Mkullo ashtushwa wingi wa bidhaa zinazoingia nchini ............

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Mkullo ashtushwa wingi wa bidhaa zinazoingia nchini
Monday, 13 December 2010 21:07

Daniel Mjema, Holili

MAMLAKA YA Mapato Tanzania (TRA), imepewa changamoto ya kufanya utafiti wa bidhaa zinazoingia nchini kutoka Kenya kupitia mpaka wa Holili, Mkoa wa Kilimanjaro ni nyingi tofauti na zinazopelekwa Kenya.
Changamoto hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, alipozungumza na wafanyakazi wa TRA, Idara ya Uhamiaji na Polisi wa kituo cha mpakani cha Holili.

Mkullo alipewa taarifa kuwa eneo la mpakani na Kenya kuna njia haramu za kuingiza na kusafirisha bidhaa kwenda nchi jirani zipatazo 450, taarifa ambayo ilimshtua waziri na kuahidi kushughulikia suala hilo kuongeza mapato ya serikali.
“Ni vigumu kwa serikali kujua mapato yake halisi kama mianya ya kukwepa ulipaji kodi stahili haitazibwa,” alisema Mkullo na kuongeza kuwa, tatizo la njia haramu za kutoa na kuingiza bidhaa ni kubwa linalopaswa kushughulikiwa kwa pamoja na nchi zote za mipakani, hususan Jumuiya ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki.
Awali, Meneja wa TRA mkoani Kilimanjaro, Patience Minga, alimweleza Mkullo kuwa Kenya imeingiza nchini, kupitia Kituo cha Holili, bidhaa mbalimbali zenye thamani ya Sh16,735,365,150.

Baadhi ya bidhaa hizo ni mafuta ya kupikia, bati, sabuni za kufulia, chumvi, mablanketi na sufuria.
“Ukilinganisha uingizaji bidhaa wa mwaka 2008 ilikuwa sawa na thamani ya Sh9,405,714,285 na usafirishaji bidhaa kwenda Kenya zilikuwa na thamani ya Sh823,340,984,” alisema Minga.

Alisema hivi sasa bidhaa hizo zinalipiwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa mujibu wa uhalisia wake na kwamba, kwa Afrika ya Mashariki Ushuru wa Forodha ni asilimia sifuri kuanzia Januari mwaka huu.
Pia, alimjulisha waziri kuwa TRA imezindua mfumo wa Central Data Processing Office Makao Makuu ya Forodha, Dar es Salaam ili kurahisisha utengenezaji nyaraka zote za bidhaa na makadirio ya ushuru wa forodha.

Wakati huo huo, TRA mkoani Kilimanjaro imekusanya mapato ya Sh56.8 bilioni kutoka Idara ya Forodha na Idara ya Kodi za ndani, hivyo kufikia lengo la asilimia 99.6 ya makadirio ya Sh57 bilioni kwa mwaka wa 2009/10.
Kwa kipindi cha bajeti ya mwaka huu, Julai hadi Novemba TRA Kilimanjaro imekusanya Sh25 bilioni ambazo ni asilimia 83.6 ya Sh30 bilioni zinazokadiriwa kukusanywa.
 
Hawa tunaowaita polisi na walinda usalama wetu wa huko pamoja na maafisa wa TRA huko, hizo njia zote za panya wanazijuwa na wanapolishwa kitu kidogo wao wanaachia tu. Hawajali hata chembe kuwa wanazidi kulididimiza Taifa.
 
Wanasiasa bwana,deudes kamara aliyekuwa waziri ea alikua akitamba eti tuna uza kenya zaidi kuliko wanavyotuuzia!hawa watu lazima tuwapime akili zao wanatudanganya kila kukicha
 
Alisema hivi sasa bidhaa hizo zinalipiwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa mujibu wa uhalisia wake na kwamba, kwa Afrika ya Mashariki Ushuru wa Forodha ni asilimia sifuri kuanzia Januari mwaka huu.
Pia, alimjulisha waziri kuwa TRA imezindua mfumo wa Central Data Processing Office Makao Makuu ya Forodha, Dar es Salaam ili kurahisisha utengenezaji nyaraka zote za bidhaa na makadirio ya ushuru wa forodha.

Wakati huo huo, TRA mkoani Kilimanjaro imekusanya mapato ya Sh56.8 bilioni kutoka Idara ya Forodha na Idara ya Kodi za ndani, hivyo kufikia lengo la asilimia 99.6 ya makadirio ya Sh57 bilioni kwa mwaka wa 2009/10.
Kwa kipindi cha bajeti ya mwaka huu, Julai hadi Novemba TRA Kilimanjaro imekusanya Sh25 bilioni ambazo ni asilimia 83.6 ya Sh30 bilioni zinazokadiriwa kukusanywa.
Sasa naanza kuelewa kwanini maafisa wa TRA hawajui chochote kuhusu mabadiliko ya kodi yafanywapo na Bunge. Bunge linatoa punguzo la kodi ya bidhaa, miezi 14 baadae, afisa wa TRA bado hana habari ya badiliko hilo. Aibu iliyoje!

Ila watu hawa ni mabingwa wa kwenda 'semina'!
 
Amestuka nini sasa, tatizo kukaa dar tu. Tuone atachofanya bla bla haisaidiiiiii.
 
Kwani walikuwa hawafahamu wanapoingia kwenye EAF wanaingia choo cha kike?
 
Back
Top Bottom