Mkulima aliyezuia ndege yetu Airbus 220- 300 huko Afrika Kusini, alipwe au asilipwe?

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
-MKULIMA ALIYEZUIA NDEGE YETU - AIRBUS 220- 300 HUKO AFRIKA KUSINI, ALIPWE, AU ASILIPWE?

Kikosi cha watu nane kilichoongozwa na Mh. Mustafa Mkulo na Mh. Andrew Chenge ndicho kilichoamua Bw. Hermanus Steyn alipwe kiasi cha Tsh. 44.7 milioni, kama fidia ya kutaifishiwa mali zake. Maamuzi hayo yalifikiwa mwezi Mei, 1984.
Wizara ya fedha ilikabidhiwa taarifa hiyo mwezi wa bajeti wa Juni,1984.

Yeye mwenyewe (Bw. Hermanus) alifungua madai ya fedha takribani Tsh. Milioni 373 ( thamani ya wakati huo), lakini serikali ilimlipa Sh. milioni 44.7 - Machi, 1985 kwa kufuata ushauri wa kamati ya Mustapha Mkulo na Andrew Chenge.

Bw. Hermanus alithibitisha kupokea hizo fedha, lakini hakuwa ameridhika na kiasi hicho.

Orodha ya mali zake zilizotaifishwa na thamani yake ya mwaka 1982 (kwa mujibu wa Hermanus mwenyewe) ni kama ifuatavyo;

Pikipiki, Matrekta, Magari na baiskeli vyenye thamani ya Sh13 million,

Pembejeo za kilimo vikiwemo mashine mbalimbali, mbolea na fanicha vyenye thamani ya Sh 13.4 million

Miundombinu ya maji yenye thamani ya Sh5.9 million.

Ofisi na vifaa vya ndani ya nyumba ya ofisi - Sh 530,400 na simu za upepo (radio calls) za Sh. 170,000.

Jengo lenye thamani ya Sh16.2 million.
Mifugo ya Sh 22.8 million

Mbao za Sh 4.1million na vifaa vya ujenzi vya Sh. 42,280,812.

Makontena, Matanki, Kemikali, Mafuta ya aina tofauti; vyote vyenye thamani ya Sh4.2 million.

Vyakula, mavazi na mali zingine za kutumia kila siku (viatu, saa, sahani, vibakuli) vyenye thamani ya Sh1.5 million.

Silaha zenye thamani ya Sh 626,850, na fedha taslimu (cash) Sh 5,827,902

Serikali ilipaswa pia kumlipa fidia ya ndege zake saba zenye thamani ya Sh. 15,350,000 (tatu kati ya hizo zilitumiwa na kampuni ya ndege ya Kenya, nne zingine zikiwa chini ya RVSL ya Tanzania)

Mali nyingine ilikuwa ardhi ya ukubwa wa ekari 18,649, ambayo Bw. Hermanus alihitaji fidia ya Sh. 211 million.

Watu wengi watajiuliza, kwanini Mahakama ya mjini J'burg (Jimbo la Gauteng) imetoa maamuzi ya kuishikilia ndege yetu ya Airbus, huko Afrika kusini leo?

Ni hivi, Mwaka 1982 serikali ya Mwl. Nyerere ilitaifisha mali za Bw. Hermanus Steyn, mzaliwa wa Namibia na mwekezaji mkubwa Tanzania, na kumlipa fidia ya Tsh. 44.7 milioni kwa kuwa serikali iliona hiyo fedha ndio anayostahili. Lakini Bw. Hermanus hakuridhika na amekuwa akidai fidia tangu wakati huo - kwa vipindi vya serikali zote. Amekuwa akiishi Tanzania kama muhamiaji - mwekezaji, pamoja na Namibia na Afrika kusini, hadi ilipofika Mwaka 2008, serikali ya Tanzania ilipomfutia uhamiaji wake na kumzuia asiingie nchini.

Sasa, serikali ya awamu ya tano, ilipoamua kumzuia Bw. Hermanus kuingia nchini, zuio hilo liliambatana na vitisho vya kushughulikiwa kikamilifu endapo angekaidi.
Bw. Hermanus, kwa mujibu wa maneno yake, aliona kama anaonewa na kuongeza kuwa hakuwahi kutamani haya yatokee. "Hili ni jambo ambalo kamwe sikutaka litokee, bila hiari yangu". Anasema.

Akaamua kubaki South Afrika. Wapi alipata wazo la kushitaki na kutumia ndege yetu kama kidhibiti -hatujui.

Maswali, kiasi alicholipwa Bw. Hermanus mwaka huo wa 1985 kilistahili? Au alipunjwa kwa sababu au kisingizio cha uhujumu uchumi?
Je! Baada ya kutaifishiwa mali zake, Bw. Hermanus alibaki na biashara gani hadi leo hii nchini Tanzania?

Ikiwa serikali ya Mwl. Nyerere ilikubali kumlipa Bw. Hermanus, bila kujali kiasi, tunapata kujua ya kuwa MKULIMA huyo alistahili kulipwa.
Je! kikosi cha akina Andrew Chenge na Mustapha Mkulo kilichopendekeza malipo ya Sh. 44.7 milioni, walikuwa sahihi au walimpunja Bw. Hermanus?

Mkulima Hermanus Steyn, mzaliwa wa Namibia aliyehamia na kuwekeza Tanzania, kisha mali zake zikataifishwa kwa ama kisingizio au sababu za uhujumi uchumi, naye akadai fidia kwa miaka 37, hadi alipowekewa zuio la kuingia Tanzania na vitisho juu - akamua kushitaki na mahakama ikaagiza ndege yetu Airbus 220-300 izuiwe kama dhamana, alipwe au asilipwe?
FB_IMG_1566991346562.jpg
 
Back
Top Bottom