Tukio la kusikitisha la mauaji ya Mkulima limetokea Kijiji cha Lukenge Kata ya Magindu tarehe 27/03/2019 , mbele ya Mkuu wa wilaya ya Kibaha ndugu Asumpta Mshana , wakati alipoenda kujaribu kusuluhisha mgogoro wa Wakulima na Wafugaji kwenye kijiji hicho .
Chanzo cha tukio hilo ni Jamii ya wafugaji wa kimasai kupeleka na kunywesha mifugo yao kwenye Lambo la Maji linalotumika na Wanakijiji kwa mahitaji ya kawaida , hivyo Mtendaji na Mwenyekiti wa Kijiji , walienda hapo lamboni kwa lengo la kuwaambia wafugaji waondoke eneo hilo na badala yake waliambulia kipigo kilichopelekea Majeruhi ya viongozi hao na kukimbizwa hospitali ya Wilaya kwa matibabu zaidi.
Mkuu wa wilaya pamoja na Askari walifika kwa lengo la usuluhishi na kuhakikisha wahusika wanakamatwa. Wakati wa kikao ukaibuka mzozo kwa wakulima kudai kwamba askari waliotangulia kabla ya mkuu wa wilaya waliwakamata wahalifu lakini inaonekana walijenga mazingira rafiki na hatimaye wahalifu hao kukimbia mbele yao.
Mzozo huo na kurushiana maneno ukapelekea Vurugu kubwa iliyosababisha askari kurusha mabomu ya machozi na wakati wananchi wanatawanyika.
Jamii ya wafugaji ya wamang’ati wakaanza kurusha mikuki na hatimaye kupelekea mwananchi mmoja ajulikanaye kwa jina la Mzee jisu kufariki kwa kuchomwa Mkuki.
Mpaka sasa hakuna mshukiwa yeyote aliyekamatwa, japo jitihada za kuwatafuta zinandelea.