kurlzawa
JF-Expert Member
- Jan 23, 2018
- 16,703
- 20,606
Hii ni habari official kutoka kwa menager wa mchezaji ameandika katika ukurasa wake wa Instagram kuwa mteja wake ameamua kustaafu kuichezea team ya Taifa ya Tanzania. Kwa sababu ambazo amesema atazitanabaisha hapo baadae kama supporting evidence ya uhuni unaofanyika katika team ya Taifa.
========
WAKATI kiungo wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Jonas Mkude, akisisitiza hakuwahi kusema hana mpango wa kuitumikia Timu ya Taifa (Taifa Stars), ameweka wazi mapenzi yake makubwa aliyonayo kwa Wekundu wa Msimbazi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkude alisema uamuzi wake wa kuitumikia Simba kwa muda mrefu unatokana zaidi na mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo kwa vinara hao wa Ligi Kuu Bara ambao wana pointi 71 baada ya kucheza mechi 28.
Mkude alisema anaumizwa na taarifa ambazo si za kweli zinazungumzwa dhidi yake na mbali na yeye binafsi, hali hiyo humuumiza pia mama yake mzazi.
"Kila mchezaji anatamani kuchezea Timu ya Taifa, kwa hiyo mimi nitakuwa mtu wa ajabu kuikataa Timu ya Taifa, sijawahi kusema kokote kwamba siitaki Timu ya Taifa," alisema Mkude.
Kiungo huyo alikanusha taarifa za 'kujivunja' na kujitoa katika kikosi cha Taifa Stars kilichokuwa chini ya Mnigeria Emmanuel Amunike na alikubaliana na uamuzi wa kuachwa na kocha huyo ambaye mwaka jana alifanikiwa kuipeleka Tanzania kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2019).
Alisema pia bado anahitaji kutoa mchango wake kwa taifa endapo ataitwa lakini akikataa kuzungumzia taarifa za klabu nyingine iwe ya ndani au nje ya Tanzania kwa sababu bado ana mkataba na Simba.
Aliongeza amekuwa akiheshimu ratiba ya mazoezi na amekiri kufanya starehe mbalimbali pale muda wa kufanya hivyo unapomruhusu na hilo hufanywa na watu wengi na si yeye pekee.
"Hakuna mkamilifu, kila binadamu ana upungufu wake, kwa hiyo hata mimi nina upungufu wangu ninakubali,... napenda kucheza zaidi kama kiungo mkabaji, lakini nawakumbusha huwezi kucheza Simba miaka 10 kama huna lolote au huna nidhamu kabisa na bado ukavumiliwa," Mkude alisema.
Jonas Mkude
Chanzo: Nipashe