya tatu ya wabunge kuhongwa ama kutaka kuhongwa ikiwamo ile maarufu ya David Jairo.

Zitto namwaminia kwa hoja na msimamo.Mkulo mtafuko Mdhihiri akufunde maana unataka kucheza na moto.
 
Tayari mkakati wa kwanza wa Mkulo umeanza kwa Mwandishi wa JamboLeo ambaye hakika ametumwa na Mkulo na fisadi mmoja akianza kutekeleza na kesho gazeti hilo linaweza kuwa na taarifa isemayo kwamba Zitto anatumiwa na vigogo wa CHC kuwatetea na wamempa milioni 100 za kummaliza Wazir Mkulo na kwamba kiwanja anachokipigania Zitto kiliuzwa na aliyekuwa Waziri wa mipango wa Mkapa, Dr Abdalah Kigoda na siyo Mkulo. Kumekuvha

Hizi habari za wabunge kuhongwa zinazidi kufichuka kila siku. Hii ni dalili kwamba bunge letu linaelekea kupoteza credibility yake kwa wananchi.

Kama wabunge kwa pamoja bila kujali itikadi zao wasipochukua hatua za haraka za kujisafisha na kujinasua katika kashfa hizi za rushwa basi hadhi yake itashuka sana.
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom