Mkulima Tajiri

Aman Ng'oma

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
954
510
*Utangulizi*

Kampuni ya *Kinasoru East Africa (T) Ltd* inakuletea semina kubwa na ya aina yake ya *Mkulima Tajiri.* *Mkulima Tajiri* ni mfululizo wa semina zinalenga kutoa elimu na mwamko mpya wa Kilimo Mkataba kwa mazao tuliyo na masoko nayo. Kwa kuanzia tutaanza na semina ya Kilimo Mkataba cha Zao la Pilipili Kichaa.

Kilimo Mkataba ni kilimo kinachompa uhakika wa soko mkulima. Katika semina hiyo mada mabalimbali zenye lengo la kutoa mwongozo kwa wawekezaji kuanzia namna ya kuzalisha, kusindika na hatimaye kuziuza zikiwa katika kiwango na ubora unaohitajika sokoni zitawasilishwa na wataalam nguli kwenye mnyororo mzima wa thamani wa uzalishaji wa Pilipili.

*Mada Zitakazowasilishwa*

1. Fursa za Masoko ya Kilimo
2. Kilimo Biashara (Agribusiness)
3. Njia Bora za Kilimo cha Pilipili (Good Agricultural Practices - GAP)
4. Kilimo cha Mkataba (Contract Farming)
5. Namna ya Usindikaji wa Pilipili Unaokidhi mahitaji ya soko
6. Nafasi za Taasisi za Fedha katika Kilimo

Katika semina hiyo tutakuwa wanunuzi wa Pilipili na hivyo Washiriki watapata nafasi ya moja kwa moja ya kuunganishwa na wanunuzi pamoja na kupatiwa mikataba ya kilimo cha Pilipili (B2B Meeting).

*WALENGWA WA SEMINA*

1. Wakulima
2. Wawekezaji
3. Wastaafu na wanakaribia Kustaafu
4. Vijana
5. Wasimamizi wa Mashamba
6. Mabwana Shamba
7. Vyuo vya Kilimo

*WATOA MADA*

1. MR. AMAN NG’OMA - Kinasoru East Africa (T) Ltd
2. MR. JOSEPHAT LIGONDO - Vergrab Organic Farming Ltd
3. JOSEPH MASIMBA - Sokoine University Graduate Entrepreneurs Cooperatives (SUGECO)
4. DR. GEORGE MKOMA - Mwenge Catholic University.
5. DR. FELIX NANDONDE – Expert in Agricultural Production and Marketing

Semina hiyo itafanyika tarehe *31/01/2020 – 01/02/2020* kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi 10:00 Jioni.

*UKUMBI*: LAPF, DODOMA Mjini.

*HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA:*- Stationaries, Vyeti vya Ushiriki, Chai pamoja na chakula cha Mchana

*ADA YA USHIRIKI:* TZS 100,000/= kwa mshiriki moja.

*NJIA YA MALIPO: NI KUPITIA BANK*

Namba ya Akaunti: *3009211317334,*
Jina la Akaunti: *Kinasoru East Africa (T) Ltd*
Benki: Equity
Tawi: Dodoma

Mwisho wa Malipo ni tarehe *28/01/2020* na unaruhusiwa kulipa Kidogo kidogo. *Wahi kuthibitiisha ushiriki wako mapema kwani nafasi ni chache.*

Mwisho wa kuthibitisha ushiriki ni tarehe *22/01/2020.* Kwa maelezo zaidi au kuthibitisha ushiriki tafadhali wasiliana na waandaaji kupitia namba. 0767989713, 0715989713 au 0786989713

*Mwaka 2020 hakuna kufeli, tukutane kwenye mafunzo!*
 
Back
Top Bottom