Mkulo apasua jipu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkulo apasua jipu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jun 14, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,420
  Likes Received: 81,470
  Trophy Points: 280
  Mkulo apasua jipu

  Imeandikwa na Shadrack Sagati, Dodoma; Tarehe: 14th June 2009 @ 09:06

  Habari Leo

  Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, amesema suala la kuondoa misamaha ya kodi kwa vifaa vinavyoagizwa na taasisi za kidini halikufanywa kwa lengo la kuua makanisa yanayojihusisha kwa kiasi kikubwa na utoaji wa huduma za kiafya na elimu, bali kuiokoa serikali kiuchumi.

  Waziri huyo pia amekanusha madai kuwa serikali imefanya hivyo kwa kuwa yeye pamoja na Rais wote ni waumini wa dini ya Kiislamu na akafafanua kuwa wanataka kukomesha tabia ya baadhi ya watu kujinufaisha na misamaha hiyo hadi kuwa mamilionea.

  “Sio mimi wala Rais ambaye ameandaa bajeti hii au kupendekeza kufutwa misamaha hii, kuna jopo la wataalamu na kule naweza kusema kuna Waislamu wawili tu, lakini wengi wao ni Wakristo, hivyo nasema sina nia ya kuua makanisa,” alisema Mkulo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana, mjini hapa.

  Mkulo alisema jopo hilo la wachumi waliobobea waligundua kuwa kuna watu ambao wananufaika na misamaha inayotolewa kwa taasisi hizo za kidini, hali inayoikosesha serikali mapato mengi. Alisema hatua hiyo ya kuondoa msamaha huo wa kodi haikulenga kuzipunguzia taasisi za kidini na zisizo za kidini uwezo wake wa kuendelea kutoa huduma za maendeleo ya kijamii kwenye nyanja za elimu, afya na huduma za maji.


  Pia alisema hatua hiyo haikulenga kuwaondolea unafuu wa kodi kwenye bidhaa zinazotumika kwenye majukumu yao ya huduma ya kiroho na ibada, ila alisema hatua hiyo inakusudia kuondoa mianya kwa wafanyabiashara wanaovitumia vyombo vya dini kujitajirisha.

  Alifafanua kuwa kuna watu ambao wanaingiza nchini vifaa vya kibiashara bila kulipa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kupitia misamaha inayotolewa kwa vyombo hivyo, hali ambayo imekuwa inaikosesha serikali mabilioni ya fedha. “Kuna watu wamekuwa mamilionea kwa kutolipa kodi kupitia mgongo wa dini…kwa kweli hawa wanaopata hii misamaha wanaitumia vibaya, kwani wanasingizia dini wakati wanaenda kufanya biashara,” alisema Mkulo.

  Waziri huyo alitoa mfano wa moja ya madhehebu lililoagiza mabati 4,000 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa likatumia mabati 200 tu na mengine mmoja wa viongozi wa kanisa hilo akaenda kuyauza kwa bei ya soko. Pia alitoa mfano wa madhehebu ya dini ambayo yaliagiza tani 5,000 za sukari kutoka Malawi kwa ajili ya kituo cha watoto yatima, lakini tani tano tu zilienda Singida kwenye kituo hicho na tani zingine zilizobaki zilikwenda Makambako na kufungwa kwenye mifuko na kuwauzia wananchi.

  Katika kuelezea namna baadhi ya watu wanavyonufaika na misaada hiyo, alitoa mfano wa kiongozi mmoja wa kidini aliyeagiza magari kwa ajili ya kanisa lakini akayatumia magari hayo kwa kuanzisha kampuni ya kitalii (tour operator) kwa ajili ya kukodisha kibiashara. Alitoa mfano wa taasisi zisizokuwa za kiserikali (NGOs) kuwa kuna zinazotumiwa na wafanyabiashara kuagiza vifaa mbalimbali sio kwa ajili ya matumizi ya kijamii bali kibiashara.

  “Hawa wanatumiwa na wafanyabiashara licha ya kuwa zipo chache zinafanya kazi vizuri.” Hata hivyo, Mkulo alisema jopo hilo la kitaalamu ambalo limefanya uamuzi huo limeona kuwa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani uendelee kutolewa kwa kwa vifaa vya elimu, huduma za afya na vifaa vya hospitali ambavyo vitaagizwa na taasisi za kidini.

  Ila alisisitiza kuwa vifaa vitakavyoingizwa na taasisi za kidini kwa lengo la biashara ni lazima zilipewe ushuru na akatoa mfano taasisi ya St Gasper inayoendesha hoteli na zingine zinazofanya biashara hiyo iwapo zitaagiza vifaa vya hoteli ni lazima zilipie kodi. Alisema serikali haiwezi kukubali kuendelea kupoteza kiasi kikubwa cha fedha kwa kutoa msamaha kwa vifaa ambavyo sio vya kiroho au ibada ila wanataka kuhakikisha vifaa vya biashara vinatozwa kodi vyote.

  Waki huo huo, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limeiomba serikali kuondoa mara moja ushuru wa bidhaa na huduma za mashirika ya dini ili shirika hilo liweze kutimiza wajibu wake kikamilifu kwa jamii. Taarifa ya Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Shaaban Simba, imesema kuwa kuwepo kwa ushuru huo kutapunguza wachamungu nchini, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa nchi na maendeleo kwa ujumla.

  ‘’Mashirika ya dini hutegemea misaada na michango ya waumini na wahisani mbalimbali na kamwe hayafanyi biashara au kupata faida yoyote katika shughuli zake, misaada kama hiyo inasaidia masikini, walemavu, wagonjwa na maeneo yenye machafuko na vita,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

  Amesema kwa kuwa serikali imeshindwa kutekeleza huduma zake katika maeneo mbalimbali, mashirika ya dini yanalenga kutoa huduma kwa wananchi katika mazingira magumu na hasa vijijini na maeneo mengine duni ya mijini. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, athari ya ushuru huu ni pamoja na wahisani kupunguza ama kuondoa misaada, huduma kwa wanyonge, kufifia na mashirika ya dini kushindwa kutoa huduma zake za msingi za ibada kujenga misikiti na kuchapisha vitabu.

  Naye Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini amesema serikali ilipaswa kuzungumza na taasisi za dini kabla ya kutangaza katika bajeti kuyafutia msamaha wa kodi mashirika ya dini na asasi za kirai. Akizungumza na HabariLeo Jumapili mapema jana, Kilaini alikiri kuwepo kwa taasisi nyingi za dini na kwamba zipo ambazo zinaweza kutumia msamaha huo vibaya hata hivyo alitahadharisha kuwa ni serikali ndio inayoziandikisha na inayopaswa kuzidhibiti pia.
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Jun 14, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  This is pure nonsense!.. sasa ikiwa kuna watu waliokutwa na makosa hayo kwa nini serikali isiwachukulie hatua na kuwapa adhabu kali ili kuweka mfano badala yake wanaovihukumu vyombo vyote...

  Hatua hii inaonyesha wazi jinsi serikali yetu inavyochukua njia za mkato kwa kila tatizo kwa sababu wao hawana muda wa kutimiza wajibu wao wa kazi. Kama kuna watu hutumia vyombo hivi kujinufaisha basi ni wakati mzuri wa serikali kukomesha vitendo vya watu hao kwa kuwafungulia mashtaka na kuweka regulations zinazoziba ufa uliotumiwa na watu hawa na sii kuwaasdhibu na wasiokuwemo..

  Kuwaondolea msamaha wa kodi vyombo hivi ni kuwazidishia matatizo wananchi wanaotegemea misaada hii. Na ajabu ni kwamba vitu vinavyozungumziwa na waziri ni vitu ambavyo vinaweza kabisa kuzuilika..

  Kama shirika au kanisa limeagiza mabati 4,000 na only mabati 200 ndiyo yametumika..mwisho wa mwaka wanapokabidhi mahesabu yao, basi hilo shirika NGO au kanisa litatozwa kodi ya mabati 3,800 ambayo yameingizwa na kuuzwa kwa wananchi..

  Itakuwa ni kazi ya kanisa kumtafuta mchawi wao, kesho watakuwa makini zaidi kutika kuendesha shughuli zao..

  Muhimu kwetu wananchi, serikali itakuwa imevuna mambo matatu kama sii manne..

  1. Kanisa limeezekwa mabati 200..
  2. Wananchi wamepata kuezeka pia nyumba zao mabati 3800.
  3. Wabangaijazi, Waezekaji wamepata ajira..
  4. Serikali itakusanya kodi yake toka mabati 3,800..

  Sisi wote tunafahamu mchezo mchafu unaotumiwa na watu kupitia vyombo hivi..lakini mara zote wanafanya hayo kutokana na mfumo mbaya wa regulations zilizowekwa kwa sababu tunaogopa lawama.

  Ni uzembe mkubwa sana kwa serikali yetu kila mara kutumia njia za mkato hasa pale wanapoona mapungufu..Wao wanatuibia sijaona msamaha wa kodi zao ukiondolewa, tunaweza kuweka mabillioni ya fedha ambayo hawa hawa viongozi wameingiza nchini kwa kutumia msamaha wa kodi kwa ofisi zao lakini mzigo umeshuka majumbani mwao..
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Jun 14, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  ..viongozi wa Kiislamu pamoja na Kikristo wamelalamikia uamuzi wa waziri wa fedha.

  ..sijui kwanini Waziri Mkullo akaamua kuwajibu viongozi wa Kikristo peke yao.

  ..halafu ktk utetezi wa hoja yake ni kwamba jopo la wataalamu waliompa ushauri wa kuondoa misamaha ya kodi lilikuwa na idadi kubwa ya Wakristo kuliko Waislamu.

  ..hoja ya namna hii niliwahi kuisikia toka kwa Raisi Kikwete wakati alipodai kwamba hoja ya Mahakama ya Kadhi iliwekwa kwenye ilani ya CCM na viongozi Wakristo wa chama hicho.
   
 4. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  ...
  Unatupeleka wapi?
   
 5. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #5
  Jun 14, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  kelele za nini? wakati viongozi wenu walisema JK chaguo la Mungu? hamjasoma dozi ya MKJJ malipo hapa hapa! mnafikiri Mungu ni Athumani?
   
 6. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  This is high time watu wote wakalipa tu kodi, wabunge, mawaziri, NGOs, n.k!

  Waendelee kusamehewa hadi lini?

  Mkulo anasema msamaha wa kodi ilikuwa about 30% ya budget! Kumbe basi hatuhitaji hata misaada ya nje kusaidia budget..tukusanye tu kodi kama Kenya wanavyofanya!
   
 7. S

  Semjato JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2009
  Joined: Jun 26, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kabisa..
  mi sioni malalamiko yanatokea wapi tena wakati hili suala litapelekea kuongezeka kwa kipato cha serikali..nadhani serikali iangalie namna za kuendelea kupunguza misamaha zaidi isiishie hapo,kila anayeweza kubanwa alipe kodi.
   
 8. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  hapa ndio viongozi wetu wanaposhangaza.kuna makampuni makubwa mengi wananjia zao za kukwepa kodi na serikali inajua, hao hawasumbuliwi.Lakini mtu wa chini wao ndio wanajiona kila siku ndio mzuri kwa kumbana inapokuja swala la kodi.
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Jun 14, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  BinMgen,

  ..ninachojaribu kusema hapa ni kwamba masuala ya Dini sasa hivi ni tete sana hapa kwetu.

  ..sasa ni vizuri basi hawa viongozi wetu wakawa makini zaidi ktk kuyazungumzia.

  ..kumbuka kwamba ktk kuwasilisha malalamiko yao viongozi wa Dini wameweka pembeni tofauti zao za kiimani. viongozi wa dini wanapigania misamaha ya kodi kwa taasisi zote za kidini.

  ..binafsi naona Waziri Mkulo "ameteleza" kwa kuzicharukia taasisi za Kikristo ktk suala hili.
   
 10. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,713
  Likes Received: 3,120
  Trophy Points: 280
  swala la kodi ni lazima kwa kila taasisi iwe serikali, mashirika ya umma, makanisa,misikiti,NGO, Mashirika ya dini, viongozi wa serikali n.k tunalipa wananchi tulio na kipato cha chini halafu wenye vipato vikumbwa wanasamehewa.. wote tulipe kodi period!!! kama serikali inafahamu mashirika ambayo yalikiuka sheria za ulipaji au utozwaji kodi basi sheria na ichukue mkondo wake.
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Jun 14, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Pakawa,
  Mkuu haya ndio maneno..
  Maamuzi yenye haki hufuata sheria sii kutunga sheria juu ya sheria isiyofanya kazi yake..
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mkandara,
  Utadhani ulikuwepo kwenye fikra zangu. Kila kitu ulichosema ndicho nilichofikiria mimi.
  Huwezi kubadilisha sheria just because a few individuals misused that law. Kuna vyombo vya sheria vya kuwakabili. Kwa nini havifanyi kazi yao?
   
 13. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Hawa viongozi wana maswali mengi sana ya kujibu.

  Kama serikali iliyajua haya yote, je wahusika wamefikishwa mahakamani?

  TRA imechukua hatua gani kukusanya kodi kutoka hizo bidhaa zilizotumika nje ya makusudio ya awali?

  That does not make any sense if the government knows what's going without taking any action.

  What's wrong with these people? Can somebody tell me!

  What's so hard about this? Do you need rocket scientist to solve this?
   
 14. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #14
  Jun 14, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Sijui kwa nini serikali imechelewa kurejesha kodi kwa hizi NGOs na mashirika ya kidini. Basically hakuna sababu ya wao kutokulipa kodi.
  Wakati mashirika haya yalipokuwa na msamaha wa kodi, ilitolewa sababu gani ya msamaha huo?
   
 15. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #15
  Jun 14, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Hii ngoma bado mbichi kabisa.......sijui ngoja tusubiri tamko la makanisa hasa CCT ...
   
 16. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #16
  Jun 14, 2009
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Mimi pia naona serikali ingeweka utaratibu (kwa kutumia jopo hilo la "wataalam") kutengeneza upya sheria au "legislation" kwamba ni nani wanapaswa kupata msamaha wa kodi, adhabu gani itakuwepo endapo watakiuka legislation hio na orodha yote ya hizo taasisi iwepo pale hazina na iwe inaratibiwa na kitengo maalum.

  Haya yanayoelezwa hapo na waziri ni porojo tupu na isio na uzito wowote.
   
  Last edited: Jun 14, 2009
 17. M

  Masatu JF-Expert Member

  #17
  Jun 14, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo huku ndio 'kupasua jipu"
   
 18. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #18
  Jun 14, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  kapasua jibu sio jipu, inaelekea jibu limetengezwa kwa kioo!!!
   
 19. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #19
  Jun 14, 2009
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Jamani polepole, hili suala nadhani Mkullo akulieleza vizuri.

  Kodi ya VAT imeondolewa kwenye vitu ambavyo havitumiki moja kwa moja kwenye kusaidia jamii kiroho.

  Mkullo kosa lake ni hapo hapo kusamehe VAT ya mafuta kwa kampuni za madini kupitia agizo la kwenye Government Gazette la 2005.

  Sasa hapa ndipo credibility ya serikali inaposhuka, vipi tupate hela za VAT za NGO, wakati Barrick na wenzao wanapewa VAT free fuel???

  Hapo ndipo kichaa cha serikali kinaposhindwa kwenye public opinion!!!
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Jun 14, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Moelex23,

  Mkuu mimi wala sifiki huko kwa Barrick na jamaa wengine maana hiyo ni sheria iliyopitishwa na inaweza kufanyiwa marekebisho bila kuathiri mfumo mzima wa kodi na huduma zinazotakiwa..

  NGOs ni non profit Organisation iwe kanisa au chombo cha watu wahisani.. Lengo lake ni kutimiza huduma pale serikali na wafanyabiashara wameshindwa kutimiza aidha iwe ni maswala ya dini, faida au yanayohusiana na jamii kidini..Sheria imeshatolewa wapewe msamaha wa kodi na wananchi tulikubali na kupitisha bungeni tukizingatia mahitaji ya jamii husika ktk huduma hizo...

  Hatuwezi kubadilisha sheria hizi kwa ushahidi ambao serikali yenyewe kwa uzembe wake wameshindwa kuchukua hatua zinazotakiwa kisheria..kuepa kodi kiujanja ni criminal case..

  Kwa mfano wako wa Barrick, ikiwa Barricks wamepewa msamaha wa kodi ya VAT kisha wakaingiza mafuta zaidi ya kiwango kinachohitajika wakayauza nje kwa wananchi..na ushahidi upo iweje tuondoe msamaha kwa mashirika yote ya njebila kuwafikisha Barricks ktk vyombo vya sheria! ili kuipa nguvu sheria iliyotangulia badala yake tunatafuta sheria nyingine inayovunja sheria ya kwanza kwa makosa yasiyohusiana..

  Kwa nini tusiwaadhibu Barricks kwa kuvunja sheria badala yake tunayaadhibu mashirika yote ikiwa ni pamoja na yale yanayotumia vizuri misamaha hiyo..

  This is my understanding! kama nimeelewa vibaya mkuu naomba somo zaidi..
   
Loading...