Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,254
Kutenga ni tisa, kumi ni kuwa wabunge watapitisha licha ya kuliona hilo na kulilalamikia
Hiki kitu ndiyo kinanitibua mpaka basi tu.... Shocking and disturbing to sane minds!!
Kutenga ni tisa, kumi ni kuwa wabunge watapitisha licha ya kuliona hilo na kulilalamikia
Mkuu, sidhani kuwa wanazungumzia kitumbua kimoja au andazi moja. Hawa huwa wanatumia sambusa zaidi, tena si moja. Nadhani pia hualika watu kuwatembelea ili wapate chai na sambusa. Kaazi kweli kweli. Ngoja waje kuniomba kura waone.Kikombe gani cha chai kinagharimu kiasi hiki... wenye datas za gharama halisi hebu tuwekeeni hapa kwa tathmini kikombe cha chai pia kitumbua kimoja au andazi moja vinagharimu kiasi gani hapo Dar...
1.hapo ni chai tu, siku tukija kuambia matumizi mengineyo kama ya stationaries and other facilities; huchelewi kuja kupewa figure ambayo utakuta kila mfanyakazi wa serikalini anatumia kalamu 3 kwa siku, rim 1 ya karatasi kwa siku, toilet paper piece/roller moja kwa siku etc etc etc
Au hii chai inayoombewa pesa Bungeni si chai ya kwenye kikombe????? Isije kuwa hatujawaelewa viongozi wetu hawa. Si ajabu ni chai ya kwenye kibahasha.
Maana wakikaa kwenye warsha/kongamano/semina na mikutano mingine yenye majina mbalimbali hupewa chai na vitafunwa vyake, chakula (caterer wanaemjua wenyewe), na mwisho kibahasha kirefu.
Wakifunga mkutano wao wa siku kibao, wanafanya sherehe. Yaani nchi hii....sijui tutafika wapi mwishowe.
Kwanini hizo seminar wasizifanye kwa mtandao (Webinar)?
Umesahau kuwa Mkulo anatafuta pesa za kampeni next year? na kawatengea mawaziri wenzake kama huyo wa miundo mbinu ini ziwanusuru kurudi bungeni tena mwakani. Huoni kuwa ni aibu kama ulikuwa waziri kushindwa ubunge?.Ndiyo maana hili li nchi letu haliendelei. Hela zinavuja kila upande... mara posho ya hili mara posho ya lile, mara fungu la chai...n.k. na kinachozalishwa wala hakilingani na matumizi! Grrrrr,
sa' mishahara yao minono minono wanatumia kufanyia nini iwapo chai na vitumbua vinanunuliwa kutoka kwenye fungu la walipa kodi - kununulia movie za kinajeria?!!
Au hii chai inayoombewa pesa Bungeni si chai ya kwenye kikombe????? Isije kuwa hatujawaelewa viongozi wetu hawa. Si ajabu ni chai ya kwenye kibahasha.
Maana wakikaa kwenye warsha/kongamano/semina na mikutano mingine yenye majina mbalimbali hupewa chai na vitafunwa vyake, chakula (caterer wanaemjua wenyewe), na mwisho kibahasha kirefu.
Wakifunga mkutano wao wa siku kibao, wanafanya sherehe. Yaani nchi hii....sijui tutafika wapi mwishowe.
Kwanini hizo seminar wasizifanye kwa mtandao (Webinar)?
Wakati mnashangaa hayo, mpasha habari wangu amenieleza kuwa kuna Idara ndani ya Wizara ya Miundombinu imejitengea mabilioni kwa ajili ya maofisa wake kwenda safari za nje na masomo huko ughaibuni, huku idara hizo zikiwa na watumishi wachache sana. Waheshimiwa wabunge mnaombwa muombe maelezo ya kutosha kuhusu matumizi hayo ya kutisha yaliyotengwa kwa ajili ya watu wachache.
Mkuu nimesoma hii habari nimebaki kichwa chini, yaani watu wana amua kuiba mchana kweupe! Jamani chai gani ya milioni 1.5 kwa siku?
Halafu hawa watu wanajilipa mishahara minono, bado wanajiwekea bajeti nono za vyai ma ofisini? vipi yule daktari anaye kesha akiokoa maisha ya binadamu wenzake hata maji ya moto hapewi kazini kwake?
Kwakweli nchi ina wenyewe.. ndo maana hadi wanajisahau na kutukana watu hovyo
Hivi credibility ya viongozi wetu wengi iko wapi? Kwanini wanaendekeza mambo yanayotia shaka kuwa wanataka kufanya wizi au kutengeneza mazingira ya fraud?Kibaya hata wafanye tatizo gani, bado wamo tu.Kwa hali hii ya kunywa chai ya gharama kuliko lunch na diner tusahau kabisa mambo ya maendeleo!!
Pamoja na hayo, kama kweli 'chai' hiyo ni ya kiwango cha milioni 1.5 kwa siku inatisha.