Mkullo rushwa Ya Mafuta ya kupikia tamu ,umesahau mawese na alizeti tunayo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkullo rushwa Ya Mafuta ya kupikia tamu ,umesahau mawese na alizeti tunayo?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Phillemon Mikael, Jun 20, 2009.

 1. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #1
  Jun 20, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  Kuna kila viashirio kuwa mkullo na kaka yake wamekula mlungula wa waagizaji wa crude palm oil ...kwani mkakati wa maendeleo uliokuwapo ni kulinda wazalishaji wa ndani wanaotumia malighafi za ndani......kitendo cha kugeuka nyuma ghafla kinaonekana kina baraka za mkuu ....na ni kashirio kingine cha mlungula...lakini akumbuke yaliyowakuta kina kilotsi mpolongomnyi .....acha wale waliokula rushwa ya minofu ya saamaki....Safari hii wabunge mkimuacha MKULLO sintawaelewa........

  Nina mashaka kama kweli mkullo ni mtoto wa mkulima anayejuwa kuwa alizeti inazalimwa tanzania...,hiyo palm hapa ndio mwake...,kigoma na kwingine...,tunasababu gani ya kutumia mafuta makapi toka india...tena yanaumiza miili yetu....

  Nani hajuwi kuwa mbegu za pamba zinatoa mafuta safi ..na kwa kushuka kwa bei ya pamba angalau mbegu za pamba zingewatoa kifuta jasho wakulima kama zikipata bei nzuri....hivi kweli mkullo na kaka yake wamesoma uchumi wapi?????...kwa nini wanauwa uwezo wa ndani namna hiyo...hawa ni raia kweli ,ninayo mashaka????

  Hiki kiwanda cha BIDCO mfano kipo hapa na uganda kipo ....lakini uliza ..walipoenda uganda museveni aliwapa sharti la kuanzisha viota vya kuzalisha palm na akawapa shamba kubwa la kuzalisha miwese [palm]..kwenye moja ya visiwa vya ziwa victoria na kwenye msitu mmoja...amewapa ardhi yote wanayohitaji kuanzisha ukulima wa palm kutosha kiwanda chao.........sisi hapa pamoja na kuwa na hilo ziwa hatujawahi kufikiria cha kuganya pale ukerewe..na visiwa lukuki...,kigoma ...etc na kote reli inafika!!

  MUKULLO akwendere!!!!..iwe indiketa kwa wenzake mawaziri na kaka yake!!! Amekula ya mbuzi ..ataota mapembe[mikono yake inanuka rushwa ya waagizaji wa mafuta machafu ya kupikia ]

  wabunge msikubali!!
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,538
  Likes Received: 81,972
  Trophy Points: 280
  PM. Wabunge wameshakula naye sahani moja Mkullo. Hii ni dalili nyingine kwamba huyu jamaa Wizara hiyo imemzidi kimo hastahili kuwa hata deputy minister wachilia mbali Waziri kamili.

  Date::6/20/2009
  Wabunge 'wafuta' msamaha ushuru wa mawese

  Ramadhan Semtawa na Tausi Mbowe, Dodoma
  Mwananchi

  WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano jana waligomea kupitisha bajeti ya Wizara ya Fedha na Uchumi hadi serikali ilipokubali kurejesha ushuru wa forodha kwenye mafuta ghafi ya mawese kutoka nje.

  Katika hotuba ya makadirio na matumizi ya serikali kwa mwaka 2009/10 na Bajeti ya Wizara ya Fedha na Uchumi, serikali iliomba kufuta ushuru wa forodha kwenye mafuta hayo kwa maelezo kuwa uamuzi huo ulitokana na maazimio ya mawaziri wa fedha wa nchi wanachama wa Afrika Mashariki na kwamba ungeongeza ushindani kwa viwanda vya ndani.

  Lakini Wabunge jana walikataa kupitishwa kwa kipengele hicho namba 25 kwenye Bajeti ya Wizara ya Fedha na Uchumi, kiasi cha kusababisha Jenister Mhagama, aliyekuwa akiongoza kikao cha Bunge jana jioni, kuliahirisha kwa nusu saa ili kutoa muda kwa kamati ya uchumi na fedha kwenda kujadili namna ya kukifanyia marekebisho kipengele hicho.

  Baada ya kurejea ukumbini na kuelezwa mabadiliko hayo ya kurejesha makato ya asilimia 10 ya ushuru wa forodha kwenye mafuta ghafi yaliyotangazwa na naibu waziri wa fedha, Jeremiah Sumari, wabunge walipitisha bajeti hiyo.

  Katika hotuba yake ya bajeti kuu, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkulo alieleza kuwa maazimio ya kufuta ushuru huo wa forodha yalifikiwa kwenye kikao cha mawaziri wa fedha cha nchi wanachama kilichofanyika Mei 20, mwaka huu, muda ambao ni nje ya mchakato wa bajeti.

  Wabunge pia walipitisha uamuzi wa kuondoa asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa viwanda vidogo vya ndani vinavyozalisha mafuta, ikiwa ni hatua ya kuchochea uzalishaji wa bidhaa hiyo.

  Huo ni ushindi mwingine kwa wabunge baada ya serikali pia kukubali kurejesha msamaha wa VAT kwa taasisi zisizo za kiserikali na za dini ambao ulipendekezwa kufutwa kwenye bajeti kuu.

  Wabunge wengi waliochangia hotuba hiyo iliyosomwa Alhamisi iliyopita walipinga kwa nguvu zote uamuzi wa kufuta msamaha huo, wakisema taasisi hizo ni wadau wakubwa wa serikali katika kuwapa wananchi maendeleo.

  Mbali na wabunge, viongozi wa dini na taasisi zisizo za kiserikali walipinga vikali uamuzi huo, kiasi cha serikali kuwaita Dodoma na kushauriana nao kabla ya kutangaza kurejesha msamaha huo, siku moja kabla ya bajeti hiyo kupitishwa na wabunge.
   
 3. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #3
  Jun 20, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  halafu nashangaa kwa nini kwa mara ya kwanza tanzania..bajeti ya mwaka huu inaanza kutumika hata kabla tarehe 30 juni haijafika ..kama ilivyo kawaida ya miaka yote na utaratibu wa kawaida....inasemekana serikali imefilisika kabisa .....kiasi kuwa bila bunge kuwakubalia kuanza kutumia bajeti kabla ya tarehe 30 juni hata pesa za kulipa wabunge posho zilikuwa hakuna....

  hii ni serikali ya panya.....imekula akiba yote ya nchi kiasi kuwa hata nchi kujiendesha kwa mwezi mmoja kusubiria bunge la bajeti liishe kwa kutumia akiba ya taifa hatuwezi tena ....maskini tanzania!!!..nchi nzuri inayoliwa na wenye meno!!
   
 4. M

  Mbangaizaji Senior Member

  #4
  Jun 20, 2009
  Joined: Jul 23, 2007
  Messages: 121
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Wakuu kwenye hili la kuondoa kodi ya crude palm oil. Mkulo kaligoroga vibaya sana. Kinachonishangaza zaidi hivi hii ni serikali moja kweli? Nagu(Waziri wa Viwanda) anasema yake, Mkulo na bajeti yake miezi 2 baadaye anaweka vitu tofauti. Halafu eti KILIMO KWANZA!

  LEONARD MWAKALEBELA in Dodoma, 25th April 2009 @ 11:32, Total Comments: 0, Hits: 279

  Tanzania is spending a lot of foreign exchange in importing edible oil while it has the capacity and resources to produce surplus of that product for export. Minister for Industry, Trade and Marketing Dr Mary Nagu said that importation of edible oil was the second in the highest cost for the country after importation of fuel.

  She made the observation here in Dodoma after making a brief visit at Nyemo Investment Company Limited which processes sunflower oil. "You can't believe that after importation of fuel oil, importation of edible oil follows in costing the country hard earned forex. It is a pity considering the fact that we've resources and the potential for producing surplus edible oil.

  "By importing edible oil, we're exporting jobs, losing forex and creating poverty to farmers who constitute 80 per cent of Tanzania's population," she lamented. Dr Nagu said that the government, through her ministry, was committed to ensuring that Tanzania becomes self-sufficient of edible oil in the next two to three years.

  "We're organizing ourselves to meet that target because we've every reason and capacity to do so and this will also boost agriculture and eradicate poverty," she added. Director General of the company, Mr Rashid Ally Mamu said that the company had aimed to increase production capacity from 800 to 2400 litres per day.

  "We and other small processing industries aim to produce as much as possible to meet domestic demand and start exporting sun flower oil," he said. Mr Mamu also said that for the past three years, production of sunflowers had increased tremendously in Singida, Manyara and Dodoma regions. He cited an example of Dodoma Region where production of sunflower had increased from 27,007 tonnes in 2006/07 to 90,025 tonnes in 2007/08 where 90,025 tonnes produces 76,098 tonnes of sunflower oil
   
 5. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu umesahau? Hii ndo serikali yenyewe ya mwendo mdundo ( Jk, 2005)
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  yaani ni kama hatuna serikali. mkulo alisema uamuzi wa kuondoa huo ushuru ulifanywa na baraza la mawaziri, lakini wabunge wameondoa hicho kipengele na serikali imeridhia bila ya hilo baraza la mawaziri kuridhia. Ninapatwa na wasi wasi hapa iwapo kweli uamuzi wa wabunge utakubaliwa na kutekelezwa na serikali. Kwa kuwa hili linaonekana kuwa ni dili lililokuwa limepangwa kati ya waagiza mafuta na baadhi ya watendaji serikalini, si ajabu wataagiza hayo mafuta na kupewa tax exemptions
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Tangu lini mswahili mwenye pete nyingi vidoleni akawa na akili? Mkullo ni sawa na shangingi tu.... hizo pete anapata wapi muda wa kuzitunza? Bum.bafu kabisa mkullo
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  hata kama baraza la mawaziri ndo walikubaliana huo uchafu...si wale wale? Wanafikiria kujaza matumbo yao na kupeleka watoto wao nje ili hali watoto wetu wanaishia kwenye shule hazina hata madawati.

  kwa mfano ukiangalia maeneo yote ambayo wanalima pamba mbegu zake zina mafuta mazuri sana lakini kwa sababu tuna miwaziri na mibunge mipu.mbavu asiyo fikiria kesho basi yenyewe yanaona bora yaagize mifuta michafu kutoka india badala ya kuimarisha ginneries zetu.

  Halafu ukishaona mtu anapenda sana umalaya basi na rushwa iko naye...ndo mkullo huyo!
   
 9. A

  August JF-Expert Member

  #9
  Jun 20, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
 10. A

  August JF-Expert Member

  #10
  Jun 20, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Anajitetea eti ilipitishwa kwenye kikao cha mawaziri wa Africa Mashariki, sasa kwa spirit ya Jumui ni kuimarisha soko la ndani na si kua, hivyo hizo nchi nyingine zinatakiwa kununua hiyo mali ghafi ambayo ni Alizeti toka tanzania na si kuia kiuchumi tanzania, kwa kuimarisha uchumi wa Malasyia etc etc. Hivi tu wajinga kiasi gani?

  Waziri wa Fedha na Uchumi Bw. Mustafa Mkulo

  *Mbunge amhusisha rushwa uagizaji mafuta
  *Yeye asema hazuii mtu kueleza hisia zake
  *Asisitiza,Tanzania haijitoshelezi mafuta  Na John Daniel, Dodoma
  SIKU moja baada ya Bunge kupitisha bajeti ya Serikali, Waziri wa Fedha na Uchumi Bw. Mustafa Mkulo, ameendelea kusakamwa kuhusu uamuzi wa kufuta kodi ya asilimia 10 kwa mafuta ya kula kutoka nje nchi huku akituhumiwa kula rushwa kupitisha uamuzi huo ambao ni mwiba kwa wakulima.

  Uamuzi wa Serikali kufuta kodi hiyo unatokana na msimamo wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) lakini hata hivyo jambo hilo limezua mjadala mkali bungeni baada ya wabunge kutaka kurejeshwa kodi hiyo ili kulinda viwanda vya ndani hususan kuwanusuru wakulima wa zao la alizeti.

  Akichangia mjadala wa Muswada wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2009, Mbunge wa Kibaha Mjini, Dkt. Zainab Gama (CCM),alieleza kusikitishwa na uamuzi wa Bw.Mkulo kukubali kufuta kodi hiyo bila kujali maslahi ya Watanzania kwanza.


  "Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesikitika
  sana! Naongea kwa uchungu sana! Mawaziri wote wa Fedha waliotangulia walikataa hili, mfano Dada yangu Zakia Meghji, lakini yeye peke yake( Bw. Mkulo) anakuja tu anakubali, katika mazingira ya kawaida, mtu anaweza kusema
  kala rushwa!

  "Viwanda vyetu vya ndani vinakufa, hamwatendei haki wakulima wa alizeti, kama wapo wakulima wa alizeti jimboni mwake wanamsikia! Wakulima wote wa Tanzania wanamsikia! Waziri alisahau kwamba sisi ndio tunazalisha alizeti zaidi kuliko wenzetu?"Alihoji Dkt. Gama.

  Alisema mtu yeyote anayewakilisha Tanzania katika Jumuiya yoyote ikiwemo ya Afrika Mashariki, lazima atambue kwamba hakuna Jumuiya husika bila Taifa la Tanzania, kikubwa cha kwanza ni kujali maslahi ya Watanzania kabla ya uamuzi wowote.


  Alisema Serikali ya CCM kupitia Ilani
  yake ina nia nzuri na wananchi wake lakini wapo baadhi ya watendaji wanaotoa maamuzi yanayokwamisha azma ya kuboresha maisha ya wananchi na kuwataka wabunge wenzake
  kutokubali kupitisha jambo lolote hususani la kisheria bila kupata ushauri
  wa kitaalamu.

  "Lakini nimegundu sisi wabunge tulimpa mtu mmoja power (mamlaka)kutoa maamuzi hata kama yana athari kwa Taifa! Tusikubali kutoa maamuzi
  bila ushauri wa wataalamu, naomba nijilaumu, tujilaumu sisi wabunge wote wazoefu ukiachilia wageni tuliopitisha Sheria hii ya kumpa
  Waziri Power ya kuamua jambo!
  "Alisema Dkt. Gama.

  Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti
  wa Wabunge Wanaopiga Vita Rushwa, alimtaka Waziri Mkulo kulieleza Bunge kama Serikali imetenga Fedha za kuwalipa fidia wakulima watakaoathirika na uamuzi huo iwapo bei ya mazao yao hususan alizeti itaporoka.

  Pia alimgeukia Waziri Mkuu, Bw. Mizengo
  Pinda na kuhoji sababu iliyofanya Serikali kusikiliza kilio cha viongozi wa dini kuhusu msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT) kwa Taasisi zao huku ikipuuza kilio cha wakulima kuhusu kodi ya mafuta.


  "Wabunge wamelalamika kuhusu kuondoa kodi ya asilimia 10 hadi sifuri kwenye mafuta ya kula na haijatekelezwa, lakini viongozi wa dini wamesikilizwa au kwa kuwa Waziri Mkuu anaogopa laana zao ?" Viongozi tumesahau kwamba hata wakulima wana laana!"Alionya, Dkt. Gama.  Akizungumza na Majira nje ya ukumbi
  wa Bunge Mbunge huyo alisema Bunge lilifanya makosa makubwa kwa kukubali kupitisha itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Sheria
  namba 140 kifungu cha 12,17 na 19 zinazompa mamlaka Waziri wa Fedha kutoa maamuzi mazito peke yake.  "Hivi sasa hizi Kampuni zinataka kuanza kuzalisha mafuta mengi katika nchi jirani kisha Tanzania inakuwa soko kuu, wamefanya hivyo baada ya kuona wakulima wa Tanzania wanazalisha alizeti kwa wingi na watakosa soko maana
  walishazoe nchi yetu kuwa dampo la bidhaa zao, sasa hili Waziri hakuona?", Alihoji, Dkt. Gama na kuitaka Serikali kufanya maamuzi mapya
  juu ya suala hilo kwa manufaa ya Watanzania kwanza.

  Alisema uchunguzi unaonesha kwamba hakuna mafuta ghafi yanayotoka nchini Indonesia wala Malysia kama inavyodaiwa na Serikali badala yake nchi jirani wanaingiza mafuta ya
  kula kupitia mwanya huo.

  Akizungumza na waandishi wa habari
  nje ya Bunge, Bw.Mkulo alikanusha tuhuma za kupokea rushwa na kueleza kwamba yeye kama Waziri hawezi kumzua mtu kutoa hisia zake na
  kuongeza kwamba anayetajataja rushwa ndiye anatakiwa kuchunguzwa kwanza.

  "Siwezi kuzua mtu kutoa hisia zake,
  watu wakitaka kuzungumza waache wazungumze, ila hao wanaozungumza sana rushwa ndio wanatakiwa wachunguzwe kwanza," alisema Bw. Mkulo na kuongeza;

  "Kwanza kufuta hiyo kodi ya asilimia 10 si maamuzi ya Mkulo, kila Waziri anapokwenda katika kile Kikao cha Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki anawasilisha maazimio kwa Baraza la Mawaziri ya nchi yake. Yale ni maamuzi ya Baraza la Mawaziri la Tanzania siwezi tu kutoa hoja zangu na nikasema kama ninavyotaka mimi, hapana,"alisema Bw. Mkulo.

  Alifafanua kuwa hata anapokwena Marekani kuzungumza na Benki ya Dunia (WB), hawezi kusema lolote ambalo halijaidhinishwa na Baraza hilo na kusisitiza kwamba takwimu za
  Serikali zinaonesha kwamba Tanzania haina uwezo wa kuzalisha mafuta ya kutosha kwa kuwa inazalisha asilimia tano hadi 10 tu ya mbengu za mafuta ya kula.

  Alipoulizwa kama Serikali itafanya
  utafiti upya juu ya suala hilo ili kuondoa utata, alisema "Utafiti ulishafanywa na Wizara ya Viwanda na Biashara, Kilimo, Chakula na
  Ushirika, CTI (Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania) na kuonesha hatuna mbegu za kutosha kuzalisha mafuta ya kula, ndio maana nchi
  zote za Afrika Mashariki tukakubaliana kufuta kodi hiyo,"alisema.


  Alipoulizwa kuhusu taarifa kwamba
  watendaji kadhaa wa kampuni kubwa zinazozalisha mafuta ya kula nje ya nchi na kuingiza pamoja na mawakala wa viwanda vya nje vinavyotegemea soko la Tanzania, vilituma wawakilishi kumwona kuhusu suala hilo ili aridhie uamuzi huo uliokataliwa na
  mawaziri wenzake, alikanusha taarifa hizo kuwa si za kweli.

  "Si kweli kwamba wenye viwanda hivyo vya BIDCO, Mohamed Enterprises Tanzania Limited na Zakaria walikuja kwangu, hapana, labda kama walionana na mtu mwingine si mimi,"alisisitiza Bw. Mkulo.


  Aliwashauri Watanzania kuelewa kwamba
  mbali ya Jumiya ya Afrika Mashariki kuwa na faida nyingi pia watambue kwamba hakuna safari isiyokuwa na mawimbi na kutoa mfano kwamba hata mtu akipanda ndege kuna mawimbi yanayosababisha ndege kuyumba angani.


  Awali akiwasilisha maoni ya Kambi ya
  upinzani kuhusu muswada huo Mbunge wa Viti Maalum Bi. Magdalena Sakaya (CUF), alisema bado kambi hiyo inasisitiza umuhimu waSerikali kufuta misamaha ya kodi kwa Kampuni zote za madini badala ya kueleza kwamba inaendelea kufanya mjadala na kampuni hizo ili kuona uwezekano wa kuondoa msamaha huo.

  Kwa Maelezo ya Dk Gama naona iko haja ya kuipitia Protocol ya Huu Mkata wa Afrika Mashariki, ama sivyo tutaumia Vibaya saana. na Zaidi ya hpo tuwe tunafanya study kwa sehemu zingine kama Ecowas na SADC wa Mafuta ya kula si wanatengeneza kwa kutumia Malighafi inayo patika within na sio hii ya kuagiza Malasyia etc.
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Bwana Mkulo, yaani umesahau kuwa hoja hii uliiwasilisha wewe kwenye baraza la mawaziri na kuitetea kwa nguvu ili ikubaliwe? Unadhani kama wewe ungewaeleza kuwa hoja hii si nzuri wangeipitisha?
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Jun 20, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwanza sina budi kumpongeza waziri wa viwanda Mama Mary Nagu kwa darsa zito alotupa..maneno yake haya machache ni tosha kabisa kupinga hoja zote za Mkullo
  Ni aibu kubwa sana kwa nchi yetu kufuta kodi ya uagizaji wa mali ghafi yoyote ambayo inaweza kuzalishwa nchini... Kwanza kuagiza mazao au mafuta yatokanayo na kilimo toka nje, kinyume cha swala la dharura ni mpango wa kuua kilimo cha ndani na mifano mingi tumeiona katika mazao kama Mahindi, Ngano, Mchele na kadhalika..Leo hii Tanzania tunaagiza kwa kiwango kikubwa mazao yote ya chakula kuliko tunavyozalisha nchini na yote haya yanatokana na maamuzi mabovu na ya kijinga tunayofungiwa na serikali yetu..

  Nakumbuka vitu vingi sana.. zamani enzi za Mwinyi tuliingiza mitumba nchini kama swala la dharura, leo hii tunamaliza miaka 20 mitumba bado ni vazi la mlalahoi kwa sababu hatukujiandaa uzalishaji wa viwanda vya nguo, viatu, chupi sidiria na kadhalika nchini.

  Ukitazama mazao mengine kama mchele, mahindi na ngano pia tuliagiza nje kama swala la dharura wakati wa Mkapa lakini sheria hiyo imeendele bila kuongeza uzalishaji wa ndani hivyo mchele mazao haya yameanza kupotea na tumeanza kuzoea mali hizi toka nje kiasi kwamba hata mchele wa Kyela tunaanza kusahau ladha ya Jasmine rice toka Kyela..kwa sababu hakuna mtu asiyetaka urahisi.
  .
  Hata khanga za wanawake ilitokea tukaanza kuagiza toka Dubai, Kenya, India, Malaysia kwa sababu za upungufu wa uzalishaji nchini.. matokeo yake tukaua viwanda vyetu ambavyo vilitegemea uzalishaji wa pamba toka ndani nchini..
  Ni muhimu sana hawa wabunge wetu wafahamu kwamba kila hatua moja ya maamuzi yao huathiri hatua nyingine nyuma na mbele kwani biashara ni mkufu unaounganisha sehemu nyingi sana za ajira na uchumi...

  Somo zima la uzalishaji halihitaji msomi wala mwanasayansi ku figure out, demand na Supply vinafanya kazi vipi. Hata mama Ntilie mpika vitumbua anajua soko lake kabla hajaanza uzalishaji wa vitumbua..Ikiwa mkulima wa Kighoma atakwenda dukani na kukuta mawese toka nje (Malaysia) yamejaa madukani hayana bei, fikra zake mara moja zitakwenda kupunguza production yake, bei yake na pengine hata kutolima tena mawese kwa sababu yamejaa madukani tena yale Wadanganyika wanayotaka kuona - Mali toka nje.

  Bila shaka kabisa demand ya mafuta hayanchini inaweza jitosheleza kwa kuagiza toka nje (supply) na kuwapa kazi ngumu wakulima wa ndani kupata soko.. Mara nyingi wanunuzi wa mafuta au bidhaa toka nje huingia mikataba ya ununuzi..Na most of the time watakao umia ni wakulima wetu kwa sababu viwanda vikisha weka mkataba kununua tani 200 za miwese toka Malaysia ni lazima waagize tani hiyo bila kujali ni tani ngapi zinazalishwa ndani nchini..

  Na mfanyabiashara ana kila haki ya kutonunua miwese ya ndani kwa sababu hana mkataba na mkulima mdogo, mali aliyoagiiza toka nje inatosheleza soko lake..mkulima wa ndani atafute soko jingine kwani hana kinga wala sheria ya kumlazimisha mnunuzi (mwenyekiwanda) unless ashuke bei na kuingia hasara.. Yaleyale ya Unyonyaji!

  Hivyo kilimo cha mawese badala ya kuongezeka nchini kitapungua kila mwaka hadi kufikia nchi kutegemea uagizaji..tumeyaona haya toka ukulima wa Pmaba, kahawa, mahindi, mchele ngano na mazao mengine mengi tu yameathirika uzalishaji wake sii tu kutokana na msisitizo mdogo wa serikali bali pia nchi yetu imekuwa ikitegemea zaidi mali kutoka nje ambayo ilikubaliwa kuingia kama ni dharura mara ikawa ndio sheria na hali halisi ya uchumi wetu.
  Siku zote budget ndipo tunapoona mikakati ya serikali kwa muda mfupi na mrefu, sera ambazo zinajenga Tanzania ya kesho na sio kubomoa kisha tunaanza kujiuliza what happened!....
  Ama kweli NDIVYO TULIVYO!
   
 13. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #13
  Jun 20, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwa vile hatuewezi kuzalisha hizo mbegu basi suluhu ni kuendelea kuangiza kutoka nje na kuwapa msamaha waagizaji. Hayo ndio maendeleo Tanzania tunayatafuta ya kuwatajirisha akina,mkulo, mohamed enterprise, bidco na wengine wachache. Na siyo kuwatangazia watanzania kuwa sasa ni wakati wa kuzalisha mbegu hizo maana viwanda vya kusindika na soko lipo. Ukanda wote wa pwani unafaa kwa kilimo cha mawese, wakulima wamekatishwa tamaa kiasi kwamba hata miti ya mawese michache waliyonayo wamewaachia ngedere wakijidai nayo. Ajira millioni nne si ndio hizo kutoka kwenye mbegu au wanataka zishuke toka mbinguni?

  Hongereni akina mkulo maana ni wakati wenu wa wakutudanganya!
   
 14. O

  Ogah JF-Expert Member

  #14
  Jun 20, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Phill......si utani hili suala limekuwa gumzo kubwa huko ndani......surprisingly......watu na hasa Mkulu ana-act kama vile everything is fine............nilifikiri kauli ya Mh Pinda kuhusu matumizi ya serikali yaliashiria jamaa kuwa wako sensitive.......lakini wapi.....its business as usual.........na kibaya zaidi madeni ya nje yanaongezeka.........
   
Loading...