Mkulima wa China Mwenye Elimu ya Shule ya Msingi Atengeneza Helikopta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkulima wa China Mwenye Elimu ya Shule ya Msingi Atengeneza Helikopta

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by MziziMkavu, Aug 10, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Mkulima huyo akiitambulisha helikopta yake kwa mamia ya wakazi waliojitokeza Wednesday, August 05, 2009 2:56 AM
  Mkulima mmoja wa nchini China kwa kutumia elimu yake ya shule ya msingi ameweza kutengeneza helikopta yenye uwezo wa kupaa mita 800 toka ardhini akiwa nyumbani kwa wazazi wake kwa kutumia mbao na injini ya pikipiki.
  Kijana Wu Zhongyuan mwenye umri wa miaka 20 mkazi wa mji wa Luoyang, uliopo katikati mwa China alitumia miezi mitatu kutengeneza helikopta akiwa nyumbani kwa wazazi wake.

  Wu alisema kuwa alitumia kumbukumbu ya elimu ya fizikia aliyoipata akiwa shule ya msingi kuweza kutengeneza helikopta hiyo ambayo alidai ina uwezo wa kupaa mitaa 800 toka ardhini.

  "Sikuwa na mchoro wa helikopta niliyotaka kuitengeneza, nilitumia simu yangu kusaka ujuzi wa kutengeneza helikopta kwa kutumia internet" alisema Wu.

  Gazeti la Dahe Daily ambalo liliishuhudia helikopta hiyo lilisema kuwa mapanga ya helikopta hiyo yalitengenezwa kwa mbao, alitumia injini ya pikipiki kama injini ya helikopta yake na bodi la helikopta hiyo lilitengenezwa kwa mabomba ya vyuma.

  Wu ambaye kijiji chake kipo mlimani alisema "Nilikuwa na ndoto hii tangia nilipokuwa mdogo, nilikuwa sipendi kupanda mlima na nilitaka kwenda shule nikiwa kwenye helikopta yangu".

  Baba yake, Wu Xizhao, alimsifia mwanae na kusema kuwa alitumia si zaidi ya Tsh. Milioni 2.5 kuitengeneza helikopta hiyo ambayo ataanza kupiga nayo misele rasmi wiki hii.

  "Anapenda sana kutengeneza mashine mbali mbali, amekuwa akivikorokochoa na kuvijenga upya vifaa karibia vyote ndani ya nyumba" alisema baba yake.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2731014&&Cat=2
   
 2. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Only challenge will make us better.

  [​IMG]
   
Loading...