Jeanclaude
JF-Expert Member
- Aug 30, 2013
- 259
- 238
Kwa hakika serikali ya chama cha Likud chini ya Bibi Netanyahu, Waziri Mkuu, yenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia, imekasirishwa mno na kitendo cha serikali ya Rais Barack Obama kufumbia macho azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lililolaani na kukemea uendelezwaji holela wa makazi ya walowezi katika ukingo wa magharibi, kwamba inavunja sheria ya kimataifa.
Waziri Mkuu wa Israel ameilaimu utawala wa Obama kwa kuanzisha na kuratibu kura ndani ya Baraza la Usalama na kisha kukaa pembeni. Itakumbukwa kuwa Benjamin Netanyahu aliamua kwenda kulihutubia Bunge la Congress mwaka 2015 bila baraka za Ikulu ya Obama.
Swali: kwa nini Obama ameamua wakati huu anapoondoka madarakani kuipiga Israel mkuki mgongoni wakati anatoka? Inawezekana Netanyahu alimsaidia Trump kumuangusha Hillary naye Obama kaamua kulipiza kisasi? Au ni kulipiza kisasi kwa kiburi cha Bibi kuamua kwenda uani kwa mwezake bila uratibu wake?