Mkulo aitengea wizara yake milion 500 za chai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkulo aitengea wizara yake milion 500 za chai

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malafyale, Jun 18, 2009.

 1. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  watz wenzangu nimesikitika sana kusoma habari hii kwenye bajeti yetu ya mwaka huu.Baada ya serikali kutenga bilion 34 kwa safari za nje;ngoma haikuishia hapo,pia ikatenga jumla ya billion 19 kwa ajili ya wizara zake kwa"chai" kwa mwaka ujao,huku wizara ya Fedha ikipewa million 500 na wizara ya Miundombinu wakichota million 226!
  Kwa mfano wizara ya Fedha imetengewa million 500 ndani ya mwaka mmoja,ndiyo kusema kila siku wizarani hapo zitatumika milion 1.5 kwa ajili ya chai ikiwepo jumamosi na jumapili siku ambazo hamna kazi wizarani!je hii ni halali?
  Dunia ipo kwenye msuko msuko mkubwa sana wa kiuchumi,iweje tz watenge billion 19 kwa chai?hela hizi zingetumika kulipa walimu wanaogoma kila siku tusinge songambele kimaendeleo?Hela hizi zingeingizwa kwenye maendeleo tungekuwa wapi?kwa nini Mkulo atengee nusu billion wizara yake kwa chai?TUJADILI

  NB.HABARI HII IPO KWENYE GAZETI LA MWANANCHI,soma hapo chini.
  Date::6/17/2009
  Wabunge wahoji Sh19bn kwa ajili ya chai, vitafunwa?

  Ramadhan Semtawa na Tausi Mbowe, Dodoma

  WABUNGE wameendelea kuichambua Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2009/10, huku mbunge akihoji uamuzi wa serikali kutenga Sh19 bilioni kwa ajili ya chai na vitafunwa kwa wizara mbalimbali.


  Kiasi hicho cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya chai na vitafunwa, kimewekwa katika kipindi ambacho nchi inapita katika wakati mgumu kiuchumi kufuatia mtikisiko wa uchumi duniani.


  Akichangia hotuba hiyo katika siku ya tatu ya mjadala wa hotuba bajeti, Mbunge wa Kojan, Salimu Yusuph Mohamed (CUF) alisema kiasi hicho cha fedha ni kikubwa ikizingatiwa kwamba, Watanzania walio wengi wanaishi katika dimbwi la umaskini.


  “Tumeona bajeti ya safari za nje ni Sh34 bilioni na leo nimepitia bajeti hii naona kuna Sh19 bilioni ambazo zimetengwa kwa ajili ya bajeti ya chai kwa wizara mbalimbali, hii inashangaza sana. Iko wapi huruma ya serikali au ndiyo ile style (mbinu) ya mamba, ambaye anamuua na kumla binadamu huku machozi yakimtoka; utafikiri analia kumbe anafurahi. Kwa hiyo serikali nayo inafanya ‘style’ ya mamba kwa wananchi.”


  Akitoa mchanganuo huo kwa baadhi ya ya fungu la chai za wizara, alisema Wizara ya Fedha na Uchumi imetengewa Sh500 milioni huku wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ikitengewa Sh 226.3 milioni.


  “Chai siyo mbaya, lakini tunapaswa kuangalia nchi yetu iko katika kipindi gani kwani sasa tuko katika wakati mgumu, hivyo kutenga kiasi hicho kwa ajili ya chai tu, nafikiri si sahihi,” alisisitiza mbunge huyo.


  Alikumbusha bunge kwamba, limepunguzwa muda kukutana ili kubana matumizi, hivyo hakuna sababu za kuwa na matumizi makubwa katika mambo yasiyo muhimu sana kwa taifa.


  Mbunge huyo alihoji: “Tumepunguza muda wa mkutano wa Bunge ili kubana matumizi, sasa haya mambo mengine ambayo tumeona kama safari za serikali kutengewa Sh34 bilioni yana maana gani?”


  Kwa ufafanuzi, alisema Watanzania walio wengi kwa sasa wanaishi katika hali ngumu ya umaskini kutokana na kuwa na kipato kidogo, ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji ya maisha.


  Mbunge huyo akisisitiza hilo, alisema hata takwimu za kimataifa (Malengo ya Maendeleo ya Milenia –MDGs) zinataka nchi zote duniani kupunguza idadi ya watu maskini wanaopata dola moja kwa siku.


  “Hata hapa ndani tulipo, hebu kwa mfano chukua Sh 2,000 umpe mtu, unafikiri ataishi vipi, ataigawa na kuitumia vipi fedha kama hiyo?” alihoji.


  Kwa upande wake Mbunge wa Kasulu Magharibi Profesa, Kilontsi Mporogomyi (CCM), aliwashambulia baadhi ya wabunge ambao wanaisifia serikali badala ya kukaa na kuikosoa kwa kuipa changamoto.


  “Hebu wabunge tuache utani hapa ndani, hatuko hapa kuisifia serikali ni kweli tunaangalia Progress (maendeleo), lakini hata Marekani wabunge wakiingia bungeni wanaiambia serikali fanyeni hivi,” alisema na kuongeza:


  “Sasa hapa, sisi tunataka kuisifia serikali, unaisifia serikali wakati baba na mama yako wanaishi kwa umaskini wa kutisha vijijini kule? Huu ni utani!”


  Profesa Mporogomyi ambaye aliwahi kuwa Naibu Waziri miaka ya nyuma, alisema kuna umuhimu wa kuwekwa miundombinu imara ya kiuchumi ili kuwaondolea Watanzania umaskini.


  Kuhusu bandari, alisema ni aibu kuzungumzia suala hilo kwani zipo nchi ambazo uchumi wake unaendeshwa kwa bandari tu.
   
 2. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu nimesoma hii habari nimebaki kichwa chini, yaani watu wana amua kuiba mchana kweupe! Jamani chai gani ya milioni 1.5 kwa siku?

  Halafu hawa watu wanajilipa mishahara minono, bado wanajiwekea bajeti nono za vyai ma ofisini? vipi yule daktari anaye kesha akiokoa maisha ya binadamu wenzake hata maji ya moto hapewi kazini kwake?
  Kwakweli nchi ina wenyewe.. ndo maana hadi wanajisahau na kutukana watu hovyo
   
 3. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Inabidi wawekewe maji ya bomba yaliyosafi ili yawe mbadala wa chai maana haya hayana gharama kubwa...

  Kama chai, chai watapewa na familia zao... Ya nini chai nyumbani, chai maofisini tena kwa fedha za walipa kodi halafu chai kwa mama ntilie...

  Maji ya bomba yatawatosha... kama ni utapiamlo au kwashakoo , kichocho au taifodi... maji hayo ya bomba yatawapa changamoto wizara inayohusika na maji kuyasafisha ili wenzao wasipatwe na maradhi yatokanayo na maji...

  Kama wizara ina wafanyakazi 1000 wanaofanya kazi kwa siku ina maana kila siku mtu atapewa si chini ya Tsh 1500... kwa mwaka wenye siku 365 ukiondoa sikukuu za kitaifa...

  Kikombe gani cha chai kinagharimu kiasi hiki... wenye datas za gharama halisi hebu tuwekeeni hapa kwa tathmini kikombe cha chai pia kitumbua kimoja au andazi moja vinagharimu kiasi gani hapo Dar...
   
 4. K

  Katiki Lamsala Member

  #4
  Jun 18, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 47
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Wakati mnashangaa hayo, mpasha habari wangu amenieleza kuwa kuna Idara ndani ya Wizara ya Miundombinu imejitengea mabilioni kwa ajili ya maofisa wake kwenda safari za nje na masomo huko ughaibuni, huku idara hizo zikiwa na watumishi wachache sana. Waheshimiwa wabunge mnaombwa muombe maelezo ya kutosha kuhusu matumizi hayo ya kutisha yaliyotengwa kwa ajili ya watu wachache.
   
 5. D

  Dina JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2009
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Hee Mungu wangu tunusuru! Are they serious? Umefika muda wa ku-review taratibu za maofisi ya serikali zetu. Nchi za wenzetu si nazo zina serikali? Huu ndio upuuzi wanaofanya na wao? Yaani pesa yenyewe portion yake unapewa mkono na nchi wahisani, halafu bado unaweka bajeti yote hiyo kwa chai! Je ni lazima wafanyakazi wapewe chai ofisini? Au vinawekwa na visingizio vya chai za wageni?
   
 6. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ndiyo maana hili li nchi letu haliendelei. Hela zinavuja kila upande... mara posho ya hili mara posho ya lile, mara fungu la chai...n.k. na kinachozalishwa wala hakilingani na matumizi! Grrrrr,
  sa' mishahara yao minono minono wanatumia kufanyia nini iwapo chai na vitumbua vinanunuliwa kutoka kwenye fungu la walipa kodi - kununulia movie za kinajeria?!!
   
 7. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Waongezewe haziwatoshi hizo...............
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kutenga ni tisa, kumi ni kuwa wabunge watapitisha licha ya kuliona hilo na kulilalamikia
   
 9. M

  M$awa Member

  #9
  Jun 18, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Holly Mackerel !!!
   
 10. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu, huko kwa wenzetu wengi wao ni mwendo wa sandwich tu. Kila mmoja analeta zake kutoka nyumbani kwake kama anapenda. Fridge na microwave ziko provided kwa wasiopenda kula visivyotengenezwa majumbani mwao. Otherwise ni mwendo mdundo kwa canteen services, si mishahara wanalipwa bwana, kwanini wapewe chai ya bure?! khaaa!

  Kwa hiyo Millioni 500 mambo kibao yangeweza kufanyika.

  -- Inatosha kabisa kununulia mabasi matatu mapya kwa ajili ya kubeba wanafunzi asubuhi kwenda mashuleni na kuwarudisha. We can work out gharama za mafuta.

  -- Inatosha kununulia shule za msingi 20 computer mbilimbili na kuzilipia umeme wa mwaka.

  -- Inatosha kukarabati hospitali moja ya wilaya katika kiwango kikubwa.

  Kama hayo hayafai..... basi waanzishe mgahawa wa nguvu hapo hapo na kwenye ofisi zake za kanda. Mgahawa huo utakuwa moja ya kitega uchumi chao kwa ajili ya kuhudumia wageni mbalimbali wanaotembelea ofisi.
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Hivi credibility ya viongozi wetu wengi iko wapi? Kwanini wanaendekeza mambo yanayotia shaka kuwa wanataka kufanya wizi au kutengeneza mazingira ya fraud?Kibaya hata wafanye tatizo gani, bado wamo tu.Kwa hali hii ya kunywa chai ya gharama kuliko lunch na diner tusahau kabisa mambo ya maendeleo!!
   
 12. B

  Bobby JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Infact mimi wala sishangai hizo 500m kutengwa kwa ajili ya chai ya mkulo. Kutokushangaa kwangu ni kutokana na story niliyopata kwa mshikaji few weeks ago. Jamaa alikuwa ananishawishi nihamie serikalini kwani mambo ni mazuri kuliko watu wanavyodhani. According to him mshahara kwa sasa ni mzuri tu lakini pia wanalazimishwa kusoma shule na kulipwa juu. Alitoa mfano wa jamaa ambaye anasomeshwa masters na serikali gharama zote 100% zinalipwa na serikali, kama haitoshi anapewa 10m kwa ajili ya kujikimu. Lakini pia mshahara wake anaendelea kulipwa in full. Mimi nikamtania kwamba nikija huko nitasoma maisha yangu yote maana kusoma kunalipa kuliko kufanya kazi akaniambia nimechemsha ukiwa kazini inalipa zaidi kwani safari nyingi na mambo fulani kibao. So hii ndio Tanzania jamani, wakati majority huko vijijini wanaishi kwa less than a a dollar per day, serikali yao inatumbua kodi zao kama inakichaaa. Mimi ninachanganyikiwa na roho inaniuma sana sana kwa kweli sielewi nifanye nini to help poor tanzanians ambao kila kukicha umaskini wao unaongezeka kwa gharama ya matanuzi ya mkulo na wenzie.
   
 13. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  1.Tuelewe hizi chai serikalini hazinywewi na kila mfanyakazi - zinanywewa ofisi kubwa, na hata kama wafanyakazi wa kawaida watakunywa basi ni ile sturungi tena ya mkono mmoja ambayo haizidi hata sh.200/- kwa kikombe maana hapo kuna majani ya chai na sukari vijiko vya chai 2!

  2. Hizi chai za serikalini huwa zinatia aibu wakati mwingine.Chai yenye kugharimu mamilioni siyo ile ya kawaida....hiyo ni ile ya mikutano/vikao.
  Unakuta kuna mkutano muhimu unaendelea tena unashirikisha watu kutoka hata taasis za kimataifa..mara utaona wahudumu wametinga ndani na masinia yaliyosheheni mapande ya kuku, chapati,mayai,maandazi, vitumbua, biskuti.Bado chai, kahawa, soda n.k.Shughuli inakuja wakati watu wananawishwa maji kwenye mabeseni ....halafu watu wanaanza kushambulia makulaji hayo! Unakuwa siyo mkutano tena bali fujo tu..watu hawasikilizani tena wala mawazo hayapo tena kwenye kikao bali kwenye ulaji.
  Huu siyo ustaarabu jamani...niliwahi kusikia mlami mmoja akikebehi... we are going for the chicken meeting again today!..hii dharau tunajitakia wenyewe Watanzania...kwa maana mikutano ya wenzetu unakuta kuna maji moto, kahawa, majani ya chai,maziwa ..imezidi sana kuna biskuti.Na hivi haviwezi kuharibu kikao...TUBADILIKE...KAMA KUNA WENZETU WAKO SERIKALINI CHONDECHONDE JARIBUNI KULETA MABADILIKO MAANA HIZI CHAI NI FEDHEHA TUPU!
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Jun 18, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Maskini Mitanzania mtaendelea kuwachagua na kuwapigia makofi kila kukicha wizi mtupu hawa na walaaniwe wanavimbiana mitumbo bilioni 19 kwa ajili ya chai na vitafunwa??? Mungu wangu hii imenikasilisha sana.
   
 15. B

  Bobby JF-Expert Member

  #15
  Jun 18, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Mi sishangai hilo la 500m kwa chai ya mkulo. Hivi do you know kwamba kuna watu wanasomeshwa na serikali kwa kulipiwa gharama 100% then wanapewa 10m ya kujikimu? Kama haitoshi mishahara yao wanaendelea kulipwa 100% Mimi kuna swali sipati jibu lake siku zote kwamba HIVI HII SERIKALI NI YA WATANZANIA AMBAO WANAISHI KWA LESS THAN DOLLAR PER DAY AU NI YA WAAMERIKA? Maana frankly speaking matumizi ya serikali tena katika kipindi hiki kigumu jamani yantia kichefuchefu.
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Jun 18, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mala mia % bora wakoloni warudi tu tujue mmoja waje wawanyoshe viongozi wetu ambaoa ni wavivu wa kufikiri na ninajua tungeendelea zaidi ya hapa....sasa hivi kimaendeleo tunapigwa bao na Msumbiji ambao juzi juzi walikuwa maskini wa kutupwa leo hii kule wapo juu.
   
 17. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #17
  Jun 18, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  "ndiyo kusema kila siku wizarani hapo zitatumika milion 1.5 kwa ajili ya chai ikiwepo jumamosi na jumapili siku ambazo hamna kazi wizarani!je hii ni halali?"

  Huu ni ufisadi laivu!! Chai kwa siku pesa yoote hiyo!!?? Haiwezekani!!
  Then kila siku kwa mwezi hamna jumamosi, j'pili na sikukuu!!!! Pana kitu hapa, hebu tutafakari kwa kina inawezekana CCM wanatafuta pesa za uchaguzi!
  Hiyo chai..ah! Wizi kabisa huuu!
   
 18. KIFARU

  KIFARU Senior Member

  #18
  Jun 18, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 172
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  duuhh, kweli serikali ni kikundi cha watu sio wananchi, hiyo ni chai tu,sipati picha marupurupu yao mtu anapokua ametoka kikazi inakuwaje? kwa tz nadhani hili tatizo la anguko la uchumi hatunalo wanandugu, na kama tunalo viongozi wana upungufu mkubwa katika uzalendo na nchi hii, au usikute tumechagua wahamiaji(viongozi) wanatafuta maisha hapa tz, oooppphhhh 500mls only for tea?
   
 19. BabaBabuu

  BabaBabuu Member

  #19
  Jun 18, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  "bajeti hiyo imewasilishwa 'kisanii' kutoka chama cha 'kisanii' kinachoongozwa kwa 'usanii' mkubwa." - Profesa Ibrahim Lipumba

  ahahahahaha Lipumba bwana, si angesema tu kiongozi wao ndo MSANII. anazunguuuka kichaka. anyway:
  1.hapo ni chai tu, siku tukija kuambia matumizi mengineyo kama ya stationaries and other facilities; huchelewi kuja kupewa figure ambayo utakuta kila mfanyakazi wa serikalini anatumia kalamu 3 kwa siku, rim 1 ya karatasi kwa siku, toilet paper piece/roller moja kwa siku etc etc etc
  2. serikali hii ni reflection yetu sisi watanzania (wengi walioipigia kura CCM wako vijijini ambao im sorry kusema kwamba majority ni vilaza na masikini, lakini wameridhika na umasikini wao kwa kuendelea kuwachagua walewale wanaowatia umasikini). VIONGOZI VILAZA HUCHAGULIWA NA VILAZA. unategemea walevi wamchague mnywa soda kuwaongoza?!
  nawakilisha.........
   
 20. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #20
  Jun 18, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hiyo pesa mnadhani ni kweli yote inanunulia chai?
  Usishangae kujua kuwa haitumiki hata 1/10 lakini mwisho wa siku mahesabu yote yanakuwa sawa.
   
Loading...