Mkullo, Fedha za EPA ni Umma

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
712
1,240
Tamko la Vijana wa CHADEMA dhidi ya kauli ya Waziri wa Fedha Mhe.

Mustafa Mkulo kuhusu fedha za EPA

Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tumeshtushwa na kusikitishwa sana na kauli iliyotolewa na Waziri wa Fedha Mhe. Mustafa Mkulo kama ilivyonukuliwa na vyombo kadhaa vya habari (Gazeti la Mwananchi na Habari Leo, Jumamosi tarehe 21.06.2008), tunanukuu;
“Mkulo asema fedha za epa hazikuwa za Serikali wala BoT”​

Tunalazimika kutoa tamko hili kwa umma wa Watanzania na Serikali yake tukiamini kuwa kauli hii si ya kupuuzwa, si msimamo binafsi wa Mhe.Mkulo bali ni msimamo wa serikali kwa kuwa imetolewa na serikali kupitia Waziri wake wa Fedha. Kwa mantiki yake kauli hii inamaanisha kuwa;

  1. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) hakustahili kukagua akaunti hiyo. Kwa hiyo alikagua kwa makosa.
  2. Fedha hizo zilikuwa za wafanya biashara na ziliingizwa BOT kwa makosa na sasa serikali imeamua kuwarudishia wafanya biashara hao fedha zao.
  3. Si lazima kwa fedha hizi kurejeshwa kwa kuwa si za serikali wala BOT.
Vijana wa CHADEMA tunasema kuwa kauli hii ya Mhe. Waziri ni upotoshaji mkubwa. Tunautaka umma wa Watanzania ujue fedha hizi ni fedha zao na huu ni wakati wa taifa zima kushikamana katika kupigania fedha hizi.
Kauli ya Mhe.Mkulo kuwa fedha za EPA si za serikali wala BOT inaashiria mambo yafuatayo kwa umma wa Watanzania;

  1. Kauli hii ni moja ya vielelezo vya kuendelea kutawaliwa na serikali isiyokuwa makini hasa katika Wizara ya Fedha, licha ya Mhe. Raisi Kikwete kufanya mabadiliko kadhaa ya baraza lake la Mawaziri. Ukosefu wa umakini wa serikali katika suala hili kwanza unajibainisha kwa viongozi wa serikali moja na ya chama kimoja (CCM) kutofautiana katika kauli zao. Mhe. Raisi Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wamewahi kutamka moja kwa moja na kutoa kauli kadhaa ambazo kimantiki zilibainisha kuwa Fedha za EPA ni Fedha za Umma chini ya usimamizi wa Serikali lakini Mhe. Waziri Mkulo kana kwamba Wizara yake si sehemu ya serikali hii alidiriki kutoa kauli tofauti na viongozi wenzake. Waziri huyu huyu hivi karibuni akishirikiana na wafanyakazi wa Wizara yake aliandaa na kusoma hotuba ya Bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2008/2009 ikiwa na mapungufu makubwa ya kitakimwu na akatoa hoja ya kulitaka Bunge liipitishe. Ukosefu huu wa umakini wa serikali hasa katika uendeshaji wa Wizara nyeti ya Fedha unadhihirisha kuwa hakuna tofauti yoyote kati ya baraza la mawaziri liliundwa mara tu ya uchaguzi na hili lililofanyiwa mabadiliko na Raisi ya Kikwete hivi karibuni. Vijana wa CHADEMA tunasikitika sana kuona kuwa Mhe. Raisi Kikwete, huu ukiwa ni mwaka wa tatu wa utawala wake, bado amekuwa akijifunza jinsi ya kuunda serikali yake bila mafanikio. Vijana wa CHADEMA tunamshauri tena Mhe. Raisi Kikwete kulitazama upya baraza lake jipya la mawaziri kwani bado lina idadi kubwa ya mawaziri wasiomakini na wanaohusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi.
    Tunamtaka Mhe.Raisi asione haya kulifanyie tena mabadiliko baraza hili la mawaziri, bali azingatie haja kupata mawaziri bora ambao angalau watamwezesha kuanza kutekeleza ahadi yake ya kuleta maisha bora kwa kila mtanzania kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010.
  2. Kauli ya Mhe. Mkulo kwamba fedha za EPA si fedha za serikali wala BOT, ni kauli yenye kuwakatisha tamaa Watanzania kuwa serikali ya CCM inafanya usanii katika kushughulikia urejeshwaji wa fedha za EPA na kuwachukulia hatua waliohusika. Vijana wa CHADEMA tunasisitiza kuwa fedha za EPA ni fedha za umma na tunawataka waheshimiwa wabunge wote bila kujali itikadi zao waendelee kuibana serikali si tu katika kuhakikisha fedha za EPA zinarejeshwa bali pia katika kuhakikisha waliozichukua wanatajwa na kuchukuliwa hatua kali.
Ukweli kuhusu CIS, EPA na DCP
I. Commodity Import Support (CIS)
Kunako miaka ya 1978/1980 na kuendelea nchi yetu ilikuwa na uhaba mkubwa wa fedha za kigeni.Uhaba huo ulisababisha wafanya biashara waliokuwa wakiagiza bidhaa kutoka nje kushindwa kulipia bidhaa hizo. Hivyo nchi ikajikuta ina deni kubwa kutokana na bidhaa ambazo hazijalipiwa.Katika kulinda heshima ya nchi yetu serikali iliomba msaada/mkopo kutoka kwa wafadhili wa nje ili zipatikane fedha za kigeni kulipia mrundikano wa madeni.
Baada ya kupata msaada/mkopo serikali ilianzisha mfuko uitwao ‘COMMODITY IMPORT SUPPORT’ (CIS), ambapo wafanya biashara waliokuwa wanadaiwa bidhaa walizoagiza kutoka nje walikopeshwa na kulipia deni kwa fedha za kigeni. Masharti yalikuwa kwamba wafanya biashara hao watakuwa wanalipa kwa Shillingi ya Tanzania wakati serikali ikiwalipia kwa fedha za kigeni kwa ‘MKOPO’ kutoka mfuko huo wa CIS.

II. External Payment Arrears (EPA)
Ili kusimamia vizuri fedha hizo za CIS na kwa kuwa wafanya biashara wengi walikuwa wateja wa National Bank of Commerce (NBC), Benki kuu (BOT) iliagiza NBC ifungue akaunti iitwayo ‘EXTERNAL PAYMENT ARREARS’ (EPA) kwa ajili ya kukusanya marejesho yaliyokuwa yakifanywa na waliokopa kwenye mfuko wa CIS. Marejesho hayo yalikuwa yakitumwa benki kuu kila mwezi ili kwenda kufidia kwenye mfuko waliokopa. NBC ilisimamia akaunti hiyo ya EPA kwa muda lakini baadae ilifungwa na kuhamishiwa BOT.
Kwa lugha ya uhasibu akaunti ya EPA ilikuwa ni ‘SUSPENSE ACCOUNT’ kwa maana kwamba ni akaunti inayotumika kwa muda ili baada ya kukamilisha vipengere fulani fedha hizo zitaingizwa katika akaunti sahihi inayohusika.
Kwa mantiki hiyo fedha za EPA kama ‘Suspense Account’ zilitakiwa zirudishwe kufidia kwenye mfuko zilikotoka/kopwa.

III. Debt Conversion Program (DCP)
Utaratibu uliobuniwa na serikali kuwakopesha wafanya biashara fedha za kigeni kwa ajili ya kulipia bidhaa zao chini ya mpango wa Commodity Import Support (CIS) na baadaye kuwataka warejeshe kwa Shillingi ya Tanzania kupitia akaunti ya External Payment Arrears (EPA) ulikuwa mpango mahususi wa kuwasaidia wafanya biashara wasikwamishwe katika uagizaji wa bidhaa kutoka nje.

Hata hivyo pamoja na ukweli kwamba wafanya biashara waliwezeshwa kupunguza madeni yao bado serikali ilibakia na mzigo wa madeni kwa wafadhili waliotukopesha chini ya mpango wa CIS. Hivyo sambamba na mpango wa CIS na EPA ilibidi serikali ibuni mkakati au mpango mwingine wa kulipa madeni yake ya nje. Ndipo ulipobuniwa mpango uitwao ‘DEBT CONVERSION PROGRAM’ (DCP).

Chini ya mpango wa DCP serikali iliwataka WAFANYA BIASHARA WENYE ‘FEDHA ZA KIGENI’ NDANI NA NJE YA NCHI KUNUNUA MADENI hayo kwa fedha za kigeni na serikali (BOT) kuwalipa kwa shillingi ya Tanzania.

Iwapo kwa huruma ya wafadhili deni lililotokana na mfuko wa CIS limefutwa, Mh. Mkulo hawezi kutuambia kwamba fedha za marejesho kwenye akaunti ya EPA hazina mwenyewe kwa sababu wafadhili wamekwisha kutufutia deni. Taratibu za uhasibu haziendi hivyo.

Iwapo wafadhili wametusamehe deni basi hapana budi fedha hizo ziingizwe kwenye vitabu vya serikali kama mapato ili zipangiwe matumizi.Vinginevyo zinaweza kuingizwa Kwenye vitabu kama malimbikizo (General Reserve). Hivyo siyo sahihi kabisa kusema kwamba fedha za EPA hazina mwenyewe.
Umuhimu wa kulinganisha hesabu za EPA na CIS (Reconciliation of accounts)

Pamoja na msaada mkubwa uliotolewa na serikali kuwakopesha wafanya biashara ili waweze kulipia bidhaa zao kwa fedha za kigeni na kuwataka walipe kwa shillingi ya Tanzania kuna wengine waliokopeshwa chini ya mpango huo lakini hadi leo hawaja fanya marejesho kwa shillingi ya Tanzania kama walivyotakiwa. Pia kuna wengine waliorejesha na kupitishia kwenye akaunti ya EPA kama ilivyotakiwa lakini baada ya kugundua kwamba fedha hizo bado zimelala tu katika Suspense Account ya BOT walishirikiana na wajanja wachache na kudai kuwa fedha hizo hazina wenyewe na hivyo wakaweza kuchota kiasi cha shs. 133bn.

Wakati wale waliochota kwenye EPA wamejulikana wapo wale ambao deni lao kwenye mfuko wa CIS hatujaambiwa ni kina nani na wanadaiwa kiasi gani.

Hapana budi kumwomba tena Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) afanye kazi ya ziada ya kulinganisha hesabu hizo na kutuambia ni kina nani bado wanadaiwa .

Inahitajika kauli ya Serikali kuondoa utata.

Pia iundwe Kamati teule/Tume ya Bunge kuchunguza fedha za CIS

Vijana wa CHADEMA tunataka serikali kupitia kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu (CAG) ituambie kama kweli fedha za EPA si za serikali au BOT kama anavyodai Mhe. Mkulo. Kwa kuwa haijaundwa tume/kamati ya kuchunguza fedha za Commodity Import Support (CIS) ni vyema sasa ikaundwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza fedha hizo zilivyotumika ili kubaini wale wote ambao bado wanadaiwa. Tunahangaika kutafuta fedha kufidia nakisi kwenye bajeti wakati fedha ziko hapa hapa karibu mifukoni mwa mafisadi wachache.
Kutokana na mfano mzuri ulioonyeshwa na kamati ya Mwakyembe inaonekana ni Tume/kamati Teule ya Bunge pekee ndiyo inaweza kufanya uchunguzi wa kuridhisha kwenye jambo zito kama hili. Tume nyingi zimewahi kuundwa kufuatilia mambo mbali mbali lakini taarifa za tume zimekuwa ni siri ambapo wananchi hawajulishwi matokeo yake. Tunawataarifu wadau kuwa kuna nyaraka BOT zinazoeleza taratibu zote za CIS, EPA na DCP hivyo ni uongo mkubwa kwa Waziri Mkulo kuzidi kuupotosha umma na kusizitiza kwamba fedha za EPA siyo za serikali au BOT.

Vijana wa CHADEMA tunamtaka Waziri Mkulo ajiuzulu haraka iwezekanavyo kwa kulidanganya Bunge na umma wa Watanzania na kuonesha ukosefu mkubwa wa umakini katika kuiwakilisha serikali kwenye kikao cha Bunge cha Bajeti kinachoendelea.

Mwisho, tunawataka vijana wote wa Tanzania kujiunga na harakati za vijana wa CHADEMA katika kutetea haki na maendeleo ya vijana wa kitanzania na hasa kuhakikisha kuwa suala la EPA na ufisadi kwa ujumla vinashughulikiwa ipasavyo. Haiwezekani vijana wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga kukosa mitaji, na vijana wa vyuo vikuu kukosa mikopo huku mabilioni ya umma yakiwa yameachwa mikononi mwa wachache huku serikali ikiendelea kusisitiza kwamba fedha hizo si za umma.

Kwa kuwa imebainika fedha zimetolewa toka kwenye EPA kwa kutumia nyaraka za kughushi; huo sio wakati wa kujiuliza fedha ni za nani, ni wakati wa kuwakamata wezi walioiba fedha za EPA na kuhakikisha fedha zinarejeshwa katika mkondo unaostahili. Waziri Mkullo asitafute kisingizio cha kukwepa ama kuchelewa kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi wa BOT.

Imetolewa na;
John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana Taifa
25/06/2008

Mjadala mwema

JJ
 
Mkuu Yohani wa Mnyika.

Hayo maelezo umeyaweka kwenye lugha rahisi ambayo nadhani itaeleweka kwa wengi wa kawaida. Sijui mmesambaza kwenye vyombo vya habari (press release) au la..

Ni vizuri maelezo kama haya wayapate watu wa kawaida maana huu mkanganyiko wa Mkulo umewachanganya watu kwa kiasi kikubwa na inaelekea kudilute issue nzima ya EPA
 
Tamko hilo liko kwenye tovuti ya chama hivyo wanahabari wanaopita hapa wanaweza kabisa kunilikuu kama kauli rasmi ya Baraza la Vijana wa CHADEMA(BAVICHA), ama wanaweza pia kulichapa kama makala.

JJ
 
Mnyika, Zitto, Kitila
Sasa hivi ngoma iko uwanjani mnaichezajie? Kila siku mimi najiuliza sana kuhusu hili swali. Matunda yako tayari kuliwa mmejiandaa vipi kuyachuma. Hapa kwenye JF ni asilimia 0.0000001 ya watanzania wanaoona na kutambua udhalimu tunaofanyiwa. Waliowengi hawajuui kitu na huko ndio mnatakiwa mpeleke neno. Nlifurahishwa na juhudi zenu kiteto japo as usual wizi ulifanyika. Lakini juhudi zile zilikuwa nzuri sana, je zinafanyika kwa ajili ya 2010? au ndiyo yaleyale ya kupiga politiki tu bila kuwa na strategies za kuturescue watanzania. Kama 2010 tukiendelea na mzigo huu tunaoubeba, lawama zitakuwa kwenu(na sisi kiasi lakini sisi wengine hatuna vyama). You know more than many people know, and i do not see what you are doing to make them know the evil which is taking place in our country.
 
Mi naiweka hapa si lazima watu kwenda kule kwa ajili ya mtiririko wa hoja.

Ila big up Mnyika!

Tamko la Vijana wa CHADEMA dhidi ya kauli ya Waziri wa Fedha Mhe. Mustafa Mkulo kuhusu fedha za EPA

Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tumeshtushwa na kusikitishwa sana na kauli iliyotolewa na Waziri wa Fedha Mhe. Mustafa Mkulo kama ilivyonukuliwa na vyombo kadhaa vya habari (Gazeti la Mwananchi na Habari Leo, Jumamosi tarehe 21.06.2008), tunanukuu;

"Mkulo asema fedha za epa hazikuwa za Serikali wala BoT"

Tunalazimika kutoa tamko hili kwa umma wa Watanzania na Serikali yake tukiamini kuwa kauli hii si ya kupuuzwa, si msimamo binafsi wa Mhe.Mkulo bali ni msimamo wa serikali kwa kuwa imetolewa na serikali kupitia Waziri wake wa Fedha. Kwa mantiki yake kauli hii inamaanisha kuwa;

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) hakustahili kukagua akaunti hiyo. Kwa hiyo alikagua kwa makosa.

Fedha hizo zilikuwa za wafanya biashara na ziliingizwa BOT kwa makosa na sasa serikali imeamua kuwarudishia wafanya biashara hao fedha zao.

Si lazima kwa fedha hizi kurejeshwa kwa kuwa si za serikali wala BOT.
Vijana wa CHADEMA tunasema kuwa kauli hii ya Mhe. Waziri ni upotoshaji mkubwa. Tunautaka umma wa Watanzania ujue fedha hizi ni fedha zao na huu ni wakati wa taifa zima kushikamana katika kupigania fedha hizi.

Kauli ya Mhe.Mkulo kuwa fedha za EPA si za serikali wala BOT inaashiria mambo yafuatayo kwa umma wa Watanzania;

Kauli hii ni moja ya vielelezo vya kuendelea kutawaliwa na serikali isiyokuwa makini hasa katika Wizara ya Fedha, licha ya Mhe. Raisi Kikwete kufanya mabadiliko kadhaa ya baraza lake la Mawaziri. Ukosefu wa umakini wa serikali katika suala hili kwanza unajibainisha kwa viongozi wa serikali moja na ya chama kimoja (CCM) kutofautiana katika kauli zao. Mhe. Raisi Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wamewahi kutamka moja kwa moja na kutoa kauli kadhaa ambazo kimantiki zilibainisha kuwa Fedha za EPA ni Fedha za Umma chini ya usimamizi wa Serikali lakini Mhe. Waziri Mkulo kana kwamba Wizara yake si sehemu ya serikali hii alidiriki kutoa kauli tofauti na viongozi wenzake. Waziri huyu huyu hivi karibuni akishirikiana na wafanyakazi wa Wizara yake aliandaa na kusoma hotuba ya Bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2008/2009 ikiwa na mapungufu makubwa ya kitakimwu na akatoa hoja ya kulitaka Bunge liipitishe. Ukosefu huu wa umakini wa serikali hasa katika uendeshaji wa Wizara nyeti ya Fedha unadhihirisha kuwa hakuna tofauti yoyote kati ya baraza la mawaziri liliundwa mara tu ya uchaguzi na hili lililofanyiwa mabadiliko na Raisi ya Kikwete hivi karibuni. Vijana wa CHADEMA tunasikitika sana kuona kuwa Mhe. Raisi Kikwete, huu ukiwa ni mwaka wa tatu wa utawala wake, bado amekuwa akijifunza jinsi ya kuunda serikali yake bila mafanikio.
Vijana wa CHADEMA tunamshauri tena Mhe. Raisi Kikwete kulitazama upya baraza lake jipya la mawaziri kwani bado lina idadi kubwa ya mawaziri wasiomakini na wanaohusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi.

Tunamtaka Mhe.Raisi asione haya kulifanyie tena mabadiliko baraza hili la mawaziri, bali azingatie haja kupata mawaziri bora ambao angalau watamwezesha kuanza kutekeleza ahadi yake ya kuleta maisha bora kwa kila mtanzania kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010.

Kauli ya Mhe. Mkulo kwamba fedha za EPA si fedha za serikali wala BOT, ni kauli yenye kuwakatisha tamaa Watanzania kuwa serikali ya CCM inafanya usanii katika kushughulikia urejeshwaji wa fedha za EPA na kuwachukulia hatua waliohusika. Vijana wa CHADEMA tunasisitiza kuwa fedha za EPA ni fedha za umma na tunawataka waheshimiwa wabunge wote bila kujali itikadi zao waendelee kuibana serikali si tu katika kuhakikisha fedha za EPA zinarejeshwa bali pia katika kuhakikisha waliozichukua wanatajwa na kuchukuliwa hatua kali.
Ukweli kuhusu CIS, EPA na DCP

I. Commodity Import Support (CIS)

Kunako miaka ya 1978/1980 na kuendelea nchi yetu ilikuwa na uhaba mkubwa wa fedha za kigeni.Uhaba huo ulisababisha wafanya biashara waliokuwa wakiagiza bidhaa kutoka nje kushindwa kulipia bidhaa hizo. Hivyo nchi ikajikuta ina deni kubwa kutokana na bidhaa ambazo hazijalipiwa.Katika kulinda heshima ya nchi yetu serikali iliomba msaada/mkopo kutoka kwa wafadhili wa nje ili zipatikane fedha za kigeni kulipia mrundikano wa madeni.

Baada ya kupata msaada/mkopo serikali ilianzisha mfuko uitwao ‘COMMODITY IMPORT SUPPORT' (CIS), ambapo wafanya biashara waliokuwa wanadaiwa bidhaa walizoagiza kutoka nje walikopeshwa na kulipia deni kwa fedha za kigeni. Masharti yalikuwa kwamba wafanya biashara hao watakuwa wanalipa kwa Shillingi ya Tanzania wakati serikali ikiwalipia kwa fedha za kigeni kwa ‘MKOPO' kutoka mfuko huo wa CIS.

II. External Payment Arrears (EPA)

Ili kusimamia vizuri fedha hizo za CIS na kwa kuwa wafanya biashara wengi walikuwa wateja wa National Bank of Commerce (NBC), Benki kuu (BOT) iliagiza NBC ifungue akaunti iitwayo ‘EXTERNAL PAYMENT ARREARS' (EPA) kwa ajili ya kukusanya marejesho yaliyokuwa yakifanywa na waliokopa kwenye mfuko wa CIS. Marejesho hayo yalikuwa yakitumwa benki kuu kila mwezi ili kwenda kufidia kwenye mfuko waliokopa. NBC ilisimamia akaunti hiyo ya EPA kwa muda lakini baadae ilifungwa na kuhamishiwa BOT.

Kwa lugha ya uhasibu akaunti ya EPA ilikuwa ni ‘SUSPENSE ACCOUNT' kwa maana kwamba ni akaunti inayotumika kwa muda ili baada ya kukamilisha vipengere fulani fedha hizo zitaingizwa katika akaunti sahihi inayohusika.

Kwa mantiki hiyo fedha za EPA kama ‘Suspense Account' zilitakiwa zirudishwe kufidia kwenye mfuko zilikotoka/kopwa.

III. Debt Conversion Program (DCP)

Utaratibu uliobuniwa na serikali kuwakopesha wafanya biashara fedha za kigeni kwa ajili ya kulipia bidhaa zao chini ya mpango wa Commodity Import Support (CIS) na baadaye kuwataka warejeshe kwa Shillingi ya Tanzania kupitia akaunti ya External Payment Arrears (EPA) ulikuwa mpango mahususi wa kuwasaidia wafanya biashara wasikwamishwe katika uagizaji wa bidhaa kutoka nje.

Hata hivyo pamoja na ukweli kwamba wafanya biashara waliwezeshwa kupunguza madeni yao bado serikali ilibakia na mzigo wa madeni kwa wafadhili waliotukopesha chini ya mpango wa CIS. Hivyo sambamba na mpango wa CIS na EPA ilibidi serikali ibuni mkakati au mpango mwingine wa kulipa madeni yake ya nje. Ndipo ulipobuniwa mpango uitwao ‘DEBT CONVERSION PROGRAM' (DCP).

Chini ya mpango wa DCP serikali iliwataka WAFANYA BIASHARA WENYE ‘FEDHA ZA KIGENI' NDANI NA NJE YA NCHI KUNUNUA MADENI hayo kwa fedha za kigeni na serikali (BOT) kuwalipa kwa shillingi ya Tanzania.

Iwapo kwa huruma ya wafadhili deni lililotokana na mfuko wa CIS limefutwa, Mh. Mkulo hawezi kutuambia kwamba fedha za marejesho kwenye akaunti ya EPA hazina mwenyewe kwa sababu wafadhili wamekwisha kutufutia deni. Taratibu za uhasibu haziendi hivyo.

Iwapo wafadhili wametusamehe deni basi hapana budi fedha hizo ziingizwe kwenye vitabu vya serikali kama mapato ili zipangiwe matumizi.Vinginevyo zinaweza kuingizwa Kwenye vitabu kama malimbikizo (General Reserve). Hivyo siyo sahihi kabisa kusema kwamba fedha za EPA hazina mwenyewe.

Umuhimu wa kulinganisha hesabu za EPA na CIS (Reconciliation of accounts)

Pamoja na msaada mkubwa uliotolewa na serikali kuwakopesha wafanya biashara ili waweze kulipia bidhaa zao kwa fedha za kigeni na kuwataka walipe kwa shillingi ya Tanzania kuna wengine waliokopeshwa chini ya mpango huo lakini hadi leo hawaja fanya marejesho kwa shillingi ya Tanzania kama walivyotakiwa. Pia kuna wengine waliorejesha na kupitishia kwenye akaunti ya EPA kama ilivyotakiwa lakini baada ya kugundua kwamba fedha hizo bado zimelala tu katika Suspense Account ya BOT walishirikiana na wajanja wachache na kudai kuwa fedha hizo hazina wenyewe na hivyo wakaweza kuchota kiasi cha shs. 133bn.

Wakati wale waliochota kwenye EPA wamejulikana wapo wale ambao deni lao kwenye mfuko wa CIS hatujaambiwa ni kina nani na wanadaiwa kiasi gani.

Hapana budi kumwomba tena Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) afanye kazi ya ziada ya kulinganisha hesabu hizo na kutuambia ni kina nani bado wanadaiwa .

Inahitajika kauli ya Serikali kuondoa utata.
Pia iundwe Kamati teule/Tume ya Bunge kuchunguza fedha za CIS

Vijana wa CHADEMA tunataka serikali kupitia kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu (CAG) ituambie kama kweli fedha za EPA si za serikali au BOT kama anavyodai Mhe. Mkulo. Kwa kuwa haijaundwa tume/kamati ya kuchunguza fedha za Commodity Import Support (CIS) ni vyema sasa ikaundwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza fedha hizo zilivyotumika ili kubaini wale wote ambao bado wanadaiwa. Tunahangaika kutafuta fedha kufidia nakisi kwenye bajeti wakati fedha ziko hapa hapa karibu mifukoni mwa mafisadi wachache.

Kutokana na mfano mzuri ulioonyeshwa na kamati ya Mwakyembe inaonekana ni Tume/kamati Teule ya Bunge pekee ndiyo inaweza kufanya uchunguzi wa kuridhisha kwenye jambo zito kama hili. Tume nyingi zimewahi kuundwa kufuatilia mambo mbali mbali lakini taarifa za tume zimekuwa ni siri ambapo wananchi hawajulishwi matokeo yake. Tunawataarifu wadau kuwa kuna nyaraka BOT zinazoeleza taratibu zote za CIS, EPA na DCP hivyo ni uongo mkubwa kwa Waziri Mkulo kuzidi kuupotosha umma na kusizitiza kwamba fedha za EPA siyo za serikali au BOT.

Vijana wa CHADEMA tunamtaka Waziri Mkulo ajiuzulu haraka iwezekanavyo kwa kulidanganya Bunge na umma wa Watanzania na kuonesha ukosefu mkubwa wa umakini katika kuiwakilisha serikali kwenye kikao cha Bunge cha Bajeti kinachoendelea.

Mwisho, tunawataka vijana wote wa Tanzania kujiunga na harakati za vijana wa CHADEMA katika kutetea haki na maendeleo ya vijana wa kitanzania na hasa kuhakikisha kuwa suala la EPA na ufisadi kwa ujumla vinashughulikiwa ipasavyo. Haiwezekani vijana wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga kukosa mitaji, na vijana wa vyuo vikuu kukosa mikopo huku mabilioni ya umma yakiwa yameachwa mikononi mwa wachache huku serikali ikiendelea kusisitiza kwamba fedha hizo si za umma. Kwa kuwa imebainika fedha zimetolewa toka kwenye EPA kwa kutumia nyaraka za kughushi; huo sio wakati wa kujiuliza fedha ni za nani, ni wakati wa kuwakamata wezi walioiba fedha za EPA na kuhakikisha fedha zinarejeshwa katika mkondo unaostahili. Waziri Mkullo asitafute kisingizio cha kukwepa ama kuchelewa kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi wa BOT.

Imetolewa na;

John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana Taifa
25/06/2008

Source: http://www.chadema.net/tamko/2008/mkulo.php
 
ndio shida ya ushikaji huu sasa...kuwa weka watu vilaza kwenye wizara nyeti namna hii eti kisa ni rafiki yako au alikusaidia..utafikiri nchi ni kampuni yake....haya sasa kashaanza kulikoroga...kikwete mssaidie mwenzako kulinywa..!!

Huyu bora angepewa wizara ya jinsia tu
 
Bado Tanzania hatujawa na upinzani wa dhati dhidi ya CCM. Naomba wanaoijua historia ya TANU watufafanulie jinsi ambavyo TANU ilifanikiwa kumng'oa Mkoloni. Viongozi wa TANU waliwafuata wananchi vijijini ambako ndiko waliko watu ambao wananguvu ya kuleta ushindi katika chaguzi hata kama tunawadharau. Wapiga kura wanaoleta ushindi sio akina sie tunaochangia kwenye forums ama tunaosoma magazeti yaliyojaa cheche za kupita za wanasiasa. Wanaoleta ushindi ni hao wengi walio vijijini ambao bila kuelimishwa kuhusu mageuzi yanayohitajika wataendelea kupewa kanga, sukari, na kuvalishwa rangi za kijani na njano wakati wa kampeni za chaguzi na siku ya kupiga kura watakipigia kura chama kilicho'wafadhili' maana ndio hulka ambayo imeishajenga mazoea.

Mnyika, mie kazi yangu ni kupika jikoni kama jina langu lilivyo, naomba tu kuuliza kwa nyie wajuzi wa siasa, hivi chaguzi zikiisha basi vyama vyenu vinakwenda likizo? Nadhani mantiki ni kwamba baada ya uchaguzi kwisha inaanza kazi mpya ya kuzidi kukusanya nguvu na idadi ya wapigakura wenu ili kujihakikishia viti zaidi bungeni hata ushindi wa kuongoza nchi. Mie sijasikia kwamba kuna mikakati ya dhati ya wazi na hata ya kichini chini kama ile iliyofanywa na 'wanamtandao' ambayo ilianza tangu Mkapa alipowapiku kwa mgongo wa Nyerere mwaka ule wa 1995 na hatimaye kumpatia urais waliyemtaka.

Wapo watu wanaodhani kwamba historia ni kitu kilichopitwa na wakati na hakihitaji kufanyiwa reference ama kuigwa, mie nadhani hao wanakosea. Waliokuwepo wakati huo waliona na wengine wanaambiwa kwamba Mwalimu Nyerere kabla na hata baada ya Uhuru alikuwa akisafiri nchi nzima akitumia Landrover moja chakavu hivi. Kabla ya Uhuru alifanya kazi kubwa ya kuwahamasisha wananchi waelewe ubovu wa kutawaliwa na Mkoloni. Baada ya Uhuru kwa makusudi mazima alijiuzulu Uwaziri Mkuu akaenda kukiimarisha Chama chake na pia kuwaelimisha zaidi wananchi kwamba kupata Uhuru sio mwisho wa mambo. Kazi iliyokuwa mbele ilikuwa ni ni kubwa zaidi. Ndio maana mnaona mpaka leo juhudi hizo za hao waasisi zinaendelea kuifanya CCM ishinde chaguzi maana bado wananchi, wapigakura walio wengi, hawajaelewa maana ya siasa za ushindani wa vyama vingi na jinsi gani ushindani huo unaweza kuwaletea manufaa iwapo wataamua kuondokana na ukiritimba wa CCM ambayo inavyoelekea sasa imekuwa si chama tena kinachojali maslahi ya wananchi bali kina kazi ya kujisafisha na kusafisha wanaojichafua makusudi!

Amkeni kina Mnyika kama kweli mna nia njema juu ya mustakabali wa taifa letu. Au nanyi mnataka 'free ride' mpate vyeo ili nanyi mtanue kwa ufisadi.
 
Mkullo ni kangusilo mwingine tu katika hili suala. Tulitegemea afanyeje katika hali iliyopo ya kulindana na kusafishana? Ningekuwa mie Mkullo wala nisingejaribu kujibu hoja zilizoibuliwa. Ningewakusanya walioandaa ile Budget Speech ya Wizara tukaenda kuserebuka kwa glasi za mvinyo baada ya Budget kupitishwa. Ya nini kuhangaika wakati tayari viongozi wa Chama na Serikali wameshatumbukia kwenye dimbwi la matope na kuibuka wanakuta watoto wako chonjo wanashangilia kuona suti za wakubwa zilivyotapakaa tope!?
 
Waziri wa Fedha azidi kukabwa koo kuhusu kashfa ya fedha za EPA

*Atakiwa ataje wenye fedha za kwa majina
*Mbowe asema mafisadi wamemzidi nguvu JK

Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

WANASIASA na wasomi nchini wamesema Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, ameupotosha umma kuhusu fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kumtaka ataje makampuni ya ndani na nje na wamiliki wake ambao waliweka fedha katika akaunti hiyo.

Wasomi na wanasiasa hao wametoa kauli hiyo jana ikiwa ni siku moja baada ya Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, kulieleza gazeti hili kwamba, mpaka sasa yuko gizani kuhusiana na suala hilo, kwa sababu haelewi mantiki ya kauli ya Mkulo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, walisema fedha za EPA ni za umma kwani zilikuwa katika mikono ya BoT.

Mhadhiri kutoka Idara ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Leny Kasoga alisema fedha yoyote hata kama ni ya misaada, ikiingia katika mikono ya serikali huwa ya umma.

Alifafanua kwamba, hata kama fedha hizo zilitokana na misaada ya Benki ya Dunia na makampuni ya nje, halafu zikaingizwa serikalini kupitia BoT au taasisi yoyote ya fedha, ni za umma.

Aliongeza kwamba, kwa kuwa Mkulo ameamua kueleza kwamba wapo wafanyabiashara wa nje na wengine wamekufa ndiyo waliweka fedha hizo, ni vema akawataja ili kuweka sawa na kuthibitisha kauli yake.

Mchumi huyo alisema, Mkulo anapaswa kuueleza umma waliokufa ni akina nani, walio hai na makampuni yao yaliyopo ndani na nje nchi ili kuondoa utata wa kauli yake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe alisema kauli ya Mkulo inathibitisha kwamba Rais Jakaya Kikwete na serikali yake amezidiwa nguvu na mafisadi wa EPA.

Mbowe alidai kwamba, wadau wakubwa wa ufisadi wa EPA wamo ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kina husika moja kwa moja katika ubadhilifu wa fedha za umma.

Alisema ni upotoshaji wa makusudi, kusema fedha za EPA si za umma, wakati zimeibwa katika mikono ya BoT ambayo ni taasisi nyeti ya umma.

''Kauli ya Mkulo inaonyesha Rais Jakaya Kikwete amezidiwa nguvu na mafisadi wa EPA, ndiyo maana sasa hivi serikali inatoa kauli na taarifa za ajabu,'' alisisisitiza Mbowe.

Mbowe aliongeza kwamba, tangu awali serikali ilipinga tuhuma za ufisadi wa EPA baada ya kuibuliwa na wapinzani hivyo hata kutafuta Kampuni ya kufanya ukaguzi kulitokana na shinikizo si dhamira ya dhati ya serikali.

''Tangu awali nilisema kwamba, serikali ya Rais Kikwete haina dhamira ya dhati kupambana na ufisadi, kudhibiti wezi ambao wako ndani ya serikali, wadau wakubwa wa EPA wako ndani ya CCM na serikalini,'' aliongeza.

Alidai kuwa kauli ya Mkulo inaonyesha kuwa ni maelezo ya chama na serikali kutapata, kwa sababu muda kutoa matokeo ya uchunguzi wa ripoti ya EPA umefika na kisha watuhumiwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani

Kwa msisitizo, Mbowe alisema ni lazima walioba fedha hizo wafikishwe mahakamani kwani wametenda kosa la jinai hivyo hawapaswi kuachwa.

''Huku kote ni kutapata kwa serikali na CCM na inathibitisha serikali nzima haifai kukaa madarakani na si waziri Mkulo tu ,'' alisisitiza Mbowe.

Naye James Magai anaripoti kuwa, Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP) Mchungaji Christopher Mtikila, amemtaka Rais Kikwete, kumuondoa mara moja Mkulo katika Wizara hiyo kutokana na kauli yake aliyoitoa bungeni hivi karibuni kuwa pesa za EPA si za umma.

''Mkulo amedhihirika bayana kwamba ni mtu hatari sana kwa maslahi ya nchi,'' alisema Mtikila.

Alimtaka Mkulo aeleze kama fedha hizo si za wananchi ni za nani na awataje hao wafanyabiashara waliokuwa wakifanya biashara BoT.

''Kama hizo fedha si za umma, ni kwa nini Rais Kikwete alimfukuza kazi aliyekuwa Gavana wa benki hiyo, Daudi Balali,'' alihoji Mchungaji Mtikila.

Katika hatua nyinigne, Baadhi ya wananchi jjijini Dar es Salaam wameelezea kushangazwa na kauli ya Waziri Mkulo na baadhi yao walilazimika kupiga simu katika chumba cha habari cha gazeti hili kuomba ufafanuzi.

''Hivi huyu Mkulo ana maana gani kusema hayo aliyoyasema bungeni? Ina maana kwamba naye anataka kuanza kula fedha hizo. Kama pesa hizo si za umma serikali ilikuwa wapi kmuda wote huo kutueleza ukweli na kwa nini Kikwete alimfukuza kazi Balali,'' alihoji Gerald Onditi, mkazi wa Tabata.

Kauli ya Mkulo pia kauli inapingana na aliyotoa Luhanjo kwa niaba ya Rais wakati akisoma tamko la serikali hapo Januari 9, ambalo pamoja na mambo mengine lilitangazwa kufukuzwa kazi Gavana wa zamani wa BoT marehemu Daud Ballali.

Katika tamko hilo kwa niaba ya Rais, Luhanjo aliziita fedha hizo kuwa ni za umma na Rais alikasirishwa na ukiukwaji wa makusudi wa sheria na taratibu za kununua madeni hayo, ambao ulisababisha hasara kubwa kwa taifa.

Hata hivyo, Mkulo wiki hii kwa mara ya pili alilisitiza kwamba, fedha za EPA si za serikali, licha ya taarifa ya Rais Kikwete kupitia Luhanjo kueleza kuwa ni za umma na ufisadi huo ni hasara kwa taifa.

Sehemu ya maneno ya Rais katika tamko la serikali la Januari 9, baada ya kubainika ufisadi wa EPA ni kama yafuatavyo: " Fedha hizo zimelipwa kwa makampuni 22 ya ndani na kwamba kati ya fedha hizo Sh 90.3 bilioni zililipwa kwa makampuni 13 ambayo yalitumia kumbukumbu, nyaraka na hati zilizo batili za kughushi na makampuni hayo hayakustahili kulipwa chochote.

''Baada ya kuipitia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na ya Mkaguzi wa Nje, yaani Ernst&Young, Mheshimiwa Rais amesikitishwa na kukasirishwa kweli na taarifa za kuwepo vitendo vya ukiukwaji wa makusudi wa sheria, kanuni na taratibu za uuzaji wa madeni ya nje vilivyofanywa katika taasisi muhimu na nyeti kama vile Benki Kuu,'' alisema Luhanjo kwa niaba ya Rais.

Takwimu alizotoa Luhanjo kwa niaba ya Rais zinaonyesha, mwaka 1999 deni katika EPA lilifikia dola za Marekani 623 milioni, ambazo kati ya hizo, dola 325 milioni zilikuwa deni la msingi na dola 298 ni riba na baadaye deni likaongezeka hadi kufikia dola 677 milioni.

Hata hivyo, alisema chini ya Mpango wa Kununua Madeni (Debt Buy Back Scheme) wa mwaka 1994 kati ya serikali na Benki ya Dunia (WB), waliokuwa wanaidai BoT waliombwa wakubali kulipwa sehemu tu ya fedha wanazodai, wapo waliokubali na wengine kukataa na kuongeza hadi mwaka 2004 taarifa zinaonyesha jumla ya dola 228 zililipwa chini ya mpango huo.

Utaratibu huo ulileta matatizo ambayo yalibainika katika Ukaguzi wa Hesabu za BoT za mwaka 2005/06, ambao ulifanyika Agosti, 2005.

''Kukatokea kutoelewana kati ya BoT na Mkaguzi Deloitte and Touche', aliyegundua tatizo hilo, serikali iliingilia kati na Desemba 4, 2006, ilimuagiza CAG kuhakikisha ukaguzi huo unafanyika kwa kina,'' alisema Luhanjo.

EPA ni akaunti ya madeni ambayo ilitumika wakati wa Mfumo wa Ujamaa, ambayo awali ilikuwa katika iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) chini ya usimamizi wa BoT, kwa madhumini ya kulipa wafanyabiashara ambao waliingiza bidhaa nchini kwasabu wakati huo serikali ilikuwa inakabiliwa na uhaba wa fedha za kigeni.

Mwaka 1985, EPA ilihamishiwa BoT, na ndipo mwaka juzi kulipoibuka utata wa tuhuma za ufisadi katika akaunti hiyo kwa mahesabu ya mwaka 2005/06, ambayo utata huo ulisababisha Ernst&Young kufanya ukaguzi kuanzia Septemba sita na kukabidhi ripoti yake kwa CAG mapema Desemba mwaka jana.
 
Back
Top Bottom